KISWAHILI KARATASI YA 2 - 2020 KCSE PREDICTION SET 1 (QUESTIONS AND ANSWERS)

Share via Whatsapp

Maagizo

 • Jibu maswali yote .
 1. UFAHAMU

  Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

  Takwimu ambazo zimetolewa na shirika la kazi la kimataifa (ILO) zinaonyesha kuwa ulanguzi wa watoto umetangaa hususan katika mataifa yanayoendelea. Ipo tumbi ya sababu za kuelezea kwa nini biashara hii imeshamiri.

  Athari mojawapo ya utandawazi ni kuunda mtandao mpana ulimwenguni . Mtandao huo unaweza kutumiwa kwa njia chanya au njia hasi. Njia chanya ni zile zinazochukuliwa kuwafaidi wanajamii kwa kuendeleza ubinadamu na kuboresha hali ya maisha kiuchumi,kisiasa na kitamaduni. Maarifa yanayosambazwa kuwa chachu ya kuumua ari ya maendeleo,elimu na mafanikio katika mataifa mengi ulimwenguni. Njia hasi ni zile ambazo maarubu yake ni kuwanufaisha wachache huku zikiwahasiri wengi.

  Kuwepo kwa mtandao kunawapa wenye nia tule kama usafirishaji na ulanguzi wa watoto fursa ya kuzitosheleza hawaa zao. Wanaoshiriki katika biashara huongozwa na pashau ya utajiri. Hawachelei kuwalangua watoto wanaochimbukia mataifa ya kimaskini huko ughaibuni wanakozongomezwa kwenye madanguro, kufanyishwa kazi za sulubu na za kitopasi na kuishi maisha duni .

  Asilimia kubwa ya watoto hurubuniwa kwa ahadi ghushi za kujiendeleza kimasomo. Wengine huuzwa kutokana na msaada wa jamaa zao wanaotovukwa na utu na kuwa mawakala katika amali hii ya kusikitisha .Biashara hii huweza kusahilishwa kwa kuwepo kwa mfumo fisadi wa kisheria ,msambaratiko wa muundo wa jamaa na ubinafsi wa kijamii. Ipo haja kubwa ya ushirikiano wa mataifa alkulihali kuikomesha biashara hii haramu. Jamii ya ulimwengu isipofanya hivi, itakuwa imekitia kizazi kizima kitanzi na kutumbukiza kesho yake kwenye matatizo kathiri.

  1. Ni kwa jinsi gani utandawazi umechangia katika biashara ya ulanguzi wa watoto? (alama 2)
  2. Mwandishi wa kifungu anapendekeza hatua zipi kusuluhisha tatizo la ulanguzi wa watoto?  (alama 3)
  3. Eleza jinsi watoto wanaolanguliwa wanavyoishi huko ughaibuni.                     (alama 3)
  4. Kulingana na muktadha, kifungu “ chachu ya kuumua ari ya maendeleo” kina maana gani ?   (alama 2)
  5. Jamii isiyosuluhisha tatizo la ulanguzi wa watoto itakuwa na hatima gani ? (alama3)                                                                                            
  6. Eleza maana ya      (alama 2)
   1. Maarubu
   2. Pashau
 2. UFUPISHO(Alama 15)

  Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

  Tangu enzi ya ukoloni mkongwe, Wakenya wamekuwa wakipigania ukombozi wao. Awamu ya kwanza ya ukombozi ilipatikana miaka ya sitini, hasa mwaka wa 1963 tulipojinyakulia uhuru wa kujitawala kutoka kwenye utawala wa Mwingereza. Ukombozi huu uliwezesha Wakenya asilia kushikilia awamu za uongozi. Ili kuwezesha Wakenya kujitawala, walikabidhiwa katiba mpya iliyotayarishwa na Mwingereza. Hata hivyo, wazalendo halisi hawakutosheka na katiba hii. Kutokana na hali hii, harakati za kujipatia ukombozi wa pili zilianza mara tu baada ya kupatikana kwa ukombozi wa kwanza. Ni kweli kuwa badiliko kwa mjukuu huanza kwa babu. Wazalendo wa zama hizo wakaanza kupigania kubadilisha na kurekebishwa kwa katiba, na hapa ndipo mbegu ya kutafuta mabadiliko ilipopandwa. Harakati hizi ziliendelea hadi mwaka 2010 wakati Wakenya walipopitisha katiba mpya inayotumiwa hivi sasa kuongoza nchi hii. Katiba hii inatarajiwa kuleta ugatuzi katika uongozi wa nchi. ‘Ugatuzi’ maana yake ni kuhamisha mamlaka kutoka kwenye viongozi wa ngazi za juu na kuyakabidhi raia wenyewe. Ni sawa na kupewa shamba ambalo bado halijalimwa ili wenyewe walifyeke, walime, wapande, wapalilie na wavune. Ijapo njia hii ya kujitawala ni ngeni na yenye changamoto nyingi, wengi wa Wakenya wanaifurahia.

  Je, unafikiria Wakenya wameichangamkia katiba hii eti kwa sababu tu ni mpya? Itategemea uamuzi na umakinifu wa kila mmoja wetu na matumaini aliyo nayo kutokana na katiba yenyewe. Mimi ninapoichunguza na kuitalii katiba hii sikubaliani na methali eti kipya kinyemi ingawa kidonda. Ni kweli kuwa macho mengi huona kuliko jicho moja. Katiba hii ni nzuri kwa kuwa inashirikisha watu wengi katika kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo. Kutokana na juhudi hii, asilimia kubwa ya wananchi hushirikishwa katika kufanya uamuzi wa masuala yanayowahusu maishani mwao. Talanta mbalimbali zinaweza kuimarishwa ili ziweze kutumika vilivyo na kuchangia juhudi za maendeleo.

  Isitoshe, katiba hii ni nzuri kwa vile inachangia kupeleka mamlaka na ugawaji wa rasilimali mashinani mwa nchi. Jambo hili litasaidia sana kuleta mamlaka na maendeleo karibu na raia ili waweze kuishi maisha bora kuliko hapo awali. Ukichunguza nchi hii, ni dhahiri kuwa kuna sehemu ambazo zimepiga hatua kubwa kimaendeleo kuliko zingine. Ili kustawisha maendeleo katika pembe zote za nchi, mfumo wa ugatuzi utagawa fedha za makadirio ya matumizi kwa kuzingatia viwango vya umaskini katika kila kaunti. Hali hii itawezesha kaunti zote nchini kujimudu na hivyo kuinua kiwango cha maendeleo katika nchi nzima.

  Mfumo huu wa utawala hubidi washika dau kuketi pamoja na kupanga mipango kabambe inayohusu maendeleo ya kaunti ama sehemu husika. Jambo hili huwapa nafasi wahusika kutambua mahitaji ya kimsingi ya maeneo yao ili yaweze kupewa kipaumbele katika utekelezaji, na hivyo wanaoshirikishwa katika utekelezaji wa mradi husika huiunga mkono kikamilifu na hivyo kuleta hali ya uelewano na utangamano. Uelewano huu huwezesha maendeleo kupatikana kwa haraka ukilinganisha na hali ambapo mipango hii ingepangwa na kutekelezwa na watu kutoka nje wasioelewa matakwa ya wakazi wa sehemu husika.

  Katiba hii pia inasaidia kueneza na kutilia mbolea mfumo wa kidemokrasia katika nyanja zote za maisha. Katika miaka ya hivi karibuni kumetokea mabadiliko ulimwenguni kote na watu wengi wanatarajia demokrasia itawale katika maamuzi ya shughuli zote za maisha yao. Wananchi hujiona kuwa wenye umuhimu mkubwa kwa vile wao wenyewe ndio hujitawala na haki zao hutiliwa maanani. Wana uhuru wa kusema, kuabudu, kutoa maoni, kushiriki, kusisitiza utawala wa kisheria na wa walio wengi, pamoja na haki za wachache kuheshimiwa. Hata hivyo, haimaanishi kuwa anapopewa uhuru huu mtu ana kibali cha kukandamiza wenzake kwa kutozingatia sheria. Katiba hii ya ukombozi wa pili wa Kenya imewapa wananchi msukumo na matumaini makuu kuwa milango ya heri itafunguliwa bila kujali umri, jinsia, tabaka, kabila, asili au hata mbari za wananchi.

  1. Kwa kurejelea aya ya kwanza, onyesha jinsi wazalendo hawakutosheka na katiba ya kwanza ya Kenya. (Maneno 40 - Alama 5, 1 mtiririko)
  2. Eleza kwa nini Wakenya wameichangamkia katiba mpya.(Maneno 60- Alama 10, 2 mtiririko)
 3. MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)                                                                            
  1. Andika sauti yenye sifa zifuatazo:             (Alama 1)
   1. Konsonanti
   2. hutamkiwa kaakaa laini
   3. kikwamizo ghuna
  2. Tofautisha maana ya sentensi zifuatazo:  (Alama 2)
   1. Kazi yote ni muhimu.
   2. Kazi yoyote ni muhimu.
  3. Andika sentensi ifuatayo katika wakati uliopita , hali isiyodhihirika. (Alama 2)
   Kenya hupokea watalii wengi.
  4. Tunga sentensi ukitumia nikama:  (Alama 3)
   1. kitenzi
   2. kiwakilishi
   3. kielezi
  5. Yakinisha sentensi hii :            (Alama2)
   Haji kukuona wala hataenda kesho.
   1. Silabi ni nini? (Alama2)
   2. Huku ukitoa mifano , eleza aina mbili za silabi za Kiswahili. (Alama 2)
  6. Ainisha virai katika sentensi: (Alama2)
   jirani mwenye lile shamba kubwa husaidia maskini.
  7. Huku ukitoa mifano mwafaka onyesha matumizi mawili ya kinyota (*) katika sarufi ya Kiswahili.      (Alama 4)
  8. Andika sentensi hii kwa usemi halisi: (Alama 2)
   Jane alimwamuru yaya wake aache uzembe kazini.
  9. Neno unga lina maana ya nafaka iliyosagwa. Eleza maana nyingine mbili. (Alama 2)
  10. Andika ukubwa wa: (Alama 2)
   Mwanamke mpiga ngoma aliiba mtoto na kumtia kwenye kikapu.
  11. Tunga sentensi mojamoja kuonyesha matumiziya vitenzi hivi katika hali ya kutendesha.    (Alama 2)
   1. nywa
   2. fa
  12. Changanua kwa njia ya mishale : (Alama 4)
   Wezi waliotaka kuiba walifukuzwa na bawabu.
  13. Unda sentensi moja yenye sehemu zifuatazo: (Alama 2)
   1. kikanushi cha nafsi ya kwanza umoja.
   2. wakati ujao
   3. yambwa tendwa
   4. mzizi
   5. kauli ya kutendesha
   6. kiishio
  14. Jaza mapengo kwakinyume cha neno lililopigiwa mstari:                          (Alama 1)
   Kuchomoza kwa jua kulimpa matumaini ambayo yalififishwa nakwake.
  15. Eleza matumizi ya kwakatika sentensi: (Alama 2)
   Kwa nini alipata moja kwa tano ilhali angesaidiwa na mwalimu kwa sababu kwa mwalimu si mbali.
  16. Tunga sentensi mbili kuonyesha matumizi mawili tofauti ya kiwakilishi ‘li’. (Alama 2)
  17. Toa maana ya nahau : (Alama 1)
   kushika miguu
 1. ISIMUJAMII(Alama 10)
  1. Fafanua sifa zozote sita za sajili yashuleni .                                               (Alama 6)
  2. Eleza jinsi malezi yanavyodhibiti mitindo ya lugha.                                   (Alama 4)


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

UFAHAMU

 1. Mtandao mpana kote ulimwenguni umefanya wenye nia tule (mbaya) kuwalangua watoto kwa urahisi. 1x2=2
  (Wasiseme njia hasi na chanya bali hasi pekee) kutaja tu“mtandao mpana”1
 2.  
  1. Ushirikiano wa mataifa
  2. Kuundwa kwa mfumo usio na ufisadi
  3. Kuzuia msambaratiko wa muundo wa jamaa
  4. Ubinafsi wa jamii uondolewe
  5. Mtandao utumike kwa njia chanya pekee       3x1=3
 3.  
  1. Huzongomezwa kwenye madanguro
  2. Hufanyishwa kazi za sulubu
  3. Hufanyishwa kazi za kitopasi
  4. Kuishi maisha duni                  3x1=3
 4. Kichocheo/ kiharakishi/chanzo/kisababishi/ kiini / motisha 1x2=2
 5.  
  1. Kukitia kizazi kizima kitanzi na kuitumbukiza kesho yake kwenyematatizo kathiri/mengi
  2. kukitumbukiza kesho yake kwenye matatizo kathiri / mengi   2x1 =3
 6.  
  1. nia/ dhamira/kusudi/ sababu/kiini/lengo/madhumuni/azma/shabaha
  2. shauku/ hamu/uchu/kiu/tamaa                                                            2x1=2

UFUPISHO

 1.  
  1. Baada ya kujinyakulia uhuru, wakenya walikabidhiwa katiba mpya iliyotayarishwa na Mwingereza.
  2. Waliendeleza vita hivi hadi walipopata katiba walioitunga wenyewe. Alama 4x1
 2.  
  1. Itazingatia mipango kabambe ya maendeleo
  2. Itasaidia kueneza mfumo wa kidemokrasia .
  3. Imewapa msukumo na matumaini makuu .                                                                  (alama 8x1) = 8
   yyyytrdsaaws4567

Matumizi ya lugha

 1. /gh/ 1x1
  1. bila kubaki/ bila kubakisha /bila kupungua/ kwa ujumla/kazi nzima 1x1
  2. bila kuchagua/ bila kupendelea / bila kubagua   1x1
 2. Kenya kapokea watalii wengi         1x2
  1. Nakuru ni mji uliostawi
  2. Nina piga pasi sasa
  3. Wanafunzi wamo darasani     3x1
 3. Anakuja kukuona na ataenda kesho     1x2
  1. tamko katika neno/
   tamko moja la neno /
   Sehemu ya neno inayotamkika kwa mpigo mmoja /
   Kipashio cha utamkaji ambacho hutamkwa kama fungu moja.1X2
  2. Silabi wazi -hizi ni silabi ambazo huishia kwa irabu                                                                
   Zaa – za + a                         lala -   La + la
   Silabi funge :huishia kwa konsonanti
   m-tu ,dak-ta-ri      2×1
 4. Jirani, shambakubwa ,maskini –RN
  Jirani mwenye lile shamba kubwa -RN                                                                                                       
  mwenye lile shamba kubwa, lile shamba kubwa –RV
  husaidia maskini – RT (Tuzavyovyoteviwili) 2x1                                                                                                    
 5. Mfano: Juma alinipigia mfira*
  Mfano : Baba kile cha kula alilkila*
  Kuonyesha neno lisilofaa katika muktadha Mfano: amegonjeka*
  Hakunanjia*
  Kuonyesha neno geni. Alikula matoke*
  Kuashiria maelezo yaliyotolewa chini ya ukurasa; yaani ufafanuzi.
  (kutaja 1, mfano 1)2x2=4
 6. ‘’√Wachauzembekazini! √’’ √Jane alimwonya yaya wake.√                                                         4x1/2=2
  Tanbihi: Akikosea kitahiniwa chochote apoteze nusu maki-akipata vyote, apate maki mbili
 7. Weka pamoja /shikanisha                                                                                                                                         
  Kuweka viungo kwenye chakula                                                                                                                  2x1=2
 8. Janajike √ piga √ goma/jigoma liliba toto √/jitoto na kulitia kwenye jikapu/kapu √               4x1/2=2
 9. Nywa- Mama alimnywesha mtoto maziwa.
  Fa- Jirani alimfisha yule mbwa kwa kutompa maji.                                                                                2x1=2
 10. S→KN+KT
  KN→N+S
  N→Wezi
  S →Waliotakakuiba
  KT→T+H+N
  T→walifukuzwa
  H→na
  H→na
  N→bawabu                                                                                                                                        8x1/2=4
 11. Sentensi: sitamsomesha.                                                                                                                                       
  Si-kikanushi cha nafsi (1)
  ta- wakatiujao
  m- yambwa tendwa
  som-mzizi
  esh-kauli
  a- kiishio
  Tanbihi – akikosa kitahiniwa chochote apate sufuri.Akipata vitahiniwa vyote apate alama 2
 12. Kuchwa/kutua                                                                                                                              1x1
 13. Kwa nini-kuulizia/swali
  Moja kwa tano- sehemu/akisami
  kwa sababu-kusudi
  Kwa mwalimu-mahali     
  Tanbihi:sharti abainishe kwa anayoirejelea 4×1.5=2          
  1. kiambishi cha wakati uliopita – musa alitutembelea
  2. kiambishi cha ngeli – tundaliliiva
  3. kiambishi cha kauli tendea- yule alikukimbilia.
 14. Kushika miguu-kuondoka                                                                                                                                         
  Kuomba radhi
  Kimbia/toweka                                     1x1=1

ISIMU JAMII

 1. sifa za sajili hii ya shuleni:
 2. Matumizi ya msamiati wa kielimu/kiusomi ‘vitabu’,’ maktaba’ ‘utafiti’  ‘mwalimu’  ‘mwanafunzi’ katika miktadha rasmi
 3. Matumizi ya lugha rasmi hudumishwa katika miktadha rasmi kama vile katika mazungumzo baina ya mwalimu mkuu na walimu wengine
 4. Shughuli za kiusomi kama vile ufunzaji huendeshwa kwa lugha sanifu
 5. Lugha ya adabu hudumishwa kutegemea wanaoshiriki katika mazungumzo.
  Mathalani: mwalimu hatarajiwi kutumia lugha yenye mzaha anapozungumza na wanafunzi wake.
 6. Ubadilishaji zamu: mwalimu ndiye huelekeza kipindi
 7. Lugha ya kuhoji. Hutumika pale mwanafunzi anapomwuliza mwalimu maswali. Pia, wakati mwalimu anataka taarifa fulani kuhusu mwanafunzi
  Lugha ya kushauri na kuelekeza .Kwa mfano, mwalimu anaweza kutumia lugha ya nasaha kumshauri mwanafunzi kutia bidii
  Hata pale mwanafunzi amekosa mwalimu humwelekeza zaidi badala ya kumhukumu na kumfanya ajihisi kuwa mhalifu
 8. Lugha yenye toni kali: mwalimu anapoonya kuhusu tendo hasi, anaweza kutumia toni kali kumfanya mwanafunzi kuliepuka
  Tanbihi :tuza za kwanza sita na pawe na mfano.                                                           6x1=6
 9. Malezi
  1. Mtoto anayelelewa kwakudhibitiwa hushindwa kujieleza vema kwasababu ya woga
  2. Mtoto anayelelewa katika unyanyasaji hutumia lugha kali ya kujihami kama vile matusi.
  3. Mtoto anayefundishwa kuepuka matumizi ya lugha kali/matusi hushikilia hivi katika mazungumzo.
 10. Mtoto asipofunzwa lugha ya mama hushindwa kujieleza katika lugha hiyo. 4x1=4

Jinsi ya kuadhibu

 1. Ufahamu
  Makosa ya hijai (h)
  Ondoa ½ alama ya hijai kwa kila kosa litokeapo kwa mara ya kwanza hadi upeo wa alama 3 (makosa 6)
  Makosa ya sarufi (s)
  Ondoa ½ alama kwa kila kosa litokeapo kwa mara ya kwanza mradi tu pana alama nzima au zaidi katika kijisehemu mahususi cha swali.
 2. Ufupisho
  Makosa ya hijai (h)
  Ondoaalama ½ kwa kila kosa hadi upeo wa alama 3 (makosa 6)
  Sarufi (s)
  Ondoa alama ½ kwa kila kosa hadi upeo wa alama 3(makosa 6)
 3. Matumizi ya lugha
  Makosa ya hijai (h)
  Ondoa alama ½ kwa kila kosa litokeapo kwa mara ya kwanza hadi upeo wa alama 3
  Makosa ya sarufi (s)
  Ondoa alama ½ kwa kosa la kisarufi litokeapo kwa mara ya kwanza mradi tu kuna alama moja au zaidi katika kila kijisehemu mahususi.
 4. Isimujamii
  h- adhibu hadi alama 2 (makosa 4)
  s- adhibu hadi alama 2 (makosa 4)
Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI KARATASI YA 2 - 2020 KCSE PREDICTION SET 1 (QUESTIONS AND ANSWERS).


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest