MASWALI
Zoezi la 1: Kusikiliza na Kuzgumza
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5.
Mhazili: Halo, asante sana kwa kutupigia simu. Mimi ni Bi Nandi, hazili wa shule ya Maarifa. Naweza kukusaidia vipi mwenzangu?
Bwana Tindo: Halo, mimi ni Bwana Tindo, mzazi wa Tamikha Tindo. Tamikha ni mwanafunzi wa Gredi ya saba Mashariki. Tafadhali naomba kuzungumza na awalimu wake wa darasa.
Mhazili: Sawa Bwana Tindo. Naomba unipe muda nifike majilisini kuangalia kama yupo au la. Tafadhali usikate simu.
Bwana Tindo: Haya, sawa. (muda unapita)
Mhazili: Halo, asante sana kwa subira yako. Huyu hapa mwalimu. (anampokeza mawasiliano)
Bwana Tembo: Halo, mimi ni Bwana Tembo, mwalimu wa darasa wa Tamikha. Nikusaidiaje?
Bwana Tindo: Naomba kukuarifu kuwa tuna safari ya ghafla, hivyo, Tamikha hataweza kuhudhuria mafunzo ya leo.
Bwana Tembo: Pole sana kwa hilo. Natumai kwema.
Bwana Tindo: Kwema mwalimu. Ni vile tu Tamikha ana miadi na daktari. Samahani mwalimu, sikuweza kukupa taarifa hii mapema.
Bwana Tembo: Hapajaharibika jambo lolote maana tayari ujumbe umefika.
Bwana Tindo: Nashukuru sana kwa kunielewa.
Bwana Tembo: Hewala bwamkubwa. Jambo jingine labda?
Bwana Tindo: Kwa sasa hapana.
Bwana Tembo: Asante kwa kutupigia simu. Uwe na siku njema.
Bwana Tindo: Hewala Bwana Tembo. Shukrani kwa huduma njema. Uwe na siku njema pia.
- Baba wa Tamikha alipopiga simu shuleni, alizungumza na nani kwanza?
- Mwalimu mkuu
- Sekretari
- Bintiye
- Bwana Tembo
- Sababu basa ya Bwana Tindo kupiga simu shuleni Maarifa ilikuwa gani?
- Kumjulisha mwalimu wa darasa wa Tamikha kuhusu hali yake ya afya.
- Kumweleza mwalimu wa darasa wa Tamikha kuhusu safari ya ghafla.
- Kueleza sababu ya Tamikha kutohudhuria masomo siku hiyo.
- Kuzungumza na Bwana Tembo
- Bwana Tindo alifuata utaratibu mwafaka pale ambapo
- alimpigia simu mhazili kwanza.
- alienda shuleni yeye mwenyewe.
- alimpigia simu mwalimu kwanza.
- aliwasiliana na mwalimu mkuu.
- Tamikha alitarajiwa kusafiri ili kuenda kumwona
- mhazigi.
- mwalimu.
- mzazi.
- mganga.
- Mazungumzo haya yanadhihirisha utele wa
- majigambo.
- ruhusa.
- maadili.
- ujeuri.
Zoezi la 2: Kusoma kwa ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 10.
Wanafunzi wa Gredi ya saba walikusudiwa kufunga safari ya kuelekea katika ziara katika mbuga ya wanyama ya Hola. Waliwasili shuleni mapema. Bwana Rungu, mwalimu wa darasa, aliwaambia, "Ingieni basini haraka. Hatuna muda wa kupoteza". Waliyafuata maagizo hayo naye dereva akalitia gari ufunguo. Hakuna aliyegundua kuwa Bwana Rungu alikuwa amerudi ofisini
mwake.
Wanafunzi waliimba kwa furaha huku basi likisafiri kwa kasi katika barabara iliyolemewa na vumbi. Walipofika langoni pa mbuga ya wanyama ya Hola, walipokelewa na mlinzi. "Karibuni sana. Hii ni mbuga ya wanyama ya Hola. Je, mwalimu wenu yu wapi?" Hapo ndipo walipogundua kuwa Bwana Rungu alikuwa amebaki shuleni.
"Ala! Muda wote huo, pilidhani mwalimu alikuwamo humu basini." dereva akamaka. "Nasikitika, wanafunzi hawaruhusiwi kuingia mbugani pasipo mwalimu," mlinzi kaeleza. Wanafunzi wote walivunjika moyo. Dereva akawasha basi tayari kuwarudisha wanafunzi shuleni. Hapo ndipo walipoona bodaboda kwa mbali. Ilipofika pale, kumbe ni Bwana Rungu alikuwa ameletwa. "Mwalimu!" Wote walimwita kwa sauti. Bwana Rungu alizungumza na mlinzi kisha wakaruhusiwa kuingia mbugani.
- Yawezekana kuwa wanafunzi walifika shuleni mapema kwa kuwa
- walitaka kuabiri basi kwa wakati.
- walitaka wapate nafasi zenye starehe humo basini.
- walikuwa na hamu ya kuizuru mbuga.
- Bwana Rungu aliwaagiza kufanya hivi.
- Kabla ya dereva kulitia basi ufunguo,
- wanafunzi waliingia basini haraka.
- Bwana Rungu alirudi afisini mwake.
- wanafunzi waliimba kwa furaha.
- basi lilisafiri kwenye barabara yenye vumbi.
- Ni kweli kuwa
- wanafunzi walisafiri pamoja na Bwana Rungu.
- barabara kuelekea Hola ilikuwa imesakifiwa vilivyo.
- wanafunzi walitekwa bakunja na safari hiyo.
- baadhi ya wanafunzi hawakufurahia ziara hii.
- Sehemu iliyopigiwa mstari inatoa wazo gani?
- Dereva hakujua idadi ya abiria wake.
- Dereva alimakinika zaidi katika uendeshaji.
- Mwalimu hakukaa sehemu iliyokuwa wazi.
- Humo basini mlikuwa na giza totoro.
- Hatimaye mwalimu alipokuja, wanafunzi
- walihuzunuka.
- walikasirika
- walisinyika.
- walifurahi.
Zoezi la 3: Sarufi.
Tumia maneno uliyopewa kujazia vihasho 11 hadi 15.
- jenereta
- masurupwenye
- viwanda
- vyerehani
- kawi
Taifa letu lina......................11..................tofauti tofauti. Hapa, mafundi wenye ujuzi uliokomaa huonyesha weledi wao wa kuzalisha mali. Bidhaa kutoka humo huuzwa humu nchini na za ziada kuuzwa katika nchi za nje. Vya kushonea nguo hutumia ......................12..................kushonea nguo kama vile . Mara nyingi, suti, makabuti na ......................13.................. Mara Nyingi, nguvu za umeme hutumika. Wasio na umeme hutumia ......................14..................ambayo huzalisha......................15..................ya umeme.
Kutoka swali la 16-30, jibu maswali kulingana na maagizo
Pigia mistari nomino za kawaida katika sentensi hizi.
- Mwanaidi alinunua saa ghali kutoka ughaibuni.
- Chungu kilichofinyangwa Alhamisi iliyopita kimevunjika.
- Dawati langu lilikuwa likiundwa jana asubuhi.
Tunga sentensi sahihi ukitumia maneno yafuatayo.
- Umati
- Mlolongo
- Shungi
Viringa vitenzi visaidizi katika sentensi hizi.
- Mtoto huyu huwa anajali usalama wake.
- Walikuwa wakiimba mvua ilipopusa.
- Mwalimu wetu huwa anaandika kwa mkono wa kushoto.
Jaza viambishingeli vinavyokosekana
- Mikono yao .............................. ilikuwa na vumbi.
- Mijusi ................................. medonolewa na kuku.
- Mwamba .............................. mevunjika vigaevigac.
Andika ngeli va nomino hizi
- Chama
- Kimbilio
- Chudere
Zoezi la 4: Kusoma kwa ufasaha.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31-35.
Jana nilipomaliza kula kilalio, nilienda kulala na kujifunika gubigubi kwa blanketi. Hivyo ndivyo nilivyosafiri katika dunia nyingine. Nilianza kutembea hapa na pale. Nilikutana na joka kubwa jeusi. Joka hilo lilikuwa likitokwa na jasho. Ulimi wake ulijianika nje. Niliogopa sana. Joka hilo lilianza kunikaribia polepole. Mimi huyo! Nikatimua mbio kama duma huku joka hilo likinifuata kwa tamaa ya kunikamata na kunila. Mara lo! Huko nilikokuwa nikielekea, nilimwona simba mkubwa. Simba huyo aliponiona, naye akamshukuru Mungu kwa kumletea chakula kwa urahisi.
Nilishindwe cha kufanya. Mbele, simba nyuma joka. Sikuzubaa. Nilifanya akili haraka. Niliupanda mti uliokuwa karibu. Joka hilo lilinifuata hadi kwenye mti huo. Ilinibidi kufanya maombi yangu ya mwisho. Simba naye alikuwa pale chini akiniangalia kwa tamaa.
Maskini mimi! Joka lile lilipokuwa lanifikia, tawi nililokuwa nimekalia lilikatika. Mimi huyo! Nilibwagika chini pu! Ghafla nikatundika miguu mbegani. Punde simba alinifuata nyuma kwa kasi. Aliponikaribia na kulifumbua domo lake kubwa kunimeza mzima mzima, niliamka usingizini na kujipata nikimiminikwa na jasho bwaibwai. Alhamdulillahi! Nilifurahi sana kwamba ilikuwa ndoto tu.
- Mwandishi ana maana gani anapo ema alisafiri katika dunia nyingine?
- Ni gani hasa lililokuwa lengo la joka lile?
- Ni wakati gani ndotoni ambapo msimulizi alionekana kuchanganyikiwa zaidi?
- Hatimaye, ni mnyama yupi aliyemla msimulizi?
- Eleza hisia za mwandishi alipoamka.
MWONGOZO
- B
- C
- A
- D
- C
- C
- A
- C
- B
- D
- viwanda
- vyerehani
- masurupwenye
- jenereta
- kawi
- saa
- Chungu
- Dawati
- Umati wa watu ulihudhuria sherehe.
- Mlolongo wa magari umeelekea katika mahafali.
- Msichana yule ana shungi la nywele kichwani
- huwa
- walikuwa
- huwa
- i
- wa
- u
- KI-VI
- LI-YA
- A-WA
- Alianza kuota
- Kumla msemaji
- Alipokumbana na simba.
- Hakuna
- Furaha
Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 7 Mid Term 2 Exams 2023 Set 1.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students