KISWAHILI PAPER 1 - KCSE 2019 ALLIANCE MOCK EXAMINATION

Share via Whatsapp

INSHA
SWALI LA LAZIMA

  1. Kama mhariri wa gazeti, andika tahariri ukipongeza hatua ya serikali kupiga marufuku matumizi ya karatasi za sandarusi.
    CHAGUA MOJA:
  2. Eleza njia za kustawisha uchumi uliosambaratika katika eneogatuzi lako.
  3. Pwagu hupata pwaguzi.
  4. Andika insha itakayomalizikia kwa maneno haya.
    “…Nilipokaa mezani kula chakula kitamu, nilikumbuka maisha magumu niliyoyapitia, nikatambua kuwa si rahisi kupata chakula kama hicho bila juhudi maishani”


MARKING SCHEME

  1. Insha hii ni ya tahariri
    Sura ya tahariri ijitokeze
    • Jina la gazeti
    • Siku na tarehe ya tahariri kutokea gazetini
    • Jina la mhariri
    • Mada
    • Mwili wa tahariri unaobeba maudhui

      Maudhui
    • Sandarusi huchafua mazingira zinapotapakaa kila mahali na hivyo kuharibu nakshi ya ardhi
    • Karatasi hizi haziozi na hivyo huharibu rutuba ya udongo
    • Karatasi hizi huwasakama viumbe wa majini kama kasa na wengine na hivyo huathiri afya yao
    • Huleta vifo vya mifugo kama vile ng’ombe walapo karatasi hizo
    • Watoto huweza kujiua kwa kujisakama hasa wanapozivalia kichwani
    • Zichomwapo, moshi huo huchafua hewa na hivyo kuleta maradhi ya mapafu
    • Chembechembe za karatasi hizi zinapoliwa na binadamu huleta saratani.

      Tanbihi :
    • Kadiria hoja za mwanafunzi.
    • Hoja zilenge athari za utumizi wa sandarusi.
  1. Maana ya msamiati
    • Kustawisha – kuimarisha/kuinua/kuboresha/fanikisha/endeleza/fanya iwe na nguvu/madhubuti/imara
    • Uliosambaratika- ulioharibika/uko katika hali mbaya/si mzuri.

      Njia za kutumia
    • Kukomesha ufisadi
    • Ujenzi wa viwanda
    • Kuongeza nafasi za elimu
    • Kuimarisha usalama/ amani

      Utafiti
    • Mikopo kutolewa kwa raia kwa riba ya chini
    • Kuhimiza watu kupenda na kuthamini bidhaa za humu nchini
    • Kuwajibika na kupiga vita uvivu na uzembe
    • Kuimarisha uchukuzi na mawasiliano
    • Kuleta usawa wa kisheria
    • Kuleta uhusiano mzuri kati ya Kenya na nchi zingine.
      Tanbihi: ikiwa mtahini atazungumzia mambo haya katika wakati uliopita atakuwa amejitungia swali atuzwe bakshishi.
  1. Maana
    Pwagu – mwizi
    Pwaguzi – mwizi mkubwa
    Maana – mtu anayejiona ni mjanja kuliko wengine huweza akapata mtu mwingine aliye mjanja kumshinda.
    • Hutumika kwa watu wanaojiona bora zaidi kuliko wengine.
    • Mtahiniwa aandike kisa au visa kuthibitisha ukweli wa methali
    • Kisa au visa vionyeshe mtu mjanja kukutana na aliye mjanja zaidi
    • Mtahiniwa azungumzie pande zote mbili
    • Aweze kuanzia upande wowote
  1. Mtahiniwa azungumzie maisha yake – safari ya maisha
    • Awe na shida katika maisha hayo
    • Afanye juhudi ili kujitoa katika shinda hizo
    • Aweze kupata mafanikio hatimaye

      Tanbihi:
      Atakayeongeza, kutoa au kutoandika maneno katika kimalizio achukuliwe kuwa amepotoka kimtindo.

MWONGOZO WA KUDUMU
UTANGULIZI.

Karatasi hii imedhamiria kutathmini uwezo wa mtahiniwa wa kuwasiliana na msomaji na kuwasilisha ujumbe kimaandishi,akizingatia mada aliyopewa. Mawasiliano haya yatategemea ukwasi wa lugha ya mtahiniwa, kwa mfano, kutunga sentensi sahihi zenye mtiririko mzuri kimawazo, lugha ya kuvutia na yenye mawazo asilia, ubunifu mwingi na hati nadhifu. Kwa kutegemea maagizo ya swali lenyewe na umahiri wa lugha, ni lazima kutilia mkazo mtindo, mada na uwezo wa mtahiniwa kufuata maagizo vilivyo. Mtahini lazima aisome insha yote huku akizingatia sarufi, hijai, hoja, msamiati na mtindo ili aweze kuikadiria kwa kurejelea viwango mbalimbali vilivyopendekezwa. Viwango vyenyewe ni A, B, C na D kutegemea uwezo wa mtahiniwa.

VIWANGO MBALIMBALI.
KIWANGO CHA D KWA JUMLA MAKI 01-05.

  1. Insha haieleweki kwa vyovyote vile ama uwezo wa mtahiniwa wa kutumia lugha ni hafifu sana, hivi kwamba mtahinilazima afikirie kile mtahiniwa anachojaribu kuwasilisha.
  2. Mtahiniwa hana uwezo wa kutumia maneno ya Kiswahili kwa njia inayofaa.
  3. Lugha imevurugika, uakifishaji haufai na insha ina makosa ya kila aina.
  4. Kujitungia swali na kulijibu.
  5. Insha ya urefu wa robo ikadiriwe hapa.

NGAZI MBALIMBALI ZA KIWANGO CHA D.
D- (D YA CHINI) MAKI 01-02.

  1. Insha haina mpangilio maalum na haieleweki kwa vyovyote vile.
  2. Kujitungia swali tofauti na kulijibu.
  3. Kuandika kwa lugha isiyo Kiswahili au kuchanganya ndimi.
  4. Kunakili swali au maswali na kuyakariri.
  5. Kunakili swali au kichwa tu.

D WASTANI MAKI 03.

  1. Mtiririko wa mawazo haupo.
  2. Mtahiniwa amepotoka kimaudhui.
  3. Matumizi ya lugha ni hafifu mno.
  4. Kuna makosa mengi ya kila aina.

D+ (D YA JUU) MAKI 04-05.

  1. Insha ya aina hii hukuwa na makosa mengi ya kila aina, lakini unaweza kutambua kile ambacho mtahiniwa anajaribu kuwasilisha.
  2. Hoja hazikuelezwa kikamilifu/ mada haikukuzwa vilivyo.
  3. Mtahiniwa hana uhakika wa matumizi ya lugha.
  4. Mtahiniwa hujirudiarudia.
  5. Insha itakayozingatia sura lakini ikose maudhui ikadiriwe hapa.

KIWANGO CHA C KWA JUMLA MAKI 06-10.

  1. Mtahiniwa anajaribu kuishughulikia mada japo hakuikuza na kuiendeleza vilivyo.
  2. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe kwa njia isiyovutia
  3. Mtahiniwa anaakifisha sentensi vibaya.
  4. Mtiririko wa mawazo unaanza kujitokeza japo kwa njia hafifu.
  5. Insha ina makosa mengi ya sarufi, ya msamiati na ya tahajia (hijai).

    C- (C YA CHINI) MAKI 06-07.
  1. Mtahiniwa ana shida ya kuwasilisha na kutiririsha mawazo yake.
  2. Mtahiniwa hana msamiati wa kutosha wala miundo ya sentensi ifaayo.
  3. Mtahiniwa anafanya makosa mengi ya sarufi, ya hijai na ya msamiati na insha yake haieleweki kwa urahisi.

    C WASTANI MAKI 08.
  1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe lakini kwa njia hafifu.
  2. Dhana tofauti tofauti hazijitokezi wazi.
  3. Mtahiniwa hana ubunifu wa kutosha.
  4. Mtiririko wa mawazo ni hafifu na hana ufundi wa lugha unaofaa.
  5. Anajaribu kushughulikia mada aliyopewa.
  6. Mtahiniwa ana shida ya uakifishaji.
  7. Mtahiniwa anafanya makosa mengi ya sarufi, ya hijai na ya msamiati lakini bado insha inaeleweka.

    C+ (C YA JUU) MAKI 09-10.
  1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri akizingatia mada lakini kwa njia isiyo na mvuto.
  2. Dhana tofauti tofauti zimejitokeza japo kwa njia hafifu.
  3. Kuna mtiririko wa mawazo japo hana ufundi wa lugha unaofaa.
  4. Misemo na methali zimetumika kwa njia hafifu.
  5. Ana shida ya uakifishaji.
  6. Kuna makosa ya sarufi, ya msamiati na ya hijai yanayoathiri mtiririko wa mawazo.

KIWANGO CHA B KWA JUMLA MAKI 11-15

  1. Mtahiniwa anaonyesha hali ya kuimudu lugha.
  2. Mtahiniwa anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi vizuri.
  3. Mtahiniwa ana uwezo wa kutumia lugha kwa ufasaha.
  4. Mada imekuzwa na kuendelezwa kikamilifu.
  5. Insha ya urefu wa robo tatu ikadiriwe katika kiwango hiki.

Ngazi mbalimbali za kiwango cha B.
B- (B YA CHINI) MAKI 11-12

  1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri kwa kueleza hoja tofauti tofauti akizingatia mada.
  2. Mtahiniwa ana mtiririko mzuri wa mawazo.
  3. Mtahiniwa anatumia mifano michache ya msamiati unaovutia.
  4. Makosa yanadhihirika kiasi.

B WASTANI MAKI 13

  1. Mtahiniwa anadhihirisha hali ya kuimudu lugha.
  2. Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika akizingatia mada.
  3. Mtahiniwa anateua na kutumia mifano michache ya msamiati mwafaka.
  4. Sarufi yake ni nzuri.
  5. Makosa ni machache/ kuna makosa machache.

B+ (B YA JUU) MAKI 14-15

  1. Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika na anajieleza waziwazi.
  2. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe kwa njia inayovutia na kwa urahisi akizingatia mada.
  3. Mtahiniwa ana mchanganyiko mzuri wa msamiati unaovutia.
  4. Sarufi yake ni nzuri.
  5. Uakifishaji wa sentensi zake ni mzuri.
  6. Makosa ni machache ya hapa na pale.

KIWANGO CHA A KWA JUMLA MAKI 16-20

  1. Mtahiniwa ana ubunifu wa mawazo yanayodhihirika na kutiririka akizingatia mada.
  2. Mtahiniwa anadhihirisha ujuzi wa lugha yenye mnato.
  3. Ana uwezo wa kutumia tamathali za usemi ili kutoa hisia zake kwa njia bora na kwa urahisi.
  4. Umbuji wake unadhihirisha ukomavu na ukakamavu wake kimawazo.
  5. Insha ina urefu kamili.

USAHIHISHAJI NA UTUNZAJI KWA JUMLA.
Mtahini ni sharti aisome insha yote akizingatia vipengee muhimu. Vipengee hivi ni maudhui, msamiati, mtindo, sarufi na hijai.

MAUDHUI.

Maudhui ni hoja au mambo yanayozungumziwa, kuelezewa au kuhadithiwa kwa mujibu wa mada iliyoteuliwa. Maudhui ndio hasa uti wa mgongo wa insha yoyote ile. Ubunifu wa mtahiniwa hukisiwa kwa kutathmini uzito wa maudhui yake kulingana na mada teule.

MSAMIATI.

Msamiati ni jumla ya maneno yatumiwayo katika lugha husika. Mtahiniwa anatarajiwa kutumia msamiati unaooana na mada teule. Kutegea ukwasi wa lugha alionao, mtahiniwa anatarajiwa kuikuza mada kwa kuifinyanga lugha kiufundi. Ni muhimu kuelewa kwamba kutokana na maendeleo na ukuaji wa teknolojia na mawasiliano, maneno mapya yanaibuka kila uchao.

MTINDO.

Mtindo unahusu mambo yafuatayo:

  • Mpangilio wa kazi kiaya.
  • Mtiririko na mshikamano wa mawazo kiaya na katika insha nzima.
  • Hati nzuri na inayosomeka kwa urahisi
  • Matumizi ya tamathali za usemi, kwa mfano methali, misemo, jazanda na kadhalika.
  • Kuandika herufi vizuri kwa mfano Jj, Pp, Uu, Ww na kadhalika.
  • Sura ya insha
  • Unadhifu wa kazi ya mtahiniwa.

SARUFI.

Sarufi ndio msingi wa lugha. Ufanisi wa mawasiliano hutegemea uwezo wa mtahiniwa wa kutunga sentensi sahihi zenye uwiano wa kisarufi. Mtahini ataonyesha makosa yote ya sarufi yaliyo katika insha anayosahihisha. Makosa ya sarufi huweza kutokea katika:

Matumizi ya alama za uakifishaji.

  1. Kutumia herufi kubwa na ndogo mahali pasipofaa.
  2. Matumizi yasiyofaa ya ngeli na viambishi, viunganishi, nyakati, hali, vihusiano na kadhalika.
  3. Mpangilio wa maneno katika sentensi.
  4. Mnyambuliko wa vitenzi na majina.
  5. Kuacha neno linalohitajika au kuongeza neno lisilohitajika katika sentensi.
  6. Matumizi ya herufi kubwa katika:
  7. Mwanzo wa sentensi.
  8. Majina ya pekee.
  9. Majina ya mahali, miji, nchi, mataifa na kadhalika.
  10. Siku za juma, miezi n.k
  11. Mashirika, masomo,vitabu n.k
  12. Jina la mungu.
  13. Majina ya kutambulisha hasa wanyama wa kufugwa, kwa mfano yale ya mbwa- Foksi, Jak, Popi, Simba,
    Tomi na mengineyo.

MAKOSA YA HIJAI/TAHAJIA.
Haya ni makosa ya maendelezo. Mtahini anashauriwa asahihishe huku akiyaonyesha yanapotokea kwa mara ya kwanza tu.
Makosa ya tahajia huweza kutokea katika:

  • Kutenganisha neno kwa mfano ‗aliye kuwa‘
  • Kuunganisha maneno kwa mfano ‗kwasababu‘
  • Kukata silabi visivyo afikapo pambizoni kama vile ‗ngan - o‘.
  • Kuandika herufi isiyofaa kwa mfano ‗ongesa‘ badala ya ‗ongeza‘
  • Kuacha herufi katika neno kwa mfano ‗aliekuja‘ badala ya ‗aliyekuja‘
  • Kuongeza herufi isiyohitajika kama vile ‗piya‘ badala ya ‗pia‘
  • Kuacha alama inayotarajiwa katika herufi kama vile j i
  • Kukosa kuandika kistari cha kuendelezea neno afikiapo pambizoni au kukosa kukiandikia mahali pasipofaa.
  • Kuacha ritifaa au kuiandikia mahali pasipofaa, kwa mfano ngombe, ngom‘be, n‘gombe, ngo‘mbe n.k
  • Kuandika maneno kwa kifupi kama vile k.v, k.m, v.v, n.k na kadhalika.
  • Kuandika tarakimu kwa mfano 27-08-2010.

    UKADIRIAJI WA UREFU WA INSHA.
  • Maneno 9 katika kila mstari – ukurasa moja na nusu.
  • Maneno 8 katika kila mstari – ukurasa moja na robo tatu.
  • Maneno 7 katika kila mstari – kurasa mbili.
  • Maneno 6 katika kila mstari – kurasa mbili na nusu.
  • Maneno 5 katika kila mstari – ukurasa mbili na robo tatu.
  • Maneno 4 katika kila mstari – kurasa tatu na robo tatu.
  • Maneno 3 katika kila mstari – kurasa nne na nusu.
Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI PAPER 1 - KCSE 2019 ALLIANCE MOCK EXAMINATION.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest