KISWAHILI PAPER 3 - KCSE 2019 MOCK EXAMINATION - KAKAMEGA

Share via Whatsapp

SEHEMU YA   A
FASIHI SIMULIZI

  1.  
    1.  
      1. Taja mbinu zozote tatu za kuhifadhi fasihi simulizi       (alama 3)               
      2. Taja aina zozote tatu za vitendawili                                                         (alama 3)
      3. Bainisha matumizi ya lugha katika vitendawili                                  (alama 3)
    2.  
      1. Ngomezi ni nini?                                                                                 (alama 1)
      2. Eleza ujumbe uliowasilishwa na ngomezi katika fasihi simulizi.         (alama 3)
      3. Fafanua sifa zozote nne za ngomezi.                                                 (alama 4)
      4. Taja mifano mitatu ya ngomezi ya kisasa                                   (alama 3)

SEHEMU YA B
USHAIRI 3
Soma shairi lifuatalo kwa makini halafu ujibu maswali yanayofuata.

  1. Kijana tuza makini, nikwambie usikile                                
    Chakula mahotelini, si kizuri usikile                                          
    Ufikapo mlangoni, kizingiti usikile                                     
  1. Nenda kaseme nyumbani, kesho asubuhi siji          
    Nitakwenda makondeni, kawashunge shunge siji       
    Na hata hapo jioni, kama nitakuja siji                                    
  1. Na kama wenda mjini, upatapo nyumba panga         
    Upahame mizimuni, palozingirwa na panga         
    Hapana tena amani, kutwa mwapigana panga    
  1. Na kesho kija shambani, uonapo mti panda 
    Kwea hadi kileleni, ujifiche kwenye panda         
    Kaziyo ulinde chini, mimea tuliyopanda                 
  1. Kishuka ola shinani, njugu merundika chungu 
    Njugu peleka nyumbani, zisije zikawa chungu                    
    Kaanga sufuriani, au pia kwenye chungu                                             

  2. Kileta maji jioni, ndoo jitwike na kata
    Kata njema ya majani, laini wezayo kata
     Kumbuka ya kisimani, huteki ela kwa kata

  3. Ninawahi kibandani, nikaliezeke paa
    Nipate lindia nyuni, na wanyama kama paa
    Kwani kiola angani, naona jua lapaa

  4. Kisha takwea mtini, nimeona bivu tunda
    Sina usono moyoni, ela tunda kisha tunda
    Nimpe wangu mwendeni, jioni nishike tunda

  5. Meanza wao uneni, hapo nami ndipo kamba
    Leo wenda hawaoni, kama wa bahari kamba
    Wajijaza kimiani, wakijitatia kamba

  6. Mtoto wachoma yakini, japo liwe moja kaa
    Ukikupata takoni, ni shida huwezi kaa
    Ela hufaa mekoni, kutoka nswi na kaa 

    Maswali.
    1. Bainisha dhamira ya mtunzi wa shairi hili                                                     (alama2)
    2. Eleza maana tatu za neno chungu kama lilivyotumika katika shairi             (alama3)
    3. Andika ubeti wa nane katika lugha nathari                                                    (alama3)
    4. Eleza muundo wa shairi hili                                                                            (alama5)
    5. Onyesha vile uhuru wa kishairi ulivyotumiwa na malenga                           (alama4)
    6. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika shairi                             (alama3)
      1. Makondeni
      2. Jitwike
      3. Kiola

SEHEMU YA TATU

KIGOGO.

  1. Viongozi huangaisha wanyonge, Ashua anasema “ …….. kuhangaisha na wenye nguvu ndio hewa tunayopumua huko?
    Eleza jinsi wanyonge wanavyohangaishwa   (al.20).
  1. Viongozi hutumia mbinu mbali mbali kuthibiti na kudumisha utawala wao. Jadili ukirejelea Tamthilia ya Kigogo.
    SEHEMU YA NNE

CHOZI LA HERI.

“ Lakini itakuwaje historical Injustice na hapo ulipo sicho kitovu chako?’’

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili (al.4).
  2. Eleza tamathali mbili za lugha zilizotumika kwenye dondoo hili? (al.4).
  3. Fafanua umuhimu wa msemaji wa maneno haya (al 6)
  4. Ni mambo gani yaliyowakumba wale ambao kituvu cho sicho walicho?   (al 6)

    Fafanua namna mwandishi alivyotumia mbinu ya kisengere nyuma katika riwaya yake.

SEHEMU YA TANO

TUMBO LISILOSHIBA

Usiteketeze umati kama kuni zinavyoteketeza moto. Rudi rudi kwa mola wako.

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili.
  2. Fafanua sifa za msemewa
  3. Tambua tamathali ya usemi iliyotumika hapo juu.
  4. Ni kwa nini msemewa anatakikana kurudi kwa mola wake?


MARKING SCHEME

  1.  
    1.  
      1. Mbinu za kuhifadhi fasihi simulizi
        • Katika akili ya binadamu
        • Maumbile na mazingira – k.m fisi kuchechemea, kinyonga kutembea polepole
        • Katika vifaa meme k.m video
        • Katika michoro 3 x 1= 3
      2. aina tatu za vitendawili
        • Sahili – vitendwa vinavyoundwa kwa maneno machache
        • Tate – huwa ni fumbo linalohitaji kuchemsha bongo ili kung’amua jawabu
        • Simulizi – husimulia hadithi kama msingi wa kitendawili.
        • Tanakali – huundwa kwa maneno yanayoiga sauti inayotolewa na kitendo k.m chururu si ndo!ndo!ndo!
        • Mkufu – huwa sehemu zinazohusiana na kuchangizana kimaana na vina urefu Fulani 3 x 1 = 3
      3. Matumizi ya lugha katika Vitendawili
        • Taswira – km kuku wangu katagia mwibani. (nanasi)
        • Sitiara – Nyumba yangu haina mlango (yai)
        • Kejeli – Uzi mwembamba umefunga dume kubwa (Usingizi)
        • Tashihisi – popote niendapo amenifuata (kivuli) 3 x 1 = 3
    2.  
      1. Ngomezi Ni fasihi ya ngoma
        1 x 1 = 1
      2. Ujumbe uliowasilishwa na ngomezi
        • Kuzaliwa kwa mtoto
        • Ndoa
        • Kifo
        • Uwindaji
        • Vita vya kikabila
        • Majilio ya mvua
        • Kuwaita kwa mchezo wa mleleka
        • Kuwaita watu kwa jambo la dharura 3 x 1 = 3
      3. Sifa za ngomezi
        • Si rahisi kupata ujumbe wa ngomezi kama wewe si mshiriki wa utamaduni husika
        • Ngoma ni muhimu kupitishia ujumbe
        • Wanajamii tu ndio wanaoweza kufasiri mdundo wa ngoma na kufasiri maana
        • Ujumbe wa dharura huwasilishwa kwa njia ambayo si ghali ikilinganishwa na njia nyingine
        • Mapigo yanayotolewa kwa maana maalumu huambatana na ngoma inayoeleweka kwa ujumbe mahsusi
        • Huongozwa na watu teule katika jamii.   4 x 1 = 4
      4. Mifano mitatu ya ngomezi uya kisasa
        • Milio ya ambulensi na magari ya polisi na mazimamoto
        • Ving’ora
        • Kengele (shuleni, mahakamani, kanisani)
        • Toni za kengele za rununu

          MWONGOZO WA USHAIRI
  2.  
    1. Kufunza maana mbalimbali za maneno                                                                                  (1x2=1)
    2. Maana za neno ‘chungu’
      1. Tele/ ingi
      2. Chachu
      3. Kifaa cha kupikia                                                                                                                               (3x1=3)
    3. Nitapanda juu ya mti, mahali ambapo nimechuna tunda lililoiva kwa sababu siwezi kutulia mpaka nilipate ili nimpe mpenzi wangu ndipo jioni niweze kupapasa titi    (alama 3)
    4. Lina mishororo mitatu – ni tathlitha
      • Kila mshororo una vipande viwili
      • Vina havifanani
      • Lina beti kumi
      • Mizani 16 (8, 8) (5x1=5)
    5.  
      1. Tabdila, mfano – usikile – usikie
      2. Inkisari, mfano – kaseme – ukaseme
        - mi         - mimi
        - kaziyo   - kazi yako
        - takwea   - nitakwea
      3. Kuboronga sarufi
        – Na kesho kija shambani
        -Na ukija shambani kesho
      4. Lahaja                       
        - Ola,
        - Ona      (Zozote 2x2)

        Kutaja alama 1 mfano alama 1
        1. Makondeni – mashambani
        2. Jitwike – weka kichwani/ mgongoni
        3. Kiola – kiona/ kiangalia/ kitazama                                                                            
  3. -Wachochole kutumikishwa na viongozi kombe,boza na sudi wanafanya kazi ya kuchonga vigogo vya mashujaa.
    - viongozi kutowajibika , kazi yao ni kukusanya tu kodi bila ya kusafishja soko.
    -viongozi kutangaza kupindi kirefu cha kusherehekea uhuru.
    -viongozi kufadhili mradi usio na msingi wa kuchonga vinyago huku watu wakiwa na njaa
    -viongozi kuwashawishi wananchi kwa ahadi ili wawaunge mkono kenga kumshawishi sudi.
    -viongozi kutumia zawadi kufumba wananchi kuwa wanawajali sudi, boza na kombe kuletewa keki ya uhuru.
    -viongozi hawalindi usalama wa wananch,i wananchi wanaishi kwa hofu, ashua anahofia usalama wake.
    - kuweko kwa migomo yawalimu na wauguzi ni ishara ya wafanyikazi kunyanyaswa.
    -viongozi kutowajali wanyonge. Kwa mfano majoka kufunga soko.
    -viongozi kuharibu mazingira kufanya mito na maziwa kukauka majoka anaruhusu ukataji wa miti ovyo ovyo.
    - Viongozi kutojali kuhusu kifo cha wafuasi wao k.m kifo cha Ngurumo, Majoka anaagiza azikwe kabla ya jua kutua.
    - viongozi kupanga mauaji ya wapinzani wao k.m kifo cha Jabali, kupanga kifo cha chafu (Tunu au Sudi).
    - Majoka kuzima juhudi za Tunu za kutambua aliyemua Jabali.
    - Pesa za kusafisha soko hufijwa.
    - Viongozi kutosikiza matakwa ya wananchi..
    - Viongozi kuthibiti vyombo vya habari kufungwa kwa runinga ya mzalendo.
    - Viongozi kuwatumia Askari kuwatawanya raia badala ya kulinda uhuru wao.
    - Viongozi kuwadanganya raia , Majoka anadanganya Tunu , anamhaidi jambo la kifahari kumwoza ngao Junior.
    - Viongozi kupanga uvamizi, Sudi avamiwa.
    - Viongozi kuruhusu unywaji wa pombe haramu ambayo inasababisha vifo vya watu. (Mamapima kupewa kibali cha kuuza pombe haramu.)
    - Viongozi kuwabagua baadhi ya wananchi na kuwapendelea wengine.
    -Asiya anapewa karatasi na kusoma haki.
    -Viongozi kujilimbikizia mali kwa Hoteli ya Majoka and Majoka modern resort.
    -Viongozi kupanga kuficha maovu yake mbele ya wageni.

  4.  
    • Kuthibiti vyombo vya Dola – Kufunga kituo cha runinga cha mzalendo.
    • Viongozi wanatumia Askari kufanya raia badala ya kulinda uhuru wao.
    • Uvumi – Watu .
    • Ahadi za Uongo – Majoka kudai kuwa anatoa chakula kwa wasiojiweza.
    • Zawadi – Kenga kuwaletea Sudi boza za kombe zawadi ya keki.
    • Vitisho – Wasagamoyo, wanafishwa kwa kurushiwa vijikaratasi wahame.
    • Polisi kuwatisha wanasagamoyo.
    • Majoka kumtishia chopi.                         
    • Mapendeleo – Ashua baada ya kufuzu kutoka chuo kikuu alipewa kazi katika majoka and Majoka Academy . akakataa sasa angekuwa mwalimu mkuu.
    • Jela – Viongozi hufungia wanaowapinga.
    • Ashua – Anatiwa ndani.
    • Matumizi ya nguvu anapanga kumkomesha Tunu, anatangaza kuwa mandamano ni haramu.
    • Ulaghai – Majoka anapanga kuongoza mishara ya walimu na waaguzi kwa asilimia kidogo kasha apandishe kodi.
    • Anatumia wavamizi Tunu anaumizwa mfupa wa mvundi, Siti, ana majeraha kutokana na uvamizi.
    • Ulinzi Mkali – Majoka na waatuu wake wana ulinzi mkali sana. Kenga ana walinzi na Majoka ana Askari.
    • Kufuta kazi wasiomuumga mkono Majoka anamfuta kazi Kengi kwa kutomtii. Kupiga watu visasi katika soko la chapa kazi.

  5. CHOZI LA HERI.
    1. Haya ni maneno ya Ridhaa yaliyokuwa yakimpitikia baada ya kumjibu Tila mawazoni. Hii ni baada ya Ridhaa kukubali maneno ya Tila ya hapo awali inadhihifika kuwa amekubali kuwa yeye ni mgeni si mwenyeji. (al.4).
    2.  
      1. Swali la balagha, hapo ulipo sicho kifoodu chako.
      2. Kuchanganya ndimi – historical injustices (al.4).
    3. Umuhimu wa Ridhaa. (Mwanafunzi ataje mhusika ndio atuzwe).
      - Amefumiwa kuponyesha hasara iletayo na ukabila.
      - Ridhaa ni kielelezo cha watu wasiobagua watu wengine.
      - Anatekeleza miradi ya maendeleo ya kuwafaidi watu wote.
      - Anatumiwa kuonyesha udhalimu wa watawala.
      - Anahadithia namna majumba yao yalivyobomolewa.
      - Kielelezo cha watu wanaopenda ushirikina.
      - Kielelezo cha watu wenye bidii.
      – Walichomewa nyumba zao.
      - Watu wao walivawana.
      - Walazimishwa kukimbia na kutorekea msituni.
      - Watoto wao walibakwa k.m binti za Kaizeri.
      - walitoroshwa makwao wakawa maskwota.
      - Walibaguliwa na wenyeji.
      - Walibandikwa jina wafuatao mvua.
      - Viporaji wa mali ya wengine.
      - Biashara ya pombe haramu na dawa za kulevyia.

  6. – Rudhaa anakumbuka namna vikaratasi vilienezwa kila mahali vikiwafahadhaisha kuwa kuna gharika baada ya kufawazwa kwa kiongozi mpya.
    - Kisa cha namna mzee Kedi (Jirani wao) alivyomsaidia Ridhaa kupata shamba lake na kuwa ameyadhamini masomo ya wao waze wawili kimetolewa kwa urejeshi.
    - Mjadala baina ya Ridhaa na Tila imetolewa kwa njia ya urejeshi.
    - Kisa cha Yule mwana wa mlowezi maarufu aliyemiliki mashamba ya theluji nyeusi katika eneo la Kisiwa bora kimetolewa kwa urejeshi.
    - Kisa cha yule kiongozi wa kiimla wa kike aliyekuwa akisimuliwa katika visakale cha majirani zao na namna alivyowatumikisha wanaume kimetolewa kwa urejeshi.
    - Kaizari anasimulia yaliyojiri baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya aliyekuwa mwanamke kwa njia ya kirejeleo.
    - Moyo wa Kaizari ulipoanza kumvuta alikumbuka kisa cha wafuasi wa Musa ambao baada ya kukosa chakula jangwani walimshtumu kwa kuwatoa kule Misiri.
    - Ridhaa alipokuwa ameketi kwenye chumba cha mapokezi katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Rubia, alikumbuka namna walivyorudi nyumbani baada ya kuishi katika msitu wa mamba kwa miezi sita. Anakumbuka pia alivyokuwa akihisi.
    - Ridhaa anakumbuka Tila bintiye alivyokuwa anapenda masuala yanayohusiana na sheria, haki na siasa.
    - mwangeka alipolitazama tabasamu la babake, alihisi kuwa sasa anazingiriwa na uzio imara akawa anakumbuka wimbo ambao mamake alizoea kumwimbia kila mara babake alipokuwa ameenda katika safari za kikazi.
    - Kisa cha namna ami zake Kengata walivyokuwa wamekatana mwana wao aolewe na mtu wa ukoo mwingine kimetolewa kwa wajeshi.
    - Kisa namna Lunga alivyosteafishwa kwa kuwa na msimamo imara kuhusiana na saketa ya mahindi kinatolewa kwa urejeshi.   
                                                     
  7.  
    1. Msemaji wa maneno haya ni mkumbukwa. Anamweleza mkubwa walikuwa kwake mkubwa.
    2. Mwenye bidii.
      Mwenye utani.
      Mtambuzi.
      Mwenye utu.
      Mwenye tamaa ya mali.
      Ni maskini mwanzoni.
      Ni fisadi.
      Mwenye msimamo dhabiti.
      Ni msiri.
      Mwenye wasi wasi.
    3. Tashbihi – Usitekeleze umati kama kuni zinavyotekeleza moto .
    4. ametenda vitendo vingi viovu kama vile;
      - Kuuza dawa za kulevya.
      - Kutoa hongo ili apate uongozi.
      - kumtapeli rafiki yake mkumbulana.
      -  Kumwingiza mkumbukano kufika uuzaji wa dawa za kulevya.
      -  Kutumia pasipoti ya kidiplomasia vibaya.
Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI PAPER 3 - KCSE 2019 MOCK EXAMINATION - KAKAMEGA.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest