Thursday, 16 March 2023 13:52

Kiswahili Questions and Answers - Grade 7 Mid Term 1 Exams 2023 Set 1

Share via Whatsapp

Swali 1 hadi 5

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali:

(Mama Taabu ameketi sebuleni akitazama runinga. Taabu anabisha mlango na kuingia)

G7T1S1002swap1

Taabu:             (Akirusha mkoba wa vitabu sakafuni) shikamoo mama?
Mama Taabu :(Kwa mshangao) Marahaba mwanangu. Umeshindaje?
Taabu:             Vyema mama.
Mama Taabu :(Akisimama na kushika kiuno) Mwanangu, mbona huthamini usafi. Tazama mkoba wako. Mchafu kama fuko.
Taabu:            Nilianguka chini mama, hata mavazi yangu yakachafuka.
Mama Taabu :(Kwa upole) Epukana na michezo inayochafua mavazi yako. Nywele zako ni kama zile ambazo hazijawahi kuchanwa.                            Ni kana kwamba hata meno yako huyapigi mswaki. Zingatia usafi wa kibinafsi.
Taabu:            Nakusihi mama unisamehe. Nitaanza kukata kucha zangu na kuvipiga rangi viatu vyangu mimi mwenyewe.
Mama Taabu :Sharti uoge kila siku na kuvaa nguo ambazo zimepigwa pasi. Ukiwa msafi hautawaudhi wanafunzi wenzako unaoishi                              nao.
Taabu:            (Kwa heshima) Asante mama kwa ushauri wako. Naamini pia usafi utanikinga dhidi ya maradhi yanayosababishwa na                            uchafu.
Mama Taabu :Hongera kwa wazo hilo, maradhi ni hatari.
Taabu:             Asante mama. Kwa kweli nimejua mengi.

  1. Kitendo cha Taabu kurusha mkoba sakafuni kinaashiria nini kuhusu tabia yake?
  2. Unafikiri Taabu atafanya nini mara tu baada ya mazungumzo yake?
  3. Kwa jumla mazungumzo haya yanahusu jambo gani?
  4. Neno lingine ambalo lina maana sawa na 'nakusihi' ni
  5. Kwa nini ni muhimu mtu aoge kila siku na kuvaa nguo zilizopigwa pasi hasa anapokuwa na wenzake?

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 6 hadi 10

G7T1S1002swap2

Kutokana na ukame uliokuwa umekithiri, mfalme Simba aliwaita wanyama wote kwenye mkutano. Kwa kuwa wanyama walimheshimu mfalme wao walijua lazima pana jambo. Mbiu ya mgambo ikilia kuna jambo.

"Ndugu zangu, ukame umeongezeka. Tusipochukua tahadhari sote tutaangamia. Inatupasa tutumie nishati ya jua kutoa maji kisimani na kupanda mimea kisha kuinyunyizia mimea yetu.Kwa kuwa wanyama walikuwa wameikumbatia teknolojia ya kisasa, walikubaliana na uamuzi wa mfalme wao.

Wanyama walilima shamba na kulitayarisha kwa ajili ya upanzi. Sungura hakuonekana shambani. Siku hizo zote licha ya kupelekewa ujumbe ajumuike na wenzake. "Ninaumwa ninapoinama kulima," hilo ndilo lililokuwa jibu lake.

Maboga na mihogo ilinawiri sana shambani lakini ajabu ni kuwa maboga yalianza kutoweka shambani wanyama wasijue aliyekuwa akiyavuna. Wanyama wakaafikiana kulinda shamba lao kwa zamu. Hatua hiyo haikuzaa matunda. Mambo yalipozidi, mfalme simba aliweka kamera za siri shambani. Baada ya siku mbili, wanyama waliitwa kwenye mkutano. Safari hii sungura alikuwa miongoni mwa wanyama waliofika mkutanoni. Alionekana mwenye furaha na kudai kuwa wanyama waliteseka shambani hivyo wana haki kujua ni nani aliyekuwa akiwadhulumu.

Runinga kubwa ilianguka kwenye miti miwili na twiga wawili kuishikilia. "Masalkheri ndugu zangu?" Simba aliwaamkua wanyama. "Ningependa mtazame runinga hii kwa makini.

Amini usiamini, kamera zilizounganishwa kwenye runinga zilionyesha namna sungura alivyokuwa akiiba mazao shambani. Wanyama walishikwa na hasira wakayavuta masikio yake na kumpeleka mbele ya hakimu. Sungura akakosa pa kuweka uso wake.

  1. Kwa nini mfalme simba aliita wanyama mkutanoni?
  2. Wanyama walikubaliana na wazo la mfalme kwa kuwa
  3. Sungura alikataa kushirikiana na wanyama wengine kulima shamba na kupanda mimea. Je, angeweza kuambiwa methali gani kumsisitizia umuhimu wa ushirikiano?
  4. Lengo la mkutano wa pili lilikuwa ni lipi?
  5. Maana ya kauli, "sungura akakosa pa kuweka uso wake?" ni

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 11 hadi 15.

G7T1S1002swap3

Kijiji cha Matopeni kipo kusini mwa gatuzi la Manga. Matopeni ni eneo la waziri wengi. Eneo hili huwavutia watu wengi hususan wanaokitembelea kijiji hiki kwa mara ya kwanza. Mandhari ya kijiji hiki yanapendeza mno. Wakazi wa eneo hili hufanya bidii ya mchwa maishani. Uzembe hauruhusiwi kamwe. Watu wazembe hutozwa faini au huuziwa bidhaa kwa bei ghali. Hivyo wakazi
hulazimika kujikakamua.

Kila mkazi hutunza mazingira. Kukata miti bila mipango maalum hakuruhusiwi kamwe. Mashamba hulimwa kwa mpango na kwa njia inayozuia mmomonyoko wa udongo. Kutokana na hali hii eneo la Matopeni huzalisha chakula cha kutosha.

Vyanzo vya maji hutunzwa vilivyo. Mito, mabwawa na maziwa hayachafuliwi na wakazi wa eneo hili. Wao huzalisha nguvu za umeme kutokana na upepo na maporomoko ya maji. Wanyama wa porini huishi bila kuhangaishwa. Mara nyingi watalii humiminika kwenye mlima wa Matopeni kuwatazama wanyamapori, maporomoko ya maji na utamaduni wa wakazi unaopendeza.

  1. Kulingana na aya ya kwanza, ni watu wa aina gani ambao huvutiwa na eneo la Matopeni?
  2. Unafikiri ni kwa nini asilimia kubwa ya wakazi wa Matopeni hufanya bidii?
  3. Kwa nini eneo la Matopeni lina uwezo wa kuzalisha chakula kwa wingi?
  4. Nguvu za umeme kwa watu wa Matopeni huzalishwa kutokana na nini?
  5. Neno, 'mazingira' limetumiwa kwenye kifungu. Maana yake ni

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 hadi 20. Umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Feli alikuwa __16__ (kati yao,katika, miongoni mwa) wanafunzi __17__ (ambaye, ambawo, ambao) walipenda sanaa ya uchoraji. __18__ (Walioungana, Alijiunga, Aliunga) na wenzake __19__ (pindi tu, bora tu, ndiyo) alipoingia shule ya Kauleni. Alijitahidi sana na hatimaye akaibuka kuwa mchoraji maarafu katika kaunti yao. Ama kwa kweli __20__ (udongo upatilize uli maji, chanda chema huvikwa pete, achanikaye kwenye mpini hafi njaa)

Kutoka swali la 21 hadi 22, chagua jibu sahihi.

  1. Chagua kundi tatu la maneno katika jedwali uliopewa lenye nomino za pekee.
     Kiswahili                Maria                         Zuhura
     Punda                  Turkana                         Shule
     Maji                        Mate                          Marashi
  2. Andika wingi wa:
    Mjenzi yule maarufu ameziba ufa kwenye ukuta.
  3. Akifisha sentensi: Aha! Kumbe umejiunga na timu yetu?
  4. Andika upya sentensi ifuatayo: Tumia 'ngali' badala ya 'ki'
    Wakifanya bidii maishani watafanikiwa.
  5. Sifuna alichapa kazi kutoka asubuhi hadi jioni. Maana ya nahau iliyopigiwa mstari ni.
  6. Fungu ni kwa maembe kama vile mtumba ni kwa _______________________.
  7. Tunga sentensi ukitumia nomino 'upendo'
  8. Taja aina moja ya tungo za fasihi simulizi.
  9. Andika sifa moja ya novela.
  10. Kwa nini watoto huimbiwa bembelezi?

Umepewa dakika 40 kuandika insha vako

Unatarajia kuandaa sherehe ya siku ya kuzaliwa kwako. Sherehe hiyo itafanyika. wakati wa likizo baada ya kufunga shule. Sherehe itahusisha watu wachache tu. Unatarajia kumwalika rafiki yako. Andika barua ya kumwalika kuhudhuria sherehe hiyo.
Zingatia mambo yafuatayo:

  1. Anwani yako, tarehe
  2. Mtajo, maamkuzi
  3. Ujumbe na lugha ya adabu
  4. Sarufi sahihi, hati nzuri na hitimisho


MARKING SCHEME

  1. Tabia ya kutojali/ anapenda uchafu
  2. Ataoga/ atajirekebisha
  3. Usafi/ usafi wa ntu binafsi
  4. Nakurai/ nakuomba
  5. Ili asiwaudhi wenzake.
  6. Ukame ulikuwa umekithiri/ umezidi.
  7. Walikuwa wameikumbatia / wanaipenda teknolojia ya kisasa.
  8. Jifya moja haliinjiki chungu (methali zinazohimiza ushirikiano) nk
  9. Kumtambulisha mwizi kwa wanyama.
  10. Aliona haya/soni / aibu.
  11. Wageni wanaozuru matopeni kwa mara ya kwanza.
  12. Kuepuka kutozwa faini au kuuziwa bidhaa kwa bei ghaii.
  13. Mashamba hulimwa kwa mpango na kwa njia inayozuia mmomonyoko wa udongo.
  14. Upepo/maporomoko ya maji.
  15. Chochote kinachotuzunguka.
  16. Miongoni mwa
  17. ambao
  18. Alijiunga
  19. Pindi
  20. achanikaye kwenye mpini hafi njaa
  21. kiswahili, mama, zuhura
  22. Wajenzi wale maarufu wameziba nyufa kwenye nyuta.
  23. Aha! Kumbe umejiunga na timu yetu.
  24. Wangalifanya bidii maishani wangalifanikiwa
  25. aliendelea kufanya kazi.
  26. nguo
  27. mwalimu atathmini sentensi za wanafunzi.
  28. hadithi/nyimbo/ushairi / semi
  29. wahusika wachache / ploti ya moja kwa moja kurasa chache n.k
  30. ili waache kulia/walale.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 7 Mid Term 1 Exams 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students