KISWAHILI PAPER 1 - 2019 LANJET JOINT MOCK EXAMINATION

Share via Whatsapp

MAAGIZO KWA MTAHINIWA:

  • Andika jina lako, nambari ya mtihani na tarehe katika karatasi ya majibu.
  • Karatas hii ina maswali manne.
  • Jibu maswali mawili pekee. Kila swali lina alamaishirini.
  • Swali la kwanza ni la lazima.
  • Chagua swali jingine lolote kutoka kwa matatu yaliyosalia.
  • Majibu yote yaandikwe katika karatasi ya majibu uliyopewa.
  • Majibu yote yaandikwe katika lughaya Kiswahili.
  1. Wewe ni Waziri wa Elimu nchini mwako.Wizi wa Mitihani ya Kitaifa umekuwa janga kuu.Andika hotuba utakayoitoa mbele ya washikadau wa elimu ilikudhibiti janga hili.
  2. Ajali za barabarani ndizo chanzo cha vifo vingi nchini.Janga hili limekuwa tatizo sugu kulingana naWaziri wa Usalama. Eleza vyanzo mbalimbali vya ajali hizi.
  3. Simulia kisa cha kusisimua kuthibitisha ukweli wa methali: Ajuaye misonoe ni alalaye naye.
  4. Tunga kisa kitakachoisha kwa maneno yafuatayo:
    ... niliyasikiliza maneno yake kwa uchungu kwa kuwa nilielewa fika kwamb maji yaki mwagika hayazoleki.


MARKING SCHEME

  1. LAZIMA
    1. Wazazi wananunukia watoto watahainiwa simu.
    2. Wasimamizi wa mitihani kufungua mitihani kabla ya wakati.
    3. Wanaopanga na kupakia mitihani kutoa siri na hata kuuza .
    4. Walinda usalama kuchukua hongo na kuwapa hifadhi washika dau potovu
    5. Walimu potovu kupewa fursa ya kuongoza watahiniwa katika kujibu maswali
    6. Wakurugenzi wa shule kuwahonga wasimamizi wa mitihani na walimda usalama .

      Jinsi ya kukabiliana na vyanzo vya hivi
      1. Kutengwa kwa wageni shuleni mitihani inapokaribia.
      2. Wazazi kupewa adhabu kali wakipatikana wamewanunulia watoto simu na kuzipeleka shuleni.
      3. Mtahini wa kukatazwa kufanya mitihani yote akipatikana akidanganya au na vifaa vya wizi wa mitihani.
      4. Makasha ya kuhifadhi mitihani kulindwa saa ishirini na nne .
      5. Kila mwalimu mkuu aajibike mitihani katika shule yake.
      6. Magari teule ya kusafirisha mitihani kupewa ulinzi.
      7. Maafisa wa elimu kutoka makao makuu kuzuru shule ghafla ili kutathmini yatakayokuwa yakiendelea .
      8. Washika dau wote wawe na vitambulisho maalum vyenye namba ya wizara .

  2. Vyanzo vya ajali
    1. Magari mabovu.
    2. Hongo kushamiri nchini.
    3. Uchovu kwa madereva /safari ndefu.
    4. Uvunjaji wa sheria za trafiki kwa wananchi na madereva .
    5. Kuwepo kwa madereva ambao wajahitimu.
    6. Kuwepo kwa barabara mbovu.
    7. Kutowepo lwa ishara za barabara .Kuonyesha mfano kubeta kwa barabara.
    8. Ukosefu wa virukio katika sehemu tofauti.

      Jinsi ya kudhibiti ajali
      1. Madereva kupokonywa leseni wakipatikana na makosa.
      2. Adhabu kali kutolewa kwa washiriki wa hongo.
      3. Ukaguzi wa magari kudhibitiwa na maafisa wa trafiki.
      4. Wananchi na madereva kufunzwa upya kuhusu sheria za barabara.
      5. Wenye magari ya masafa marefu kuajiri madereva wawili.
      6. Idara ya kurekebisha barabara kujituma kazini.
  1. Ajuaye misonoe ni yule alalaye naye.
    Maana ya juu ni kuwa anaye jua mikoromo ya mtu ni Yule alalye karibu naye.
    Maana ya ndani
    Anayelijua jambo vizuri ni yule alifanyalo na kulishughulikia kwa kina.
    Mfano anayejua hulka ya mtu fulani ni Yule anayemjua vyema .

  2. Kisa kilemge mhusika ambaye yumo matatani na mambo yamemwendea segemnege .Mhusika huyu hawezi akapata msaada wowote na kwa njia yoyote ile .Kudhibitisha sehemu ya methali maji yakimwagika hayazoleki.

                        

Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI PAPER 1 - 2019 LANJET JOINT MOCK EXAMINATION.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest