Nyakati za Kiswahili - Sarufi na Matumizi ya Lugha Kiswahili Notes

Share via Whatsapp


Wakati Uliopita - LI

 • Hutumia kiambishi 'LI' na hurejelea kitendo kilichokamilika muda mrefu uliopita.
 • Ifuatayo ni mifano katika sentensi.
  k.m: nilienda, tulilima, walikufukuza
  - mama alienda sokoni
  - Ndoto hio ilinisumbua usiku kucha


Wakati Timilifu (Uliopita Muda Mfupi) - ME

 • Hutumia kiambishi 'ME' na hurejelea kitendo ambacho kimekamilika muda usio mrefu.
  k.m: amepona, nimewachagua, zimechanganyika
  - Tumeuona wema wake Bwana
  - Dada yake amepagawa


Wakati Uliopo - NA

 • Hutumia kiambishi 'NA' kurejelea jambo linalotendeka sasa hivi.
  k.m: 
  anaugua, yanametameta, unatisha
  - Ninakupenda kwa yale unayonitendea
  - Nyumba zote zinabomolewa mwaka huu


Wakati Ujao - TA

 • Huchukua kiambishi 'TA' na hurejelea kitendo ambacho bado hakijafanyika lakini kinatarajiwa kufanyika..
  k.m: 
  atakupa, kitajulikana, utapokelewa
  - Mtoto atalifunga dirisha litakalokuwa likiingiza hewa
  - Je, utaenda sokoni kesho kutwa?


Wakati wa Mazoea - HU

 • Hutumia kiambishi 'HU' na hurejelea kitendo ambacho hufanyika mara kwa mara au kila siku n.k.
  k.m: 
  hutembea, husoma, huzilinda
  - Dkt. Matumbo hutibu wagonjwa
  - mchungwa ule huzaa machungwa matamu


Wakati Usiodhihirika - A

 • Hutumia kiambishi cha ngeli au nafsi pamoja na kiungo 'A' kurejelea kitendo kinachoendelea kutendeka katika wakati usiodhihirika.
  k.m: 
  achukua, zapepea, twaangamia
  - Baba atusubiri nyumbani
  - Vitabi vyako vyote vyachomeka


Wakati Timilifu Usiodhihirika - KA

 • Hutumia kiungo 'KA' kurejelea kitendo ambacho kinakamilika katika wakati usiojulika. Pia hutumika kurejelea kitendo kifanyika baada ya kingine.
 • Hutumiwa katika masimulizi.
  k.m: ikawalemea, tukazichukua, likampendeza
  - Latifa akaangalia juu akamwona nyoka
  - Akawanyeshea mana wakiwa jangwani
Join our whatsapp group for latest updates

Download Nyakati za Kiswahili - Sarufi na Matumizi ya Lugha Kiswahili Notes.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest