Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - KCSE 2021 Past Papers

Share via Whatsapp

MASWALI

  1. Lazima
    Rafiki yako anasomea ng'ambo. Alipoondoka nchini, Kaunti yenu ilikuwa inakabiliwa na kutojitosheleza kwa chakula. Mwandikie barua kumweleza hatua ambazo Kaunti yenu imechukua kutatua tatizo hili.
  2. Fafanua manufaa ya kuboresha miundomsingi nchini.
  3. Tunga kisa kinachodhihirisha maana ya methali ifuatayo: Aliye kando haangukiwi na mti.
  4. Tunga kisa kinachoanza kwa maneno yafuatayo: "Maskini, anaonekana kuemewa na hisia za kupoteza. Huu mchezo wa bahati nasibu utakuja kutuangamizia kizazi," akajisemea Kutu huku akimtazama mja aliyekuwa kainamia meza huku ameshika kichwa...


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. Hii ni barua ya kirafiki. Vipengele vifuatavyo vijitokeze:
    1. Muundo
      Anwani ya mwandishi
      Tarehe
      Kongowezi/Mtajo -- kwa mpendwa
      Utangulizi: Maamkuzi yajitokeze
      Uonyeshe anayeandika.
      Unaweza pia kuonyesha kiini cha barua
      Mwill - hoja zijadiliwe hapa. Kila hoja kwenye aya.
      Hitimishto-ajumuishe mawazo yake.
      Hitimisho kuhusiana na hoja/kiini cha barua ijitokeze kimalizio- Jina la mwandishi.
    2. Mtindo : Mtindo wa barua ya kirafiki uzingatiwe. Mwandishi atumie lugha faafu inayozunguru moja kwa moja na anayeandikiwa.
    3. Maudhui
      Mtahiniwa ajadili kikamilifu hatua ambazo kaunti imechukua kujitosheleza kwa chakula Baadhi ya hoja ni:
      1. Kaunti imehakikisha kwamba befo pembejeo za ukulima kama vile mbolea, mbegu na vifaa imepunguzwa ili kdoosha uzalishaji wa chakula
      2. Kuhifadhi maji ya mvua ili kunyunyizinyea maji wakati ambapo hakuna mvua ya kutosha.
      3. Kuimarisha/kuanzisha na kuhimiza utafiti su kilimo na ufugaji ili kuelekeza kuhusu njia bora za uzalishaji wa chak
      4. Kuwapa wakulima mikopo ili kuwawezesha ganunulia pembejeo zinazohitajika.
      5. Kuimarisha miundomsingi hasa barabara, mashinani ili kuisha usafirishaji wa chakula.
      6. Kupanua soko ili kuwapa wakulima motisha kuzalisha chakula zaidia
      7. Kuboresha usimamizi na matumizi ya maji, hasa ya unyuwiaji mashamba
      8. Kushirikisha sekta ya kibinafsi kuwekeza katika sekta ya kilimo.
      9. Kuimarisha njia za uhifadhi wa mazao ili kukinga dhidi ya kuharibika/ ili yatumike kwa chakula wakati wa uhitaji.
      10. Kuwapa wakulima wa eneo kame mbegu zinazostahimili mazingira ya ukame ili itokeapo kwamba mvua itaacha kunyesha mapema, mazao yasiharibike.
      11. Kuimarisha njia za kununua mazao ya ukulima na kuyahifadhi kwa matumizi wakati wa uhaba.
      12. Kununua mifugo kutoka kwa wakulima wakati wa ukame ha kaltumia kupata nyama
      13. Kuhimiza kilimo cha kisasa.
      14. Kuinyunyizia mimea dawa ili kukinga dhidi ya wadudu waharibifu.
      15. Mikakati ya kuhakikisha kuwa fedha zilizotengewa uzalishaji wa chakula anatumiwa kwa madhumuni hayo
      16. Kutafuta njia mbadala ya kuzalisha chakula kama vile kufuga kuku wa kututumuliwa au kukuza mimea kama vile nyanya zinazokua kwa muda mfupi.
      17. Kuchimba visima au mabwawa ili kuhifadhi maji kwa matumizi ya baadaye.
      18. Kutojenga kwenye ardhi iliyotengewa upanzi wa mimea itoayo chakula.
      19. Kuepuka shughuli zinazochangia mmomonyoko wa udongo, kama vile kulima kando kando ya mto.

Tanbihi

  1. Pamoja na kwamba hii ni barua, inatoa taarifa/ habari kuhusu suala la kujitosheleza kwa chakula. Mtahiniwa sharti azingatie ukweli katika masuala anayojadili.
  2. Vigezo vingine vya usahihishaji vizingatiwe kulingana na mwongozo wa kudumu. 
  3. Mtahiniwa atathminiwe kipaudhui kulingana na jinsi anavyojieleza. 
  4. Jina la kaunti linastahili kujitokeza. Hata hivyo, lisipojitokeza mtahiniwa asiadhibiwe. Atakuwa tayari amejiadhibu kimtindo
  1. Hii ni insha ya kutoa habari/arifu. Mtahiniwa anastahili kuandika insha ambayo inazingatia ukweli kuhusu manufaal haja ya kuimarisha miundomsingi. Anaweza kutoa mifano ya nchi ambayo iliimarisha miundomsingi na kupata manis Baadhi ya hoja ni:
    1. Kuboreshwa kwa barabara kumechangia usafiri wa haraka wa abiria na pia usafirishaji wa bidhaa. Umeokoa saa. Raia wametumia saa hizi kuzalisha mali.
    2. Kukarabatiwa kwa mabomba ya maji kumepunguza mafuriko nyakati za mvua. 
    3. Upanuzi wa nyanja za ndege umechangia ongezeko la idadi ya wasafiri na hivyo kuboresha uchumi.
    4. Kusambazwa kwa umeme katika sehemu za mashinani kumeinua hali ya maisha ya raia. 
    5. Mifumo bora ya kutuma na kupokea pesa imerahisisha shughuli za ubadilishanaji wa bidhaa na huduma, na kuimarisha uchumi.
    6. Kuboreshwa kwa barabara mashinani kumewezesha kupungua kwa gharama yarashara na hiyvo kupungua kwa bei ya bidhaa muhimu. Hali ya maisha ya raia imeimarika kutokana na haya.
    7. Kuboreshwa kwa mifumo ya usafiri kumechangia umoja na ushirikiano; raia wameweza kutangamana kwa wepesi.
    8. Kuboreshwa kwa miundomsingi, kama vile mifumo ya mawasiliano kumechangia kuimarika kwa usalama wa kitaifa na kubadilishana mawazo kwa urahisi.
    9. Upanuzi wa hospitali na kuajiriwa kwa madaktari k kumeboresha huduma za matibabu na kuimarisha afya ya kijamii.
    10. Ujenzi wa shule na vyuo umeimarisha sekta ya elimu. Idadi ya watoto wanaojiunga na shule imeongezeka na kupunguza ujinga/ kupunguza asilimia ya watu ambao hawajui kusoma na kuandika

Tanbihi

  1. Dhana ya miundomsingi ni pana. Isichukuliwe tu ni barabara. Kuna miundomsingi ya kijamii kama vile shule na hospitali.
  2. Mtahiniwa anaweza kuzingatia aina moja ya miundomsingi kama vile barabara, akatoa manufaa ya kuziimarisha.
  3. Kigezo cha maudhui kikadiriwe kulingana na jinsi mwanafunzi anavyofafanua hoja. Hoja zifafanule kikamilifu Mwongozo wa kudumu urejelewe.
  4. Kipengele cha suundo kitathminiwe kwa kuzingatia sehemu zifuatazo:
    1. Utangulia
    2. Mwili
    3. Hitimisho
  5. Mwongozo wa kudumu uziwe kwa usahihishaji wa kutegemewa zaidi.
  1.    
    1. Hii ni insha ya methali. MtahiniwFinastahili kutunga insha ya masimulizi imayodhihirisha maana na matumizi ya methali hii
    2. Mtahiniwa atunge kisa kinachodhihirisha kwamba mtu ambaye hujiepusha na mambo yenye hatari/ athari/yanayoleta aibu, huepuka hatari/aibu changamoto zinazotokana na hali hiyo.
    3. Hali zifuatazo zinaweza kujitokeza:
      1. Msimulizi awe rafiki ya kundi linaloendeleza utovu wa nidhamu shuleni. Kundi lipange njama za kutisidi shule. Moja kati ya njama hizo inaweza kuwa kuchoma shule au tendo lolote la kihalifu. Msimulizi aone hatari katika haya; akatae kujiunga na kundi hilo. Ajiepushe na madhara kama vile kufukuzwa shuleni kukatiza masomo yake kufungwa jela
      2. Msimulizi agundue kwamba wenzake wanadanganya katika mtihani. Akakataa kushiriki katika tendo hilo. Matokeo ya mtihani ya wenzao yafutiliwe mbali. Yeye asalimike.
      3. Msimulizi aonywe dhidi ya kushiriki katika vitendo hasi vya marafiki. Akaidi/akose kusikiliza onyo hili. Ajiingize katika tendo hilo. Aathirike vibaya.
      4. Msimulizi/Mtahiniwa anaweza pia kusimulia kisa cha jamii au nchi ambayo ilikataa kushiriki katika shughuli za kiuchumi au za kijamii ambazo nchi nyingine katika kanda zilishiriki kwazo. Shughuli hizo zinaweza kuwa kuziwekea baadhi ya nchi vikwazo vya kiuchumi, uundaji wa zana hatari za kivita kushiriki katika tamaduni kandamizi zilizopitwa na wakati au hata kutumia maliasili kwa njia isiyo endelevu. Nchi hiyo iepuke athari mbaya za shughuli ambayo nchi au jamii hizo nyingine ziliendeleza

        Tanbihi 
        1. Lazima pande zote mbili za methali zijitokeze.
        2. Mtahiniwa aonyeshe mhusika aliyejitenga na jambo hatari, kisha akasalimika akaepuka madhara
        3. Mtahiniwa aonyeshe mhusika aliyejiingiza katika tendo hatari na kuathirika vibaya
        4. Mwongozo wa kudumu urejelewe katika utuzaji.
  2.       
    1. Hii ni insha ya mdokezo wa kuanzia
    2. Ni insha ya masimulizi. Mtindo wa kimasimulizi utumiwe.
    3. Mtahaniwa atuage kisa ambacho kinaoana na mwanzo.
    4. Kisa kionyeshe wthari za mchezo wa bahati nasibu.
    5. Kinaweza pia kuonyeha hali ambayo imemkumba anayetazamwa na Kutu hadi akawa amevunjikiwa kiasi hiki
    6. Ruwaza zifuatazo zinaweza kujitokeza
      1. Mhusika aanze kucheza mchezo wa bahati nasibu. Mwanzoni ashinde kiasi. Apate kidogokidogo mshawasha wa kuendelea. Ashinde donge kubwa/pesa nyingi. Awe mraibu wa mchezo huu. Atumie pesa yupi katika mchezo fulani, apoteze. Kila kitu.
      2. Ndipo anajiinamia.
      3. Mhusika tajiri awe na mali nyingi ajiingize katika uchezaji huu ili atajirike zaidi. Apoteze kila kitu.

Tanbihi

  1. Kisa kinaweza kuanza kisha kiturudishe nyuma kusimulia matukio ya awali hadi mhusika kufikia hali hii.
  2. Mtahiniwa anaweza kuanza kwa maneno hayo kisha kukiendelee kisa moja kwa moja.
  3. Kwa vyovyote vile hali/toni ya kukata tamaa kuharibikiwa sharti ijitokeze
  4. Kisa kinaweza pia kuwa na hali/toni ya kuharibikiwa, kisha mhusika akasaidiwa kujirekerbisha, insha ikawa na mwisho mwema.
  5. Mja aliyekuwa ameinamia meza apewe jina. Hata hivyo, mhusika huyu anaweza kurejelewa kwa jina hilohilo, 'mja aliyekuwa kainamia meza, kuanzia mwanzo hadi mwisho wa insha, mradi imedhihirika wazi ni huyuhuyu mhusika anayerejelewa katika swali.
  6. Mwongozo wa kudumu urejelewe katika utuzaji.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - KCSE 2021 Past Papers.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?