Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Pavement Pre-Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

Maagizo

  • Jibu maswali manne pekee
  • Swali la kwanza ni la lazima.
  • Maswali mengine matatu ya chaguliwe kutoka sehemu zilizobaki yaani; Riwaya, Tamthilia,Fasihi Simulizi na Hadithi Fupi.
  • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
  • Kila swali lina alama ishirini(20)
  • Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.

SEHEMU YA A (LAZIMA) TAMTHILIA-KIGOGO

  1. “………………………… huoni kisima kimeingiwa paka na maji hayanyweki tena?”
    1. Eleza muktadha wa dondoo (alama 4).
    2. Eleza sifa zozote nne za msemaji wa maneno haya (alama 4)
    3. Fafanua umuhimu mbili za mzungumzaji . (alama2)
    4. Thibitisha ukweli wa kauli kuwa kisima kimeingia paka na maji hayanyweki tena ukirejelea tamthilia ya kigogo (alama 8)

SEHEMU YA B: CHOZI LA HERI (RIWAYA) A.K.MATEI
Jibu swali la 2 au 3

  1. “Unajua kwamba mimi sikuumbiwa ujaalana, walimwengu ndio walionifinyanga upya,wakanipa moyo wa ujabari”.
    1. Eleza muktadha wa ndondoo (alama 4.)
    2. Fafanua sifa zozote mbili za mzungumzaji (alama 2)
    3. Mzungumzaji ana umuhimu gani katika riwaya?
    4. Fafanua kilichomsababisha mzungumzaji kuwa na moyo wa ujabari (alama 2)
    5. Taja tanakali zozote mbili zilizotumika katika dondoo (alama 2)
    6. Eleza jinsi maudhui ya ujaala ilvyojitokeza kwenye riwaya (alama 12)
  2. Ukiukaji wa haki za kibinadamu ni jambo la kawaida katika baadhi ya nchi zinazoendelea. kwa kurejelea riwaya ya chozi la heri, thibitisha ukweli wa kauli hii (alama 20).

SEHEMU YA C: HADITHI FUPI- TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE
(Dumu kayanda na alfa chokocho)
Jibu swali la 4 au la 5

  1. Akanyagapo chini ardhini inanatetemka…………………………………………………
    Amejitia hamnazo.Kabwela kama mimi nina faida gani?
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
    2. Fafanua mbinu tatu za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili (alama 6)
    3. Eleza madhila kumi yaliyompata kabwela .(alama 10)
  2. Huku ukirejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba na Shibe Inatumaliza. Fafanua maudhui ya ukiukaji wa haki
    (alama 20)

SEHEMU YA D: USHARI
Jibu swali la 6 au 7

  1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali:

    Kila mdharau chake

    Kuzimu wenda kuona, kila mdarau chake,
    Cha kwake akakikana, kutumai cha mwenzake,
    Fahamu anayo lana, mpiga chake mateke,
                Kila mdharau chake, kuzimu enda kuona.

    Siringe na kujivuna, chako ukakipa teke,
    Unajivuna, chako ukakipa teke,
    Unavunja lako jina, ili watu wakucheke,
    Ana lana kwa Rabana, kila mdharau chake,
                  Kila mdharau chake, kuzimu enda kuona

    Chako japo si cha mana, kibaya mtu ni chake,
    Unavunja lako jina, ili watu wakucheke,
    Ana lana kwa Rabana, kila mdharau chake,
                   Kila mdharau chake, kuzimu enda kuona

    Awe Fatu na Amina, Asha ndung yake,
    Katu hawatafanana, kila mtu hadhi yake,
    Kila mjuzi wa mama, huwa hadharau chake
                      Kila mdharau chake, kuzimu enda kuona

    Tama naomba amina , kilicho chetu tushike,
    Kidumu na kulingana, na tukipe hadhi yake,
    Ana lana kwa Rabana, kila mdharau chake,
                        Kila mdharau chake, kuzimu enda kuona

    Maswali:
    1.  
      1. Eleza ujumbe unaosisitizwa katika shairi hili (alama2)
      2. Mshairi anatoa ushauri gani katika utungo huu? (alama 2)
    2. Neno lana limefupishwa:
      1. Kwa nini limefupishwa (alalma2)
      2. Kutokana na shairi hili toa neno jingine lililofupishwa, kisha uliandike ukamilifu wake. (alama2)
    3. Eleza maana ya;
      1. chako ukakipa teke. (alama2)
      2. unavunja lako jina (alama 2)
    4.  
      1. Mstari wa mwisho wa kila ubeti wa shairi hili huitwaje (alama 1)
      2. Andika methali yenye maana karibu sawa na mstari wa mwisho wa kila ubeti wa shairi hili   (alama2)
    5. katika ubeti wa 4 kwa nini mshairi akasema (alama 2)
      Awe Fatu na Amina, au Asha ndungu yake, katu hawatafanana?
    6. Eleza maana ya:
      1. Kuzimu
      2. Kutumai
      3. Hadhi
  2. Soma shairi lifualalo kisha ujibu maswali

    Sikate tama

    Umeanguka, inuka, simama kama mnazi
    Umechunika,inuka, tia dawa kwa ujuzi
    Sasa inuka,inuka, kijana ianze kazi
    Sikate tama

    Usife tama, nyanyuka, ni muweza wa kutenda
    Kuna hadaa ,nyanyuka,anza tena kujipinda
    Dunia baa, nyanyuka,anza tena kujiunda
    Sikate tamaa

    Sivunjwe moyo, dunia hivyo itakunyanyasa
    Futa kiliyo, dunia hiyo idhibiti sasa
    Ipe kamiyo, dunia kamwe, siache kufusa
    Sikate tama.

    Una nguvuu, simama, wewe upambano nao
    Una werevu, simama, uzepuke njama zao
    Usiche kovu, simama, ujifunze vumilio
    Sikate tamaa
    (S.A Mohamed)

    Maswali:
    1. Eleza lengo la shairi hili (alama2)
    2. Mshairi anatumia mtindo gani ili kusisitiza ujumbe wake? Toa mfano moja. (alama 3)
    3. Kulingana na mshairi tungewezaje kuepuka njama unazofanyiwa? (alama 1)
    4. Mshairi anamaanisha nini kwa kusema usicho kovu? (alama2)
    5. Kwa nini mshairi akasema: sikate tama badala ya usikate tama? (alama2)
    6. Kuvujwa moyo kunaleta matokeo gani? (alama 1)
    7. Eleza muundo wa ubeti wa kwanza wa shairi hili (alama 4)
    8. Taja sifa mbili zozote zinazoewa msomaji (alama2)
    9. Mshairi anasema: “ umeanguka, umechunika,futa kiliyo.” Mambo haya matatu yanachangiza vipi katika kuendeleza lengo la mshairi. (alama 3)

SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI

  1. Tofautisha baina ya
    1. Hurufa na hekaya (alama 4)
    2. Hadithi za mazimwi na hadithi za mtanziko (alama 4)
    3. Usuli na visasili (alama 4)

      He! he! he! weee!
      Unayeogopa kutahiriwa
      Nani atatahiri badala yako
      Eh, eh… ni babu yako
      Eh, Eee!... kisu kikali mno!
      Lakini nitavumilia.
    4. Huu wimbo unaitwaje? (alama 1)
    5. Nini dhamira ya wimbo huu (alama 2)
    6. Taja sifa zozote tano za utanzu wa nyimbo kwa jumla (alama 5)


MARKING SCHEME

SEHEMU YA A: USHAIRI

  1.  
    1. Msemajii ni Babu akiwa amemjia Majoka ndooni baada ya Majoka kudungwa sindano ya kulala hapo chumbani mwa wagonjwa hospitalini.
    2. Sifa za msengi(Babu)
      • Ni mshauri mwema-anamshauri majoka abadili mienendo yake na asikie vilio vya wanasagamoo
      • Ni mwenye hekima: anathibitisha kauli kuwa maisha ni mabadiliko na maovu yana mwisho.
      • Ni mwenye utu-amawanjia majoka watendee watu(wanasagamoyo) mema.
      • Ni mwenye kudadisi-alimhoji majoka kwa undani sana.
    3. mwandishi ametumia kuonya umma kuwa si vyema kutendea wengine mabaya.
      • Anashauri wanadamu kuishi bila kunyanyasa wengine wala kutoongozwa na tamaa.
    4. uongozi wa majoka umefika mwisho.
      • Wanasagamoyo hawampendi tena majoka.
      • Tabia mbovu zimejulikana
      • Uongozi dhalimu wa majoka umejulikana.
      • Hapendi jimbo la sagamoyo
      • Wanasagamoyo wameupenda tunu na hawageuki hata.
      • Mapinduzi yanamkabili majoka.

SEHEMU YA B: RIWAYA

  1.  
    1. Ni wakati ambapo sauna anafika jinsi alivyobadilika na kuwa mtu mbaya. Anakumbuka
      Udhalimu uliofanyiwa na baba yake mlezi. Alikuwa kwa tajiri wake Bi. Kangara (4x1)
    2. Mzungumzaji ni sauna
      • Mlaguzi wa binadamu.
        Anafanya hii kazi na Bi-Kangara ya kuwauza watoto.
      • Mwenye bidii
        alifanya kazi yake iliyompa riziki kubwa.
    3. Mtumwa
      • Alifanya kazi chini ya masharti ya Bi. Kangara (2x1)
    4. Alikuwa ametendewa unyama na Babake mlezi alipewa mimba na babake mlezi.
      • Mamake anamwambia asimwambie mtu yeyote kuhusu huo unyama na ataiavya hiyo mimba.
    5.  
      • Kisengere nyuma - anakumbuka unyama aliotendewa.
      • Uzungumzaj nafsi- anajizungumzia akilini.
    6. Ujaala
      • Kuhusisha mwenyezi Mungu ambayo binadamu hana uwezo wa kuyabadilisha.
      • Ridhaa hakuwa mkazi asilia wa msitu wa Heri alikuwa mfuata mvua.
      • Mabadiliko ya sauna yalikuwa kwa uwezekano wa Mungu.
      • kifo cha bwanake Apendi,mzee mondu na kifo cha mkewe mwangeka alafu hawa wajane wawili kukutana na kufunga ndoa ilikuwa uwezo wa mwenyezi Mungu.
  2.  
    • Uendelezaji wa biashara haram ya kuwauza watoto Bi .kangara .
    • Watoto wachanga kuturukutwa kuuza na kutumia dawa za kulevya. Dick anafanya kazi ya kusambaza mihadarati nchi za ulaya.
    • Uavyaji wa mimba. Sauna anapata mimba kiholela na kutaka kujiua.
    • Baba mlezi kulala na mtoto wake. Mzee maya alimpa mimba suna.
    • Mwalimu fumba anampa Rehema aliyekuwa mwanafunzi wake ujamzito.
    • uvamizi na uwaji. Familia ya Ridhaa inavamiwa na mzee kedi na kuiangamiza.
    • Zohali anapopata mimba familia yake inamtelekeza.
    • Subira ananyanyaswa na wakwe zake kubaguliwa,kufitiniwa na kulaumiwa.
    • Kuozwa kwa mapema. Pete anapopashwa tohara anaozwa kwa mzee Fungo.
    • Naomi kuondoka na kuwaacha wanawe wabaki na kijakazi.
    • Lunga kuachishwa kazi(kustaafishwa0 kwa kuwa alimpinga Bwana Kalima. Wahafidhina kutokubali kuongozwa na kiongozi mwekevu, mwanamke.

SEHEMU YA C: HADITHI FUPI

  1.  
    1. Ni Dennis machora anapowaza alipomuona mamake shakila, mwanamke, pandikizi la mtu kirumbi cha mtu alipokuwa ameenda afisi ya shirika la kuchapisha magazeti.
    2.  
      • Chuku- Akanyakapo chini ardhi inatetetemeka au
      • ubalagha –kabwela kama mimi nina faida gani?
      • Uzungumzaji nafsi
    3.  
      • Alikosa kazi.
      • Alishindwa kujibu swali aliloulizwa.
      • Alijuta kuwa wazazi wake walimsomesha ilihali hana cha kuwapea.
      • Alifukuzwa na penina.
      • Aliishiwa na tama ya kuwa mwanahabari.
      • Alijutia na kusuta nafsi yake kutokana na mapenzi ya penina,ya kifaurongo.
      • Alitusiwa na penina kuwa yeye alikuwa mkata.
      • Maneno matamu ya mapenzi huwa uongo mtupu.
      • Alijua kuwa hakuna mapenzi bila pesa.
  2. Shibe inatumaliza
    • Dj alipewa pesa nyingi ili kuendesha shughuli katika sherehe kwa mzee mambo.
    • Dj. Alijinyakulia bohari kubwa ya dawa za serkali na kueka kwenye duka lake.
    • Dj hupata huduma za bure kama vile maji, umeme,matibabu na huduma zote za msngi huku mwananchi akiteseka.
    • Magari ya serikali yanatumika katika shughuli za kibinafsi.
    • Shere hizo kwa mzee mambo zinapeperushwa kwenye vyombo vya habari.
    • Mzee mambo kama kiongozi kuakizia wananchi Basmati badala ya kufanya kilimo nchini.
    • Kujipakulia mishahara mikubwa sasa nambura kula, kula kula bila kujali wananchi wenzake.
      Tumbo lisiloshiba.
    • Jitu la mraba mine kusema kuwa kesho tena lingekuja, chakula kipikwe mara dufu.
    • Baraza la mji kuwahamisha wanaporongomoka kwa lazima.
    • Polisi kutumika kuwafukuza watu wasio na hatia na kuwapiga virungu.
    • Wanamadongoporomoka kukosa pahali pa kulala.
    • Kubomolewa makaazi yao.
    • Jitu linatoa mbaya mle hotelini.

SEHEMU YA D: USHAIRI

  1. Shairi la kwanza
    1.  
      1. Yule anayedharau kitu chake na kukiona kuwa hakina thamana aatakuja kujuta.
      2. Mtu kama huyo pia atapata laana kutoka kwa mola. Chako hata kama hakina thamani ukipende na kukipalilia, usitamani cha mwingine. Kila mtu ana bahati yake alioumbiwa na Mungu.
        Penda chako na kukipalilia usitamani cha mwenzako.
    2.  
      1. Kutosheleza mizani/kupata idadai kamili ya mizani
      2. Wenda-unaenda/enda-anaenda/japo—ijapo/mana-maana/tama-tamati/kutumai-kutumaini.
    3.  
      1. Kuachana nacho/ kukidharau chako/kukiona chako duni/kikiona hakifai.
      2. Unaharibu sifa zako/unaharibu hadhi yako/unalizika jina lako/ unajipaka tope
    4.  
      1. Kibwagizo/kipokeo/mkarara/kiitikio.
      2. Kitu cha mwenzio usikilalie mlango wazi.
    5. Kila mtu ana bahati yake na uwezo wake. Hakuna watu wawili duniani walio na bahati/uwezo sawa,haa kama ni nduguyo.
    6.  
      1. Jehenamu/kuona mabaya/mabaya kukufukia/kujutia.
      2. Kutamani/kutegemea.
      3. Bahati/ kipawa/ uwezo.
  2. Shairi la pili
    1. Mshairi ana himiza aliyepata shida asife moyo bal ajitokokote na aanze tena
    2. Takriri-kurudia kibwagizo-sikate tama.kikwamba-kuruda kwa neno/maneno umeanguka,umechunika inuka.
    3. Kusimama imara,kutumia akili ulizonazo.
    4. Usifikirie yaliyopita(shida) lakini utie bidii na kuangalia na kutenda ya sasa.
    5. Kufupisha ili kutosheleza mizani
    6. Kuangamia.
    7. Mishororo mine(tarbia).Migao 3 kwa mishororo 10 kwa ubeti –ka-ka-zi isipokuwa kibwagizo
      Mizani 5-3-8=16
    8.  
      • Ana uwezo wa kutenda
      • Ana werevu wa kutenda
      • Ana nguvu za kutenda
    9. Yanamhimiza aliyepata shida afute kilio(ajitahidi kuweza kutatua shida aliyopata).

SEHEMU YA E FASIHI SIMULIZI

  1.  
    1. Hurafa ni aina ya ngano ambazo wahusika wake ni wanyama lakini wanao wakilisha binadamu ilihali Hekaya ni ngano pia lakini wahusika wake ni binadamu wanaowakilisha tabia za binadamu wa aina hiyo katika jamii.
    2. Hadithi za mtanziko ni zile ambazo mhusika hukumbwa na hali ngumu ya kuamua baina ya mambo au hali mbili ilihali hadithi za mtanziko ni hadithi ambazo wahusika ni mazimwi.
    3. Usuli ni aina ya ngano ambazo huelezea sababu za kuwepo kwa hali, tabia ama mahusiano Fulani k.m. mwewe na kifaranga ilihali visasili ni hadithi za kale ambazo huelezea imani na mtazamo wa jamii kuhusu asili ya ulimwengu na mwenendo wake.
    4. Nyiso
    5.  
      • Huwafahamisha kijana kuhusu matarajio ya uchungu huasa dhidi ya uoga woga.
      • Huwaandaa kihisia wanaotahiriwa kwa kuwapa ari ya kupitia kijembe cha ngariba.
    6.  
      • Nyimbo hutumia lugha nzito yenye kuibua twasira na hisia nzito.
      • Hutolewa kwa mahadhi ya kupanda na kushuka kwa sauti
      • Huandamana na uchezaji wa viungo kama vile mabega, kupiga makofi.
      • Baadhi ya vifungu katika nyimbo hurudiwarudiwa
      • Hufungamana na muktadhaa Fulani. 
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Pavement Pre-Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest