Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Lanjet Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

MAAGIZO:

  • Jibu maswali yote.
  • Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.

SEHEMU A.(Alama 15)
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali

Ulimwengu unapaswa kuzuka na mbinu za kulitandarukia tatizo ambalo linakwamiza juhudi za maendeleo. Umaskini unaokabili mataifa yanayoendelea, unayatosa kwenye dhiki kubwa huku mataifa ya kimagharibi yakipiga hatua kubwa kimaendeleo. Ufa uliopo baina ya mataifa yanayoendelea na yale kama vile marekani, nchi za ulaya na ujapani unapanuka kila uchao.

Vyanzo vya umaskini huu ni anuwai mathalan, ufisadi uongozi mbaya, turathi za kikoloni, uchumi kuegemezwa kwenye kilimo kinachotegemea mvua isiyotabirika, idadi ya watu inayoupiku uwezo wa uchumi wa taifa linalohusika na ukosefu wa nyenzo na mali za kuwakwamua raia kutoka lindi la umaskini, ukosefu wa elimu na nafasi adimu za ajira huchangia pia katika tatizo hili.

Jamii ya ulimwengu inapaswa kuelea kuwa umaskini unaothiri nchi fulani una athari pana sana. Uvunjifu unaotokana na umaskini unaweza kuwa mboji ambako matendo mabaya huchipuka. Raia maskini huweza kushawishiwa haraka kujitosa kwenye matendo ya kihalifo ili kujinasua kutoka dhiki ile. Hii inaweza kuwa mbegu ya kuatika maovu kama ugaidi na uhalifu wa kila aina.

Mataifa ya magharibi yanapaswa kuyaburia madeni ya mataifa yanayoendelea kama kama njia mojawapo ya kupambana na umaskini. Asilimia kubwa ya pato la kitaifa katika mataifa mengi hutumika kuyalipa madeni hayo. Katika hali hii inakuwa muhali kwa mataifa hayo kujikwamua kutokana na pingu za umaskini. Njia nyingine ni kustahabu kutoa ruzuku za kimaendeleo badala ya mikopo kwa nchi zinazoendelea.

Kwa upande wake, mataifa yanayoendelea yanapaswa kuibuka na mikakati bora ya kupambana na umaskini. Ni muhimu pawepo na sera zinazotambua ukweli kuwa asilimia kubwa ya raia wa mataifa hayo ni maskini. Pana dharura ya kuzalisha nafasi za ajira, kupanua viwanda hususan vinavyohusiana na zaraa ambayo ni tagemeo kuu la mataifa mengi, kuendeleza elimu na kuimarisha miundo msingi. Ipo haja pia ya mataifa haya kuhakikisha kuwa mfumo wa soko huru unaotawala ulimwengu sasa hauishii kuwa chanzo cha kufa kwa viwanda asilia na kuendeleza umaskini zaidi. Kwa ufupi ,maamuzi yote ya sera za kiuchumi lazima yauzingatie uhalisia wa maisha ya raia wa mataifa hayo.

Maswali:

  1. Kwa nini umaskini umetamalaki katika mataifa yanayoendelea? (alama 4)
  2. Madeni yana athari gani kwa mataifa yanayoendelea. (alama 2)
  3. Ni mapendekezo yapi ambayo mwandishi anatoa kwa mataifa machanga kuhusu utatuzi wa tatizo la umaskini? (alama 4)
  4. Mfumo wa soko huru una madhara gani kwa mataifa machanga (alama 2)
  5. Ukirejelea kifungu, eleza maana ya: (alama 3)
    1. Kulitandarukia……………………………………………………………………………………
    2. Kuatika……………………………………………………………………………………………
    3. Kuyaburia madeni………………………………………………………………………………

SEHEMU YA B :UFUPISHO.(alama 15).
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata

Kadiri jamii mbalimbali zinavyotagusana, ndivyo lugha zinazozungumzwa na jamii hizi nazo zinavyoingiliana na kuathiriana . Mojawapo ya athari hizi ni ukopaji wa msamiati kutoka kwa lugha jirani na kuutumia kuelezea dhana mpya zinazoingia katika utamaduni wao kupitia kwa mitagusano ya kijamii.

Lugha ya Kiingereza kwa mfano, imekopa kutoka lugha nyingine kama vile Kifaransa na Kilatini. Mathalani, istilahi nyingi za kisheria zimekopwa kutoka lugha ya kifaransa. Aidha,Kiingereza kimekopa kutoka lugha ya Kiswahili. Maneno ya Kiswahili kama vile mwalimu, jiko, mandazi, panga , buibui, ngoma na hata wananchi, sasa yameingia katika kamusi za Kiingereza, kumaanisha kuwa yamekubaliwa kama msamiati rasmi wa lugha ya Kiingereza.

Kiswahili nacho kimeathiriwa na lugha nyingine. Kimekopa msamiati wa Kiingereza na hata Kiarabu. Katika tungo nyingi za kishairi, kwa mfano, utenzi wa Mwanakupona utapata msamiati wa Kiarabu uliotoholewa. Lugha nyingine ambazo zimeathiri Kiswahili ni pamoja na Kijerumani ambako msamiati kama vile ‘shule’ ulikopwa na kutoholewa kutokana na neno schule. msamiati kama vile ‘leso’, ‘karata’ na ‘mvinyo’ yamekopwa kutoka lugha ya Kireno, huku majina ‘balozi’ na ‘bahasha’ yakikopwa kutoka Kituruki.

Pamoja na ukopaji wa vipengele vya lugha, mtagusano wa lugha una athari nyingine. Lugha zinapokuja pamoja, mazingira ya wingi-lugha hazuka. Baadhi ya watu hujifunza zaidi ya lugha moja. Mtu anayeweza kuzungumza zaidi ya lugha moja anaweza kujieleza kwa urahisi kwa kuchanganya msamiati wa lugha tofauti. Aidha, anaweza kubadilisha msimbo kulingaa na matilaba yake. Ikiwa anataka kukubalika na jamii-lugha anayotagusana nayo,anatumia lugha ya jamii hiyo ili kujinasibisha nayo. Wazungumzaji hupata visawe vya maneno kuelezea dhana zile zile, hivyo kuboresha mitindio yao ya mawasiliano

Kadhalika, kutagusana kwa lugha kunaweza kusababisha kubuniwa kwa lugha ngeni ambayo inarahisisha mawasiliano. Wakati mwingine, watu wanaozungumza lugha tofauti wanapokutana, hubuni mfumo sahili wa lugha ili kufanikisha mawasiliano. Pijini ni mfano wa lugha iliyobuniwa kwa njia hii. Pijini huchota msamiati kutoka lugha zilizotagusana. Sheng ni mfano mwingine wa lugha ambayo ilibuniwa kutokana na kutagusana kwa lugha ya Kiswahili, lugha za kiasili na kiingereza.

Japokuwa kuna faida nyingi za wingi-lugha, hasara pia zipo. Mazingira ya wingi-lugha huwapa wazungumzaji fursa ya kuchagua lugha wanayotaka kuwasiliana kwayo. Katika hali hii, lugha yenye ushawishi mkubwa kijamii, kiuchumi na kisiasa ndiyo inayopendelewa zaidi. Wingi-lugha unaweza kusababisha kukweza kwa lugha moja na kudunishwa kwa lugha nyingine, mathalini. Kuwepo kwa lugha nyingi nchini kulizua haja ya kukwezwa kwa lugha ya Kiswahili huku lugha nyingine za kiasili zikipuuzwa.

Lugha hukua kwa kutumiwa. Lugha isipozungumziwa kwa muda mrefu, watu hupoteza umilisi ambao huifanya kuwa vigumu kuirithisha kwa vizazi. Lugha inaweza pia kukosa wazungumzaji ikiwa wale wanaozungumza ni wachache au ikaathiriwa na mtagusano na lugha nyingine iliyo na wachache au ikaathirisha na mtagusano na lugha nyingine iliyo na wazungumzaji wengi. Katika hali kama hii, lugha hiyo hukubaliwa na tisho la kudidimia au hata kufa. Ikiwa jamii itakosa kudhibiti sera za matumizi ya lugha yake, baadhi ya lugha zitafifia au zitakufa na kusahaulika kabisa.

  1. Bila kupoteza maana,fupisha aya za kwanza tatu(maneno 50)alama 8,2mtiririko)
  2. Kwa mujibu wa taarifa hii,mtagusano wa lugha una athari gani?(maneno 30) alama 7,1mtiririko)

MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)

  1. Andika neno lenye muundo ufuatao wa sauti (alama 2)
    Kipua cha kaakaa laini, irabu ya kati tandazwa, kipasuo sighuna cha ufizi, irabu ya chini.
  2. Taja aina mbili kuu za ala za sauti kisha utoe mfano mmoja mmoja (alama 2).
  3. Tumia kivumishi kionyeshi cha karibu pamoja na nomino katika ngeli ya I-ZI, Kisha utunge sentensi katika ukubwa –wingi. (alama 2).
  4. Yakinisha sentesi ifuatayo katika wakati ujao hali timilifu wingi. (alama 1)
    Msomi hakutuzwa siku hiyo
  5. Tumia mzizi –w- katika sentensi kama (alama 2)
    1. kitenzi kisaidizi
    2. kitenzi kishirikishi
  6. Ainisha viambishi kwa kurejelea majukumu ya kisarufi katika neno hili (alama 3)
    Alijipelekea
  7. Maneno yaliyopigiwa mstari yametumikaje? (alama 1)
    Pahali pema pako si pema pa mwenzako.
  8. Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha matawi (alama3)
    Mlango umevunjwa na fundi aliyeujenga.
  9. Onyesha matumizi ya chagizo ya mfanano katika sentensi (alama 2)
  10. Andika katika usemi wa taarifa. ( alama 3)
    “Hicho kijicho cha paka cheupe leo marufuku kwangu”alisema mzee Kambumbu.
  11. Ainisha sentensi ifuatayo kwa kuzingatia jukumu lake. (alama 2)
    Pika ugali kwa kuku kila Jumamosi ukitumia gesi.
  12. Panda ni kuatika mbegu ardhini au kuparaga mti. Andika maana nyingine mbili. (alama 2)
  13. Tunga sentensi moja ukitumia kihisishi cha bezo ( alama 1)
  14. Tunga sentensi na ubainishe kijalizo (alama1)
  15. Tunga sentensi yenye muundo wa: (alama 3)
    Kiima, kiarifa, yambwa tendwa, yambwa tendewa na yambwa ala.
  16. Eleza maana ya msemo ufuatayo (alama1)
    Piga unyende
  17. Eleza tofauti iliyopo kati ya jozi hii ya sentensi. ( alama 1)
    1. Kerubo alinikimbilia.
    2. Kerubo alinikimbia.
  18. Weka nomino ifuatayo katika ngeli yake (alama 1)
    Mbalungi
  19. Tumia kiungo ‘na’ katika sentensi kuonyesha (alama1)
    1. ufupisho wa nafsi ya kwanza umoja fulani
    2. kihusishi kuonyesha aliyetenda jambo fulani.
  20. Andika sentensi ifuatayo upya ukizingatia kinyume cha maneno yaliyopigiwa mstari: (alama2)
    Ubora wa kazi zao ulifichika baada ya kuanzishwa kwa mradi ule.
  21. Tunga sentensi yenye muundo ufuatao.(alama 2)
    KN(N) + KT (T+E) + U+KN(N)+KT(T+E)
  22. Eleza matumizi ya kiambishi ‘ki’katika sentensi hii. (alama2)
    Njia hii haipitiki

ISIMU JAMII(ALAMA 10).

(George anakutana na Wanjiru nje ya kanisa baada ya ibada)
George:Hujambo dada Wanjiru?Mungu asifiwe!
Wanjiru:(akimsogelea kwa bashasha)Amen!Asifiwe sana.
George:Ni siku nyangi sijakuona.umekuwa wapi?
Wanjiru:Ndugu,Yesu anaendelea kujionyesha maishani mwangu.kwa majuma matatu sasa tulikuwa na crusade huko malishoni.Tulihubiri na wengi kumgeukia Mola.
George:Amen!mlienda na kina nani?
Wanjiru:Tuliandamana na mhubiri Petero na Kiongozi wa vijana .Zaidi ya watu 100 walihutubu na kumrudia BWANA.
George:Halleluya!
Wanjiru:wetu ni Mungu wa miujuza .nilipoulizwa kwandamana na wengine,niliitikia wito kama anavyoahidi Bwana ,tulibisha na akatushishia Baraka.Neno sasa limeeneahuko Lolo Kusini…
George:Ni Mungu mpaji ,hamsahau mja yeyote!
Wanjiru:Amen
George :Hata name nimeona akimmininia Baraka za ajabu.Nilikubwa na matatizo mengi lakini dada tukiomba tutapewa.Lazima tuwe kama Ruth,Naomi na Esher hata tunapomngojea Yesu kuja kutuchukua.
Wanjiru:(akimkatiza)kama ambavyo mhubiri ameseema leo,hizi ndizo siku za mwisho.Ndugu lazima tuombe tukikesha bila kumpa shetani nafasi yoyote.
George:Ashindwe!...

  1. Taja sifa tano za sajili ya mazungumzo haya.(alama 5)
  2. Dondoa msamiati unaotambulisha sajili hii (alama 5)


MARKING SCHEME

SEHEMU A.(Alama 15)

Maswali

  1. Kwa nini umaskini umetamalaki katika mataifa yanayoendelea?(alama 4)
    • ufisadi
    • uongozi mbaya
    • turathi za kikoloni
    • uchumi kuegemezwa kwenye kilimo kinachotegemea mvua isiyotabirika.
    • idadi kubwa ya watu inayoupiku uwezo wa uchumi wa taifa linalohusika.
    • ukosefu wa nyenzo na mali za kuwakwamua raia kutoka lindi la umaskini.
    • ukosefu wa elimu na nafasi za ajira. Zozote (4*1=alama 4)
  2. Madeni yana atahari gani kwa mataifa yanayoendelea(alama 2)
    • Asilimia kubwa ya pato la kitaifa katika mataifa mengi hutumika kuyalipa madeni hayo. (2*1=alama 2)
  3. Ni mapendekezo yapi ambayo yapi ambayo mwandishi anatoa kwa mataifa machanga kuhusu utatuzi wa tatizo la umaskini?(alama 4)
    • kuibuka kuwa mikakati bora ya kupambana na umaskini.
    • pawepo na sera zinazotambua ukweli kuwa asilimia kubwa ya raia wa mataifa hayo ni maskini.
    • kuzalisha nafasi za kazi kwa dharura.
    • kupanua viwanda hususan vinavyosuhiana na zaraa ambayo ni tegemeo kuu la mataifa mengi.
    • kuendeleza elimu.
    • kuimarisha miundo msingi. (4*1=alama 4)
  4. Mfumo wa soko huru una madhhara gani kwa mataifa machanga (alama 2)
    • Ni chanzo cha kufa kwa viwanda asilia na kuendeleza umaskini zaidi. (1*2=alama 2)
  5. Ukirejelea kifungu,eleza maana ya:(alama 3)
    1. Kulitadarukia-kulishughulikia,kulitatua,kulikabili
    2. Kuatika-kuanzisha kutia,kuzua.
    3. Kuyaburia madeni-kuyasamehe madeni,kuyaondolea madeni. (3*1=alama 3)

SEHEMU YA B :UFUPISHO.(alama 15).

  1. Bila kupoteza maana,fupisha aya za kwanza tatu(maneno 50)alama 8,2mtiririko)
    Nakala chafu
    hoja za kuzingatia
    • mitagusano ya kijamii hufanya lugha kuthiriana.
    • ukopaji wa vipegele vya lugha ni moja ya athari hizo.
    • Msamiati hukopwa ili kueleza .
    • lugha zote hukopa.
    • kiingereza kimekopa kutoka kilatini,kifaransa na kiswahili.
    • kiswahili nacho kimekopa kutoka kiingereza,kiarabu,kireno,kituruki na kijerumani
  2. Kwa mujibu wa taarifa hii,mtagusano wa lugha una athari gani?(maneno 30) (alama 7, 2 mtiririko)
    Nakala chafu
    • kuzuka kwa hali ya uwingi-lugha.
    • ukuaji wa lugha.
    • kuzuka kwa lugha mpya.
    • Kudunishwa kwa lugha.
    • Kufa kwa lugha

MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)

  1. Andika neno lenye muundo ufuatao wa sauti (alama 2)
    Kipua cha kaakaa lainiirabu ya kati tandazwa,kipasuo sighuna cha ufizi,irabu ya chini tandazwa.
  2. Taja aina mbili kuu za ala za sauti kisha utoe mfano mmoja mmoja (alama 2)
    • Ala tuli-meno,kaakaa gumu,ufizi,koromeo.
    • Ala sogezi-midomo,ulimi.
  3. Tumia kivumishi kionyeshi cha karibu pamoja na nomono katika ngeli ya I-ZI, Kisha utunge sentensi katika ukubwa –wingi. (alama 2)
    • madege hayo yalitua hapa jana.
  4. Yakinisha sentesi ifuatayo katika wakati ujao hali timilifu wingi. (alama 1)
    Msomi hakutuzwa siku hiyo
    Wasomi watakuwa wakituzwa siku hizo.
  5. Tumia mzizi –w- katika sentensi kama (alama 2)
    1. kitenzi kisaidizi- amekuwa akicheza mpira
    2. kitenzi kishirikishi-Janet amekuwa mwizi.
  6. Ainisha viambishi kwa kurejelea majukumu ya kisarufi katika neon hili (alama 3)
    Alijipelekea
    a-kiambishi cha nafsi
    li-kiambishi cha wakati
    ji-kiambishi cha mtendwa
    pelek-mzizi
    e-mnyambuliko/kauli
    a-kiisho
  7. Maneno yaliyopigiwa mstari yametumikaje? (alama 1)
    Pahali pema pako si pema pa mwenzako.
    • Pahali pema pako-kivumishi.
    • Si pema pa mwenzako-kiwakilishi.
  8. Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha matawi (alama3)
    Mlango umevunjwa na fundi aliyeujenga
    kiswa PP2 ansh LJM 2122
  9. Onyesha matumizi ya chagizo ya mfanano katika sentensi (alama 2)
    Mwanafunzi atunge sentensi akitumia vielezi vya namna mfanano kama:
    Alitembea kitausi kupokea zawadi.
  10. Andika katika usemi wa taarifa. ( alama 3)
    “hicho kijicho cha paka cheupe leo marufuku kwangu”alisema mzee Kambumbu.
    Mzee kambumbu alisema kuwa kile kijicho cha paka cheupe,siku hiyo kingekuwa marafuku kwake.
  11. Ainisha sentensi ifuatayo kwa kuangazia jukumu lake. (alama 2)
    Pika ugali kwa kuku kila Jumamosi ukitumia gesi.
    • ni sentensi agizi (ya masharti)
    • ni sentensi ya kuamuru (masharti)
  12. Panda ni kuatika mbegu ardhini au kuparaga mti. Andika maana nyingine mbili. (alama 2)
    • kugawika kwa njia.
    • ingia katika chombo cha kusafiria.
    • paji la uso.
    • pembe kubwa inayopigwa nchani.
    • manati /chombo cha kurushia mawe.
  13. Tunga sentensi moja ukitumia kihisishi cha bezo ( alama 1)
    Kihisishi cha bezo k.m. mm! Nyoo!, Po ! Mnh! Mawe! Ebo! Wapi! Zii! Aka!
    Mtahini atathmini sentensi ya mwanafunzi.
  14. Tunga sentensi na ubainishe kijalizo (alama1)
    Yeye ni mkurugenzi.
  15. Tunga sentensi yenye muundo wa: (alama 3)
    Kiima,kiarifa,yambwa tendwa,yambwa tendewa na yambwa ala.
    Mama alipika chakula cha mjomba kwa sufuria.
    Tanbihi:Mtahini atathmini sentensi ya mwanafunzi
  16. Eleza maana ya msemo ufuatayo (alama1)
    Piga unyende
    Lia kilio kinachoonyesha hofu.
  17. Eleza tofauti iliyopo kati ya jozi hii ya sentensi. ( alama 1)
    1. kerubo alinikimbilia.-kerubo alikimbia kuja upande nilipokuwa /upande wangu kunilaki/kwa niaba
    2. kerubo alinikimbia.-kerubo alinitoroka kwenda mbali nami.
  18. Weka nomino ifuatayo katika ngeli yake (alama 1)
    • (U-I)
  19. Tumia kiungo ‘na’ katika sentensi kuonyesha (alama1)
    1. ufupisho wa nafsi ya kwanza umoja Fulani -Nami
    2. kihusishi kuonyesha aliyetenda jambo fulani.-Alipigiwa na mama yake.
  20. Andika sentensi ifuatayo upya ukizingatia kinyume cha maneno yaliyopigiwa mstari: (alama2)
    Ubora wa kazi zao ulifichika baada ya kuanzishwa kwa mradi ule.
    Ubovu wa kazi zao ulifichuka kabla ya kumalizwa kwa mradi ule.
  21. Tunga sentensi yenye muundo ufuatao.(alama 2)
    KN(N) + KT (T+E) + U+KN(N)+KT(T+E)
    Metobo huandika vyema lakini Kerubo huandika vibaya.
  22. Eleza matumizi ya kiambishi ‘ki’katika sentensi hii. (alama2)
    Njia hii haipitiki
    • kutowezekana kwa kitu fulani.
      Kiambishi –U hutambulisha majina yote ya ngeli ya U. (umoja)
    • Hata hivyo baadhi ya majina haya huchukua viambishi tofauti tofauti katika wingi

ISIMUJAMII(ALAMA 10)

(George anakutana na Wanjiru nje ya kanisa baada ya ibada)
George:Hujambo dada Wanjiru?Mungu asifiwe!
Wanjiru:(akimsogelea kwa bashasha)Amen!Asifiwe sana.
George:Ni siku nyangi sijakuona.umekuwa wapi?
Wanjiru:Ndugu,Yesu anaendelea kujionyesha maishani mwangu.kwa majuma matatu sasa tulikuwa na crusade huko malishoni.Tulihubiri na wengi kumgeukia Mola.
George:Amen!mlienda na kina nani?
Wanjiru:Tuliandamana na mhubiri Petero na Kiongozi wa vijana .Zaidi ya watu 100 walihutubu na kumrudia BWANA.
George:Halleluya!
Wanjiru:wetu ni Mungu wa miujuza .nilipoulizwa kwandamana na wengine,niliitikia wito kama anavyoahidi Bwana ,tulibisha na akatushishia Baraka.Neno sasa limeeneahuko Lolo Kusini…
George:Ni Mungu mpaji ,hamsahau mja yeyote!
Wanjiru:Amen
George :Hata name nimeona akimmininia Baraka za ajabu.Nilikubwa na matatizo mengi lakini dada tukiomba tutapewa.Lazima tuwe kama Ruth,Naomi na Esher hata tunapomngojea Yesu kuja kutuchukua.
Wanjiru:(akimkatiza)kama ambavyo mhubiri ameseema leo,hizi ndizo siku za mwisho.Ndugu lazima tuombe tukikesha bila kumpa shetani nafasi yoyote.
George:Ashindwe!...

  1. Taja sifa tano za sajili ya mazungumzo haya.(alama 5)
    • …sajili ya kidini inatumia msamiati unaohusishwa na kuabadu na dini.kama vile kuitana dada,ndugu ,amen.
    • Kando na lughainayotyumika,msamiati wa shughuli za kuabudu,pia huwa ni nyepesi na inayoweza kueleweka kwa urahisi na jumuiya ya wanaoabudu.
    • Kwa kawaida,huwa kuna urejeleaji wa maandishi matakatifu yanayohusiana ama vifungu fulani k.m kulingana na maandiko ama kitabu cha Matayo ama Kurani.
    • Lugha na msamiati wenye kuonyesha upole.Haleluya,Mungu wangu,Alhamdullahi
    • Lugha inayoonyesha unyonge alionao binadamu mbele za nguvu nyingine.k.m.ashindwe shetani,Mungu ni mkuu
  2. Dondoa msamiati unaotambulisha sajili hii.(alama 5).
    • Dada
    • Asifiwe
    • Yesu anaendelea kujiionyesha maishani
    • Amen
    • Shetani
    • Baraka
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Lanjet Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest