KISWAHILI PAPER 3 - KCSE 2019 ALLIANCE MOCK EXAMINATION

Share via Whatsapp
  1. HADITHI FUPI       ALAMA 20
    TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE :Alifa Chokocho Na Dumu Kayanda
    Mtihani wa Maisha
    1. “..Acha nijiondokee duniani niwaachie wafanisi wafanikie.”
    2. Eleza muktadha wa dondoo hili.          Alama 4
    3. Taja na ufafanue sifa tatu za msemaji.          Alama 6
    4. Eleza jinsi maisha ya msemaji yanavyoafiki anwani ya hadithi.        Alama 10
  2. RIWAYA                CHOZI LA HERI :   Assumpta Matei                                ALAMA 20
    1. Eleza jinsi maudhui ya ufisadi yalivyoshughulikiwa katika riwaya ya Chozi la Heri. Alama 20
    2. “…liandikwalo ndilo liwalo? Since when has man ever changed his destiny?”
    3. Eleza muktadha wa dondoo hili.          Alama 4
    4. Bainisha mbinu tatu za kimtindo zinazojitokeza katika dondoo hili.          Alama 6
    5. Kwa kuzingatia hoja kumi, jadili jinsi ambavyo hali ya, “ liandikwalo ndilo liwalo’’, inavyojitokeza katika Chozi la Heri.        Alama 10.
  3. TAMTHILIA         KIGOGO : Pauline Kea                                                       ALAMA 20
    1. “Utawala wa Majoka katika jimbo la Sagamoyo umejaa sumu ya nyoka.” Jadili. Alama 20
    2. Eleza jinsi mbinu zifuatazo zilivyotumika katika tamthilia ya Kigogo
      1. Kinaya      Alama 6
      2. Majazi      Alama 8
      3. Jazanda      Alama 6
  4. FASIHI SIMULIZI                                                                                                ALAMA 20
    1.  
      1. Eleza aina tano za wahusika wa fasihi simulizi.                                        Alama 10
      2. Eleza sifa za wahusika wa mighani.                                                         Alama 10
    2.  
      1. Eleza namna amabavyo hadhira wanahusishwa katika utambaji.Toa hoja nne.   Alama 8
      2. Taja na ueleze sifa nne bainifu za hadithi.                                                      Alama 4
      3. Taja viungo vinavyopambanua muundo wa nyimbo katika jamii               Alama 4
      4. Andika majukumu manne ya nyimbo katika jamii                                       Alama 4
  5. USHAIRI                                                                                                               ALAMA 20
    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
    Zitavuma,
    Zitakoma,
    Nitakwima,
    Mti-mle.
    Na muda nikisimama,
    Nitatongoa nudhuma,
    Kwa tenzi zilizo njema,
    Nilisifu mti – mle.
    Tazipanga tathlitha, tungo zilizo na hekima,
    Za huba na thiatha, za kuburudi mitima,
    Mashairi mabuthutha, musome mnaosoma.
    Mti nishainukia,namea kuwa mzima,
    Mizizi yadidimia, ardhini imeuma,
    Nanena kitarbia, tungo zilizo adhama
    Japo ni tungo za zama, mti-mle hutumia.
    Zingavuma zitapusa, pepo kali zitakoma,
    Dharuba kinitikisa, mti-mle huinama,
    Huyumba nikaziasa, matawi yakakingama,
    Gharika ikishapisa, hurudi nikawa wima,
    Na tungo za takhimisa, mti-mle huzipima.

    Maswali
    1. Shairi hili ni la kimapokeo. Toa sababu mbili kuunga kauli hii.                                   (Alama.2)
    2. Taja bahari kuu ya ushairi ambayo imetumiwa na mshairi. Fafanua.                        (Alama.2)
    3. Fafanua dhamira ya mshairi.       (Alama.2)
    4. Kwa kutoa mifano bainisha tamathali mbili za usemi zilizotumika katika shairi hili. (Alama.2)
    5. Eleza jinsi mshairi ametumia idhini ya ushairi katika utungo huu.                             (Alama.2)
    6. Andika ubeti wa nne kwa lugha natharia.   (Alama.4)
    7. Mshairi anamaanisha nini anaposema ‗zingavuma zitapusa, pepo kali zitakoma,‘ (Alama.2)
    8. Eleza toni ya shairi hili.         (Alama.2)
    9. Eleza maana ya msamiati ufuatao.
      1. Nitatongoa
      2. Zitapusa.   (Alama.2)


MARKING SCHEME

  1. Swali la kwanza
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. Alama 4
      • Ni mawazo ya Samweli
      • Akiwa kando ya bwawa
      • Anataka kujitosa majini
      • Alikuwa amefeli mtihani na hivyo kutamauka. 1x4=4
    2. Taja na ufafanue sifa tatu za msemaji. Alama 6
      • Ni msaliti-amelipiwa karo asome lakini badala ya kusoma anafanya mahoka na hivyo kufeli
      • Ni mwoga- anaonyesha kuogopa mbele ya mwalimu mkuu alipoenda kuchukua matokeo yake ya mtihani/anasitasita kuongea na kujibu maswali aliyoulizwa na mwalimu mkuu.
      • Ni mtiifu-alitii mamake alipomwambia waende nyumbani
      • Mwenye hasira-anakasirishwa na wanafunzi wengine walipotaka matokeo yake ya mtihani.
      • Ni msiri-hataki mtu yeyote ajue matokeo yake ya mtihani/alitaka kujiua kisiri
      • Ni mwongo-aliwadanganya wazazi wake kuwa hakupata matokeo kwa sababu hakuwa amekamilisha karo/alimdanganya ninake kuwa alikuwa mwerevu shuleni.
      • Ametamauka- alitaka kujiua kwa kujitosa majini alipofeli mtihani.
      • Ni mwenye maringo/kiburi-anajigamba kuwa mwalimu mkuu angeaibika kwa kuwa aliona amefaulu mtihani.
      • Mshirikina-anasema hakukutana nap aka mweusi alipokuwa anaenda kufanya mtihani hivyo hangefeli.
         3x2=6
    3. Eleza jinsi maisha ya msemaji yanavyoafiki anwani ya hadithi. Alama 10
      • Samweli anasoma shule ambayo dadake Bilha na Mwajuma walisoma na kufaulu.Kwa vile ni mvulana anatarajia kufaulu lakini anafanya mahoka shuleni hadi anafeli.Kwa hivyo alifeli mtihani wa shule na wa Maisha kwa sababu hakuona matumaini mbele yake.
      • Samweli alimdanyanya mamake kuwa alikuwa mwerevu shuleni kumbe sivyo.Alitarajia kuendeleza uhusiano huu baada ya kufaulu mtihani lakini anafeli.Nina labda angemshuku, angejua ukweli kuwa mwanawe hakuwa mwerevu na hivyo akamfeli mamake na kufeli maishani.
      • Samweli kutaka kujitosa majini ni kwa sababu ya kupoteza matumaini.Alikuwa na maoni kuwa ili awe na Maisha mazuri ilimlazimu apite mtihani na hivyo kufeli mtihani, ilimaanisha kuwa alifeli maishani.
      • Wazazi wa Samweli walitumia raslimali yao yote kwa kumlipia karo wakitarajia angewaokoa kutoka lindi la umaskini kama mtoto wa kiume.Anapofeli shuleni anafeli pia katika Maisha na hivyo hangewaauni wazazi.
      • Baba Samweli anamletea Kamba ya kujinyonga kwa sababu ya kufeli shuleni kuonyesha kuwa pia katika Maisha alikuwa amefeli na hakustahili kuishi.
        5x2=10
  2. CHOZI LA HERI
    1. Eleza jinsi maudhui ya ufisadi yalivyoshughulikiwa katika riwaya ya Chozi la Heri.
      -Nyumba za maskini zinapobomolewa Tononokeni, mabwanyenye wanaanza kutoa milungula ili nyumba zao zisibomolewe.
      -viongozi wanapowapoka raia ardhi zao, raia walalamikapo hupozwa roho kwa kuambiwa kuwa kumeundwa tume za kuchunguza kashfa hizo.
      -wakati wa uchaguzi, wanasiasa wanawahonga raia ili wawachague, Papa aliwahonga kwa pesa na unga.
      -Hazina ya Jitegemee inalenga kuwafaidi vijana wa taifa la Wahafidhina lakini ukabila na unasaba unapoliandama hawanufaiki.
      -nyumba zinazolengwa kupewa maskini katika mtaa duni wa Sombera zinachukuliwa na viongozi baada ya ujenzi kukamilika.
      -familia ya Bwana Kute inajigawa na kuwa familia tatu ili wapate msaada mwingi kuliko wakimbizi wengine.
      -Serikali inabomoa majengo ya raia katika mtaa wa Tononokeni na Zari bila kuwafidia.
      -raia wanaiba mafuta ya lori ili wawauzie madereva wa wakubwa au walinda usalama ili wayauze kwingine.
      -madereva wa wakubwa wanafyonza mafuta kwa mirija na kuwauzia wenye magari ya kibinafsi
      -askari wananunua mafuta ambayo yameibiwa na kuyauza kwingine
      -matapeli wanawauzia wananchi wenzao ardhi ya makaburi bila kujali
      -raia matapeli wanauza ardhi zao mara mbili kwa watu wawili tofauti na kutoa hati miliki mbili-halali na bandia
      -viongozi wananyakua ardhi iliyotengewa upanzi wa chakula na kujenga nyumba zao mf. Madhabahu kwenye mlima wa Nasibu yalinyakuliwa ili kujenga hoteli za kitalii.
      -vigogo wanauza mahindi yanayotolewa na mataifa ya nje kama msaada.
      -vigogo wanawalazimisha wataalamu wa maswala ya lishe kuidhinisha uuzaji wa mahindi yaliyoharibika.
      -viongozi wanapasua mbao na kuchoma makaa katika msitu wa mamba baada ya msitu huo kupigwa marufuku.
      -viongozi wanahamisha wakimbizi kutoka msitu wa Mamba na kuanza kuvuna mahindi yaliyopandwa na wakimbizibadala ya kuwaruhusu kuyavuna kabla ya kuwaondoa.
      -Baada ya Fumba kumpachika mimba mwanafunzi wake, aliachishwa kazi kwa muda kisha akahamishwa kwinginehivyo kumsababishia Rehema kutopata haki yake.
      -Baadhi ya walinda usalama wanashirikiana na wahalifuili wagawane mali iliyoibiwa.
      -magari ya vigogo hayaondolewi barabarani na askari licha ya kuwa mabovu.
      -Buda anawahonga askari wanapoenda nyumbani kwake kumtia mbaroni (biashara ya ulanguzi wa mihadarati)
      Tathmini jibu la mwanafunzi.                                                              Zozote 20x1=10
    2. “…liandikwalo ndilo liwalo? Since when has man ever changed his destiny?”
      1. Eleza muktadha wa dondoo hili. Alama 4
        • Maneno ya Terry
        • Akimwambia Ridhaa
        • Nyumbani kwao
        • Baada ya kugundua kuwa anaamini ushirikina
          Au
        • Ni mawazo ya Ridhaa akikumbuka maneno aliyoambiwa na mkewe Terry
        • Kwa sababu ya kuamini kuwa milio ya bundi na kereng’ende huashiria jambo Fulani lingefanyika.
        • Yuko kando ya vifusi vya nyumba yake iliyochomwa
        • Baada ya familia yake kuchomewa ndani
          4x1 =4
      2. Bainisha mbinu tatu za kimtindo zinazojitokeza katika dondoo hili.     Alama 6
        • Methali-liandikwalo ndilo liwalo
        • Kuhamisha ndimi/msimbo-kauli ya kutumia sentensi nzima kwa lugha nyingine.
          Since when has man ever changed his destiny?
          Tanbihi: mbinu hii si kuchanganya ndimi.Atakayeandika hivi asituzwe.
        • Swali la balagha- “…liandikwalo ndilo liwalo?
          Since when has man ever changed his destiny?”
           3x2=6
      3. Kwa kuzingatia hoja kumi, jadili jinsi ambavyo hali ya, “ liandikwalo ndilo liwalo’’, inavyojitokeza katika Chozi la Heri. Alama 10.
        -Neema na Mwangemi wanajitahidi kupata mtoto lakini hawafanikiwi na wanaishia kumpanga Mwaliko.
        -Wafuasi wa Mwanzi wanajaribu kushinda ushindi wa Mwekevu lakini wanashindwa.
        -Kaizari anajitahidi kuzuia wahuni wasiwabake binti zake lakini wanamzidi nguvu na kuwabaka.
        -Lunga anajitahidi kumrithia na kumpendeza mkewe Naomi lakini hatimaye anamtoroka na kumwachia Watoto
        -Kiriri anampinga Annette asiende ughaibuni lakini anampuuza na kuhamia huko.
        -Kiriri anawasihi wanawe warudi nyumbani lakini waliendelea kuishi ughaibuni hata baada ya kukamilisha masomo yao.
        -nyanyake Pete anajizatiti kupinga ndoa ya Pete lakini hatimaye Pete anaozwa.
        -Kipanga anataka kuambiwa babake halisi baada ya aliyemdhania kuwa babake kumkana lakini mamake hakumwambia.
        -hata baada ya mabwanyenye kutoa hongo ili nyumba zao zisibomolewe katika mtaa wa Tononokeni, zianbomolewa.
        -Dick anakataa kutumiwa na Buda kulangua dawa za kulevya lakini anamtishia na baadaye kuuza dawa za kulevya.
        -Naomi alimtoroka Lunga kwa sababu ya umaskini lakini anaishia kuteseka Zaidi na baadaye kufa
        -Amize Lucia wanajizatiti kupinga ndoa ya Lucia lakini baadaye Lucia anaolewa.
        -Wanaume wanatishia kumtusi Mwekevu anapojitosa siasani ili kumvunja moyo lakini anavumilia mpaka anachaguliwa kuwa kiongozi wa Wahafidhina.
        -Pete anakunywa dawa ya kuua panya ili afe lakini anapelekwa katika kituo cha afya cha Mwanzo Mpya na kuendelea kuishi.
        -Pete anajaribu kuavya mimba ya mtoto wake wa pili na wa tatu lakini anaishia kuwazaa Watoto hawa.
        Zozote 10x1=10
  3. KIGOGO : Pauline Kea
    1. “Utawala wa Majoka katika jimbo la Sagamoyo umejaa sumu ya nyoka.” Jadili. Alama 20
      -unyakuzi wa ardhi-Majoka na mshauri wake wamenyakua soko la chapakazi
      -mauaji ya watu-vijana watano wanuawa wakati wa maandamano
      -vitisho-wanaharakati wanaompinga majoka wanatishiwa kwa vikaratasi vinavyowaamuru wahame makazi yao
      -kuangamiza wapinzani wake-Jabali aliuawa ili kusambaratisha chama chake na Tunu nusura auawe anapotetea haki.
      -ukatili- majoka hadhamini uhai wa watu hivyo anaamuru wapigwe risasi bila kujali wana haki ya kuwachagua viongozi wanaowataka
      -tengatawala-analeta uhasama katika jamii mf. Kati ya Sudi na Boza ili atimize malengo yake ya kisiasa-Ngurumo na kundi lake la walevi wameshatiwa sum una utawala wa majoka.
      -kuzorota kwa maendeleo-Sagamoyo imetimiza miaka sitini ya uhuru lakini wako nyuma kimaendeleo.
      -ubadhirifu-Majoka anatumia mamlaka yake kujilimbikizia mali, kampuni, hoteli, academy.
      -ufisadi-mamapima anatoa hongo ya uroda kwa ngurumo ilia pate mradi wa kuoka keki ya uhuru
      -elimu duni-Elimu inayotolewa kwa vijana inawalemaza badala ya kuwaaandaa kujenga nchi baada ya masomo.
      -utawala wa kiimla- Majoka anataka kuendelea kutawala ingawa ameshindwa kutawala vyema/anawaua wapinzani wake
      -utabaka-kuna tabaka la mabwanyenye na la wanyonge ambapo la mabwanyenye linanyonya la wanyonge
      -uvivu/ubwete- katika kuadhimisha miaka sitini ya uhuru, wananchi wanapewa muda wa mwezi mmoja wa kupumzika.
      -ukiritimba-Majoka anamiliki mali nyingi, raslimali na miradi mikubwa
      -Ukoloni mamboleo- Sagamoyo ina mikopo mingi ambayo italipwa kwa muda mrefu hivyo kuwa wategemezi wan chi za ulaya.
      -ufujaji wa mali ya umma-mikopo inayochukuliwa haitumiki vizuri.
       10x2 =20
    2. Eleza jinsi mbinu zifuatazo zilivyotumika katika tamthilia ya Kigogo

      Kinaya alama 6
      -anwani ni kinaya-Kigogo ambaye ni mheshimiwa lakini Majoka haheshimiki kwa kukiuka maadili
      -ni kinaya kuamrisha askari wapige waandamanaji risasi ilhali ndio unao waongoza na kuwategemea wakupe kura
      -wafanyabiashara wanatozwa kodi kubwa wanapouzia katika soko la chapakazi hivyo ni kinaya kwa kiongozi kulinyakua soko hili ili kupunguza kodi.
      -wanasagamoyo kujivunia kampuni kubwa ya uzalishaji wa sumu ya nyoka ambao utawaangamiza.
      -wanasagamoyo kusherehekea miaka sitini ya ukombozi ilhali wao bado ni watumwa katika nchi yao-vitoza machozi, risasi, marungu n.k.
      -Ashua anapomgeuka Sudi na kumlaumu kuwa hatimizi wajibu wake katika kumtunza ilhali ndiye anamtoa korokoroni.
      -Boza kumsifu Asiya kuwa mke mwema ilhali wana uhusiano na Ngurumo
      -shule ya kifahari Majoka Academy kushindwa kutoa wanafunzi wazuri na wanaishia kuwa makabeji.                                                                                                                  6x1=6

      Majazi alama 8
      -Majoka-nyoka kubwa linalomeza wanasagamoyo
      -Tunu-Kitu cha dhamani/zawadi kwa wanasagamoyo, anajitolea kupigania haki
      -Sudi-bahati- ana talanta ya uchongaji
      -Husda -huegemea kuwa na ubaya juu ya mtu.Yeye ana chuki na kinyongo dhidi ya Majoka na kumfananisha na chui katika Ngozi ya kondoo/ana chuki na wivu kwa Ashua
      -Ngurumo-radi/mngurumo wa simba-anatenda vitendo vya kutisha. Mf : ana cheche za matusi, miongoni mwa wahuni waliomvamia Tunu na kumvunja mguu.
      -Mamapima-anapima pombe kwa kipimo
      -Sagamoyo-mahali pa mateso
      -Chapakazi-bidii
       8x1=8

      Jazanda alama 6
      -Ramani ya Maisha-kumaanisha maamuzi ya mtu yatakwenda sambamba na Maisha atakayoishi-tajiri/maskini
      -kigogo- kurejelea mtu mashuhuri kwa mfano Sudi anasema Kigogo hachezewi
      -keki ya uhuru-kurejelea raslimali za jimbo la Sagamoyo
      -rubani-kueleza viongozi wan chi wanaoshindwa kuongoza na kufanya chombo kiende mrama.
      -kisima kuingia paka na maji hayanyweki-kisima ni uongozi, kuingia paka ni kuharibika kwa mambo, maji hayanweki ni kutotawalika.
      -shamba-kumrejelea Ashua mke wa Sudi, Chopi anamwambia Sudi kuwa ameshindwa kulima shamba.
       6x1=6
  4.  
    1.  
      1. Msimuliaji/fanani
        Wasikilizaji
        Wanyama na viumbe wengine
        Binadamu wengine
        Vitu visivyo hai
        Kutaja Alama 1
        Kueleza kwa kutumia mfano Alama 1
      2. Sifa za wahusika wa mighani
        • Mashujaa wa jamii
        • Wameheshimika sana katika jamii
        • Huwa na wapinzani wao ambao hujulikana kama majahili na huwa na hisia za kibiinafsi
        • Majahili huwa wakatili na wakandamizaji
        • Mapambano huwa baina ya majagina na majahili
        • Majagina hufaulu/hushinda
        • Wahusika hupewa sifa zisizo za kawaida
        • Huwa watu wa miraba minne
          Hoja zozote 5(5x2)
          Kutaja Alama 1
          Kufafanua Alama 1
          Alama 2 kila hoja                   
    2.  
      1. Eleza namna ambavyo hadhira wanahusishwa katika utambaji.Toa hoja nne.(ala. 8)
        • Kuulizwa kutoa mafunzo ya hadithi
        • Kuimba
        • Kuchekeshwa
        • kupiga makofi
        • Kuulizwa maswali yanayoilenga hadithi
        • Kukamilisha sentensi za mdokezo
        • kuchangia maendeleo ya hadithi      
        • kutambua milio katika utambaji     4x2=8
      2. Taja na ueleze sifa nne bainifu za hadithi.      (ala.4)
        • Hutumia lugha elezi
        • Hufunza maadili fulani katika jamii
        • Huwa na mwanzo na vimalizio maalumu
        • Hubeba utamaduni wa jamii husika
        • Huambatana na mazingira ya jamii husika
        • Lengo kuu ni kuadilisha jamii
        • wahusika huwa wachache
        • urefu wake hutegemea umri wa hadhira
           4x1=4
      3. Taja viungo vinavyopambanua muundo wa nyimbo katika jamii          (Alama 4)
        • Hutumia tamaduni za usemi
        • Misitari/mafungu hurudiwarudiwa
        • Hugawanyika katika mafungu/beti/stanza
        • Mafungu yana mistari/mishororo
        • Hutumia lugha ya mkato
        • Mistari ina silabi
        • Baadhi ya nyimbo zina urari wa vina
          Zozote 4x1=Alama 4
      4. Andika majukumu manne ya nyimbo katika jamii                              (Alama 4)
        • Hutambulisha jamii
        • Hutakasa na kutoa hisia za binadamu
        • Huhifadhi na kuendeleza utamaduni
        • Hutumbuiza/huburudisha/hufurahisha
        • Hupitisha amali kutoka kwa kizazi hadi kingine
        • Huhamasisha na kuchochea hisia
        • Huakisi ukwasi wa tamaduni
        • Hukuza ubunifu/vipawa k.v uimbaji
          Zozote 4x1=Alama 4
  5. Ushairi
    1.  
      1. Lina beti
      2. Lina mishororo
      3. Lina vina
      4. Lina mizani
      5. Ubeti wa tatu, nne na wa tano una vipande (ukwapi, utao)                        za kwanza 2 x 1 = 2
    2. Sakarani
      Lina zaidi ya aina moja ya bahari za ushairi. Utenzi, tarbia, tathlitha na takhimisa Kutaja 1
      Ufafanuzi 1 Jumla 2
    3. Kujinaki, au kujisifu kwa uwezo wake wa kutunga mitindo tofauti tofauti ya mashairi (Alama. 2)
      1. Tanakuzi / kinyume/ ukinzani kama vile - Zitavuma – zitakoma
        zingaruma – zitapusa/zitakoma
      2. Jazanda – mti-mle – Bingwa wa ushairi
        Gharika / Dharuba – changamoto anazopitia katika utunzi
      3. Lakabu (msimbo) - Mti – mle (amejiita mti-mle) Alama 2
        1. Inkisari - Tazipanga – Nitazipanga
          -Na nena – ninanena
          -Kuburudi – Kuburundisha
        2. Mazida -Nishainukia – nishainuka
        3. Lugha ya kikale –huba – mapenzi.
          tongoa - sifia
        4. Lahaja m.f thiatha – badala ya siasa
          Yoyote 1 –kutaja 1
          Mfano 1 Alama 2
    4. Mimi mti nina ujuzi mpana wa utunzi
      Nimekita mizizi yangu barabara katika taaluma hii. Naweza kutunga mashairi aina ya tarbia ambazo ni ungo za heshima. Ingawa ni tungo za zamani, mimi, Mti - Mle huzitunga Alama. 4
    5. Hata kukiwako na matatizo /upinzani/changamoto aina yoyote kutakuwa na mwishi wake. Alama 2
    6.  
      1. Kuna dharau – kuwaita mashairi ni pepo ambazo zitafuma na kukoma
      2. Kuna majivuno -Anajiita mti – mle
    7.  
      1. Nitatongoa – Nitasifu/Nitaeleza
      2. Zitapusa – acha, / koma                                                              2x1=2
Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI PAPER 3 - KCSE 2019 ALLIANCE MOCK EXAMINATION.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest