Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Murang'a County Mocks 2020/2021

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  • Jibu maswali manne pekee.
  • Swali la kwanza ni la lazima.
  • Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki ; yaani Tamthiliya fupi, Ushairi na Riwaya.
  • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
  • Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
  1. LAZIMA  

    SEHEMU YA : FASIHI SIMULIZI

    Hapo zamani za kale paliishi sungura na ndovu. Wanyama hawa waliishi baharini.Maulana alikuwa amewatunukia mapenzi si haba.Makazi yao yalikuwa yamepambwa yakapambika.Walitegemea matunda mbalimbali yaliyokuwa baharini kama mapera, matomoko matikitimaji na kadhalika.

    Siku moja usiku wa manane, maji yakaanza kupwa.Ndovu aliathirika zaidi. Alijaribu kuinama majini lakini hakuweza . Alimwita sungura amsaidie lakini sungura alikuwa ametoweka. Ndovu aliamua kwenda kumtafuta sungura. Alimtafuta hadi msituni lakini hakumpata. Alihofia kurudi baharini na hadi wa leo yumo msituni.

    MASWALI
    1. Tambua utanzu na kijipera chake. (al.2)
    2. Taja fomyula zingine mbili za kutanguliza kifungu hiki. (al.2)
    3. Eleza umuhimu wa kijipera hiki. (al.5)
    4. Eleza sifa za kifungu hiki. (al.5)
    5. Eleza umuhimu wa fomyula:
      1. Kutanguliza (al.3)
      2. Kuhitimisha (al.3)

SEHEMU YA B : TAMTHILIA   (P.KEA KIGOGO)

Jibu Swali la pili au la tatu.

  1. “……… Udongo haubishani na Mfinyanzi. Acha porojo zako. Kigogo hachezewi; watafuta maangamizi!”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (al.4)
    2. Fafanua mbinu mbili za kimtindo zilizotumika katika dondoo hili. (al.2)
    3. Eleza sifa zozote nne za msemaji. (al.4)
    4. Onyesha ukweli wa kauli hii katika dondoo hili ukirejelea hoja kumi. (al.10)

                            AU

  1.  
    1. Tatizo la uongozi katika bora la Afrika ni kikwazo kikubwa cha maendeleo. Kwa kurejelea matukio kwenye Tamthilia ya Kigogo. Jadili ukweli wa kauli hii. (al.10)
    2. Eleza mbinu alizotumia Majoka kufanikisha utawala wake. (al.10)

SEHEMU YA C : RIWAYA     (A.MATEI : CHOZI LA HERI)

Jibu swali la nne au la tano

  1. “Lakini itakuwaje historical injustice, nawe Ridhaa hapo ulipo sicho kitovu chako?”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (al.4)
    2. Eleza tamathali mbili za lugha zilizotumika kwenye dondoo hili. (al.4)
    3. Fafanua sifa tatu na umuhimu tatu wa msemaje wa maneno haya. (al.6)
    4. Taja mambo sita yaliyowakumba wale ambao kitovu chao sicho walicho? (al.6)

                        AU

  1.  
    1. ”Siasa mbaya maisha mabaya.”Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kurejelea riwaya ya Chozi la Heri. (al.10).
    2. Fafanua athari za umaskini katika jamii ukirejelea Riwaya ya Chozi la Heri.

SEHEMU YA D : HADITHI FUPI (Alifa Chokocho na D.Kayanda (Wahariri)

Jibu swali la sita au la saba.

  1. ”Lazima niache kazi maana mume wangu haniamini.”
    1. Fafanua muktadha wa dondoo hii. (al.4)
    2. Eleza sifa sita za mzungumzaji katika dondoo hili. (al.6)
    3. Eleza mbinu zifuatazo kama zilivyotumika katika hadithi.
      1. Sadfa (al.6)
      2. Majazi (al.4)

                           AU

  1. ”Hatuwezi kumaliza kula, kila leo tuna kula”.
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (al.4)
    2. Fafanua tamathali ya usemi iliyotumika. (al.2)
    3. Eleza umuhimu wa mnenaji. (al.4)
    4. ”Lakini nakwambia tena, kula kunatumaliza”. Kwa kudokeza hoja kumi jadili ukweli wa kauli hii. (al.10)

SEHEMU YA E : USHAIRI

  1. Soma shairi kisha ujibu maswali yafuatayo

    HEKO JESHI LETU

    Hebu niwatangazieni, mitimani yalotanda,
    Katu si ya furahani, bali ya mori kupanda,
    Kenya yetu I motoni, Al Shabaab katenda,
    Katuchokoza yakini, kututeka kama punda,
    Lo! Vyombo vya baharini, kwa telki kavidanda.

    Wakashambuliya pwani, watalii wakadinda,
    Kawapora mifukoni, ilo ndarama mabunda,
    Maguruneti jijini, mabomu ja parapanda,
    Waasi hawa kidini, kajifunga kwa magwanda,
    Wakavuruga amani, ya wakenya waso inda.

    Hawa sisi twalaani, kwa usalama kuvunda,
    Toka Somalia baini, kuteka Kenya kapenda,
    Ndo kavamiya wageni, kisha nao wakaenda,
    Kawatesa matekani, kuwafunga kwa mikanda,
    Sote kajawa huzuni, kutendewa kama kinda.

    Wanajeshi wa nchini, chonjo pasi kusarenda,
    Wakenda hivyo vitani, nyoyo bila kuwatunda,
    Ka’nzisha operesheni, ya jeshi nchi kulinda,
    Kajitoma mipakani, huku vikosi meunda,
    Somalia sadikini, kawa wa kondo ukanda.

    Kwa silaha mikononi, mahandakiyo karanda,
    Vita vya anga, jangwani, kulo maji na migunda,
    A’Shabab nuksani, kamegwa mfano tunda,
    Chao kawa hatarini, wanajeshi kawawinda,
    Mchana piya jioni, ngomezi zao kaganda.

    Wanamgambo sikieni, kazingirwa kikandanda,
    Kavunjavunjwa usoni, miguuni piya vyanda,
    Kahasiriwa mwilini, huku kabaki mepinda,
    Haramia kawa duni, wakangamizwe manunda,
    Jeshi kajitahidini, matunda mema katunda.

    Habari ulimwenguni, kamoma propaganda,
    Kuenezeka kampeni, nazo nchi kama Rwanda,
    Jeshi kajitoleeni, siku kadha’ za kalenda,
    Jeshi letu shukurani, kutulinda ja makinda,
    Twakusihi E Manani, tujali kwa kutupenda.

    MASWALI

    1.  

      Pendekeza kichwa kingine kinachofaa shairi hili. (al.1)
    2. Onyesha toni ya shairi hili. (al.1)
    3. Eleza nafsi neni katika shairi hili (alama 1)
    4. Ni madhila gani yametendwa na Al Shabab? (al.6)
    5. Fafanua uhuru wa kishairi uliotumiwa na mtunzi katika ubeti wa pili. (al.4)
    6. Eleza muundo wa shairi hili. (al.4)
    7. Eleza maana ya maneno haya yalivyotumwa na msanii. (al.3)
      1. Magwanda.
      2. Mahandaki
      3. Maharamia

MWONGOZO WA FASIHI

  1.  
    1. Utanzu – Hadithi     (1x1)
      Kipera  – Hurafa      (1x1)
    2.  
      1. Fanani : paukwa
        Hadhira : pakawa
      2. Fanani : Hadithi! Hadithi
        Hadhira : Hadithi njoo
    3.  
      1. Huburudisha wanajamii husika
      2. Huelekeza wanajamii husika
      3. Huelimisha wanajamii husika
      4. Huhifadhira huziona ya jamii husika
      5. Huonya wanajamii wa jamii husika
      6. Hujenga ushirikiano wa jamii husika
      7. Hujenga kumbukumbu ya wanajamii
        zozote (5x1)
    4.  
      1. Huhusisha wahusika wanyama
      2. Wanyama hupewa tabia za binadamu
      3. Huwa na ucheshi mwingi
      4. Hutoa matumaini kwa wanyonge kwamba mwishowe watakuwa washindi
      5. Hutoa maadili na kuonya kwa njia ya kuchekesha isiyoumiza.
        Zozote 5x1
    5.  
      1. Umuhimu wa fomyula ya kutanguliza
        • Humtambulisha mtambaji
        • Huvuta makini ya hadhira
        • Hutoa hadhira kutoka ulimwengu halisi hadi wa ubunifu
        • Hutofautisha kipera cha hadithi na vipera vingine
        • Huashiria mwanzo wa hadithi
        • Hushirikisha mtambaji na hadhira
          zozote 3x1
      2. Umuhimu wa fomyula ya kuhitimisha
        • Hupisha shughuli nyinginezo
        • Huashiria mwisho wa hadithi
        • Hutoa funzo kwa hadithi
        • Humpisha mtambaji mwingine
        • Hupumzisha hadhira
        • Hutoa hadhira kutoka ulimwengu wa hadithi hadi ulimwengu halisi.
          Zozote 3x1

MWONGOZO WA KIGOGO

  1.  
    1.  
      1. Msemaji ni Boza
      2. Msemewa ni Sudi
      3. Karakana yao katika soko la chapakazi
      4. Sudi alikuwa amekataa kumchongea Majoka kinyago cha Ngao bin Marar.
    2.  
      1. Methali – udongo haubishani na mfinyanzi
      2. Nidaa – watafuta maangamizi !
      3. Istiara / Jazanda – udongo (wanyonge) mfinyanzi – viongozi
    3.  
      1. Mlevi – Anabugia pombe Mangweni kwa Asiya
      2. Mwenye dharau – Anamwambia Sudi kuwa kukosa jina jingine yake inaitwa redio kwa kwa kukosa jina jingine.
      3. Mwenye taasubi ya kiume – Boza anadai kuwa Tuno anauza nyonga ilia pate mali (uasherati)
      4. Mcheshi – Anasema Sudi na Kombe walikuwa wanamwangalia kama ameota pua la pili.
      5. Mbinafsi – anakataa kuwajulisha Kombe na Sudi kuwa kulikuwa na mradi wa kuch0nga kinyago.
      6. Kikaragosi – Anaunga mkono utawala wa Majoka licha ya utawala huo kufunga soko la chapakazi aliko na karakana.
      7. Mjinga – Hakufahamu kuwa mkewe alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Ngurumo.
      8. Mwepesi wa hasira – yuko tayari kupigana na Sudi.
        Za kwanza 4 x1
    4.  
      1. Majoka alipanga njama iliyosababisha kifo cha Jabali aliyekuwa mpinzani wake mkuu.
      2. Majoka aliagiza kufungwa kwa runinga ya mzalendo kwa kupeperusha habari za mpinzani wake Tunu.
      3. Majoka aliagiza Ashua atiwe mbaroni ili kumshinikiza Sudi kumchongea kinyago cha Ngao bin Marara.
      4. Majoka aliagiza kuuawa kwa Tunu kwa kumpinga Tunu alivunjwa mguu.
      5. Majoka alitishia kufuvusha familia za kina Sudi na Kombe kwao kupitia vijikaratasi vya vitisho kwa kumpinga.
      6. Majoka alimwagiza Chopi kumchapa Ashua akiwa selini kwa kuwa alikuwa akimpinga.
      7. Majoka na Kenga wanapanga njama ya kumwangamiza Chopi wakihojia kuwa anaunga mkono Tunu.
      8. Majoka anawaongezea walimu na wauguzi waliogoma mshahara kisha anawaongezea kodi.
      9. Majoka anatishia kuwafurusha wafadhili waliokuwa wakimfadhili Tunu.
      10. Majoka anawaagiza maafisa wa polisi kutumia visasi na vitoza machozi kuwatawanya waandamanaji vijana watano waliouawa.
      11. Kingi alipokiuka amri ya Majoka ya kuwapiga visasi wanaSagamoyo waliokusanyika nje ya soko la chapakazi, Majoka alimfuta kazi.
      12. Majoka analifunga soko la chapakazi kama njia ya kuwafukarisha wanaSagamoyo waliokuwa wakimpinga kama vile Sudi.
        Za kwanza (10x1)
  2.  
    1.  
      1. Ufisadi: Majoka anamteua Kenga, binamuye kuwa mshauri wake mkuu.
      2. Usaliti: Watawala wanakusanya kodi lakini soko halisafishwi linanuka uvundo kutokana na maji ya taka.
      3. Ukatili: Vijana watano waliokuwa wakifanya maandamano wanauawa na polisi.
      4. Chuki za kikabila: vijikaratasi vinaenezwa kuwatia watu woga kutoka kabila Fulani.Kina Sudi wanatishiwa wahame Sagamoyo si kwao.
      5. Unafiki: Majoka anasema kuwa wanasagamoyo wasiruhusu watu wachache waliojazwa kasumba za kikoloni kuwarejesha katika utumwa. Anafanya mambo yaleyale anayoyakashifu.
      6. Ubadhirifu: Serikali ya Majoka inakopa pesa na kuziweka kwenye miradi isiyo na faida kama vile ya kuchonga kinyago cha Ngao bin Marara.
      7. Unyakuzi wa ardhi ya umma: Majoka ananyakua ardhi ya soko la chapakazi kujenga hoteli ya kifahari.
      8. Matumizi mabaya ya mamlaka. Kenga anamshauri Majoka kutumia mamlaka yake kuharamisha maandamano.
      9. Matumizi ya dawa za kulevya za pombe haramu.Wanafunzi katika shule ya Majoka and Majoka Academy wanageuzwa makabaji na dawa za kulevya/ Tunu anasema juzi waliwazuka watu waliofariki kwa kutumia pombe haramu na wengine wakageuka vipofu.
      10. Uozo: Mama pima anapewa kibali cha kuuza pombe haramu.
      11. Umaskini umekithiri katika eneo la sagamoyo.Watu waliosoma kama Sudi wanafanya kazi duni ya uchongaji vinyago.
      12. Tenga utawale. Majoka anatumia mbinu ya tenga utawale kuwaganya wanasagamoyo. Anawatenga Sudi na Tunu na kuwaleta karibu Ngurumo asiya na kenja.
      13. Ukosefu wa uhuru wa vyombo vya habari. Majoka anatishia kufunga runinga ya mzalendo na kubakisha tu sauti ya mashujaa.
      14. Tamaa: viongozi wamejawa na tamaa ya mali. Majoka anafunga soko la chapakazi ili ajenge hoteli yake ya kibinafsi.
      15. Uharibifu wa mazingira. Kigogo anafungulia biashara ya ukati miti na kutishia kuileta ukame sagamoyo.
      16. Mapendeleo ya kinasaba.Majoka anamteua Kenga binamuye kuwa mshauri wake mkuu.
      17. Majoka anapanga kumtambulisha Ngao junior kama mrithi wake.
        Zozote 10x1
    2.  
      • Anatumia jela. Majoka aliwafunga jela waliompinga.Alimfunga jela Ashua kwa kuwa alikuwa analipinga suala la kufunga soko la Chapakazi.
      • Anatumia askari. Majoka alitumia askari ili kuwatawanya waliokuwa wakiandamana kwa sababu ya kufungwa kwa soko. Ni askari wawa hawa ambao waliwaua vijana watano na kuwaumiza wachuzi kadhaa pale sokoni wakati wa maandamano.
      • Majoka anatumia mauaji. Majoka anajaribu kumuua Tunu kupitia askari wake Chopi japo hakufanikiwa. Vilevile alimwua Jabali, aliyekuwa mpinzani wake wa karibu kisiasa msimu aliopita kisha kusingizia kauawa kupitia ajali.
      • Vilevile anatumia vitisho ili kuwakomesha.Majoka, kupitia kwa Kenga, anamtishia Sudi kwa kumwambia kuwa asipomchongea kinyago siku moja atakuja kumtafuta.
      • Pia, anatumia ,mbinu ya tenga utawale. Wakati Tunu na Sudi wanakwenda kwenye ofisi ya Majoka, anaomba kuongea nao kila mmoja peke yake. Vilevile Majoka anajaribu kumwangamiza Tunu amtenganishe na Sudi.Hivyo itakuwa rahisi kubaki uongozini.
      • Anatumia mabarakala/ vibaraka. Hawa ni wafuasi sugu wa viongozi wanaosaidia viongozi kuwakomesha wapinzani. Ngurumo alitumiwa na Majoka ili kumwangamiza Tunu japo hawakufanikiwa.
      • Anatumia propaganda ili kuwatenganisha wapinzani. Majoka na watu wake wanaeneza uvumi kwamba Sudi na Ashua ndio wanaoiwinda roho ya Tunu.
      • Anatumiaushawishi. Kenga, mshauri wa Majoka anamshawishi Sudi kuchonga kinyago cha Ngao ili ipate malipo mazuri na maisha yake kubadilika. Kuwa jina lake litashamiri na apate tuzo nyingi, Zaidi ya hayo apate likizo ya mwezi mzima ughaibuni. Ahadi hizi zote ni za uongo.
      • Anatumiazawadi. Kenga anawaletea Sudi, Boza na Kombe zawadi ya keki kuwafumba macho ili wamuunge mkono Majoka.
      • Viongozi hutumia nguvu.Majoka anadai wafadhili wa wapinzani lazima wavunje kambi zao sagamoyo, kuwa Sagamoyo yajiweza.Anapanga kumkomesha Tunu dhidi ya kuongoza maandamano kwa kutumia nguvu kisha maafisa wa polisi watumie nguvu Zaidi.
      • Kudhibiti vyombo vya habari. Majoka anapanga kufunga vituo vya runinga Sagamoyo ili abakie na vichache anavyotaka vya kutangaza habari anazotaka.
      • Kufuta kazi wasiomuunga mkono: Majoka anamfuta kazi Kenga kwa kutomtii kupiga watu risasi sokoni Chapakazi.
        Zozote 10x1

SEHEMU YA B : RIWAYA           (Assumpta Matei : Chozi la Heri)

  1.  
    1.  
      • Haya ni maneno ya Ridhaa.
      • Yalimpitikia baada ya kumjibu Tila mawazoni.
      • Hii ni baada ya Ridhaa kukubali maneno ya Tila ya hapo awali.
      • Inaadhihirika kuwa amekubali kuwa yeye ni mgeni wala si mwenyeji.Al.4
    2. Swali la balagha – hapo ulipo sicho kitovu chako?
      Kuchanganya ndimi – historical injustice. Al.2
      1. Umuhimu wa Ridhaa
        • Ametumiwa na mwandishi kutuonyesha hasara iletwayo na ukabila.
        • Ni kielelezo cha watu wasiobagua watu wengine. Yeye hakujali wanakijiji wenzake wa ukoo gani bali yeye alitekeleza miradi ya maendeleo ili kuwafaidi wote.
        • Ametumiwa kuonyesha udhalimu wa watawala – anahadithia namna majumba yake yalivyobomolewa.
          Zozote 3x1 = alama 3
      2. Sifa za Ridhaa :
        • Ni mshirikina – milio ya kereng’ende na bundi inamtia kiwewe. Anamwambia Terry mkewe kuwa milio hii ni kama mbiu ya mgambo, huenda kukawa na jambo.
        • Ni mwepesi wa moyo – anapopatwa na mawazo ya hapo awali ambayo ni ya kukatisha tamaa, Analia kwa urahisi, kinyume na matarajio ya jamii kuwa mwanamume hafai kulia.
        • Ni mwenye bidi: alikuwa na bidi kubwa katika kazi yake ya kila aliyoiita ‘ujenzi wa taifa’.
        • Ni mvumilivu: Alivumilia matukio yaliyokumba kijijini mwake, yakiwemo kutotakikana huko na kufukuzwa, mali yake yaliharibiwa na familia yake kuuliwa. Anapiga moyo konde kukabiliana na hali hiyo mpya.
          Zozote 3x1 = alama 3
    3.  
      • Walichomewa nyumba zao – Ridhaa alichomewa nyumba yake ya kifahari.
      • Watu wao waliawa – familia ya Ridhaa ilichomwa na bwana Kedi jirani yao.
      • Watoto wao walibakwa – mabinti zake Kaizari walibakwa na vijana wenzao.
      • Walitoroka na kuacha makwao wakawa maskwota au wakimbizi wa ndani kwa ndani.
      • Walibaguliwa na wenyeji na kubandikwa majina subira anaitwa Maki.
      • Walikimbia na kutorokea msituni. 6x1 = 6
  2.  
    1.  
      1. Kuleta mauaji – Mamia ya roho zisizo na hatia zilisalimu amri chini ya pambaja za visasi.
      2. Uharibifu wa mali - Vita vilipozuka baada ya bi.Mwekevu kuchaguliwa, nyumba nyingi na mali ziliteketezwa.
      3. Wizi wa mali – Maduka ya wafanyabiashara yaliporwa walipotoroka vita vilivyozuka baada ya Bi. Mwekevu kuchaguliwa.
      4. Kusababisha wakimbizi wa ndani. Mamia ya watu walilazimika kutoroka kwao na kupiga kambi kwenye msitu wa mamba.
      5. Uharibifu wa mazingira – mizoga ya watu na wanyama, magufu ya majumba yaliyotekelezwa kwa moto na viunzi vya mumea iliyonyong’onyezwa na moto ilijikita kila mahali.
      6. Ubakaji – mwanaheri na lime walibakwa na mabarobaro watu, kwa sababu babake alikuwa akimwunga mkono Bi. Mwekevu.
      7. Vitisho – Bi.Mwekevu alipokea vitisho kutoka kwa wanaume kuna sababu ya kujitosa kwesa siana kama wanaume.
      8. Matusi – Bi. Mwekevu alipokea matusi kutoka kwa wanaume waliopinga azima yake ya kutoania uongozi.
      9. Kutengwa – Bi. Mwekevu alitengwa na jamii ya wanawake kwa kujitosa kwenye ulingo wa kisiasa uliotengewa wanaume.
      10. Hofu – Familia ya kaizari na wanafidhina wengine walipokuwa wakitoroka kwao walishuhudia mabasi yakichomwa, mifyatuko ya risasi na tanzia nyingine zilizowatia shaka na shauku.
      11. Kutenganisha ndoa. Subira walitengana na kaizari walitenganishwa.
      12. Ukabila – Jirani wa Ridhaa alikataa kuzungumzwa naye baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa.
      13. Utegemezi – ilibidi wageni kutoka mataifa ya nje kuja kudumisha Amani.
      14. Ukosefu wa ajira. Watu walikosa kazi baada ya machafuko yaliyozuka baada ya uchaguzi.
        Zozote (10x1)
    2.  
      1. Ndoa za mapema – pete aliozwa mapema akiwa darasa la saba ili kugharamia karo ya nduguye wa kiume.
      2. Ajira ya watoto – chandachema alilazimika kufanya kazi ili kugharama mahitaji yake.
      3. Kuleta taasubi ya kiume – pete anaozwa ili nduguye wa kiume.
      4. Utengano wa ndoa – Naomi alimwacha Lunga baada ya Lunga kufutwa kazi.
      5. Kutekeleza watoto – Naomi alitekeleza wanawe kutokana na umaskini wa babake.
      6. Kufanya kazi duni – Pete alilazimika kuuza pombe ili kukidhi mahitaji ya wanawe.
      7. Uozo – Pete alijaribu kuavya mimba kwa sababu hangeweza kuwalisha watoto wengi.
      8. Kukosa mtaji wa kuanzisha biashara – Mamake Kairu alikosa pesa za kuanzisha biashara nyingine baada ya biashara ya samaki kukumbwa na mzozo.
      9. Ulanguzi wa dawa za kulevya – Dick alishiriki biashara ya kulangua dawa za kulevya ili kutosheleza mahitaji yake.
      10. Wizi – Wanafidhina kadhaa wanangamana wakijaribu kufyonza mafuta kutoka kwa lori lililoanguka.
      11. Vifo – Makaa aliaga dunia alipokuwa akijaribu kuwaokoa maskini wakichota mafuta.
        Zozote 10 x 1
  3.  
    1.  
      1. Msemaji : kidawa
      2. Msemewa : Mwalimu mkuu
      3. Mahali : ofisini mwa mwalimu mkuu
      4. Mumewe Dadi alikuwa akishuku kuwa alikuwa na uhusiano na mwalimu mkuu hivyo akahiari kuacha kazi. (4x1)
    2.  
      1. Mwenye bidi – Anafanya kazi ya umetroni usiku na mchana alikuwa mchuuzi.
      2. Mwajibikaji – Anawajibikia familia za kazi yake ya umetroni.
      3. Mwenye mapenzi ya dhati – Anajipondoa ili kumfurahisha mumewe.
      4. Ni mpenda usasa – Anavalia mavazi ya kisasa. Alitaka Dadi amwoe kisasa.
      5. Mwenye mapuuza – Mwanzoni alimpuuza Dadi alipomtaka kimapenzi.
      6. Msomi – Alikuwa amesoma.
        (zozote 6x1)
    3. Sadfa : Mbinu inayonyesha kutendeka kwa mambo mawili au Zaidi kwa wakati mmoja bila matarajio au mpango. Mifano katika hadithi:
      • Dadi ambaye amekuwa akimpenda Kidawa kwa muda, lakini hajafanikiwa kamwe kumpata msichana huyu anayemvutia sana anaendelea na shughuli zake. Kisadfa anatokea Kidawa na kumfahamisha kwamba anampenda na sasa angetaka apange mpango ndipo amwoe. Haya ni mambo ndipo amwoe. Haya ni mambo mawili yanayotokea kwa wakati mmoja bila mpango.
      • Dadi anapitia mitaani akiwauza samaki anaowabeba kwa baiskeli. Kisadfa, Zuhura anayejifanya anataka samaki anatokea na kuanza kumpiga vijembe mwanaume huyu kutokana na kutumikishwa na mkewe katika shughuli za pale nyumbani. Hapa hakukuwa na mpango Dadi akutane na mwanamke huyu ndipo aanze kumpiga vijembe.
      • Inasadifu kwamba wakati mwalimu mkuu anapoendelea kushughulikia kazi zake nyingi mle ofisini ndipo Kidawa anapoingia kwa kutaka kuiacha kazi yake ya umetroni. Hapa hakukuwa na mpango mwanamke huyu aingie katika ofisi hii wakati mwalimu huyu anaposhughulikia kazi zake amfahamishe kutaka kuacha kazi kwake.
      • Dadi anapanda juu ghorofani ndipo afikie ofisi ya mwalimu mkuu kwa kutumia paipu ndipo achungulie kinachoendelea baina ya mwalimu mkuu huyu na mkewe Kidawa. Inasadifu kwamba wakati anapotaka kuchungulia hivi ndipo mkewe anapoingia katika ofisi hii.
      • Inasadifu wakati Dadi anapochungulia dirishani mwa ofisi ya mwalimu mkuu ndipo anapoonekana na watu akiwa amepanda kule juu kwa paipu kama mwizi anayetaka kuiba. Hakukuwa na mpango kwamba Dadi angapanda huko juu kwa paipu achungulie ofisini ndipo watu hao watokee.Hapo mambo haya mawili yametokea kisadfa.
      • Kuna mtu anayeanguka chini kutoka katika paipu aliyoning’inia kule juu ghorofani kutokana na kuonekana na watu na kuwaita walinzi wa shule. Inasadifu kwamba Kidawa anapofika pale anagundua kwamba ni mumewe aliyeanguka na kuumia sana. Hapa hapakuwa na mpango mwanamume huyu aanguke ndipo Kidawa atoke nje ya ofisi akiwa na mwalimu mkuu na kupata yule aliyeanguka ni mumewe.
      • Inasadifu kwamba Dadi anapoenda nyumbani kwa mwalimu mkuu kwa ajili ya kutaka kujua kama ameenda shuleni anafahamishwa na mke wa mwalimu huyo kwamba mumewe ameenda shuleni kwa kuwa ana kazi nyingi za kufanya kule. Hii ni sadfa kwa kuwa hapakuwa na mpango mwanamume huyu ampate pale nyumbani ama ampate akiwa ameenda shuleni.
        Zozote 3x2 = alama 6
        Majazi
        Kidawa – Kidawa amekuwa kama dawa kwa maradhi ya Dadi ya mapenzi.(2x2 = 4)
        Dadi – Dadi ni babake msichana kwa jina Shara. Huyu ni mtoto wa pekee wa Dadi na Kidawa kutokana na hali yao ya upangaji wa uzazi ambayo hairuhusu kupata watoto wengi.
  4.  
    1.  
      1. Mnenaji ni Mbura.
      2. Mnenewa ni Sasa.
      3. Wakiwa nyumbani kwa mzee Mambo.
      4. Walikuwa wamehudhuria sherehe kwa mzee Mambo na mwingine bila ualishi katika siku ya kusherehe ya kuingia darasa la chekechea kwa mtoto wa mzee Mambo na mwingine kutoa vijino viwili. Wanafika shereheni ikula, hata hivyo wanakula kilafi mpaka Mbura anaanza kujilaumu pamoja na Sasa, kwamba wanakula vyovyote wavipatavyo bila kuvichunguza n ahata kuvila vya wenzao waliowatangulia na watakaozaliwa. (4x1 =4)
    2. Fafanua tamathali ya usemi iliyotumika. (al.2)
      Istiara/ Jazanda – wanakula lakini hawawezi kumaliza kula – wanakula kila leo nab ado wanaendelea kula.  Ya kwanza 1x 2
    3.  
      1. Ni mfano mzuri wa watu walafi katika jamii.
      2. Ni kielelezo cha watu wanaofanya kazi ngumu na nzito lakini kufaidi mapato duni.
      3. Ni mfano wa watu walio na mapuuza. Wanafahamu uzembe uliopo miongoni mwa wafanyikazi wa serikali na unyakuzi wa mali ya umma, lakini hawachukui hatua mwafaka.
      4. Ni kielezo cha wanyonge katika jamii: Wanafaidi mabaki baada ya matajiri kujitwalia vyao.
      5. Ni mfano wa watu wanaojitolea kulihudumia taifa lao hata kama wametengwa mbali na hawatambuliwi katika taifa lao. Zozote 4x1 = 4
    4.  
      1. Viongozi wa mataifa yanayoendelea kutowajibikia kazi zao. Wanakubali bidhaa duni kurudidikwa katika mataifa yao: mchele wa basmati.
      2. Mali ya umma kunyakuliwa: DJanafungua duka la dawa zilizotolewa katika bohari ya serikali huku wanyonge wakiteseka.
      3. Serikali kuwalipa watu ambao hawafanyi kazi mishahara kubwa hivyo kudhoofisha uchumu wan chi – mzee Mambo.
      4. Kituo cha televisheni ya taifa kutumika kupeperusha matangazo ya sherehe ambazo hazina umuhimu wowote katika ujenzi wa taifa.
      5. Wananchi wengine badala ya kuchukua hatua mwafaka dhidi ya wanyakuzi, hungojea wakati wao ili nao wanyakue: Sasa na Mbura “… nasi si tuende – tusogee.
      6. Viongozi wananyakua mali ya mabilioni kwa hila na hawajali : Mzee Mambo anaandaa sherehe kubwa kwa sababu moto wake wa kwanza ameingia shule ya chekechea na yule wa mwisho ameota vijino viwili.
      7. Watu walio karibu na viongozi kupewa vyeo ilhali wanyonge hawana kazi : Mzee Mambo ana vyeo viwili.
      8. Wanyonge kufanya kazi ngumu na nzito kwa malipo duni : Sasa na Mbura; ilhali viongozi hawafanyi kazi bali wanapakua mishahara minono: Mzee Mambo.
      9. Viongozi kutowajibika katika kuchunguza utendakazi wa wanyikazi wao kwani hishinikiza wafanyi kazi kwenda kazini na sio kufanya kazi. Jambo linalohujumu uchumi wataifa.
      10. Wananchi kuchangia kuzorotesha uchumi wan chi izao kwa kufumbia macho unyakuzi unapoendelea na viongozi: Sasa na Mbura.
      11. Viongozi kutochunguza ubora wa vyakula vinavyoletwa shereheni. Vyakula vyenyewe vinaweza kuwa hatari kwa afya ya binadamu.
      12. Magari ya serikali kutumika katika sherehe za kibinafsi badala ya kuwahudumia wananchi.Magari haya yana beba mapambo; kupeleka watoto kuogeshwa katika sherehe ya Mzee Mambo.
      13. Watu kunyongana na kuuana ili wapate shibe hasa katika mataifa yanayoendelea.
      14. Wenye hadhi ya chini kuruhusiwa kuvitwaa vyao baada ya mabwanyenye kujinyakulia vyao. Wafanyavyo Sasa na Mbura.Za kwanza 10x1
  5. MAJIBU YA HEKO JESHI LETU
    1.  
      1. Hongera wanajeshi.
      2. Twashangilia jeshi.
      3. Heko ushindi Kenya.Yoyote 1x1
    2. Toni ya huzuni, hasira/ furaha jeshi liliposhinda.   (ya kwanza 1x2)
    3. nafsi neni –mzalendo, mkenya
      1. Kuanzisha/ kuleta uchokozi.
      2. Kuyashambulia maeneo ya pwani.
      3. Kupora watalii fedha.
      4. Kutupa maguruneti mijini.
      5. Wamevuruga Amani ya Wakenya. (Hoja zozote 3x2 = 6)
    4. tabdila-wakashambuliya
      Inkisari-ja,ilo,waso (zozote 2x2 = 4)
    5.  
      1. Beti = 7
      2. Mishororo = 5
      3. Vipande = 2
      4. Anwani – Heko jeshi letu. Zozote 4x1
    6. Maana za maneno :
      1. Magwanda – Mavazi rasmi ya kikundi fulani. (al.1)
      2. Mahandaki – Mashimo yanayochimbwa na wanajeshi ili kujihifadhi wakati wa vita. Mashimo hayo huwa na umbo maalum. (al.1)
      3. Maharamia – Wanyang’anyi, watu au kundi la watu wanaoumiza watu wasio na hatia. (al.1) 
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Murang'a County Mocks 2020/2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest