KISWAHILI PAPER 2 - KCSE 2019 ALLIANCE GIRLS MOCK EXAMINATION (WITH MARKING SCHEME)

Share via Whatsapp
  1. UFAHAMU (ALAMA 15)
    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanavyofuata

    Wakati wananchi katika kila pembe ya dunia waliadhimisha siku ya wapendanao maarufu kama “Valentine Day,” kwa mitindo mbalimbali, hali hiyo ilikuwa tofauti kwa baadhi ya wanaume nchini Kenya, baada ya kulalamika kuhusu kunyanyaswa na wake zao.

    Kulingana na mwenyekiti wa chama cha kutetea haki za wanaume nchini, idadi ya wanaume wanaopigwa na wake zao imeongezeka mno.Alisema juzi kuwa utafiti wa chama chake umeonyesha kuwa harakati za kumpa mwanamke uwezo zimeathiri maadili na kusababisha kuwadharau wanaume. Mwanaharakati huyo alidai kuwa tatizo hilo limechochewa zaidi na hali ya kuwa wanawake wengi sasa wanakipato kikubwa kuliko waume zao.

    Mwishoni wa mwezi polisi walimtia mbaroni mwanamke mmoja mjini Nyeri,baada ya kumshambulia mumewe na kumjeruhi kwa panga.Mwanamme huyo bado anapata matibabu hospitalini. Yeye alirudi nyumbani kama amevaa miwani ndipo akakatwa katwa usoni na uchunguzi kuhusu tukio hilo bado unaendelea.

    Inadaiwa kuwa zaidi ya wanaume 460,000 walinyanyaswa na wake zao mwaka jana na kwamba utafiti wa shirika la kuwatetea wanaume umeonyesha kuwa kesi nyingi za wanaume kuteswa na wake zao zinaripoti wakati kakati mwanchi.

    Hata hivyo, baadhi ya wanaume katika eneo hilo wameunga mkono hatua ya wanawake kuwashambulia waume zao. Wanasema kuwa wanapigwa kwa sababu wamekosa kuwajibika kwa familia zao.Wanadai kuwa wanaume wengi hawajulikani nyumbani kwao. Wake zao wanawajua makasisi ambao huja kuwaombea kuhusu matatizo ya nyumbani huku mabwana zao wakizama katika ulevi.Wanawake na waume wa Nyeri wametaka serikali kukomeshe uuzaji na unywaji wa pombe haramu ambayo imechangia sana katika ugomvi wa nyumbani.
    Maswali
    1. Yape makala haya anwani inayofaa (alama 1)
    2. Eleza sababu za wanaume kupigwa na wanawake katika ndoa (alama 4)
    3. Mwandishi anamaanisha nini anaposema kuwa wanaume wengine hawajulikani nyumbani kwao?(alama 2)
    4. Fafanua majukumu ya makasisi katika jamii kwa mujibu wa kifungu hiki (alama 2)
    5. Ni mabadiliko yepi yametokea katika asasi ya ndoa kwa mujibu wa kifungu? (alama 3)
    6. Eleza maana ya msamiati kama ulivyotumika kifunguni (alama 3)
      1. Mwanaharakati
      2. Amevaa miwani
      3. Waliadhimisha
  1. UFUPISHO (ALAMA 15)

    Ujambazi wa kimataifa ni tatizo linalo wasumbua walimwengu kwa muda mrefu sana. Serikali nyingi zimetumia mapesa mengi kwa miaka mingi sana zikijitahidi kupambana na janga hili. Hata hivyo, fanaka haijapatikana, wala haielekei kuwa itapatikana leo au karne baadaye.

    Yamkini tatizo kubwa lililopo ni kuhusu jelezi la dhana ya ”Ujambazi” tena “wakimataifa”. Hili ni tatizo moja wapo na yapo mengi sana. Tatizo la pili ni kibusi. Kuna wale wafu binafsi na hasa viongozi wa nchi kubwa kubwa na serikali zao zilizojiaminisha kuwa ujambazi ni balaa kweli, tendabelua, lakini huo ni wa huko, wala hauwezi kuwagusa licha ya kuwashtua wao.

    Kulingana na maoni ya watakaburi hao, ujambazi ni wa watu washenzi wasiostarabika, wapatikanao katika nchi zisizoendelea bado. Ujambazi wa pekee wanaouona unafaa kukabiliwa ni dhidi ya mbubujiko wa dawa za kulevya iliosababishwa na vinyangarika kutoka nchi hizo maaluni za “ulimwengu wa tatu”. Kulingana na wastaarabu wa nchi zilizoendelea, vinyangarika hivi ndivyo hasa adui mkubwa wa ustaarabu ulimwengu na ni sharti vifagiliwe mbali bila huruma.Baada ya kusagwa sagwa, ulimwenguni mstaarabu utazidi kutononoka na ahadi ya mbingu hapa ardhi ni itakamilika.

    Imani ya watu hawa yakuwa ujambazi, hata hivyo upo, hauwezi kuwashtua wala kuwatingisha wao ilikuwa kamili na timamu. Ilikuwa kamili na timamu hadi hapo mwezi Septemba terehe kumi na moja, mwaka wa 2001, ndege tatu za abiria zilizoelekea katika majumba mawili ya fahari,yenye urefu wa zaidi ya ghorofa mia moja na kuyatwangilia mbali. Mstuko na kimako! Kimako kwa kuwa kabla ya siku hiyo, wamarekani hangeweza kudhani kwamba ingewezeka mataifa lolote au mtu yeyote kuthubutu kuishambulia nchi yao,taifa wasifali lilojihami barabara dhidi ya aina yoyote ile ya uchokozi kutoka pembe yoyote ya dunia.

    Hakuna ulimwengu mzima, aliyeamini kuwa marekani ingeweza kushambuliwa.Kwa ajili hiyo, mshtuko ulitingisha ardhi yote na huzani kutanda kote, kama kwamba sayari nzima imeshambuliwa, wala sio marekani pekee.

    Mintarafu hiyo,marekani ilipolipiza kisasi kwa kuwaunguza waliokuwemo na wasiokuwemo kwa mabomu hatari huko Afghanistan,idadi kubwa ya watu dunia ni ilishangilia na kusheherekea. Kwa bahati mbaya, tafsiri ya shambulizi la minara-pachaya New York na ile ya Pentagon, uti wa uwezo wa Marekani ilizorota. Kuna wengi waliodhani huo ni mwanzo wa vita vya Waislamu dhidi ya Wakristo na kwa muda, Waislamu wote wakashukiwa kimakosa kuwa ni majambazi wa kimataifa.

    Maswali.
    1. Bila kubadilisha maana, fupisha aya za kwanza.(maneno 65-70) (alama6)
    2. uKizingatia aya tatu za mwisho, fafanua fikira za watu na mambo yote yaliyotendeka baada ya Septemba 11,2001.( maneno65-70) ( alama 7)
  2. MATUMIZI YA LUGHA (alama 40)
    1. Eleza sifa mbili bainifu za sauti /a/ (alama 2)
    2.  
      1. Mofimu ni nini? (alama 2)
      2. Ainisha mofimu katika kitenzi; (alama 2)
        Alimwona 
    3. Andika kitenzi chenye muundo ufuatao; (alama 2)
      Kiambishi ngeli, wakatiu liopita, mzizi, kauli tendwa na kiishio.
    4. tunga sentensi mbili tofauti kudhihirisha kiimbo
    5.  
      1. Barabara nyingi zimesakafiwa. (Tumia wakati ujao hali ya mazoea)
    6. Andika sentensi ifuatayo katika usemi halisi (alama 4)
      Cherotich aliwahakikishia wazazi wake kwamba angetia bidii katika masomo yake ili apite mtihani wake
    7. Unganisha sentensi zifuatazo kwa kutumia rejeshi-amba (alama 2)
      1. Mshukiwa alipelekwa mahakamani
      2. Mshukiwa alichukuliwa hatua
    8. Changanua sentensi ifuatayo kwa mtindo wa jedwali (alama 4)
      Mto uliofurika mwaka jana uliwaua mamba wengi
    9. Tambua shamirisho, chagizo na kihusishi katika sentensi (alama 3)
      Mgonjwa alitibiwa na daktari jana jioni.
    10. Taja ngeli za nomino zifuatazo (alama 2)
      1. Sandarusi 
      2. Saa
    11. Yakinisha sentensi ifuatayo (alama 2)
      Mamlaka makubwa ya Rais hayakwazi juhudi za upinzani
    12. Unda nomino mbili kutokana na kitenzi kifuatacho (alama 2)
      La
    13. Tunga sentensi kudhihirisha maana za vitate vifuatavyo (alama2)
      1. Bure
      2. Pure
    14. Andika katika hali ya ukubwa wingi (alama 2)
      Msichana mrembo ameolewa na mwanamume hodari.
    15. Kamilisha tanakali za sauti zifuatazo (alama 2)
      1. Majiyalijaa
      2. Barabara imenyooka 
    16. Eleza maana ya mzizi wa kitenzi (alama 1)
  3. ISUMU JAMII (ALAMA 10)
    1. Lugha rasmi ni nini? (alama 2)
    2. Eleza sababu zozote tatu ambazo huenda zikamfanya mzungumzaji afanye makosa ya kisarufi na kimatamshi (alama 3)
    3. Huku ukitoa mifano mwafaka fafanua sifa tano za sajili ya bungeni


MARKING SCHEME

  1. UFAHAMU
    1. Ndoa/kunyanyaswa kwa wanaume ( 1 x1=alama 1)
    2.  
      1. Kutowajibika kwao
      2. Wengine hawajulikani nyumbani kwao.
      3. Wamezama katika ulevi
      4. Wanawake kuwa na kipato kikubwa kuliko waume zao ( 4 x 1=alama 4)
    3. Hawafiki nyumbani kwa jamaa zao ( 1 x 2=alama 2)
    4. Kuwaombea kuhusu matatizo ya kinyumbani ( 1x2=alama 2)
    5.  
      1. Wanaume kutowajibika
      2. Wanawake kupewa uwezo
      3. Wanawake kuwadharau na kuwapiga waumezao                                         ( 3x1=alama3)
    6.  
      1. Anayepigania haki za wengine
      2. Kulewa
      3. Walisherehekea                                                                                             ( 3x1=alama3)
  2. UFUPISHO
    1. Fanaka haija patikana wala haielekei kupatikana
      Tatizo kubwa ni kuhusu jelezi la dhana ya ujambazi wa kimataifa.
      Vinyang’arika sharti viangamizwe ili ulimwengu mstaarabu uzidi kutotonoka
      (zozote 6x1=alama 6)
    2. Marekani ililipiza kisasi kwa kuwaunguza waliokuwemo na wasiokuwemo kwa mabomu huko Afghanistan.
      Tafsiri ya shambulizi la minara pacha ya New York na Pentagon ulizorota.
      Wengi walidhani kuwa huo ulikuwa ni mwanzo wa vita dhidi ya Wakristo
      (zozote 6x1=alama6)
      a=6,
      b=6
      ut=3                15
  1.  
    1.  
      1. Ni irabu
      2. Ni irabu ya kati ya ulimi
      3. Hutamkwa mdomo ukiwa umetandazwa.                              (za kwanza 2x1=alama 2)
    2.  
      1. Mofimu ni sehemu ndogo yanew yenye maana ya kisarufi na isiyoweza kuvunjwa vunjwa zaidi.
      2. Alimwona
      3. Mofimu ya nafsi/ngeli
        li-Mofimu ya wakati
        mw-Mofimu ya kitendewa
        a- Mofimu ya kiishio                                                                                             (4x½=alama 2)
    3. Mfano :Ilipandwa
    4.  
      1. Sentensi ya swali – Ulimwona mwalimu saa ngapi?
      2. Sentensi ya mshangao – Hoyee! Timu yetu imeshinda.
      3. Sentensi ya taarifa – Nilimwona Simba msituni jana.
      4. Sentensi ya ombi – Naomba/tafadhali nisaidie na nauli
      5. Sentensi ya amri – Toka nje haraka!
    5.  
      1. Kijitabu kiki hiki kilirushwa na kiranja ( 1x2=alama2)
      2. Barabara nyingi zitakuwa zimesakafiwa/zitakuwa zikisakafiwa (1x2=alama2)
    6. Cheroitich aliwahakikishia wazazi wake, “Nitatia bidii katika masomo yangu ili nipite mtihani wangu.” (8x½=alama 4)
    7. Mshukiwa ambaye alipelekwa mahakamani alichukuliwa hatua.                   (1x2=alama2)
    8. (8x½=alama4)
    9. Shamirisho – Mgonjwa
      Chagizo – jana jioni
      Kihusishi–na                                                                                                        (3x1=alama3)
    10.  
      1. I-ZI
      2. I-ZI (2x1=alama2)
    11. Mamlaka makubwa ya Rais yanakwaza / hukwanza juhudi za upinzani. (1x2=alama2)
    12.  
      1. Kula
      2. Mlo
      3. Chakula
      4. Mlaji (2x1=alama2)
    13.  
      1. Bure
        Kitukinachopatikanebilajasho/bwerere
        Ovyo
        Kitukisichonathamani (1x1=alama1)
      2. Pure – Chakula cha mchanganyikowapunjezamahindinamaharagwe. (1x1=alama1)
        Tan: Kadiriamatumizimwafaka.
    14. Masichanamaremboyaliolewanamajanaummehodari.                                     (4x½=alama2)
    15.  
      1. Pomoni
      2. Twaa (2x1=alama2)
    16. Mzizi wa kitenzi ni sehemu inayobeba maana kuu na ambayo haiwezi kubadilishwa.                                                                                                                                            (1x1=alama1)
  2.  
    1. Lugha rasmi ni lugha ambayo hutumika katika shughuli za kiofisi.
    2.  
      • Kutofahamu ngeli za Kiswahili
      • Kuwa na upungufu katika baadhi ya viungo vya kutamkia
      • Kuzungumza kwa haraka
      • Kuwa na athari ya lugha ya kwanza/lafudhi
      • Kimaksudi hasa wakati wa uigizaji (za kwanza 3x1=alama3)
    3.  
      • Ni lugha yenye msamiati teule K.V spika, mswada, mbunge.
      • Ni lugha ya majibizano kwani huhusisha maswali na majibu
      • Ni lugha ya kimaelezo hasa mbunge anapochangia hoja.
      • Ni lugha inayotumia viziada lugha na ishara za mikono.
      • Lugha huwa rasmi
      • Lugha yenye ucheshi
      • Lugha yenye heshima na adabu             (zozote 5x1=alama5)
Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI PAPER 2 - KCSE 2019 ALLIANCE GIRLS MOCK EXAMINATION (WITH MARKING SCHEME).


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest