Utangulizi
- Shada(Shadda) na Kiimbo ni namna ya kutamka neno au fungu la maneno kwa namna tofauti kuleta maana mbalimbali
Shadda/Shada
- Mkazo unaowekwa kwenye silabi fulani ya neno ikiwa imetamkwa kwa msisitizo.
- Silabi ni tamko moja katika neno/herufi moja au zaidi ambazo hutamkwa pamoja
- Alama ya ritifaa hutumiwa kutambulisha shadda
- Huwekwa kwenye silabi ya pili kutoka ya mwisho, kwenye vitenzi vishirikishi vya silabi moja au kubadilisha maana ya neno
k.m.
- ka'lamu, i'mba, thu,mni, 'leta n.k.
- Kitabu 'ki mezani
- Bara' bara (njia), ba'rabara (sawa sawa), wala'kini (lakini), wa'lakini (kasoro/dosari/ila)
Kiimbo
- Jinsi sauti inavyopanda na kushuka mtu anapoongea.
- Huibua maana halisi ya maneno yanayosemwa kama ifuatavyo:
Sentensi za taarifa
- Mtoto anaandika barua.
Sentensi za maswali
- Mtoto anaandika barua?
Sentensi za mshangao
- Mtoto anaandika barua!
Sentensi za amri
- Kachezeeni nje!
Sentensi za rai/ombi
- Nisaidie/eni.
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download Shadda na Kiimbo - Sarufi na Matumizi ya Lugha Kiswahili Notes.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students