KISWAHILI KARATASI YA 3 - 2019 KCSE Prediction Maswali Set 1

Share via Whatsapp

MAAGIZO

 • Jibu maswali manne.
 • Swali la kwanza ni la lazima
 • Chagua maswali mengine matatu kutoka kwa sehemu zilizosalia:

Riwaya, Tamthilia, Hadithi fupi na Ushairi.

 • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.

SEHEMU YA  A

 1. SWALI LA LAZIMA
  1.  
   1. Semi nini? (alama 1)
   2. Fafanua sifa nne za misimu (alama 4)
  2. Soma wimbo ufuatao kisha ujibu maswali

   Ewe kilizi
   Ulozowea kujificha
   Nyuma ya mama kujikinga, dhidi ya milio
   Yanadi ilo juu mbinguni
   Jua kesho ni siku ya siku
   Siku ya kujua mbivu na mbichi
   Kutofautisha jogoo na vipora
   Na riba takaposhika, chake kisu
   Ndipo utakapojua bayana
   Ukoo wetu si wa kunguru
   ikiwa hutayari
   kisu kukidhihaki
   sithubutu kamwe, wanjani kuingia
   sije kuniaibisha miye, amiyo na akraba nzima!

   Maswali

   1. Huu wimbo huitwaje? (alama 1)
   2. Eleza majukumu yoyote manne yanayotekelezwa na wimbo huu katika jamii (alama 4)
  3.  
   1. Mivigha ni nini? (alama 2)
   2. Eleza sifa tatu za mivigha (alama 3)
  4. Fafanua matatizo matano ambayo yanaikumba fasihi simulizi duniani (alama 5)

SEHEMU YA  B

RIWARA: CHOZI LA HERI: ASUMPTA MATEI

 1. “…haifai kucheza na uwezo wavijana, wao ni kama nanga. Huwezi kuzamisha na kuiongea merikebu.”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
  2. Bainisha tamathali mbili za usemi zilizotumika katika dondoo (alama 4)
  3. Kwa kurejelea riwaya hii, onyesha jinsi vijana wamezamisha merikebu ya wahafidhina. (alama 12)
 2. Baada ya dhiki faraja. Onyesha vile ukweli wa methali hii unavyodhihirika kwenye riwaya. (alama 20)

SEHEMU YA  C

TAMTHILIA: KIGOGO: PAULINE KEA

 1. “Sitaki kuaibishwa na mwanamke mimi, siwezi.”
  1. Yaweke maneno haya katika muktadha wake. (alama 4)
  2. Fafanua kwa hoja nane kuwa msemaji wa maneno haya anafaa kuaibishwa     (alama 16)
 2.  
  1. Jadili jinsi kumi ambazo kwazo maudhui ya ukatili yanajitokeza katika tamthilia ya Kigogo (alama 10)
  2. Eleza mifano mitano ya matumizi ya kinaya katika tamthilia ya Kigogo (alama 10)

SEHEMU YA D : HADITHI FUPI

TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE

 1. Eleza nafasi ya vijana katika jamii ukirejelea hadithi fupi zifuatazo.
  1. Mapenzi ya kifaurongo (alama 5)
  2. Shogake Dada ana ndevu (alama 5)
  3. Mame Bakari (alama 10)
 2. Ndoto ya mashaka: Ali Abdalla Ali
  “Sasa nimechoka mja. Nimechoka hata naradua kufa kuliko kuishi. Hadi lini haya mashaka ya kutengenezwa? Mashaka ya mashaka!
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
  2. Tambua mbinu mbili za lugha zilizotumika (alama 4)
  3. Fafanua mambo sita yanayomfanya mrejelewa aradue kufa. (alama 12)

SEHEMU YA E: USHAIRI

 1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali

  Barabaraba do ni ndefu
  Nami tayari nimecho katiki
  Natama ni kuketi
  Ni’nyooshe misuli
  Nitulize akili

  Lakini

  Azma ya nisukuma
  Mbele ikinihimiza kuendelea
  Baada ya miinuko na kuruba
  Sasa naona unyoofu wake
  Unyoofu ambao unatisha zaidi

  Punde natumbukia katika shimo
  Nahitaji siha zaidi ili kupanda tena
  Ghafla nakumbuka ilivyosema
  Ile sauti zamani kidogo
  “Kuwa tayari kupanda na kushuka”.

  Ingawa nimechoka
  Jambo moja dhahiri
  Lazima hufuate barabara
  Ingawa machweo yaingia
  Nizame na kuibuka
  Nipandenakushuka

  Jambo moja na kumbuka; Mungu
  Je nimwombe tena? Hadi lini?
  Labda amechoshwa na ombaomba zangu
  Nashangaa tena!
  Kitu kimoja na kiamini
  Lazima niendelee kujitahidi kwa kila hatua mpya
  Nijikokote kuiandama hii barabara yenye ukungu
  Nikinaswa na kujinasua
  Yumkini nitafika mwisho wake
  Ikiwa wangu mwisho haitauwahi kabla.

  Maswali

  1. Taja naueleze aina ya shairi hili (alama 2)
  2. Eleza toni ya shairi hili (alama 2)
  3. Huku ukitoa mifano mwafaka eleza tamathali tatu za usemi ambazo zinajitokeza katika shairi (alama 3)
  4. Mshairi ametumia uhuru wake wa utunzi. Eleza mifano mitatu huku ukitolea mifano. (alama 3)
  5. Fafanua dhamira ya mtunzi wa shairi hili (alama 2)
  6. Andika kifungu cha mwisho katika lugha ya nathari. (alama 4)
  7. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi (alama 4)
   1. Kuruba
   2. Siha
   3. Machweo
   4. Kujinasua
Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI KARATASI YA 3 - 2019 KCSE Prediction Maswali Set 1.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest