Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Kapsabet Mocks 2020/2021

Share via Whatsapp
  1. Lazima
    Wewe ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Upili ya Mamboleo. Mwanafunzi wako aliyefanya mtihani wake wa KSCE mwaka jana na kupita vizuri amepewa nafasi katika Chuo Kikuu cha Tumaini.
    Andika wasifu wake.
  2. Mitandao ya kijamii ina faida na hasara zake. Thibitisha.
  3. Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali ifuatayo:
    Wakosanao ndio wapatanao.
  4. Andika kisa kinachomalizikia kwa kauli ifuatayo:
    …Tangu siku hiyo kijiji kizima kilipata funzo kwamba umdhaniaye ndiye kumbe siye na umdhaniaye siye kumbe ndiye.


Marking Scheme

Lazima

Wewe ni mwalimu mkuu wa Shule ya Upili ya Mamboleo. Mwanafunzi wakoaliyefanya mtihani wake wa KCSE mwaka jana na kupita vizuri amepewanafasi katika Chuo Kikuu cha Tumaini. Andika wasifu wake.

  1. Hii ni insha ya kiuamilifu.
  2. Wasifu ni maelezo ya kina kuhusu mambo,matendo na tabia za mtu na ambayo huelezwa na mtu mwingine.

SURA YA WASIFU

A. KICHWA/MADA

  1. Mada ianze kwa neno ‘wasifu.’
  2. Itaje ni wasifu wa nani—Lulu.
  3. Iandikwe kwa herufi kubwa kisha kupigiwa mstari.
  4. Isiwe na alama nyingine ya uakifishaji kando na mstari.

WASIFU WA LULU

Au

WASIFU WA MWANAFUNZI LULU

B.UTANGULIZI

C. MWILI (YALIYOMO)

  1. Iandikwe kwa nafsi ya tatu.
  2. Iandikwe kwa wakati uliopita, hali timilifu au pamoja na hali ya kuendelea.
  3. Matukio yatiririshwe na mtahiniwa kiwakati.
  4. Baadhi ya maudhui/masuala yanayostahili kushughulikiwa ni:
    1. Tambulisha jina la mwanafunzi.
    2. Elezea alikozaliwa
    3. Fafanua kuhusu utoto wake; alikokalia na kukua kwake.
    4. Elezea kuhusu aila yake/jamaa yake, wavyele wake.
    5. umri wake
    6. Tambulisha jinsia yake.
    7. Elezea kuhusu lugha anazozifahamu.
    8. Elezea kuhusu masomo yake alipokuwa chekechea—alisomea wapi,ufanisi wake katika kiwango hiki, ushindi wake na pingamizializokumbana nazo.
    9. Elezea kuhusu masomo yake katika shule ya msingi na upili:
      • Alisomea wapi, akiwa na umri upi?
      • Alishiriki katika vyama vipi?
      • Aliingiliana vipi na wanafunzi wenzake: je, aliwasaidia wasiojiwezakimawazo, kifedha?
      • Nidhamu yake?
      • Alileta mchango upi/ushindi wake/tuzo zake/alianzisha mradi upiambao labda ulichochea ndoto yake ya kuwasaidia wenzake?
      • Alihusiana vipi na walimu wake?
      • Elezea pingamizi alizokumbana nazo na alikabiliana nazo vipi?
      • Alifanya vipi katika mitihani yake; darasa la nane na kidato cha nne?
      • Azima yake baada kuhitimu masomo ya kidato cha nne—kusoma zaidi ijitokeze waziwazi
      • tabia zake
      • tajiriba zake

D. HITIMISHO

Mtahiniwa ahitimishe kwa kuelezea:

  1. umaarufu wa mwanafunzi
  2. sababu za mwanafunzi huyo kuhitaji utambulisho

Lulu amekuwa mfano bora kwa vijana wote vitongojini na mjini. Amekuwa akiwahamasisha wanahirimu wenzake baada ya masomo yake ya kidato cha nne kuhusu umuhimu wa mshikamano mwema. Kwa upande mwingine, amekuwa akiwanasihi vijana kuasi matumizi ya afyuni na ulanguzi wa mihadarati. Hivi majuzi, amekuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za watoto kimasomo.

Mitandao ya kijamii ina faida na hasara zake. Thibitisha.

  1. Hii ni insha ya mjadala.
  2. Mtahiniwa lazima aangazie sehemu zote mbili; faida na hasara.
  3. Mifano ya mitandao ya kijamii—facebook, whatsapp, imo,zoom, wavuti,baruapepe,Instagram,telegram,Twitter,SnapChat,WeChat,Messenger,Pinterst,Youtube,Linkedln
  4. Baadhi ya maudhui ni kama yafuatayo:

FAIDA ZA MITANDAO YA KIJAMII

  1. Hurahisisha mawasiliano/mawasiliano ya haraka na kwa watu wengi.
  2. Hutoa nafasi za ajira kwa urahisi.
  3. Huunganisha wanajamii/hukuza umoja wa kitaifa na kimataifa.
  4. ni njia mojawapo ya kupata burudani
  5. ugwe wa kukuza vipawa
  6. Husaidia wasomi katika kufanya utafiti.
  7. Hutumiwa kutoa mafunzo kwa wanafunzi.
  8. Hujenga mahusiano mazuri—ndoa kupitia mitandao
  9. Huimarisha biashara katika maeneo mbalimbali/kote ulimwenguni.
  10. Husaidia kupitisha wakati.
  11. Husaidia kuenea kwa utamaduni, mila, lugha(Kiswahili) kote ulimwenguni.
  12. ni hifadhi nzuri ya ujumbe, miswada, video na picha
  13. Baadhi huweza kuwa na kamera.

HASARA ZA MITANDAO YA KIJAMII

  1. Imechangia kuongezeka kwa ajali za ndege, meli au za barabarani.
  2. Imechangia kuzorota kwa maadili kwa sababu zina filamu chafu na picha zangono.
  3. Imetumika na matapeli kuwalaghai watu na kuwaibia pesa.
  4. Imesababisha kuvunjika kwa familia au mahusiano mabaya ya kimapenzi.
  5. Haina siri—mashirika yanayoimiliki hupokea kila ujumbe.
  6. Hutumiwa na wanafunzi kuibia mitihani.
  7. Imeharibu lugha ya watu hasa wanafunzi kisarufi na kimsamiati.
  8. Huwa na mionzi (aina ya miale yenye sumu) ambayo ni hatari kwa afya yawatumizi.
  9. Huwa ni ya gharama kali kwa sababu ya kununua kadi/data ya mtandao kilawakati, gharama ya kuongeza moto.
  10. Hufanya wafanyakazi kuwa watepetevu kazini kutokana na uraibu wakuitumia.
  11. Huchangia sana vijana kujiunga na makundi ya kiuhalifu/kiharamu.
  12. Wasioifahamu/kumudu hupitwa na habari muhimu.

Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali ifuatayo

Wakosanao ndio wapatanao.

  1. Mtahiniwa atunge kisa kinachoonyesha ukweli wa methali hii.
  2. Kisa kibebe sehemu mbili ya methali:
    1. Wakosanao—mtahiniwa aangazie wahusika ambao wametofautiana/ wanamzozo na kuwa maadui
    2. Ndio wapatanao—wahusika waliokuwa na mzozo/waliotofautiana/maaduiwanakuja kupatana/kusuluhisha matatizo yao/tofauti zao kisha kuishi kamamarafiki au wasameheane.

Andika kisa kinachomalizikia kwa kauli ifuatayo:

…Tangu siku hiyo kijiji kizima kilipata funzo kwamba umdhaniaye ndiyekumbe siye na umdhaniaye siye kumbe ndiye.

  1. Mtahiniwa atunge kisa kinachooana na mdokezo huu.
  2. Kisa kimalizike kwa maneno haya.
  3. Kisa kilete maana ya kauli kwamba umdhaniaye ndiye kumbe siye na umdhaniayesiye ndiye.
  4. Insha hii ina sehemu mbili: mtu/mhusika aliyedhaniwa vibaya/vizuri baadayeaonekane kama mzuri au mbaya
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Kapsabet Mocks 2020/2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest