KISWAHILI PAPER 1 - 2019 MOKASA II MOCK EXAMINATION

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  1. Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima
  2. Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
  3. Kila insha isipungue maneno 400.
  4. Kila insha ina alama
  5. Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili
  1. Lazima

Wewe ni Mwalimu Mkuu katika Shule ya Upili ya Poromoka ambapo pamekuwa na visa vingi vya utovu wa maadili miongoni mwa wanafunzi. Waandikie wanafunzi wote memo ukiwaonya dhidi ya mambo haya.

  1. “Utandaridhi una athari mbaya katika maisha yetu.” Jadili.
  2. Andika kisa kitakachoafikiana na methali: Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi.
  3. Andika kisa kitakachomalizikia kwa: ... walijifunga vibwebwe kuwavua wahasiriwa waliokuwa wamefunikwa na vifusi lakini jitihada zao ziliambulia patupu.


MARKING SCHEME

Swali la lazima

Wewe ni Mwalimu Mkuu katika Shule ya Upili ya Poromoka ambapo pamekuwa na visa vingi vya utovu wa maadili miongoni mwa wanafunzi. Waandikie wanafunzi wote memo ukiwaonya dhidi ya mambo haya.

  1. Pawe na sura ya memo ifuatayo:
    Jina la shule: Shule ya Upili ya Poromoka
    Anwani: Memo
    Kutoka kwa: Mwalimu Mkuu
    Tarehe:
    MADA: MINT: KUH:
    Yaliyomo
    Tamati sahihi ya mwandishi
    Jina la mwandishi
    Cheo chamwandishi (Mwalimu Mkuu Shule ya Upili ya Poromoka)
  1. Baadhi ya hoja
    1. Visa vya utovu wa nidhamu
      • Wizi miongoni mwa wanafunzi vitanja na walimu.
      • Matumizi ya dawa za kulevya.
      • Migogoro na hata vita miongoni mwa wanafunzi.
      • Kutohudhuria vipindi darasani au / na masomo ya ziada.
      • Wizi katika mtihani.
      • Mimba miongoni mwa wanafunzi wa kike.
      • Mahusiano ya kimapenzi miongoni mwa wanafunzi.
      • Kukaidi kanuni za shule kama vile kuvaa nguo za nyumbani, kuwatusi viranja na walimu.
      • Kushiriki migomo na uharibifu wa mali ya shule.
    2. Maonyo/ hatua zitakazochukuliwa
      • Kuadhibiwa kwa wanafunzi wanaowatusi.
      • Kuchukuliwa kwa hatua za kisheria dhidi ya wale wote watakaopatikana wakitumia dawa za kulevya.
      • Kuwatoza karo ya ziada watakaohusika katika vitendo vya uharibifu wa mali ya shule.
      • Kuwauliza wanafunzi wezi kununua maradufu ya vile walivyoiba.
      • Wanafunzi wanaofanya vibaya masomoni kulazimika kujieleza mbele ya walimu na wazazi wao.
      • Wanafunzi wanaopuuza kufanya kazi ya ziada walazimishiwe kupitia adhabu.

TANBIHI

  1. Mtahiniwa anaweza kuzingatia hoja nyingi iwezekanavyo; kwa vyovyote vile zisipungue tano.
  2. Hoja hizi zinaweza kuambatana na maonyo au yakaja baadaye.
  3. Mkwaju wa wima utumiwe kuonyesha hoja ya utovu wa maadili na wenye kikia utumiwe kuonyesha maonyo pale yanapokamilikia pembezoni.
  4. Hoja tano za pande zote mbili zikiambatana na maonyo (angaa ya aina mbili) zinaafiki.
  5. Toni iwe ya maonyo.

Swali la pili

Utandaridhi una athari mbaya katika maisha yetu.” Jadili.

Hili ni swali la kujadili. Mtahiniwa ashughulikie pande zote mbili za swali.

Utandaridhi ni uhusiano wa vipengele vya maisha miongoni mwa jamii za ulimwengu. Mahusiano haya yaweza kuwa ya kijamii, kisiasa nk yanayokiuka mipaka ya kitaifa na kufanya ulimwengu kuwa kijiji kimoja.

Athari nzuri

  1. Kuhimiza maingiliano ya jamii mbalimbali.
  2. Kusambaza maarifa kutoka sehemu moja hadi nyingine.
  3. Kuchangia katika kusambaza haki au maarifa ambayo hayapatikani kwingineko.
  4. Kuharakisha maendeleo katika sehemu mbalimbali za ulimwengu.
  5. Kuwawezesha watu ulimwenguni kufaidika kutokana na teknolojia bora.
  6. Kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi ya maeneo mbalimbali kutokana na na biashara kama utalii.
  7. Kuchangia kuwaelimisha raia kuhusu haki zao za kisiasa.
  8. Kupanua elimu kwa kutumia mtandao.
  9. Kuwa msingi wa ukuwaji wa chumi mbalimbali kutokana na biashara baina ya mataifa.

Athari mbaya

  1. Uwezekano wa kusambaza tabia na tamaduni za kigeni zenye madhara mabaya kutokana na mtandao.
  2. Kuwepo kwa bidhaa zinazotoka mataifa mengine ambazo huathiri ukuwaji wa viwanda nchini.
  3. Uchafuzi wa mazingira kwa ujumla.
  4. Bidhaa kutoka ng’ambo huathiri ukuwaji wa viwanda vyetu.
  5. Uwezekano wa kuichochea jamii dhidi ya serikali zao.
  6. Mataifa machanga yanadhibitiwa na mataifa yaliyoendelea kiuchumi.
  7. Uhamaji wa watu kutoka nchi za ulimwengu wa tatu hadi nchi za ulimwengu wa kwanza.
  8. Matendo mabaya ya wizi, mauaji, ulawiti nk kwa sababu ya mtandao.

Swali la 3

Andika kisa kitakachoafikiana na methali: Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi.
Hili ni swali la methali.
Mtahiniwa aandike kisa kimoja kitakachodhihirisha maana ifuatayo:
Usidhanie unaweza kufaidika kutokana na bahati ya mtu mwingine. Kuwa mtu asidhanie kuwa atafaidika kutokana na kufanikiwa kwa mtu mwingine.
Mtahiniwa aweza kuandika kisa ambamo mhusika au wahusika wanajaribu kufaidika kutokana na kufanikiwa kwa mwenzake/ wenzake lakini juhudi zake/zao hazifanikiwi.

TANBIHI

  1. Si lazima mtahiniwa aeleze maana ya methali: aandike kisa moja kwa moja.
  2. Sehemu mbili za methali zijitokeze wazi: Kuwe na kufanikiwa kwa mtu mwingine upande mmoja, na upande mwingine kuwe na mhusika yule kujaribu kutegemea huko kufanikiwa na asiweze kufaidika.
  3. Mtahiniwa akishughulikia sehemu moja tu ya methali asituzwe zaidi ya C+ 10/20.
  4. Kanuni nyingine zote za kusahihisha zizingatiwe.

Swali la 4

... walijifunga vibwebwe kuwavua wahasiriwa waliokuwa wamefunikwa na vifusi lakini jitihada zao ziliambulia patupu.

  • Mtahiniwa asimulie kisa kuhusu jumba/jengo lililoporomoka na kuwafunika watu.
  • Lazima aonyeshe jinsi yeye na wengine walivyojitolea kuwaokoa watu waliokuwa wamekwama kwenye vifusi.
  • Aonyeshe namna walivyokumbana na tatizo hili na namna walivyojizatiti kuwaokoa wahasiriwa lakini wakashindwa.
  • Mtahiniwa aonyeshe sababu zilizochangia kuporomoka kwaa jengo ama jumba; kama vile ujenzi mbaya, mlipuko wa bomu au shambulizi la kigaidi.
  • Aonyeshe jinsi ambavyo mkasa huu uliishia kusababisha maafa na hasara isiyokadirika.
  • Mtahiniwa akidondoa maneno hado kufikia matatu, asiadhibiwe ila lichukuliwe kama kosa dogo tu la kimtindo.
  • Mtahiniwa akikosa kumalizia kwa maneno ya mdokezo huu, atakuwa amejitungia swali. Atuzwe D- 02/20
  • Mtahiniwa azingatie nafsi ya tatu wingi na ajihusishe katika usimulizi.
  • Vipengele vingine vya kimsingi vya usahihishaji wa insha uzingatiwe.
Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI PAPER 1 - 2019 MOKASA II MOCK EXAMINATION.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest