Mofimu - Sarufi na Matumizi ya Lugha Kiswahili Notes

Share via Whatsapp


Utangulizi

 • Mofimu ni sehemu ndogo zaidi ya neno inayowakilisha maana ya neno hilo. Mofimu inaweza kuwa silabi moja au zaidi.


Aina za Mofimu

Kuna aina mbili za mofimu:

 • Mofimu huru
 • Mofimu Tegemezi

Mofimu Huru

 • Mofimu huru ni silabi moja au zaidi yenye maana kamili ya neno na inaweza kujisimamia yenyewe bila msaada wa viambishi au silabi nyingine. Aghalabu mofimu huru huwa nomino, vivumishi au vielezivisivyochukua viambishi vya ngeli. Kwa mfano:daktari, ndoa, nyumba, Miranda

Mofimu Tegemezi

 • Mofimu tegemezi ni mofimu ambazo huhitaji viambishi au mofimu nyingine tegemezi ili kuleta maana iliyokusudiwa. Mofimu hizi hujumuisha hasa mzizi wa neno (au shina la kitenzi), vivumishi, nomino au vielezi ambavyo vinahitaji viambishi viwakilishi vya ngeli ili kutoa maana iliyokusudiwa.
 • Shina la kitenzi au mzizi wa neno au kiini cha kitendo ni sehemu ndogo zaidi inayosimamia kitenzi chenyewe bila mnyambuliko, nyakati au viambishi vinginevyo. Viambishi ni mofimu tegemezi ya silabi moja inayowakilisha dhana fulani kama vile hali, ngeli, nafsi, wakati na kadhalika.
  k.m:
  1. mtangazaji => m-tangaz-a-ji
   m => mofimu ya ngeli ya M-WA kwa umoja
   tangaz => mzizi wa neno, kiini cha kitendo cha kutangaza
   a => kiishio cha kitenzi
   ji => inaonyesha kazi au mazoea
  2. wametusumbua => wa-me-tu-sumbu-a
   wa => kiambishi kiwakilishi cha nafsi ya tatu wingi
   me => kiambishi cha wakati timilifu
   tu => kiambishi kiwakilishi cha nafsi ya kwanza wingi - kitendewa/mtendwa
   sumbu => shina la kitendo cha kusumbua
   a => kiishio
  3. wakulima => wa-ku-lim-a
   wa => kiambishi kiwakilishi cha ngeli ya A-WA wingi
   ku => kiambishi cha KU ya kitenzi jina
   lim => mzizi wa kitendo cha kulima
   a => kiishio
Join our whatsapp group for latest updates

Download Mofimu - Sarufi na Matumizi ya Lugha Kiswahili Notes.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest