Kenya Certificate Of Secondary Education (KCSE 2009) Kiswahili Karatasi ya Pili

Share via Whatsapp
  1. UFAHAMU

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.

    Wanasaikolojia wanahainisha kati ya sehemu mbili kuu katika akili ya binadamu; Ung'amuzi na ung'amuzibwete. Ung'amuzi ni sehemu ya ubongo ambayo kimsingi hupanua na kudadavua yanayotendeka hususan mchana . Ung'amuzi bwete ni kibini methali chake;hufanya kazi wakati binadamu anapolemazwa na usingizi.Baadhi ya mambo anayoshuhudia binadamu mchana yanaingia kwenye ung'amuzibwete wake na kutokeza katika ndoto zake usiku.

    Kwa mujibu wa mawazo ya Sigmund Freud ,mwanasailologia wa jadi anayechukuliwa na wengi kama mwasisi wa taaluma ya saikologia , mambo yanayopatikana katika unga'amuzibwete yana sifa hasi. Freud alidahili kuwa binadamu huyaficha na kuyabania kwenye ung'amuzibwete mambo ambayo hawezi kuyasema kudamnasi. Alieleza kuwa matamanio yasiyokubalika, makatazo ya jamii, fikra na kauli zilizoharamishwa na miko ya kijamii hubanwa katika ung'amuzibwete. Shehena hiyo ndiyo inayochipuza kwa njia ya ishara za ndoto, mitelezo ya kauli, yaani maneno au kauli zinazotukoka bila wenyewe kukusudia, ishara ya lugha ya kitamathali katika uandishi wa kibunifu na kadhalika.

    Ung'amuzibwete una uwezo mkubwa wa kuadhiri matendo ya binadamu. Huu ndio msingi unaowafanya wanasaikolojia wengi, akiwepo Freud, Kusema kuwa tajribia ya mtoto inaweza kifichwa kwenye sehemu hiyo na hatimaye kuishia kutokelezea katika utu uzima wake. Kwa kuwa tunapoingiliana na binadamu wenzetu kila siku tunayang'amua tuyafanyayo, ung'amuzi unaotuwezesha kutambua jema na ovu unatawala. Ung'amuzibwete unapotawala binadamu wenzetu watashindwa kutuelewa. Hii ndiyo hali anayokuwa nayo mwendawazimu. Ung'amuzibwete wake hutawala. Sisi tunaotawaliwa na ung'amuzi tunashindwa kumwelewa; naye bila shaka anashindwa kutuelewa.

    Carl Guslav Jung, aliyewahi kuwa mwanafunzi wa Freud, aliupinga mwelekeo wa Freud wa kuungalia ung'amuzibwete kama jaa la mawazo mabaya, matamanio, nia, fikira tuli na dhana ambazo ni hasi. Jung alizuka na dhana mbili muhimu: Ung'amuzibwete wa kibinafsi na ung'amuzibwete jumuishi. Alisema mambo, fikra na uzoefu wowote mbaya unaomhusu mtu binafsi hupatikana katika ung'amuzibwete wa kibinafsi. Dhana ya ung'amuzibwete jumuishi aliitumia kuelezea sehemu ya akili ya binadamu ambayo inamfanya ayatende matendo fulani kama binadamu wenzake licha ya tofauti zao kiwakati na kijiografia. Kwa mfano, binadamu wengi wana sherehe za kuzaliwa mtoto , kuoza, ibada au mviga unaohusiana na kifo licha ya tofauti zao. Jung alisema kuwa kinachochochea hali hii ni urithi fulani katika binadamu. Urithi huo  unapatikana katika ung'amuzibwete jumuishi.

    Upo mwafikiano kati ya wataalamu hawa wawili kuwa ung'amuzibwete una uwezo wa kuathiri ung'amuzi matendo ya binadamu ya king'amuzi. Wanasaikolojia wanashikilia kuwa binadamu hawezi kukamilika bila kuzihusisha sehemu zote mbili kwa sababu zinaathiriana.

    1. Kwanini ung'amuzibwete unaelezwa kama kinyume cha ung'amuzi? (alama 2)
    2. Eleza mtazamo wa Freud Kuhusu ung'amuzibwete. (alama 3)
    3. Kwa mujibu wa Freud yaliyomo kwenye ung'amuzibwete hudhihirika vipi? (alama 4)
    4. Eleza tofauti ta mawazo kati ya Sigmund Freud na Carl Gustav Jung. (alama 3)
    5. Taja hoja inayowafungamanisha Jung na Freud. (alama 2)

  2. MUHTASARI

    Utaifa ni mshikamano wa hisia zinazowafungamanisha watu wanaoishi katika taifa moja. Taifa huundwa na watu wanaoishi katika nchi moja na ambao wanajitambua kisiasa kama watu wenye mwelekeo, mwono na hatima sawa. Utaifa umejengwa kwenye hisia za mapenzi kwa nchi na utambuzi wa kwamba rangi, cheo, hadhi, eneo, kabila au tofauti nyinginezo baina ya watu wanaoishi katika nchi moja si sababu ya kuwatenganisha.

    Nchi moja huweza kuwa na watu wa makabila tofauti, wenye matabaka ya kila nui na mawazo ainati. Watu hao wanapotambua kuwa kuna sherisi nyingine inayowaunganisha kama fahari ya kuwa watu wa nchi hiyo, falsafa na imani sawa ambayo ishara yake kuu ni wimbo wa taifa na kuwa tofauti kati yao muhimu huwa wamefikia kuunda taifa.

    Mhimili mkuu wa taifa ni uzalendo. Uzalendo ni mapenzi makubwa aliyo nayo mtu kwa nchi yake. Mapenzi haya ndiyo yanayoongoza matendo yake, matamanio yake, mawazo yake, itikadi yake mwonoulimwengu wake na muhimu zaidi mkabala wake kuihusu nchi yake na hatima ya nchi yenyewe. Uzalendo ni nguzo muhimu sana ya taifa. Mzalendo hawezi kuyatenda mambo yanayoweza kuiletea nakama nchi yake.

    Matendo ya mzalendo huangazwa na mwenge wa mema anayoitakia nchi au taifa lake. Hawezi kushiriki kwenye harakati na amali ambazo zinahujumu au kufumua mshikamano wa taifa zima au kutawaliwa na kitiba cha kutaka kujinufaisha yeye mwenyewe au jamii yake finyu. Matendo ya mzalendo wa kitaifa yanaongozwa na mwelekeo wa kuiboresha nchi yake. Swali linalomwongoza mtu huyo ni: nimeifanyia nini nchi yangu au taifa langu? Alhasili mtu anayeipenda nchi yake hawezi kuongozwa na umero wa kibinafsi tu wa kujilimbikia mali, ujiri au pesa. Yuko radhi kuhasirika kama mtu binafsi ili taifa au nchi yake inufaike.

    Utaifa ni mche aali ambao unapaliliwa kwa uzalendo, kuepuka hawaa za nafsi , kusinywa na taasubi za kikabila na kuacha tamaa ya kujinufaisha. Hali hiyo inapofikiwa, hatima ya wanajamii wa taifa linalohusika kuwa nzuri na mustakabali wao na wa vizazi vyao huwa na matumaini makubwa.

    1. Dondoa sifa kuu za utaifa (maneno 40-50) (alama 6, 1 ya mtiririko)

    2. Kwa kutumia maneneo kati ya 60-70, onyesha misingi ya kumtathmini mzalendo.

  3. MATUMIZI YA LUGHA

    1. Andika sentensi mbili zifuatazo kama sentensi moja kwa kutumia kiwakilishi kirejeshi.
      1. Duka la Bahati lina bidhaa nyingi.
      2. Juma anafanya kazi katika duka la Bahati.  (alama 2)

      1. Eleza matumizi mawili ya kiambishi -ji- (alama 2)
      2. Tunga sentensi moja kuonyesha moja ya matumizi hayo. (alama 2)

    2. Tumia visawe vya maneno yaloyopigwa mstari kuandika tena sentensi ifuatayo;
      Ukuta umemwumiza mvulana alipokuwa akiuparaga. (alama 3)

    3. Chora vielezo matawi vya sentensi ifuatayo;
      Bakari, Roda na Hirsi wamefurahi kupita mtihani. (alama 4)

    4. Tambua sauti ambazo si za ufizi katika sauti hizi.
      m, t, n, z, gh. (alama 1)

    5. Tunga sentensi sahihi ukitumia -fa- katika hali ya mazoea. (alama 2)
    6. Onyesha kwa kupiga mstari iliko shadda katika maneno mawili yafuatyo;
      1. Malaika
      2. Nge   (alama 2)

    7. Eleza maana mbili za sentensi:
      Kiharusi chake kimewatia hofu. (alama 2)

    8. Tunga sentensi ukitumia kielezi cha jinsi cha nomino ifuatayo;
      Uganda (alama 2)

    9. Bainisha sentensi sahili zilizo katika sentensi mseto ifuatayo:
      Hamali ambaye ameugua alisema kuwa angekwenda hospitali jana. (alama 3)

    10. Andika ukubwa wa sentensi;
      Ndovu wa Kiafrika ameharibu kichaka (alama 2)

    11. Iandike tena sentensi ifuatayo bila kutumia vitenzi visaidizi.
      Wachezai huenda wakawa wanaweza kushinda mchezo wa leo. (alama 2)

    12. Andika kwa msemo halisi:
      Baba alipotuuliza kama tungependa kwenda Mombasa wakati wa likizo tulimjibu kwamba tulitaka kwenda Kisumu kwa kuwa tulikuwa hatujaliona Ziwa Victoria. (Alama 3)

    13. Huku ukitoa mfano mwafaka onyesha matumizi mawili ya kinyota (*) katika sarufi ya Kiswahili. (alama 3)
    14. Kanusha sentensi ifuatayo;
      Hapo napo ndipo nitakapo. (alama 1)

    15. Andika kinyume cha;
      Furaha amehamia mjini. (alama 1)

    16. Andika maneno yafuatayo katika kauli zilizoonyeshwa katika mabano
      1. imba (tendesha)......................................
      2. Choka(tendea)..........................................

  4. ISIMUJAMII
    Eleza majukumu matano matano ya Kiswahili kama lugha ya kitaifa na kimataifa. (alama 10)
 
 
 
 
 
 
 

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kenya Certificate Of Secondary Education (KCSE 2009) Kiswahili Karatasi ya Pili.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest