SEHEMU A
UFUPISHO
Soma kifungu kifuatacho kisha uandike ufupisho wake.
Maji ni muhimu katika maisha ya binadamu, wanyama, ndege, samaki, wadudu na hata mimea, Ni kweli kuwa maji ni uhai. Maji hupatikana baharini, maziwani, mitoni na hata visiwani. Matumizi ya maji ni kama vile; kupukia, kuoshea, kunyunyizia mimea na kuwapa mifugo kunywa. Maeneo ya nchi ambayo hayana mito au mvua hayavutii watu wengi kuishi huko. Wenyeji wa sehemu hizo hukabiliwa na ukame.
Milima, misitu na maziwa huwa vianzo vya mito. Mlima Kenya huwa ni chanzo cha Mto Tana nayo Milima ya Cherengani na Mlima Elgon ni vianzo vya Mto Nzoia. Mito hii ni miongoni mwa mito muhimu katika nchi ya Kenya. Faida ya mito hii ni chungu nzima. Hutupatia maji ya matumizi nyumbani na viwandani, mito mingine hutumika kuzalisha nguvu za umeme na usafiri pia. Maji haya ya mito pia hunywewa na wanyama na vilevile huvutia watalii. Hivyo basi tunastahili kuyatunza maeneo mbalimbali ya maji.
Tusiharibu misitu yetu kwa kukata miti kiholela. Ikiwa tutakata mti mmoja, tupande miwili au zaidi. Ni jukumu la kila mmoja kuyalinda mazingira yetu. Tusitupe takataka ovyo ovyo. Mvua inaponyesha huyabeba takataka zilizo tapakaa hadi katika mito. Wajenzi waviwanda pia wanatahadharishwa dhidi ya kuelekeza majitaka katika mito na maziwa.
Andika ufupisho wa kifungu hiki kuhusu umuhimu wa maji.
Zingatia yafuatayo:
- Maneno yasizidi 60
- Iwe katika mpangilio kuendelea
- Iwe aya moja
Tumia maneno yako mwenyewe bila kughairi maana ya kifungu. (alama 10)
SEHEMU B
UFAHAMU
Nchini Kenya, kuna aina nyingi za mimea inayokuzwa. Mimea hii ni kama mibuni, michai, mipamba na mengineo mingi.
Mimea hii hukuzwa katika sehemu mbalimbali. Huwaletea wakulima faida kubwa wanapouza maazao yao. Aidha nchi yetu hupata manufaa ya pesa za kigeni. Pesa hizi hutumiwa kununulia bidhaa mbalimbali ambazo hazipatikani hapa kwetu.
Hebu tutazame mmea wa mpamba. Kutokana na mmea huu tunapata vitu tofauti tofauti kama; mafuta ya kupikia, vitambaa vya nguo, nyuzi za kushonea, chakula cha ng'ombe na hata pamba zinazotumika katika hospitali.
Je,pamba hutengenezwaje hadi ikawa nguo? Ikishavunwa shambani, hupelekwa viwandani. Pamba ikifikishwa viwandani humu, mna mashine kubwa ambazo huipokea na kuichanuachanua, huku ikitoa mbegu na uchafu kutoka kwa pamba. Pamba hiyo inapotoka hapo, hupitishwa katika mashine nyingine ambazo huifinyafinya mpaka inakuwa kama blanketi refu la pamba tupu.
Blanketi hiyo hutiwa katika mashine zenye meno ambazo huchana nyuzi hizo za blanketi na kuzifanya namna ya kama nene kidogo. Kamba hiyo hupitishwa kwenye mashine ambazo huigawanya katika nyuzi za unene mbalimbali. Nyuzi zenyewe huwa laini, nyembamba na zingine nene zinazotumiwa kufumia vitambaa nyepesi au vizito.
Vitambaa hivyo baada ya kupitishwa katika mitambo ambayo huvifua ili viwe safi. Kwa hivyo hatuwezi kuwa na vitambaa vya rangi ya aina moja, vitambaa hivi hupitishwa katika mitambo ya kutia rangi na maridadi mbalimbali.
Mwishowe vile vitambaa hukaushwa na kufungwa katika majora tayari kwa kuuziwa wenye maduka. Hivyo basi, wananchi hununua majora hayo na kushona mavazi kama mashati, marinda, suruali na shuka.
Jibu maswali haya
- Taja mimea mitatu inayokuzwa nchini mwetu iliyotajwa katika kifungu hiki. (Alama 3)
- Nchi hufaidikaje kutokana na mimea hiyo? (Alama 1)
- Taja faida mbili za pamba. (Alama 2)
- Ni hatua gani ya kwanza inayochukuliwa kutengeneza pamba ifikapo kwenye kiwanda? (Alama 1
- Ni nyuzi aina gani zinazitengenezwa kufumia nguo nzito na nyepesi? (Alamal)
- Kwa nini vitambaa hufuliwa baada ya kufumwa? (Alama 1)
- Eleza vile tunavyopata vitambaa vya nguo vya aina mbalimbali. (Alama 2)
SEHEMU C: SARUFI (Aiama 30)
Soma na ujaze kifungu kifuatacho. Kina nafasi kuanzia 8-14. Jaza wa kuchagua jibu bora kati ya yale uliyopewa.
Wakenya ___8___ kwa wingi siku ya ___9___ kura. Uchaguzi huu ulikuwa ___10___kihistoria tangu kupitishwa kwa ___11___ mpya. Baadhi ya vituo vya kupigia kura vilianza kupata wateja asubuhi na mapema kabla ya jogoo ___12___. Hata hivyo, vituo hiyvo vilistahili
___13___ kuanzia mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi. Wananchi wa ___14___ ya Kenya walipiga foleni ndefu mchana kutwa ili kuwachagua viongozi wapendao.
- (watajitokeza, walijitokeza, wanajitokeza, hujitokeza)_________________________
- (wupiga, kupiga, kupigiwa, kupigia)_____________________________
- (ya, la, cha, wa) ________________________
- (kanuni, amri, katiba, sharia). __________________________
- (kutetea,kuwika,kubweka,kuvuma) ______________________
- (kufunguka, kufunguliwa, kufungwa, kufungulia) __________________________________
- (taifa, seneti, kaunti, jamhuri) ______________________
Kuanzia nambari 15-22, chagua jibu sahihi.
- Wanjaa na Anita walikuwa ________________________. Walipotayarisha sherehe ya kuzaliwa kwao, walipanga kuita watu ili kuwa __________________________ habari hizo. (Alama 1) (pasha, pacha)
- Wote walioalikwa kwenye _________________ waliandikwa kwenye daftari kwa ___________________
(karamu, kalamu) (alama 1) - Wimbo huu unawalaani watu wenye ku ________________________ vitu vya wenzio. (imba, iba) (alama 1)
- Piga mstari kivumishi cha sifa katika sentensi hii. (Alama 1)
Mpishi hodari hupika chakula chenye ladha. - Jibu salamu; Alamsiki?________________________________ (alama 1)
(alamsiki, binuri, alheri) - Chagua jibu sahihi; Abiria wamefunga mikanda ________________________________ (alama 1)
(gani,wote,zipi) - Tumia "amba" ipasavyo. Zizi ___________________________ limejengwa litahifadhi mbuzi wetu. (alama 1)
(ambazo, ambayo, ambalo) - Tegua kitendawili; Nanywa supu na nyama naitupa. _________________________ (alama 1)
(firigisi, muwa, moto)
Kuanzia swali la 23-24, tunga sentensi ukitumia maneno uliyopewa. (Alama 2)
- askari
- mpenzi
- Chagua kiwakilishi kifaacho (Alama 1)
___________________________ aliniazima kalamu yake jana. (Sisi, Wao, Yeye) - Akifisha
Ewaa ____________________________ Shule yetu imeshinda katika somo la Sanaa (Alama 2)
(!na.) (?na,) (.na!) - Andika vitu viwili vinavyopatikana katika ngeli ya I-I. (Alama 2)
- Kamilisha sentensi hii; Pahali ______________________________ patapigwa dawa. (Alama 1)
(huku, humo, petu) - Taja sehemu nne za ndani ya mwili. (Alama 4)
- Tunaposema Faiza ni chiriku. Hii ni fani gani ya lugha? (Alama 2)
SEHEMU YA D:
FASIHI
Soma shairi hili kisha ujibu maswali
Wakati umeshafika, mimea kuitambua,
Mingi inayosifika, yatupasa kuijua,
Na matumizi twataka, tupate kuyaelewa,
Mimea tuisomeni, tuweze kuitambua.
Tuanze na mkahawa, jina jingine mbuni,
Huo huzaa kahawa, iuzwe ulimwenguni,
Ambayo yananunuliwa, Tena kwa kubwa thamani,
Mimea tuisomeni, tuweze kuitambua.
Nao huo mpareto, nchini tunakuza,
Watuzalia pareto, maua ya miujiza,
Dawa yenye kubwa pato, Kwa mbu kuwafukuza,
Mimea tuisomeni, tuweze kuitambua.
Pia tusiuschau, mmea wa mzabibu,
Tuujuwe angalau, ndiye mama wa zabibu,
Zatumika kwa pilau, au kwenye matibabu,
Mimea tuisomeni, tuweze kuitambua.
Sote twapenda sukari, chaini inayotiwa,
Tulijueni vizuri, inayotokana na miwa,
Mikate hata mahamri, ni kawaida kutiwa,
Mimea tuisomeni, tuweze kuitambua
Someni bila dharau, mimea kuitambua,
Pia kuna mlimau, tusiache kuujua,
Mara watupa limau, kwa bei twalinunua,
Mimea tuisomeni, tuweze kuitambua.
Maswali
- Shairi hili linahusu nini? (Alama 1)
- Shairi hili lina beti ngapi? (Alama 1)
- Andika vina vya kati na vya mwisho katika ubeti wa tatu.(Alama 2)
- Ubeti wa pili una mizani ngapi? (Alama 2)
- Andika kibwagizo cha shairi hili. (Alama 1)
- Hili ni shairi la aina gani? (Alama 1)
- Mimea ifuatayo huzaa nini? (Alama 2)
- Mlimau
- Mzabibu
MARKING SCHEME
SEHEMU YA A-UFUPISHO
- Mwanafunzi aweze kufupisha kifungu hadi
kitimie maneno 60. - Zingatia hoja kuu inayojitokeza
- Mtiririko was kifungu uwe wa kuendelea
- Aya iwe moja tu
SEHEMU B-UFAHAMU
- Mimea iliyotajwa Ni: mpamba, mbuni, michai,m
- Nchi hufaidika kwa kupata pesa za kigeni/kununulia bidhaa mbalimbali
- Faida za pamba Ni mafuta ya kupikia,vitambaa vya nguo,nyuzi,chakula Cha ngombe
- Hatua ya kwanza ni kuichanuachanua ili kutoa mbegu na uchafu
- Nyuzi Aina nyembamba,laini na nene
- Vitambaa hufuliwa ili viwe safi
- Vitambaa mbalimbali hupatikana kwa kupitisha katika smashine ya kutia rangi mbalimbali
- walijitokeza
- kupiga
- wa
- katiba
- kuwika
- kufunguliwa
- jamhuri
- pacha, pasha.
- Karamu, kalamu.
- Iba.
- Hodari.
- Binuri.
- Gani.
- Ambalo.
- Muwa.
- zingatia jinsi neno askari limetumika.
- Zingatia jinsi neno mpenzi limetumika.
- Yeye.
- ! na
- Sujari,chumvi, chai,mvua n.k.
- Petu.
- Ini,ubongo, figo,moyo, pafu,damu,n.k.
- Sitiara/Istiari.
SEHEMU D-USHAIRI
- Mimea/mazao ya mimica/matumizi ya mimea.
- Sita/6.
- -to, -za.
- 63/sitini na tatu.
- Mimea tuisomeni tuweze kuitambua.
- Tasdisa.
-
- Mlimau-limau,
- mzabibu-zabibu.
Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 7 Opener Exams Term 1 2023 Set 1.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students