Swali 1 hadi 4
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali:
Mwalimu: Masalkheri wanafunzi?
Wanafunzi: (Kwa pamoja) Hatujambo mwalimu.(Mwalimu anasimama mbele ya darasa na kuwatazama wanafunzi).
Mwalimu: Nashukuru. Kipindi cha leo ni spesheli. Kinahusu ulanguzi wa watoto. Ni jambo linalosikitisha kuwa watoto wanalanguliwa na watu wasiowajua na hata wale wanaowajua.Mara nyingi watotohad bufanywa watumwa;vitwana na vijakazi. Wanaowajua watoto huwahadaa kwa maisha mema. Mbinu zinazotumiwa na wanaowachukua watoto ni nyingi mno. Kuwateka nyara, kuwapatia zawadi na watu hao kujifanya wema kwao. Ulanguzi wa watoto ni kinyume cha sheria. Nimeamua kuwapatia habari hizi ili ziwasaidie. Kila mmoja wenu anapaswa kutohadhari. Kuna mwanafunzi aliye na swali? (Mwanafunzi mmoja anainua mkono na mwalimu anamchagua.)
Mwanafunzi: Je, nitatofautishaje watu wasio na nia mbaya na walanguzi?
Mwalimu:Mara nyingi walanguzi hawataki siri zao kujulikana. Hupenda kuzungumza kwa siri, huwa na wasiwasi usio wa kawaida, huonyesha urafiki haraka haraka na huja kwa ukarimu kupita kiasi. (Wanafunzi wanashtuka kusikia habari hizo)
- Mazungumzo haya yanahusu jambo gani?
- Haya ni mazungumzo ya aina gani?
- Taja njia moja inayoweza kutumiwa kuwatambua walanguzi?
- Mazungumzo haya yalifanyika wakati gani?
Ufupisho
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata:
Ni jambo linalosikitisha uhalifu unapoongezeka katika taifa letu. Wahalifu wanashiriki katika visa hivi bila kujali athari na maafa wanayosababisha. Juhudi za serikali kukabiliana na tatizo hili bado hazijafanikiwa vilivyo.
Uhalifu husababisha hasara nyingi. Watu hupoteza maisha yao. Watu wenye taaluma mbalimbali hujifia tu na ikumbukwe kuwa hawa huchangia kwa asilimia kubwa ukuaji wa uchumi.
Majumba yanapoharibiwa na biashara kuteketezwa, nchi kupoteza wawekezaji.
Uhalifu ni wa aina nyingi mbali na ugaidi, wizi, ubakaji, upotoshaji watu, wapo wahubiri bandia wanaopotosha watu na hatimaye huwapora mali yao. Wengine hudanganya waumini wao kuwa mali ya ulimwengu hayana umuhimu. Wao hulazimisha waumini kufunga; kukaa bila chakula hadi kufa. Kisa cha Shakahola kilituatua moyo. Uhalifu ni wa aina nyingi.
Je, tutaukabili uhalifu namna gani? Tushirikiane kwa kila namna. Tusisahau kuwa jifya moja haliinjiki chungu. Tuwaeleze watoto wetu madhara ya kujiingiza kwenye uhalifu; tuwafunze maadili ili hata watakapobaleghe, mienendo yao itakuwa mizuri. Wakoseapo, tusiogope kuwaadhibu kwani usipoziba ufa utajenga ukuta.
Ikiwa kuna mhalifu miongoni mwetu, basi mfichue. Fichua njama za kutekeleza uhalifu kwa kuwafahamisha maafisa wa usalama ili wachukue hatua. Tusikubali kutengwa kikabila. Sisi sote ni wana wa Adamu. Tukemee siasa duni ambayo inaweza kutugawanya. Tuchukue tahadhari kabla ya hatari.
- Andika habari kuu za kila aya katika kifungu ulichosoma kwa kuzielezea kwa sentensi moja. (Kila aya ielezwe kwa sentensi moja)
(alama 5)
Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali yanayofuata.
Baada ya kuguguna mifupa na minofu ya nyama kwenye sherehe, fisi alirejea nyumbani kwake. Alijibwaga chini ya mnazi kupumzika. Baada ya muda, usingizi ulimchukua akalala fofofo. Akaanza kuota ndoto mbaya. Aliota kuwa milima na majengo marefu yanaporomoka, watu na wanyama wanaangukia na majabali na mawe. Wakati huo huo, nyani aliyekuwa kilele cha mnazi aliangusha nazi kavu mchangani tifu! Karibu na kichwa cha Fisi. Fisi alizinduka kutoka usingizini ghafla akaanza kutimua mbio za ajabu. Kishindo cha nazi kilimfanya kudhani kuwa milima na majengo yanaporomoka kweli na maisha yake yalikuwa hatarani.
Njiani alikutana na Fisi wengine akikimbia na wakati huo huo akitweta. Wenzake walishtuka. Aliwaeleza kuwa milima ilikuwa ikiporomoka na majumba marefu. Wenzake hawakupoteza muda. “ Afua ni mbili, kufa au kupona." Fisi wa kwanza alisema. Mbio za ghafla zikaanza Fisi mmoja baada ya mwingine alijiunga na wa kwanza kukimbia, baada ya kupata habari za milima na majengo marefu kuporomoka. Wanyama wengine waliuliza sababu ya panya kukimbia. Walipoelezwa nao pia walianza kuenda shoti.
Mfalme wa pori alipopata habari kuhusu hangaiko la wanyama, aliamua kuingilia kati. Alisimama kwenye kilele cha mlima na kunguruma mara tatu. Wanyama wote wakaacha kukimbia na kutii amri ya mfalme wao. Simba aliuliza kwa hamaki, "kwa nini mnakimbia kama walio kwenye shindano?"
"Ewe mfalme wetu, huna habari kuwa milima na majengo marefu marefu yanaporomoka? Mbweha alimuuliza.
"Nani aliyeona hayo yakitendeka."
"Si mimi, Mbweha alijitetea, "nilifahamishwa na Fisi mmoja."
Fisi mmoja baada ya mwingine alisema kuwa hakuona ila alipashwa habari na Fisi mwingine. Hatimaye Simba alimfikia Fisi wa kwanza aliyeeneza uvumi kuwa milima na majengo yanaporomoka.
"Madai hayo ni ya kweli mfalme." Fisi wa kwanza alisema,
"Nilikuwa nimelala chini ya mnazi na nikaota kuwa milima na majengo marefu marefu yanaporomoka. Wakati huo huo nikasikia sauti ya mlima ukiporomoka na majengo kuanguka. Niligutuka kutoka usingizini na kuanza kutoroka niyanusuru maisha yangu." Simba aliamua kuandamana raye hadi mahali milima na majengo yanaporomoka.
Simba alichuchuma naye Fisi akapanda juu ya mgongo wake. Akatimua mbio kama mshale. Walipoufikia ule mlima Fisi alimwonyesha Simba alipolala. Hapakuwa na ishara yoyote ya milima wala majengo kuporomoka. Alichokiona Simba ni iliyoanguka mchangani. Simba aliangua kicheko akarudi kwa wale wanyama kuwaelezea hali halisi.
- Kwa nini Fisi alilala chini ya mnazi?
- Chanzo cha wanyama kukimbia kilikuwa ni nini?
- Maana ya 'akitweta' ni ___________________________
- Unafikiri ni kwa nini Simba alimbeba Fisi mgongoni?
- Je, ungekuwa mnyama ungewashauri nini wanyama waliojiunga na Fisi na kuanza kukimbia
Matumizi ya lugha.
Soma kifungu hiki kisha uchague jibu lifaalo:
Wanafunzi wote walimpa __11__ Maria kutokana na juhudi zake za __12__ wa mashairi. Alitunga shairi la mishororo minne kila ubeti yaani; __13__ lililoshinda __14__ ya kipekee katika mashindano ya kitaifa. Aliibukia kuwa __15__ tajika shuleni __16__.
(mwetu, tuzo, malenga, tarbia, utunzi, mkono wa tahania)
- Andika wingi wa:
Seremala aliitengeneza meza nzuri akamuuzia rubani. - Chorea mviringo nomino ya kawaida katika sentensi:
Zainabu alininunulia kalamu ya kupendeza. - Kamilisha sentensi: Kichala ni cha matunda ilhali mkungu ni kwa
- Badilisha sentensi ifuatayo iwe katika wakati ujao:
Kipchoge anashiriki katika shindano la riadha. - Tamara alikutana na Mateso kisha akamwamkua sabalkheri Mateso? Je, unafikiri wawili hao walikutana wakati gani?
- Bainisha kwa kupigia mstari kitenzi kikuu na kitenzi kisaidizi katika sentensi:
Mwalimu angali anasahihisha madaftari ya wanafunzi. - Andika kisawe cha neno. 'makao'
- Kanusha sentensi:Mfugaji angewapa mifugo wake chakula cha kutosha, wangemnufaisha.
- Tumia nomino yoyote katika ngeli ya II kutunga sentensi.
- Akifisha sentensi:
Mpendaraha hufanya biashara ya kuuza vitu kama vile nguo viatu soksi kofia shuka na kanga. - Andika jozi moja ya maneno iliyo na sauti /dh/ na /th/
Fasihi
- Andika tungo mbili za fasihi simulizi. (alama 2)
- Nyimbo za watoto zina umuhimu gani? (alama 1)
- Ni tofauti gani iliyopo kati ya novela na riwaya? (alama 1)
INSHA
Andika insha ya maelezo yenye mada:
Namna ya kuzuia mmomonyoko wa udongo shuleni mwetu.
MARKING SCHEME
Sehemu A: Mazungumzo
- Ulanguzi wa watoto
- Mazungumzo ya kupasha habari/ ujumbe.
- Huwa na wasiwasi/ huzungumza kwa siri/ huonyesha ufanisi haraka na huwa karimu kupita kiasi.
- Jionil
Sehemu ya B: Ufupisho
-
- Uhalifu unaongezeka katika taifa letu na juhudi za serikali kuukabili hazijafanikiwa.
- Uhalifu husababisha maafa, kuteketezwa kwa majumba, blashara na nchi hupoteza wawekezaji.
- Mifano ya uhalifu ni kama vile ugaidi, wizi, ubakaji, uporaji, kulazimisha watu kufunga hadi kufa kama vile kisa cha shakahola
- Tushirikiane ili kuukabili uhalifu, tuwafunze watoto maadili na tuwaadhibu wanapokosea
- Wahalifu wafichuliwe wakabiliwe kisheria, tuache ukabila na siasa za kutugawanya
Sehemu C: Ufahamu wa kusoma
- Ili kujipumzisha/kupumzika
- Ndoto aliyoota fisi
- Akihema
- Ili akimbie naye wafike haraka mahali milima na majengo yanaporomoka
- Kuchunguza jambo kabla ya kufunga maamuzi. (Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi)
Sehemu D: Matumizi ya lugha
- Mkono wa tahania.
- Utunzi
- Tarbia
- Tuzo
- Malenga
- Mwetu
- Maseremala walizitengeneza meza nzuri wakawauzia marubani.
- Kalamu
- Ndizi
- Kipchoge atashiriki katika shindano la riadha
- Asubuhi
Mwalimu angali anasahihisha madaftari a wanafunzi- Maskini/makazi/kitende/hashuo
- Mfugaji asingewapa mifugo wake chakula cha kulosha wasingemnufaisha.
- Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi
- Mpendaraha hufanya biashara ya kuuza vitu kama vile nguo, viatu, soksi, kofia, shuka na kanga
- dhamini, thamini - rithi/ridhi - dhibiti/thibiti - adhiri//athiri n.k mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi
- hadithi/ maigizo/ mazungumzo/ semi/ vitendawili/ ushairi simulizi n.k
-
- Kufanya michezo yao ipendeze
- Huwatumbuiza
- Hukuza ushirikiano
- Riwaya huwa ni hadithi ndefu yenye visa na wahusika wengi ilhali novela ni utungo mfupi kuliko riwaya na huwa na wahusika wachache na wazo sahihi.
Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 7 End Term 2 Exams 2023 Set 1.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students