UFAHAMU (Alama 15)
Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali.
Kila mtoto ana mambo anayotarajiwa kuyatekeleza akiwa kiamboni. Mambo haya anafaa kuyatekeleza kwa hiari mtoto yeyote Yule akitenda anayopaswa kuyatenda akiwa nyumbani, atakuwa amewajibika. Majukumu ya watoto wakiwa nyumbani ni ya aina mbalimbali.
Kuwaheshimu wazazi au walezi ni mojawapo ya majukumu ambayo watoto wanastahili kuyafanya wanafaa kuwatiii kwa kufuata maagizo na ushauri wao bila kunung'unika. Ni muhimu kwa kila mtoto kuelewa kuwa jungu kuu halikosi ukoko. Ushauri wa wazazi au walezi ni muhimu kwa kuwa wameona mengi duniani; mema na mabaya.
Isitoshe, watoto wana wajibu wa kuwasaidia wazazi au walezi wao kufanya shughuli mbalimbali. Hizi ni kama vile; kupiga deki, kuosha vyombo, kufanya kazi za shambani miongoni mwa shughuli nyingine watoto wakiwasaidia wazazi au walezi kwa kazi za nyumbani, watakuwa wakijitafutia Baraka. Vile vile, watapalilia msingi imara wa maisha yao yajayo kama wazazi au walezi.
Pia, watoto wana jukumu la kusaidia kutunza mazingira wakiwa nyumbani. Baadhi ya shughuli za utunzaji mazingira ni kama vile, uzoaji taka, upandaji miti na uzuiaji wa mmomonyoko wa udongo. Mazingira safi huwahakikishia wanajamii afya njema.
Zaidi ya hayo, watoto wana jukumu la kudumisha umoja wakiwa nyumbani. Wanastahili kushirikiana na wenzao ipasavyo katika familia. Aidha, wanafaa kuhakikisha wanaishi kwa umoja na majirani wao.
Isitoshe, watoto wanastahili kuendelea kujifunza mambo ambayo wameyasoma shuleni wakiwa nyumbani wanafaa kuwaeleza wazazi au walezi wao na ndugu zao kuhusu baadhi ya mambo wameyasoma shuleni. Kwa kufanya hivi, wataweza kutumia katika maisha yao maarifa na stadi ambazo wamezipata shuleni. Ni muhimu kwa kila mtoto kuwajibika na kuendeleza masomo yake akiwa nyumbani.
Majukumu ya watoto wakiwa nyumbani hayawezi kupuuzwa. Mtoto afanyapo majukumu tofauti nyumbani huwa anajijengea msingi imara wa mustakabali wake. Kila mtoto anastahili kuelewa umuhimu wa kutekeleza majukumu yake. Nao wazazi au waleezi wanastahili kuwahimiza na kuwamotisha watoto wao kutekeleza wajibu wao kila wakati.
- Mambo anayotarajiwa kufanya mtoto huitwa? (alama 1)
- Taja methali moja iliyotumika katika makala haya? (alama 2)
- Mtoto anayafanya mambo yaliyotajwa akiwa wapi? (alama 1)
- Eleza maana ya maneno haya jinsi yalivyotumika katika makala haya? (alama 2)
Kuyatekeleza
Mstakabali - Neno jingine lenye maana sawa na jukumu ni ______ (alama 1)
- Taja mambo matano ambayo watoto wanastahili kufanya wakiwa nyumbani? (alama 5)
- Taja tamathali iliyotumika kuonyesha usafi. Toa maana yake (alama 2)
- Ni kichwa kipi kifaacho kwa makala haya? (alama 1)
Matumizi ya lugha (alama 20)
- Tambua nomino za pekee zinazopatikana katika sentensi ifuatayo (alama 2)
Mukesi atasafiri kwa ndege siku ya Alhamisi, tarehe tatu mwezi wa pili kwenda kumtembelea dada yake - Geuza sentensi ifuatayo katika wakati ujao. (alama 1)
Mzazi wake amewasili akiwa na zawadi kochokocho - Tambua nomino jamii ifaayo kujazia pengo lililowachwa wazi (alama 1)
Kaka yake alienda sokoni akanunua cha mboga. - Akifisha sentensi hii; (alama 3)
Mwalimu nekesa aliwaambia wanafunzi kuleta bidhaa zifuatazo karatasi, penseli, vitabu na vifutio. - Tunga sentensi kuonyesha hali na nyakati hizi (alama 3)
- Wakati uliopita hali endelezi (alama 2)
- Wakati ujao (alama 1)
- Andika kinyume cha maneno yaliyopigiwa mstari. (alama 2)
Mwanafunzi mwepesi ana matunda mengi. - Unganisha sentensi hizi kuwa moja (alama 2)
Mama alienda sokoni.
Mama alikatakata sukumawiki - Andika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa (alama 2)
''Chungeni ng'ombe ili wasiingie shambani," baba aliwambia wanawe - Tofautisha kati ya barua rasmi na barua ya kirafiki (alama 2
- Nomino jumba, jitu, jijino huorodheshwa katika ngeli gani? (alama 1)
Fasihi (alama 15) - Lala mtoto lala,
Lala mtoto lala,
Mama akija atakupa maziwa,
Mama akija atakupa maziwa- wimbo huu ni wa aina gani
- Taja sifa nne za aina ya wimbo uliotaja (alama 4)
- Tofautisha kati ya nyimbo za kazi na kidini? (alama 2)
- Mhusika ni nani? (alama 2)
- Nyimbo hutumia lugha kwa namna maalum. Lugha hii hudhihirisha vipengele Fulani. Taja mifano ya vipengele hivi na mifano ya vipengele vyenyewe. (alama 8)
INSHA
Andika insha ukifuata maagizo uliyopewa.
Mwandikie rafiki yako barua ukimwalika sikukuu ya jamhuri.
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
- Majukumu
- Jungu kuu halikosi ukoko
- Kiambo/nyumbani
- Kuyatekeleza/mustakabali
- Wajibu
-
- Kuwaheshimu wazazi au walezi
- Kuwasaidia wazazi au walezi katika shuguli kama vile kuosha vyombo
- Kutunza mazingira kwa kuoza taka kupanda miti
- Kudumisha umoja wa wenyewe kwa wenyewe na pia majirani
- kuendelea kujifunza waliyoyasoma shuleni
- Pangusa na kusafisha nyumba
- Majukumu ya watoto wakiwa nyumbani
- Mukesi, Almasi
- Mzazi wake atawasili akiwa na zawadi kochokocho
- Kaka yake alienda sokoni akanunua kicha cha mboga
- Mwalimu Nekesa aliwaambia wanafunzi kuleta bidhaa zifwatazo:
- karatasi, penseli
- vitabu na vifutio.
- (a)(likuwa....ki) (b) (ta)
- Mwanafunzi mwepesi ana matunda mengi.
Mwepesi-mzito, mengi-machache -
- Mama alikatakatia sukumawiki sokoni
- Sukumawiki zikikatakatiwa sokoni na mama
- Baba aliwaamuru wanawe wawachunge ng'ombe ili wasiingie shambani
-
- Barua rasmi hua na anwani mbili ilihali barua ya kirafiki hua na moja
- Barua rasmi ina sahihi ilihali ya kidugu haina
- LI-Ya
-
- Bembelezi
-
- Huwa fupi
- Huimbiwa watoto wachanga
- Huibua hisia za upendo
- huimbwa na wazazi au walezi
-
- Nyimbo za kazi huimbwa na watu wanapofanya kazi mbalimbali ilihali nyimbo za kidini huimbwa na watu wakati wa shuguli mbali mbali za kidini
- Kiumbe au kitu kinachoshiriki katika matendo yanayosimuliwa katika kazi za fasihi
-
- Nahau - chapa kazi
- Methali - haba na haba hujaza kibaba
- Sitiara - pesa ni sabuni ya roho
- Urudiaji wa maneno
- Kutumia maneno yasiyo na maana '' Aiyaiya''
Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 7 End Term 3 Exams 2023 Set 1.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students