ALAMA 30
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5
Hakimu: Wewe jina lako kamili ni Mboko, sio?
Mboko: Ndiyo, Mheshimiwa
Hakimu: Unakiri mashtaka haya mawili, yaliyoelezwa na kiongozi wa mashtaka?
Mboko: La, sikiri, Mheshimiwa.
Hakimu: Kiongozi wa mashtaka, unaweza kuendelea na maelezo zaidi kuhusu kesi hii.
Kiongozi wa mashtaka: Mheshimiwa, huyu mshtakiwa alikamatwa amekaa ndani ya gari la Bi. Cheupe. Maelezo ya alama ya usoni pa Mboko tuliyopewa na Bi. Cheupe yalitusaidia kumkamata.
Karani wa korti: Mheshimiwa huyu shahidi ni mfanyi kazi katika kituo cha petroli. Jina lake ni Mwema. Ana alama ya kovu usoni pake.
Hakimu: Unaweza kuionyesha korti huyo uliyemwona akiwacha gari la Benz na kuchukua la Toyota?
Mwema: Ni yule mle kizimbani aliye na pingu Mheshimiwa.
Mboko: Mheshimiwa ningependa kumuuliza Kiongozi wa mashtaka swali moja. Polisi aliyenikamata alinikuta mimi nimeketi kiti cha mbele cha dereva au cha abiria?
Kiongozi wa mashtaka: Mheshimiwa huyu ni mhalifu sana. Tuna ripoti kuwa huyu ni mwizi sugu wa magari.
Hakimu: (Akimwelekea Mashtaka) Una lolote la kusema ili kujitetea?
Mboko: Mimi sina hatia, Mheshimiwa. Mimi nilikuwa abiria tu niliyekuwa nikipelekwa nyumbani. Mwizi wa gari ni huyo aliyekuwa ameketi kiti cha dereva.
Hakimu: Mimi nitatoa uamuzi wiki ijayo. Kwa hivyo mshtakiwa atabaki korokoroni na kuletwa tena hapa kortini siku nitakayo toa hukumu
- Aliyeulizwa jina lake na hakimu ni ___________________
- Je, mshtakiwa alikubali mashtaka yake? (Ndio, la) ________________
- Ni watu wangapi wametajwa katika mazungumzo haya?
- Neno kukiri limetumika katika mazungumzo maana yake ni ____________________
- Unafikiria ni nani hakusema ukweli kati ya watu waliotajwa kwenye mazungumzo?
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6-9
Watu wa Afrika mashariki hutumia ala za muziki ambazo zinafanana sana. Kuna ala za nyuzi kama vile gita, zeze, kinubi na udi. Piano pia ni aina ya ala ya nyuzi ingawa nyuzi zake zimefichika ndani.
Ala nyingine hutoa sauti kwa kupuliziwa upepo. Ala hizi ni kama vile kipenga ambacho pia hutumiwa na refa, yaani mwamuzi katika michezo. Zumari na parapanda vile vile ni miongoni mwa ala za kupulizia upepo. Ala nyingine hutoa sauti kwa kutikiswa. Mfano wa ala hizi ni njuga, kayamba, tari na manyanga.
Kuna ngoma ambazo huchezwa uwanjani na kuangaliwa na watu wote, wake kwa waume. Mfano wa ngoma hizo ni kama zile ngoma za kusherehekea mavuno au sikukuu za taifa au za kutumbuiza wageni.
Ngoma na muziki ni njia ya watu kujipatia ajira. Hoteli nyingi huajiri wanamuziki na wachezaji ngoma za kienyeji ili kuwavutia wateja katika hoteli hizo. Inapasa kuhakikisha kuwa hatuwashirikishi wasichana na wavulana wadogo katika ngoma hizi za kutumbuiza watalii katika hoteli.
- Ala za muziki zinazofanana mara nyingi hutumiwa na
- Taja aina mbili za ala zinazo chezwa kwa kupulizwa.
- Ni aina ngapi za ala zimetajwa katika kifungu hiki?
- Chora na utaje ala moja ya muziki iliyotajwa.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 10 - 12
Mfalme alikuwa na jozi kumi na mbili za soksi. Jozi sita zilikuwa nyeusi na sita zilikuwa rangi ya kahawia. Alimtuma mtumishi wake kumchukulia jozi moja ya soksi kabatini. Alipofika kabatini, taa zote za umeme katika chumba zilizima.
- Mfalme alikuwa na jumla ya soksi ngapi?
- Neno jozi limetumika lina maana ya
- Unafikiria mtumishi atapeleka soksi ngapi kwa mfalme ili apate jozi moja?
Soma kifungu kifuatacho kisha uyajibu maswali 13 - 15
Ni wajibu wa kila mwanafunzi kufanya kazi kwa bidii na kwa dhati. Tukumbuke kuwa Wahenga hawakukosea waliposema ajizi ni nyumba ya njaa. Hivyo basi haifai kulaza damu darasani.
Ni sharti tufanye juu chini kuwa na adabu na juhudi. Taifa letu linahitaji watu walioelimika, kwani bila elimu itakuwa vigumu sana kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo.
Wakulima nao kwa upande ule mwingine kuzidisha mazao mashambani kwa sababu idadi ya watu inazidi kuongezeka.
Isitoshe, wanabiashara ni lazima kama ibada wajishughulishe na biashara ambapo kwa sasa ni Wakenya wachache sana ambao wanatambua umuhimu wa biashara. Wengi wa wananchi ni wale ambao wana mawazo kuwa ni sharti kila mtu aajiriwe maishani.
nchi
Hivyo basi ni lazima tujitoe mhanga na kuona kuwa nchi yetu imeimarika kiuchumi. Kila mzalendo anafaa kujikaza kisabuni kuona amefanya jukumu lake ili kuona maendeleo ya yamepatikana.
- Kulaza damu ni sawa na kusema kuwa
- Unadhani ni kwa nini biashara haijaimarika nchini?
- 'Ajizi ni nyumba ya njaa' ni aina gani ya tamathali ya lugha?
Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 mpaka 20. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.
Idadi kubwa ya mashabiki ___16___ mchuano wa soka ___17___ Man City na Man United. Nchi yetu, Kenya, ___18___ kushiriki katika mashindano haya___19_-_ si mwanachama wa kombe la Uropa. ___20___ mashabiki wa Kenya, walitazama mechi hiyo moja kwa moja kwenye runinga zao.
A | B | C | D | |
16. | yalihudhuria | walihudhuria | ilihudhuria | ilihuthuria |
17. | baina ya | dhidi ya | badala ya | katikati ya |
18. | haiwezi | inaweza | haiezi | hawawezi |
19. | endapo | sembuse | almuradi | maadamu |
20. | Licha ya | Kwa hivyo | Hata hivyo | Minghairi ya |
Kutoka swali la 21 hadi la 30, chagua jibu lifaalo zaidi kulingana na maagizo uliyopewa.
- Binuru ni jibu la maamkuzi gani?
- Kanusha:
Angeniita kwa sauti ningeitika. - Ni nini maana ya nahau 'kupiga deki'?
- Tunasema baraza la wazee. Tutasema______________________ya watu. (umati, halaiki)
- Chagua sentensi sahihi.
- Hapa ndiko kwenye hospitali itajengwa.
- Huku ndiko penye hospitali itajengwa.
- Humu ndimo kwenye hospital itajengwa.
- Huku ndiko kwenye hospitali itajengwa.
Katika maneno yafuatayo, chagua nomino mbili za dhahania.
kucheza Kenya wema thureya daftari nyota maji utulivu ndege uzalendo |
- _________________
- __________________
- Dereva _________________________ gari barabarani vizuri. (dhibiti, thibiti)
- Barua ya kirafiki ina anwani ngapi?
- Kinyume cha mtu mwangalifu ni mtu _____________________
MARKING SCHEME
- Mboko
- La
- Watano
- Kukubali kosa ulilolifanya
- Mboko
- Watu wa Afrika Mashariki
- Zumari, firimbi, kipenga, paapanda
- nne
- mchoro sahihi
- ishirini na nne
- vitu viwili vikiwa pamoja/ vinafanana
- soksi nne
- mvivu/mzembe/mtepetevu/mkunguni/mlegevu
- wengi wanaegemea kuajiriwa
- methali
- C
- B
- A
- D
- C
- Alamsiki
- Asingeniita kwa sauti nisingeitika
- Panguza sakafu kwa kutumia maji
- Halaiki
- D
- wema, utulivu uzalendo
- '' " "
- dhibiti
- moja
- msahaulifu
Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 7 Opener Exams Term 1 2023 Set 3.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students