Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Asumbi Girls High School KCSE Mock 2021

Share via Whatsapp

Maswali

Maagizo

  • Jibu maswali manne pekee.
  • Swali la kwanzani la lazima.
  • Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani Tamthilia, Ushairi, Hadithi Fupi na Fasihi Simulizi.
  • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
  • Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.

SEHEMU A : LAZIMA
RIWAYA: CHOZI LA HERI: AsumptaMatei

  1. ...haifai kucheza na uwezo wa vijana, wao ni kama nanga. Huweza kuzamisha na kuiongoa merikebu.”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
    2. Bainisha tamathali mbili za usemi zilizotumika katika dondoo. (alama 4)
    3. Kwa kurejelea riwaya hii, onyesha jinsi vijana wamezamisha merikebu ya Wahafidhina. (alama 12)

SEHEMU B :TAMTHILIA
KIGOGO:Pauline Kea

Jibuswali la 2 au la 3.

  1. Chombo chenye rubani imara huhimili vishindo na hasira ya mawimbi makali.
    1. Weka dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)
    2. Tambua na ufafanue fani iliyotumika katika dondoo hili. (alama 2)
    3. Onyesha jinsi msemewa alivyofeli kuhimili ‘vishindo na hasira ya mawimbi makali’.(alama 4)
    4. Eleza kwa tafsili mambo yoyote kumi yanayokwaza usawa katika jamii ya kigogo. (alama 10)
  2.  
    1. Jadili jinsi kumi ambazo kwazo maudhui ya usaliti yanajitokeza katika tamthilia ya Kigogo. (alama 10)
    2. Eleza kwa kutolea mifano kumi ya matumizi ya Jazanda katika tamthilia ya Kigogo. (alama 10)

SEHEMU YA C: USHAIRI
Jibuswali la 4 au la 5

  1. USHAIRI
    1. Naja sasa ni ndiyani, naja kwetu mzalendo
      Naja nirudi nyumbani, nilowe kwa nako kando
      Kwetu mi nakutamani, kulona wingi uhondo
      Nijaye niile nyundo, misumari hadharani

    2. Naja kwingine kuwapi, kuloja alangu pendo?
      Nenda nende kwinginepi, sawa nako kwa muundo?
      Kaa kwingine anapi, ela kwenye lake gando?
      Nijaye niile nyundo, misumari hadharani

    3. Naja nijerudi papo, panale ndeme mgando
      Ningambwa kwetu hapo, kwamba kunuka uvundo
      Sitakwenda penginepo, ‘tarudi kuko kwa mwando
      Nijayeniile nyundo, misumari hadharani

    4. Naja sitapaki mbiya, ningambwa kuna vimondo
      Takuja kuvilekeya, vingani jiya kwa rundo
      Nilipozawa ‘tafiya, sikimbii kwenda kando
      Nijaye niile nyundo, misumari hadharani

    5. Najahiwa ‘mekomaa, kuzidi nilivyo mwando
      Tenan najiandaa, kwafikira na vitendo
      Kwetu nije kuifaa, nakitilio ya pondo
      Nijaye niile nyundo, misumari hadharani.

    6. Naja na ingawa naja, siwaekei mifundo
      Moyo wangu ushatuja, mawi nalotendwa mwando
      Ela wataoningoja, navyao viwi vitendo
      Nijaye niile nyundo, misumari hadharani.

      1. Huku ukitoa mifano mwafaka, liweke shairi hili katika bahari nne.(alama 4)
      2. Andika ubeti wa tatu kwa lugha tutumbi. (alama 4)
      3. Katika ubeti wa tano mshairi amepitia mabadiliko fulani. Yataje na udhibitishe jibu lako. (alama 2)
      4. Nafsi neni ni nani katika shairi hili? Thibitisha jibu lako. (alama 2)
      5. Yaandike maneno haya kwa Kiswahili sanifu. (alama 2)
        1. Mwando
        2. Ningambwa
      6. Onyesha kwa kutoa mifano miwili vile uhuru wa mshairi umetumika katika shairi hili. (alama 4)
      7. Nafsi nenewa ni nani katika shairi hili? Thibitisha. (alama 2)

  2. Soma Shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata.

    Ukabila ukabila, ukabila wa uzima
    Kenya yetu tamalizwa na janga hili ukabila.
    Makabila kaumba Jalali ukabila kaumbwa nani?
    Wakenya tutahadhari tusizongwe na hatari.

    Wauliza jina langu nakwambiya la ubatizo.
    Hutosheki na la kwanza wataka na la pili.
    Si kwamba wasaidia. Wajali kabila langu.
    Kabila langu walitakiani? Mimi ni Mkenya tosheka
    Na hilo.

    Wanasiasa watuchochea, kwa misingi ya kikabila,
    Mshike mshike ikitokea, wanasiasa tachana mbuga,
    Mwananchi wa kawaida, tabaki katika janga,
    Tuwaamini mpaka lini, wanasiasa matapeli?
    Wasituhadae watu hawa, hawana ukiritimba
    mawazo!

    Tuipende nchi yetu tupendane si Wakenya,
    Tuipende nchi yetu, raslimali tuipendayo,
    Tuaunina wenzetu, kwa vyovyote tuwezavyo,
    Tukumbuke kweli kuwa, nyumbani ni nyumbani,
    Hata kama ni pangoni.
    Kueneza ukabila ni matusi kwa nchi yetu,
    Ni aibu, laani anasikitiko, kwaye yote kumtukana
    Nina yake!

    Nchi yetu nchi yetu raslimali tuipendayo,
    Tuitunze ipasavyo, tusije kuiangamiza,
    Makabila ni mazuri ni maumbile yake Mola,
    Ukabila ni ushetani uloumbwa na wanadamu,
    Haufai haufai tukomeshe janga hili,
    Tukomeshe janga hili kabla tuangamiye!

    Maswali
    1. Lipe shairi hili kichwa mwafaka. (alama 1)
    2. Eleza dhamira ya msanii wa shairi hili. (alama 2)
    3. Fafanua muundo wa shairi hili. (alama 4)
    4. Andika ubeti wa nne kwa lugha tutumbi. (alama 4)
    5. Eleza mbinu mbili za fasihi zilizotumika katika shairi hili.(alama 4)
    6. Ni njia gani mwafaka ya kumaliza ukabila nchini Kenya? Toa maoni yako. (alama 1)
    7. Kwa kutolea mifano mwafaka onyesha jinsi mtunzi ametumia uhuru wa ushairi. (alama 4)

SEHEMU YA D: HADITHI FUPI
A. Chokochona D.Kayanda -Tumbo Lisiloshiba na HadithiNyingine.
Jibu swali la 6 au 7.
M.K. Ghassany-MameBakari

  1. ‘Lakini kwa nini, na kwanini hasa? … Je !,nimetendewa haya kwasababu ya udhaifu wangu- kwa sababu ni mwanamke...’
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili.(alama 4)
    2. Bainisha mbinu mbili za lugha ambazo zimetumiwa katika kauli hii.(alama 2)
    3. Fafanua sifa nne za mhusika anayerejelewa na kauli hii. (alama 4)
    4. Huku ukijadili hoja kumi eleza athari za maneno yaliyopigiwa mstari katika jamii. (alama 10)
  2. “Madhila ya mtoto mvulana katika karne ya ishirini na moja ni mengi” Tetea kauli hii ukirejelea hadithi zifuatazo:(alama 20)
    1. Mapenzi ya Kifaurongo
    2. Masharti ya Kisasa
    3. Ndoto ya Mashaka

SEHEMU E : FASIHI SIMULIZI

  1. “Magwiji wa uwando mpana wa tamaduni za kiafrika: wazee walioila chumvi wakabobea katika falsafa za turathi zetu, maghuluma wenye misuli tinginya na vifua vya mfumbata vinavyo stahimili hujuma za kila nui na malaika wa kike aliyesheheni mizinga na chemichemi ya urembo, nawasabahi. Wazamani waliamba kuwa mwacha mila ni mtumwa. Turathi zetu ni uhai. Turathi zetu ni msingi wa ubinadamu wetu. Turathi zetu zinabeba mustakabali wetu. Tuzienzi kama tuienzivyo asali.”
    1.        
      1. Tambua kipera cha utanzu wa mazungumzo kinachohusishwa na kifungu hiki. (alama 1)
      2. Thibitisha jibu lako katika (i) kwa mifano yoyote mitatu. (alama 3)
    2. Iwapo umehudhuria utendaji wa kipera hiki nyanja nieleza sifa tano za utendaji utakazoziona zisizojitokeza kwenye kifungu. (alama 5)
    3. Taja na ueleze miktadha minne ambamo kipera hiki kinaweza kutumiwa katika jamii ya kisasa. (alama 4)
    4. Eleza sifa zozote nne za jamii ya nafsi neni katika utungo huu. (alama 4)
    5. Eleza njia tatu za ukusanyajiwa data unazoweza kutumia kukusanya data kuhusu kipera hiki. (alama 3)

Mwongozo wa Kusahihisha

  1.      
    1.          
      1. Ni maneno yake Mwangeka (uk49.)
      2. Anamwambia Ridhaa
      3. Wamo katika uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Rubia.
      4. Ni baada ya kuyakumbuka maneno ya Tila kuwa haifai kucheza na uwezo wa vijana katika jamii. (4 x 1 = 4)
    2.   
      1. Tashibihi – wao ni kama nanga.
      2. Jazanda – merikebu inasimamia taifa la Wahafidhina.
      3. Taswira – Picha ya merikebu inayozamishwa. (2 x 2 = 4)
    3. Jinsi vijana walizamisha merikebu ya Wahafidhina.
      1. Genge la wavulana watano linawabaka Lime na Mwanaheri kwa kukisia kwamba wazazi wao hawakuchangia uchaguzi wa Mwanzi.
      2. Wanazorotesha usalama kwa kumvamia Subira na kumkata kwa sime kwa kumdhania kuwa hakumpigia kura Mwanzi.
      3. Vijana wanawavamia abiria barabarani wakiongozwa na kijana aliyekuwa amevaa shati lenye maandishi “Hitman” na kuwachome ndani ya magari.
      4. Wanayachoma magari barabarani.
      5. Sauna anaiba watoto wake Lunga-Dick na Mwaliko na kuwatenga na dada yao Umu.
      6. Pete anameza vidonge ili kuavya kitoto chake cha pili ila hakufanikiwa.
      7. Zohali anajiingiza katika mapenzi na kupata mimba akiwa kidato cha pili.
      8. Wanawe Kiriri wanakataa kurudi nyumbani- Kutoka ughaibuni walikoenda kusoma.
      9. Vijana wanamdhalilisha Mwekevu baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi.
      10. Kipanga anaachia masomo kidato cha pili na kuanza kunywa kangara – ananusurika kifo.
      11. Wanafunzi shuleni – wanakomsea Ridhaa- wanaendeleza ukabila dhidi ya wanafunzi walowezi.
      12. Vijana wanapokea hongo kutoka kwa wanasiasa kama papa ili wawachague, hivyo kuimarisha uongozi mbaya.
      13. Vijana wasichana wanajifungua watoto na kuwatupa kwenye majaa ya taka kama yule aliyeokolewa na Neema.
      14. Wanavunja sheria kwa kuandamana huku wamebeba picha za Mwanzi na kumhimiza atawale ingawa alikuwa ameshindwa n.k. (12 x 1 = 12)
  2.            
    1. (uk.83)
      • msemaji ni babu
      • anamwambia Majoka
      • Wako katika ambulensi
      • Majoka anadhani daktari wake ni babu yake anapoongea naye akipelekwa hospitalini. (4×1=4)
    2. Jazanda – chombo na rubani inalinganishwa na nchi na kiongozi.(alama 2 x 1 = 2)
    3.  
      • Msemewa ni Majoka.
      • Anawaua wapinzani wake.
      • Anawafunga watetezi
      • Anatumia wahuni kutisha wapinzani.
      • Anaamuru polisi kuwapiga risasi raia. (alama 4 x 1 = 4)
    4. Mambo yanayokwaza usawa:
      • Ubabedume
      • uharibifuwa mazingira
      • Unyakuzi wa ardhi
      • kukubalia biashara haramu.
      • Ukatili
      • matumizi mabaya ya vyombo vya dola.
      • Mauaji 
      • upiro miongeni mwa viongozi
      • Unyanyasaji
      • ukwere miongoni mwa viongozi.
      • Ufisadi
      • Uongozi mbaya.
        (Zozote 10 x 1 = 10) (atoe maelezo mafupi)
  3.       
    1. Maudhui ya usaliti.
      1. Kombe anamuunga mkono Majoka kisiasa lakini Majoka anashurutisha kufurushwa kwake kupitia kwa vijikaratasi vilivyosabazwa.
      2. Ngurumo alisoma na Tunu lakini anamsaliti kwa kumuumiza miguu.
      3. Majoka anawasaliti wafanyi biashara wa Sagamoyo kwa kumwaga kemikali katika soko lao.
      4. Majoka anasaliti juhudi za kuhifadhi mazingira kwa kufungulia biashara ya ukataji miti.
      5. Mkuu wa polisi Kenga anamsaliti Majoka kwa kumtoroka hali ya kisiasa ilipokuwa mbaya.
      6. Raia wa Sagamoyo wanasaliti wajibu wao wanapoendelea kumuunga mkono Majoka “dikteta”.
      7. Shule ya Majoka and Majoka Academy inasaliti wanafunzi kwa kuwaruhusu kutumia mihadarati.
      8. Ngurumo anamsaliti Boza kwa kushiriki mapenzi na Asiya mkewe.
      9. Majoka anasaliti raia kwa kufunga soko la Chapakazi.
      10. Majoka anasaliti wapiganiaji haki kwa kumuua Jabali mpinzani wake.
      11. Kenga anawasaliti Wanasagamoyo kwa kuunda genge ambalo lilizorotesha usalama.
      12. Majoka anasaliti Chopi kwa kupanga na Kenga ili auwawe licha ya kwamba alikuwa amemtumikia kwa muda mrefu.
      13. Majoka anawasaliti raia kwa kuchukua mikopo na kuitumia kwa mirandi isiyo wanufaisha.
      14. Serikali inamsaliti Ashua kwa kukosa kumwajiri licha ya kuwa amehitimu.
        (zakwanza 10 x 1 = 10)
    2. Jazanda
      1. Rubani – Viongozi wa jimbo la Sagamoyo
      2. Kigogo – kiongozi wa Sagamoyo
      3. Keki ya Uhuru – Raslimali za nchi
      4. Kutoa tonge mdomoni – tonge la Husda – Majoka ambaye ni mumewe.
      5. Kuku – Sudi ambaye ni mumewe Asha
      6. Chatu mmoja kutolewa kafara – chatu ni Sudi au Tunu auwawe.
      7. Majoka kutotumia bomu kuua mbu – hangetumia nguvu nyingi kuua Tunu. – anauwezo.
      8. Chatu kumaanisha watu wanaotekeleza mauaji wanapoambiwa na kiongozi – akina Ngurumo.
      9. Majoka kumshauri Sudi anawe mikono ili ale na watu wazima – akubali kuchonga kinyago ili Ashua aachiliwe.
      10. Majoka kuwa katika chombo cha safari ya jongomeo – uongozi wake unakaribia kuisha.
      11. Kisima kuingiwa na paka na maji hayanyweki – mambo yameharibika Sagamoyo.
      12. Chombo cha Majoka kwenda kinyumenyume – Majoka haleti maendeleo Sagamoyo.
      13. Marubani wasioendesha vyombo vyao vizuri – Viongozi wabaya
      14. Husda anafananishwa na chui anayeishi ndani ya ngozi ya kondoo – hampendi Majoka - unafiki
      15. Hashima anamuonya Tunu asijipeleke kwenye pango la nyoka – kujitia kwenye hatari
      16. Tunu anadai moto umewaka – harakati za kumng’oa Majoka zimeanza.
      17. Sumu ya nyoka – dawa za kulevya.
      18. Kanga – Majoka – mumewe Husda
        (za kwanza 10 x 1 = 10)
  4. USHAIRI
    1. Bahari nne
      1. Ukara – vina vya mwisho vina urari
      2. Mathnawi – vipande 2 ukwapi na utao katika kila mshororo
      3. Tarbia/unne – mstari minne kwa kila ubeti
      4. Kikwamba – neno (naja) limeanza mshororo katika kila ubeti (4 x 1 = 4)
    2. Lugha tutumbi
      1. Ninarudi hapo kwetu na nitakuwa hapo
      2. Hata nikiambiwa pananuka nitakaa tu
      3. Siendi pengine hivyo narudi hapo tu
      4. Nyundo ninakuja misumari jihadharini (4 x 1= 4)
    3. Amekomaa – anasema amekomaa kuliko mwanzo (2 x 1 = 2)
    4. Mzalendo anayeipenda nchi yake – hata kama pananuka atarudi tu
      Anataka kurudi kufaa nchi yake. (kutaja alama 1, kueleza alama 1 = 2)
    5.           
      1. mwando – mwanzo
      2. Ningambwa – ningaambiwa (2 x 1 = 2)
    6. Uhuru wa kishairi
      1. Inkisari
        • ametumia ritifaa – ‘mi – mimi
        • ‘tarudi – nitarudi
        • ‘mekomaa – nimekomaa
        • ‘tafiya - nitafia
      2. Tabdila
        • Sitapakimbiya – sitapakimbia
        • tafiya – tafia
      3. kilahaja
        • ndiyani – njiyani
        • Mwando – mwanzo
        • Ningaambwa – ningaambiwa.
      4. kuboronga sarufi –
        • naja kwetu mzalendo – mzalendo ninakuja/naja kwetu
        • kwetu ‘mi nakutamani – ninatamani kwetu
        • kulo na mwingine uhondo – kuna uhondo mwingi (2x2=4)
    7. Wananchi wa kwao hasa waliomtendea maovu (ubeti wa mwisho) (2 x 1 = 2)
  5.                 
    1. ukabila (1 x 1 = 1)
    2. dhamira
      1. kueleza jinsi nchi yetu ilivyokubwa na ukabila
      2. Athari zinazotokana na ukabila(2 x 1 = 2)
    3. Muundo
      1. beti tano
      2. idadi tofauti ya mshororo katika kila ubeti
      3. idadi tofauti ya mizani katika kila mshororo
      4. idadi tofauti ya vipande katika kila mshororo(4 x 1 = 4)
    4. ubeti wa nne – tutumbi
      Tuipende nchi yetu na tusaidie wanaohitaji usaidizi wetu. Tukumbuke kuwa nyumbani ni nyumbani hatakama haliyake ni gani. Ni tabia mbaya kueneza ukabila katika nchi yetu kwa sababu ni aibu kwa mtu kumtukana mama yake. (4 x 1 = 4)
    5. Mbinu mbili
      1. Takriri – ukabila ukabila
      2. Balagha – Wanasiasa matapeli?
      3. Istiari – ukabila ni shetani. (2 x 2 = 4)
    6. Njia ya kumaliza ukabila
      1. Kuhakikisha kuwa kila jamii imeshirikishwa katika uteuzi wa kiserikali.
      2. Kuanzisha kampeni za kumaliza ukabila.
        (1 x 1 = 1) (atoe maoni yake)
    7. Uhuru wa Ushairi
      1. inkisari – waumiza – unaumiza
      2. kuboronga sarufi – wasituhadae watu hawa – watu hawa wasituhadae.
      3. Tabdila – tuangamiye – tuangamie
      4. msamiati kale/lahaja – Jalali – Mungu, Nina – Mama (zozote 4 x 1 = 4)
  6.              
    1.     
      1. Maneno ya Sara
      2. “uzugumzi nafsia”
      3. akijiambia anarejelea alivyobakwa na jitu
      4. Tayari alikuwa mjamzito kutokana na ubakaji. 4x1=4
    2. mbinu za lugha
      1. takriri – kwa nini kwani nini
      2. balagha – kwa nini hasa?
      3. uzungumzi nafsi – wa Sara (2 x 1 = 2)
    3. sifa nne za Sara
      1. mwenye mapenzi ya dhati
      2. mwenye utu
      3. mwoga
      4. mwenye busara
      5. mkakamavu
      6. msamehevu.
        (lazima atoe maelezo, lazima amtaje Sara, za kwanza 4 x 1 = 4)
    4. Athari za ubakaji.
      1. Sara anahisi mdidimo na mkadamizo wa kiwiliwili chake.
      2. ujauzito
      3. kuvunjwa ujana jike.
      4. kuharibiwa maisha.
      5. Aibu na kudunishiwa na wandamu wenzake.
      6. kutengwa na wanajamii.
      7. Sara anaona laana na masumbuko kutoka kwa kila mtu aliye karibu naye.
      8. kilio na maombolezo katika familia.
      9. uoga kwa babake – atakavyokejeliwa na jamii.
      10. kufukuzwa shuleni na mwalimu mkuu.
      11. hisia za kujiua.
      12. wazo la kutoa mimba – unyama
      13. maafa – jitu linauwawa na wanakijiji.
        (za kwanza 10 x 1 = 10) (lazima atoe maelezo mafupi na mifano kutoka kwa hadithi husika.)
  7.  
    1. Mapenzi ya kifaurogo
      1. malezi duni – Dennis alalelewa katika mazingira ya kimaskini
      2. kuishi kwa majuto – Dennis anaishi kujihurumia
      3. kuaibishwa – Dennis anaaibishwa na Dkt Mabonga.
      4. upweke – Dennis anakumbuka wenzake wanavyojigamba.
      5. Maisha duni chuoni – Dennis anaishi kwenye chumba kisicho na vitu vya dhamani.
      6. kupuuzwa – Dennis anapuuzwa na wachapishaji vitabu.
      7. kushindwa kukidhi masilahi ya kibinafsi.
      8. Dennis anakosa chakula akiwa chuoni.
      9. kulazimishiwa mapenzi – Dennis analazimishiwa mapenzi na Penina
      10. kuishi maisha ya utegemezi – Dennis anamtegemea Penina.
      11. Ukosefu wa ajira – Dennis anaishi kipindi kirefu bila ajira.
      12. kusalitiwa kimapenzi – Dennis anasalitiwa na Penina baada ya kukosa kazi.
        (zozote 8 x 1 = 8)
    2. Masharti ya kisasa
      1. kuhangaika kutafuta mapenzi- Dadi anahangaika akimtafuta Kidawa
      2. Kuadhibiwa kimapenzi – Dadi anapewe masharti magumu na Kidawa
      3. Wasiwasi katika ndoa – Dadi anaishi kwa wasiwasi kwa kudhania kuwa mkewe anamwendea kinyume.
      4. Kudhibitiwa na mke – Dadi alazimika kufanya kazi za nyumbani ambazo hazimwafiki mwanamume.
      5. Dhihaka ya majirani – Dadi anadhihakiwa na Bii Zuhura.
      6. Kupata majeraha ya mwili – Dadi alianguka na kupoteza fahamu pale shuleni akichunguza kama kidawa ana uhusiano wa kimapenzi na mwalimu mkuu. (zozote 6 x 1 = 6)
    3. Ndoto ya Mashaka
      1. upweke na ukiwa wakuvunjikiwa na ndoa. – Mashaka anaingiwa na upweke baada ya ndoa yake kusambaratika.
      2. Uyatima – Mashaka alipoteza wazazi wake akiwa mtoto mdogo.
      3. kazi ngumu – Mashaka analazimika kufanya kazi ngumu shambani.
      4. kukosa Elimu – Mashaka hakuweza kuendelea na masomo yake.
      5. Malezi duni – Mashaka alilelewa na Bi. Kidebe aliyekuwa maskini.
      6. Pingamizi za familia katika suala la mapenzi – Mapenzi kati ya Mashaka na Waridi yalipingwa nafamilia ya Mzee Rubeya.
        (zozote 6 x 1 )(mtahini akadirie jibu la mwanafunzi katika swali hili. )
  8.          
    1.           
      1. Ulumbi 1 x 1
      2.        
        • matumizi ya lugha yenye mnato/tamathali za usemi – mwacha mila ni mtumwa
        • Taswira – ya urembo, misuli tinginya.
        • Takriri – turathi zetu, turathi zetu.
        • Kusema moja kwa moja mbele ya hadhira – nawasabahi.
        • Anafahamu hadhira yake (utamaduni)
          (za kwanza tatu 3 x 1 = 3)
    2. Sifa zisizojitokeza katika kifungu
      1. kupanda na kushuka kwa toni.
      2. kupaza sauti.
      3. kuvaa maleba maalum.
      4. matumizi ya viziada lugha.
      5. miondoko jukwaani
      6. kutua kidrama katika maongezi
      7. huenda akaimba, akauliza maswali, akaulizwa maswali na hadhira yake
        (za kwanza 5 x 1 = 5)
    3.    
      1. Asasi ya ndoa – mijadala ya mahari, utatuzi wa migogoro au kuchumbia
      2. Maabadini
      3. mahakamani
      4. Siasani
      5. Asasi ya elimu
      6. Muktadha wa upatanishi
        (za kwanza 4 x 1 = 4)
    4.   
      1. Inaenzi uzee
      2. inaenzi urembo
      3. wavulana wanastahili kuwa na nguvu.
      4. utamaduni unaenziwa
      5. Niwafugaji wa nyuki
        (za kwanza 4 x 1 = 4)
    5.  
      1. kutumia vinasa sauti
      2. kutumia kanda za kunasa video
      3. kuandika mazungumzo ya mtendaji
      4. kusikiliza kwa makini.
        (za kwanza 3 x 1 = 3) (mtahiniwa atoe maelezo mafupi katika swali hili. Mtahini akadirie jibu la mwanafunzi.)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Asumbi Girls High School KCSE Mock 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest