MASHARTI YA KISASA - Alifa Chokocho - Mwongozo wa TUMBO LISILOSHIBA

Share via Whatsapp


Muhtasari

Kisa hiki kinahusu Kidawa mwanamke mrembo ambaye alipendwa na mvuvi na muuza samaki aitwaye Dadi. Dadi alimpenda sana

Kidawa na akataka amchumbie awe mkewe. Kidawa alimkataa

Dadi na kumkwepa kabisa. Hata hivyo mambo yalibadilika ambayo yalimshangaza sana Dadi. Kidawa alimwambia kwamba yu radhi kuolewa na Dadi kwa masharti ya ndoa ya kisasa. Dadi kwa shangwe alizonazo hakuzingatia undani wa Kidawa " Ujue kwamba mimi ni mwanamke wa kisasa, na mwanamke wa kisasa hutafuta mwanamume wa kisasa mwenye mapenzi ya kisasa (Uk 58)

Dadi akamwoa Kidawa mwanamke wa kisasa. Baadhi ya mambo aliyotakiwa kuyatekeleza ni kusaidia kazi za nyumbani, kukuna nazi, kuosha vyombo, kufua na kupiga pasi. Pia amruhusu Kidawa afanye kazi ya umetroni kwa Shule ya wasichana usiku. Kidawa alifanya kazi hio kwa zamu. Aidha kidawa akawa na biashara ya kutembeza bidhaa za Uarabuni mitaani. Kidawa aliyafanya haya ili

"Kuunganisha ncha nyingi za mahltaji ya maisha " (Uk 61) Baada ya miaka tisa ya ndoa, Dadi alianza kuingiwa na shaka. Akamshuku

Kidawa, akachukia kujipamba kwake, akachukia kwenda kufanya kazi usiku, akachukia alivyosimama na kuongea na wanaume wengine na vile vile akachukia uchuuzi wa bidhaa alizofanya.

Furaha ile ya kumwoa Kidawa hadi akaitwa Dadi kichekacheka kwa kumpata mke wa kisasa Kidawa ikamtoka. Chakula kikamshinda jioni moja. Masharti ya kuosha vyombo kwa zamu pia yakamshinda.

Dadi alimfuata Kidawa kazini ili kumfumania na mwalimu mkuu kama alivyoshuku. Dadi akaenda nyumbani kwa mwalimu mkuu akaelezwa hakuweko. Ana kazi zilizomzidi shuleni. Dadi akawa na hakika ya kuwa mtego wake ungenasa. Mpango wake wa awali alivyopanga — akapanda paipu inayoelekea gorofani ili amwone mwalimu mkuu na Kidawa wake. Dadi alikosea mwalimu alikuWa peke yake na rundo Ia karatasi akisahihisha. Kidawa alipojitoma ndani alitaka kujiuzulu kazi kwa kuwa mumewe anamshuku.

Dadi alionekana juu ya paipu "Wewe nani? Unachungulia nini hapo juu? Wewe mwizi, nini? Au mpiga bodi... Nyinyi walinzi bwenini kuna mtu amepanda juu ya paipai anachungulia ndani, " (Uk- 68).

Sauti iliwavutia Kidawa na mwalimu mkuu. Kidawa akakuta ni mumewe. Dadi aliangukia kokoto na damu ikamtoka kichwani.

Mwalimu mkuu akapiga simu kuita ambulensi.



Anwani

Anwani ya hadithi hii ni "Masharti ya Kisasa". Anwani hii inasawiri maudhui yaliyomo ndani yake. Mambo yote yanayomkuta Dadi yanatokana na yeye kutoelewa ni nini mke wake anachomaanisha anaposema "masharti ya kisasa". Hatimaye anajaa wivu, wivu unaopelekea tatizo ambalo yumkini lingeweza kutwaa maisha yake.



Dhamira

Mwandishi amedhamiria kuonesha jamii kuwa wivu wa kupindukia ni hatari sana.



Maudhui

Migogoro ya wanandoa

  • Kidawa alijua mabadiliko yaliyomo maishani. Ingawa wanaume wengi walimtaka yeye aliahiri yule atakayefuata masharti yake. Alimtaka Dadi atoe uamuzi. Dadi alitoa uamuzi bila kuelewa kwa undani. Kutokana na hayo kukaingia kutoaminiana. Ukale aliokuwa nao Dadi, na desturi za kitamaduni zikaleta mgongano. Laiti angalijua
  • Kidawa alikuwa mwaminifu na kwake angetulia. Masharti ya kisasa aliyotoa Kidawa yalikuwa pia mageni kwa jamii. Dadi alihisi dunia inamchekelea. Yote haya ndiyo yaliyoleta
  • Sio vyema Kudhamana Jambo hata hivyo, mtu anaposhuku kitu, ni vyema kutafuta njia nzuri na salama ya upelelezi. Njia aliyotumia Dadi ya kupanda paipu ilikuwa ya kubahatisha na kudhani kuwa hangeonekana. Kwa sadfa alionekanm

Ahadi maishani

  • Kidawa alijua anataka maisha ya aina gani na akafanya uamuzi wake. Aliamua kuwa mume atakayemuoa afuate masharti ya kisasa. Dadi anapewa masharti na ayakubali. Alijitahidi sana kuyashikilia kwa miaka tisa. Hata akakubali kwamba wapate mtoto mmoja kufuatilia usasa. Kwa Dadi hakuyaelewa yale masharti vyema baadae yanamletea karaha na maisha yake yakavia. Ni vyema kuchunguzajambo lolote vyema kabla ya kukubali masharti.

Elimu

  • Elimu ni muhimu maishani. Kutokana na mwanga wa elimu mtu husika anapata maarifa na ujuzi wa kupanga maisha yake. Kidawa alimaliza kidato cha nne na akatumia ujuzi wake kuandaa maisha. Kuna wanaume wengi waliomtaka, akawakataa na kumfuata Dadi ambaye alimkubali "Wewe nimekupa mitihani mingi, na naona umefaulu " (Uk 58)
  • Kutokana na elimu duni ya Dadi, anaingiwa na shaka na kumshuku mkewe. Akaona kwamba japo hajasoma, amebaini kuwa Kidawa anamwendea kinyume. Ukweli kwamba Kidawa ni metroni na anaenda kazini usiku, na usiku, kukamzidishia Dadi fikra zake hizo Mume wake anafanya kazi ya kuuza samaki. Mja apatapo fursa ya kazi ni bora aifanye " Kuunganisha ncha nyingi za mahitaji " Msimamo wa Dadi kuhusu shughuli za Kidawa ni finyu na umepitwa na wakati. Kutokana na mapato ya kazi za Kidawa, anavaa vizuri na kujipamba atakavyo.

Urembo

  • Mwanamke akivaa vizuri asichukuliwe kwamba ana macho ya nje. Kidawa alipenda kudumisha urembo wake. Dadi akamdhania anamvalia mwalimu mkuu. Kidawa alijimudu kwa ajili ya biashara ya uchuuzi — alitembeza bidhaa zake. Hayo yote Dadi aliyaelewa vibaya na vikamzidishia hofu isiyokuwa ya msingi.

Umbea na masengenyo

  • Dadi alihofia minong'ono ya watu ambao walikuwa wanamsema kwa vile alisaidiana na mkewe. Jambo hilo likamnyima raha. Wanawake na wanaume walimsema kuwa alidhibitiwa na Kidawa. Jambo hilo linamwumiza mno. Walidai sio mwanamume tosha. Dadi anapozungumza na Zuhura anajishikilia ili asimpashe maneno makali akijua kuwa bibi huyo ni mmbea.

Itikadi na Utamaduni

kukuna nazi? Dadi anachukulia kuwa mwacha mila mtumwa, akasahau pia kuwa mwacha mila ni jasiri. Dadi hakuwa na huo ujasiri kutokana na msimamo wa jamii yake

Mapenzi ya dhati

  • Dadi alimpenda mno Kidawa, hata alipopewa masharti ya kisasa Pindi wakioana aliyakubali bila kufikiria kwa makini maneno hayo baada ya miaka tisa anashindwa kushikilia masharti, akajjiumiza bure bilashi akitafuta ithibati.
  • Kwa upande wa Kidawa naye alikuwa na mapenzi ya dhati. Wanapotembea njiani alimkemea Dadi — hakutaka aangalia wanawake wengine. Anapojipamba vyema alimwuliza mumewe ikiwa amependeza. Dadi alichukulia vibaya swali


Wahusika

Dadi

  • Huyu ni mchuuza samaki. Alimpenda mwanamke mmojaKidawa kupita kiasi. Dadi alijaribu kumpata Kidawa kwa kila njia lakini hakuweza. Alikata tamaa kabisa. Kidawa alibadilisha mtazamo wake. Dadi akapewa masharti ya kisasa katika ndoa yao. Hayo masharti yanamuumiza rohoni na kumsononesha.
  • Hajiamini: kutojiamini kwake kunatokana na elimu duni aliyokuwa nayo.
  • Ana bidii maishani: anachuuza samaki kwa bidii hadi wamalizike.
  • Hana msimamo: anayumbishwa na maneno ya watu hadi akakosa raba kabisa.
    mwalimu mkuu na kupanda paipu ili kuhakikisha alilipanga kwa siku nyingi.

Umuhimu

Si vizuri kuzingatia tuhuma kabla ya kuhakikisha. Sio rahisi kuleta mabadiliko katika jamii.

Kidawa

Mwanamke mrembo ambaye alitaka kuolewa na wanaume wengi. Aliwakataa na kuwachuja hadi akamchagua Dadi.

Yeye alisoma hadi kidato cha nne. Alitaka mwanandoa ambaye angezingatia masharti ya kisasa ya ndoa.

Ni mzingatifu: anajua alitaka nini maishani na akazingatia matakwa yake — ya ndoa ya kisasa.

Alithamini ndoa yake: ili kuiauni ndoa yake anaamua kwenda kujiuzulu.

Ni jasiri: mwacha mila ni jasiri. Hakuyumbishwa na umbeya wanajamii kama Dadi.

Umuhimu

Kidawani kielelezo cha mwanamkewakisasa ambayehatakl kushikilia mila za kizamani. Ni vyema mtu atoe msimamo wake maishani ili ujulikane bayana.

Mnunuziwa samaki. Mwenye manenoya karaha. Anakashifu samaki wa Dadi na kudhani kuwa wameoza.

Ni mmbeya: anampiga Dadi vijembe kuhusu anavyoindesha ndoa yake.

Mwalimu Mkuu

Mwenye utu: anapiga simu mara moja kuita ambulensi baada Dadi kuanguka na kuumia kichwani.



Mbinu za Lugha

Taharuki

Baada ya kupelekwa hospitali, Je alipona au aliaga dunia, ukizingatia kuwa aliumia vibaya kichwani. Je, Kidawa alikichukuliaje kitendo hicho cha mumewe kupanda juu ya paipu na kuchungulia ndani?.

Taswira oni

Wakati Dadi yuko juu ya baiskeli yake akiita wanunuzi.

Kuna taswira ya Kidawa akiwa amevalia viatu vipya na kanzu tayari kwenda kazini usiku. Zipo taswira nyingine nyingi.

Aidha kuna taswira ya kile chakula cha jioni cha ndizi na samaki ambacho Dadi hakukigusa kwa wivu.

Sadfa

  • Dadi alienda kuona iwapo mwalimu alikuwa kwake jioni.Alipomkosa akajihakikishia kwamba alienda kukutana naKidawa.
  • Aidha ilikuwa sadfa kuwa taa ya nje ilikuwa haiwaki naDadi akapata mandhari mazuri ya kujificha akipanda ile paipu.

Kuchanganya ndimi

Kuna maneno ya Kiingereza yaliyotumika kama "Stop your gaze!" my dress my choice celeb, socialite n k.

Mdokezo

  • Kidawa alijaribu kumhakikishia mumewe uaminifu wake na kumkumbusha ahadi zao, alipogeuka na kuona chakula hakikuguswa alikatisha usemi wake (Uk 66)
  • Dadi alipokuwa akienda shuleni kumwangalia mwalimu mkuu, alijiapiza kuwa leo ni leo na hakumaliza msemo huo.
  • Wakati mwalimu mkuu alipokuwa akimwasa Kidawa kuhusu kuacha kazi, mdokezo umetumika "Mtu ana kazi nanga zinapaa, sikwambii "(Uk 68)

Takriri

Neno kisasa limerudiwarudiwa kusisitiza kiini cha hadithii hii "Mwanamke wa kisasa hutafuta mwanaume wa kisasa, mwenye mapenzi ya kisasa (Uk 58)

Misemo

  • Nyota ya jaha (Uk 57)
  • Pweleo la tamasha (Uk 56)
  • Kugeuka maji kuzima moto (Uk 57)

Koja

Mapenzi ni mateso, ni utumwa ni ukandamizaji, ni udunishaji, ni ushabiki ni ugonjwa usio dawa (Uk 56)

Tashbihi

…kama anga lolote Ia dunia (Uk 57)

Tanakuzi

Matumiziyamaneno yanayopingana. Waliosoma wasiosoma wenye uwezo na wasio nao (Uk 57)

Join our whatsapp group for latest updates

Download MASHARTI YA KISASA - Alifa Chokocho - Mwongozo wa TUMBO LISILOSHIBA.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest