Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Mang'u Mock 2020 Exam

Share via Whatsapp

KISWAHILI
KARATASI YA TATU
MUDA: SAA 2

Maagizo

  • Jibu maswali manne pekee.
  • Swali la kwanza ni la lazima.
  • Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu zilizobaki yaani: Riwaya, Hadithi fupi na Ushairi.
  • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja. 

SEHEMU A: FASIHI SIMULIZI .

  1. Ngano za kichimbakazi zina sifa.(al. 2)
  2. Lakabu ina dhima tofauti. Toa mifano mitatu.(al. 3)
  3. Eleza kwa mifano mitatu matumizi ya lugha katika vitendawili.(al. 3)
  4. Eleza sifa nne za maapizo.(al. 4)
  5. Taja vipera viwili vya ushairi simulizi.(al. 2)
  6. Eleza vikwazo vitatu vinavyokumba fasihi simulizi.(al. 6)

SEHEMU B: RIWAYA: CHOZI LA HERI
Jibu Swali la 2 au la 3

  1. Maovu yametamalaki katika jamii ya Riwaya ya Chozi la Heri tetea kauli hii kwa kutolea hoja kumi zisizopingika (al. 20)
  2. Ukabila ni tatizo sugu katika nchi nyingi za kiafrika. Tetea kauli hii ukirejelea Chozi la Heri. (al. 20)

SEHEMU C: HADITHI FUPI: TUMBO LISILOSHIBA BA HADITHI NYINGINEZO
Jibu Swali la 4 au la 5 4.

  1. Shogake dada ana ndevu Alifa Chokocho
    Jadili sifa kumi za Safia (al. 20)
  2. "Mimi nimeamua kwa hiari yangu kukupa wewe zawadi hizo."
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili (al. 4) b)
    2. Eleza sifa za anayeambiwa maneno haya(al. 6)
    3. Huku ukitumia hoja, onyesha jinsi mzungumzaji alivyoitumia hiari yake vizuri (al. 10)

SEHEMU D: TAMTHILIA; KIGOGO
Jibu Swali la 6 au la 7

  1. Takwimu zako wazitia na kuzitoa visivy
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili (al. 4)
    2. Jadili sifa sita za mzungumziwa (al. 6)
    3. Fafanua kwa kina matatizo kumi yaliyowakumba Wanasagamoyo (al. 10)
  2. "Nilikuwa ninawaponza.......nilijua ninawadhuru wanasagamoyo lakini nilimezwa na tamaa."
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili (al. 4)
    2. Bainisha tamathali moja ya usemi inayojitokeza katika dondoo hili (al. 2)
    3. Jadili sifa nne za mzungumzaji (al. 4)
    4. Kwa kutukia hoja tano, onyesha jinsi tama ilivyowameza baadhi ya Wanasagamoyo (al. 10)

SEHEMU E: USHAIRI
Jibu Swali la 8 au la 9

  1. Soma Shairi lifuatalo kasha ujibu maswali yatakayofuata

    Vyote tumeuza
    Ni nyaka arobaini, tangu uhuru kupata
    Na bado tu baharini, bandari twaitafuta
    Uchumi u taabani, matopeni umenata
    Uhuria wa mapeni, bado hatukuudata
    Uchumi wetu benibeni, ufakiri watufata
    Umeanzia shambani, hata miji ukakita
    Kuiona afueni, ni ndoto ilokatika
    Vyote vyetu tumeuza, utamaduni hatuna

    Utamaduni hatuna, wa sisi kujitambua
    Desturi mezichana, vipande vimebakia
    La kulishika hatuna, mila tumeshaziua
    Hapana pa kukutana, muwili na nafsia
    Lugha asili hamna, Swahili hakikutua
    Si miaka mbali sana, ng'ambo 'tenda kinunua
    Kule tutajijazana, kusudi kutumegea
    Lugha yetu tumeiua, uyatima twajitia.

    Uyatima twajitia, tumeua utu wetu 
    Wenzetu kufikiria, si tena jukumu letu 
    Utumwani tumejitia, biashara tu vimatu 
    Bei watuamulia, kujibu hatuthubutu 
    Vikwazo metutilia, hatuna kauli katu
    Thamani wao waamua, ya mazao hapa kwetu 
    Ni fisadi kichungua, walinyonyajasho letu 
    Utu wetu wametwaa, uhuru wametuhini.

    Uhuru wametuhini, nasi twajidhalilisha
    Lugha yetu hatuoni, yao ndo twaimarisha
    Twajikaza kisabuni, kila hali jifundisha
    Imani hatwoneani, yumbishano hatujesha
    Hatuna utu asilani, twapatana kwa rashasha
    Zin'toka ughaibuni, risasi zisiponyesha
    Mebaki kuturubuni, wao wajitajirisha .
    Uwezo wetu meuza, huku twajiangamiza.

    Maswali
    1. Fafanua mambo matatu ambayo wanaonenewa wameuza (al. 3)
    2. Eleza kea kutoa mifano mitatu mbinu ambazo mshairi ametumia kutosheleza mahitaji ya kiarudi(al. 6)
    3. Ainisha shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo(al. 3)
      1. Mpangilio wa vina
      2. Mpangilio wa maneno
      3. Idadi ya mishororo katika beti
    4. Bainisha nafsineni katika shairi hili (al. 2)
    5. Fafanua toni ya shairi hili. (al. 2)
    6. Bainisha umuhimu wa tamathali mbili za usemi zilizotumika katika shairi hili (al. 4)
    1. Shairi A
      Ng'aa ninalia
      1. Ng'aa ng'aa ninalia, duniani ‘meingia
        Asante kuvumilia, miezi hiyo tisia
        Haki zote 'lipatia, nikala na kusinzia
        Endelea hudumia, mama 'sinitupe mama.

      2. Siwe mwisho ‘mefikia, wa tumbo kunijazia
        Makao nayo sikia, naomba kunikidhia
        Viguo hata kofia, mama zidi nipatia
        Joto lije nifikia, mama 'sinitupe mama.

      3. Chanjo zote nipatia, bila moja kuachia
        Ni haki wasimulia, binadamu kupatia
        Kiniacha 'taumia, sijiwezi ma sikia
        Nikuze sina hatia, mama 'sinitupe mama

      4. Nikue nipate afia, upate kufurahia
        Makao yaso udhia, niweze kujikalia
        Ni mwana sijatimia, sijiwezi na sikia
        Matusi kunepushia, mama 'sinitupe mama.

      5. Nipate pa kukulia, makuzi mema jazia
        Heshima 'takupatia, kinifunza njema tabia
        Elimu njema jazia, niwe mwema raia
        Nisimame kusifia, mama 'sinitupe mama.

      6. Mazingira kipatia, shidani sitakutia
        Uzima nahitajia, kula na kupumua
        Usafi wa kuvutia, ‘kinipa 'tafurahia
        Ya aibu hutasikia, mama 'sinitupe mama.
    2. Shairi B
      Baba mie naumia, elimu ninaitaka
      Najua kuwamama, tunayo mengi mashaka
      Wako wakati tumia, shule uje nipeleka
      Ada hutateseka, ni bure sasa kisomo.

      Mama nawe pimia, mlo upate kupika
      Hata uje nipimia, kidogo cha kuonjeka
      Hivyo sitaumia, njaa itajanitoka
      Nikila bila mashaka, takua n'ongeze kimo.

      Maswali
      1. Ni haki gani za kibinadamu zinarejelewa katika mashairi haya?Toa hoja mbilimbili kwa kila shairi(al. 4)
      2. Katika shairi B mtoto ana wasiwasi gani?(al. 2)
      3. Linganisha mashairi haya upande wa umbo(al. 6)
      4. Uhuru wa kishairi umetumika katika mashairi haya. Thibitisha kwa mifano minne, miwili kutoka kwa kila ushairi(al. 4)
      5. Eleza maana ya(al. 2)
        Haki zote lipatia, nikala na kusinzia
      6. Andika ubeti wan ne shairi 'A' kwa lugha nathari (al. 4)

MAAKIZO

SEHEMU A: FASIHI SIMULIZI .

  1. Ngano za kichimbakazi zina sifa.(al. 2)
    • Mhusika hukumbana na hasira nyingi/movu mwingi
    • Huhusisha uchawi, uganga, sihiri ambazo huchukua sehemu kubwa sana .
    • Huwa na matendo ya ukia maumbile
    • Mhusika mkuu hushinda mwishewe na kuishi maisha ya raha mstarehe.
  2. Lakabu ina dhima tofauti. Toa mifano mitatu.(al. 3)
    • Hutumiwa kusifia matendo chanya ya mhusika
    • Kukashifu/ kukejeli matendo hasi
    • Huwa kitambulisho cha mhusika kwani husa viri tabia au hali ya mtu Fulani kwa maneno mafupi.
    • Hutumiwa kama ishara ya heshima kama kumtaja jina la mkaza mwana ni mwiko kwa hivyo yeye hupewa lakabu 
    • Hutumiwa na baadhi ya wahusika kuficha utambulisho wao k.m waandishi
    • Hutumiwa kujigamba/kujinaki ili kuonyesha ubingwa wao
    • Hutumiwa kuhiadhi siri mtu asijue ndiye anaerejelewa
    • Hukuza uhusiano bor miongoni mwa watani
    • Hutumiwa kuondoa urasmi katika mahusiano ya kijamii na kurahisha mawasiliano
  3. Eleza kwa mifano mitatu matumizi ya lugha katika vitendawili.(al. 3)
    • Sitiri/ janda/ istiari
      • Fatuma mchafu (ufagio)
    • Tashihisi uhuishi
      • Amenifunika kotekote kwa blanketi lake jeusi - giza
    • Taashira/ Ishara
    • Sihizai dhihaka (kukashifu mienendo hasi)
      • Upera wa mwarabu unafukia moshi - chai ya maziwa
    • Kwelikinzari
      • Anjenga ingawa hana mikono - ndege
    • Tanakali za sauti
      • Prrr! Mpaka makka -utelezi
    • Takriri
      • Amezaliwa Ali, amekufa Ali, amerudi Ali - nywele
    • Taswira 
      • Nimemwona bikizee kajitwika machicha-mvi
    • Utata
      • Gani ka kila mtu - kifo, jeneza miguu
      • inachurwa, inaganda - damu, asali, gundi
    • Methali Ukichukua mamo, umchukue na mtoto - Sagio
  4. Eleza sifa nne za maapizo.(al. 4)
    • Hutolewa kwa mtu au watu ambao wameenda tofauti kinyume na matarajio ya jamii
    • Maapizo yalitolewa kablaya ulajiwa viapo
    • Yanaweza kutolewa moja kwa moja na Yule aliyethirika
    • Mtu maalum huteuliwa kutoa maapizo hasa wakati wa ulaji kiapo
    • Mungu, miungu au mizimu huweza kutoa maapizo kuhusu maisha ya baadae ya mhusika/ laana baada ya mhusika kukaidi amri za (adui)
    • Huaminiwa yataleta maangamizi kwa jamii hinyo wanajamii huelekezwa kuyaepuka kwa kutenda wema
    • Hutumia lugha fasaha (ulumbi) hasa kwa watoaji viapo
    • Lugha huwa kali inayotumiwa kujaza woga ili kuonya dhidi ya maevu
  5. Taja vipera viwili vya ushairi simulizi.(al. 2)
    • Maghani
      • Ngonjera ushairi wa kisemezano
    • Ngomezi
      • Mashairi ya kawaida
  6. Eleza vikwazo vitatu vinavyokumba fasihi simulizi.(al. 6)
    • Ushindani mkubwa kutoka kwa filamu/ video
    • Tarakilishi
    • Mafanano hawako tena
    • Ukosefu wa wakati wa masimulizi
    • Nyumba ndeu ni kikwamzo kwa ngomezi
    • Fasihi Simulizi kuhifdhiwa katika maandishi
    • Mkengeuko- utamaduni haudhaminiwi tena
    • Kuingiliana kwa tamaduni kwa sababu ya ndoa za mseto, uhamiaji na uhamaji nk.

SEHEMU B: RIWAYA: CHOZI LA HERI
Jibu Swali la 2 au la 3

  1. Maovu yametamalaki katika jamii ya Riwaya ya Chozi la Heri tetea kauli hii kwa kutolea hoja kumi zisizopingika (al. 20)
    • Katika jamii kuna biashara haramu kama ile uuzaji wa dawa za kulevya. Dick alipotekwa alilazimika kuuza dawa za kulevya kwa muda wa miaka kumi.
    • Kuna ukabila. Suala hili la ukabila ilijitokeza kikamilifu wakati kulizuka vita vya baada ya kutawazwa. Majironi waliwageuko wenzao ambao walikuwa wametoka katika kabila au ukoo tofauti na wao.
    • Kuna mauaji. Watu wengi walipoteza wapendwa wao kutokana na migogoro iliyozuka baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya.
    • Katika jamii kuna matumizi ya pombe haramu. Vijana wa vyuo vikuu wanabugia pombe hii ya suma inayowafanya wengine kuiaga dunia
    • Kuna ukeketaji wa watoto wa kike. Wasichana wa shule ya msingi wanapashwa tohara. Wasichana wengine wanayapoteza maisha yao huku wengine wakiponea chupu chupu na kuwa hospitalini kwa mfano Tuama anayeitetea mila hii iliyopitwa na wakati. Aliponea kidogo kuiaga dunia
    • Ndoa za mapema. Wasichana wachanga wanalazimishwa waolewe na wazee na kuacha masomo yao.
    • Kuna wizi, uporaji wa mali ya wengine. Wakati vita vya baada ya kutawazwa kuzuka, watu walionekana kupora maduka ya kihindi, kiarabu na hata ya wafrika wenzao
    • Katika jamii hii wanawake kuavya mimba. Sauna alipachikwa mimba na babake mlezi. Mamake mzazi akamsaidia kuavya kasha akamwonya dhidi ya kumwambia yeyote kuhusu unyama wa bebake.
    • Wanawake wengine katika jamii hii wanawache waume zao na kwenda kuyaishi maisha yao kwingineko. Mamake umekheri aliwaacha na kwenda kuishi mjini. Rejelea mhusika Naomi.

  2. Ukabila ni tatizo sugu katika nchi nyingi za kiafrika. Tetea kauli hii ukirejelea Chozi la Heri. (al. 20)
    • Ukabila ni matendo au fikira za mta za kuhamini kabila lake mwenyewe tu na kuwabagua wa makabila mengine. Ukabila umejitokeza kama ifuatavyo katika chozi la heri.
    • Subira alitengwa na familia ya mume wake kwa kuwa wa kabila tofauti na lao.
    • Mwana heri anatueleza kuwa mama yake alikuwa ametoka kwenye jamii ya mamwezi lakini babake alikuwa wa jamii tofauti. Kila Subira aliitwa 'mukit su huyo wa kuja kwa miaka mingi aliwezakuvumilia kubaguliwa, kufitiniwa na kulaumiwa kwa asiyoyatenda. Mwishowe alihiari kijiondokea na kwenda mjini ulikojinywea kinywaji kikali, akfaia alitegwa katika miche yao
    • Kijana mmoja alimwita 'mfuata myua' jambo lililomuumiza sana
    • Ridhaa. - Mzee Kedi alimtendea udhalimu Ridhaa nakuteketeza sila yake licha ya wao kuwa majirani kwa miaka hamsini.
    • Ridhaa alifanyiwa hivi kwa kuwa alikuwa ametoka kwenye kabila tofauti na Kedi.
    • Ami zake Kana walimsuta mno kwakumwoza mwana wao kwa mtu wa jamii tofauti na yao.
    • Walishangaa ni vipi mwana wao ataozwa kwa mtu wa ukoo ambao huvaa nguo ndani nje.
    • Waliamini kuwa ukoo huo huzaa majoka ambao hata kiporo cha juzi hayawezi kukupa ndoa ya Selume ilisambaratika baada ya vita vya kutawazwa kwa kiongozi mpya.
    • Alibaki mwenye kilio baada ya wambea kumfikishia ujumbe kuwa mume wake amekwisha kuoa msichana wa kikwao.
    • Tulia alimsaidia kaizai kufunganya na kumsindikiza hadi njia panda
    • Alimkumbatia na kumwambia kuwa mwenyezi Mungu ndiye hupanga na nguvu na mamlaka pia hutoka kwake.
    • Akamjuvya kuwa uongozi mpya umezua uhasama kati ya koo ambazo zimeishi kwa karibu kame moja

SEHEMU C: HADITHI FUPI: TUMBO LISILOSHIBA BA HADITHI NYINGINEZO
Jibu Swali la 4 au la 5 4.

  1. Shogake dada ana ndevu Alifa Chokocho
    Jadili sifa kumi za Safia (al. 20)
    • Huyu ni binti wa Bw. Masudi na Bi. Hamida.
    • Anasifika mno kwa tabia yake nzuri isiyokuwa na doa lolote.
    • Katika masomo yake alikuwa anaiongoza darasa
    • Ana kipawa cha uzingativu wa kiwango cha juu.
    • Ni msaidizi wa mama yake Bi. Hamida
    • Anamudu kazi zote za nyumbani
    • Anazifanya bila manung'uniko yoyote 
    • Ni mwenye tamaa: anatamani kufanya mapenzi na akatumia hila kutimiza lengo lake .
    • Alikuwa amejivika ngazi ya kondoo nje, ndani mbwa mwitu
    • Ni mjanja: anatumia maarifa na hila za kila namna ili kupata fursa ya kufanya mapenzi
    • Ni mwenye hasira: Bi Hamida anapomdadisi kuhusu hali yake ya kutapika, anapandisha hasira na kukimbia chumbani mwake.
    • Ni mwongo anadanganya kuwa ana malaria sugu
    • Anadanganya kuwa Kimwana anakuja ili wajadiliane kumbe anayekuja ni mvulana mwenye ndevu ndevu na wanafanya mapenzi
    • Ni muuaji anatoa mimba na kukidhulumu kiume kisicho na hatia. Mambo hayakwenda sawa na yeye akafariki
    • Ana ubinafsi: anafikiria yeye tu bila kujua madera ya kiumbe kilichomo ndani tumboni mwake
    • Ni mchangamfu: 'eye ana tabia ya uchangamfu ndiyo sababu mama aliyabaini mabadiliko haraka

  2. "Mimi nimeamua kwa hiari yangu kukupa wewe zawadi hizo."
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili (al. 4)
      • Haya ni maneno mwalimu Mosi.
      • Anamwambia Jairo
      • Wamo nyumbani mwa mwalimu Mosi 
      • Ni baada ya Mosi kumpa zawadi alizopewa siku yake ya kustaafu na Jairo akarudi kwake akiteta kwamba kufanya hivyo kulimuaibisha sana.

    2. Eleza sifa za anayeambiwa maneno haya(al. 6)
      • Mwenye parapara - Nusura aanguke alipopanda jukwaani kuhutubu kwa sababu ya haraka zake kukosa makini
      • Mwenye wivu - Kauli yake kwamba Baraka, Festo, Mshamba na Nangeto walikuja na magari kwenye sherehe za kustaafu kwa Mwalimu Mosi ili kuwatisha inadhihirisha wivu aliokuwa nao kwao
      • Mburbumbu - Hakuelewa chochote masomoni.
      • Katili - Anumwendea mwalimu Masina panga kwa lengo la kumkata baada ya kusikia uvumi kwamba Mosi alikuwa amemwoa bintiye
      • Mpyaro - Anamwita mwanafunzi aliyempelekea zawadi nyumbani kwake "hambe". Vilevile anamwita mwalimu Mosi maluumi.
      • Muungama - Anaungama na kumwomba Mosi msamaha kwa kumuumbulia jina kwamba alikuwa amemwoa bintiye .
      • Amekosa uwajibikaji - Ameitekeleza familia yake kwa kuiacha kwa Mwalimu Mosi.

    3. Huku ukitumia hoja, onyesha jinsi mzungumzaji alivyoitumia hiari yake vizuri (al. 10)
      • Anawasuta wanafunzi wake wa zamani kwa kuendeleza ubaguzi walipokuwa wakihutubu. Anawahimiza kuwapa watu wa matabaka yote nafasi ya kuzungumza Awaambia watu kumpigia Jairo makofi licha ya kutoa hotuba ya kumkashifu.
      • Anamwaalika Jairo kuketi kwenye jukwaa la wageni mashuhuri licha ya kwamba alikuwa amemuumbua katika hotuba yake.
      • Alimpa Jairo kumwita Mwendawazimu, yeye anamwambia kwamba hamna mwendawazimu wala mahoka kati yao.
      • Anitunza familia yao Jairo baada ya kuitoa kwake. Kama zawadi anaipa familia hiyo hata kiambo cha lushi.
      • Anawashauri wanafunzi wake kama Jairo kuendelea kufanya bidii masomoni licha ya kuwa zumbukuku.
      • Anawashauri wanafunzi wake kama vile Jairo dhidi ya ulevi na ufuska
      • Anamnunulia mwanawe Jairo; Sabina vitabu alipofukuzwa shuleni.
      • Anampeleka Sabian, mwanawe jairo kama mkewe wa pili licha ya kumlipa karo
      • Alikataa kumchukua mkewe Jairo kama mkewe wa pili licha ya mkewe Sera kumkubalia
      • Anamsifu Jairo kumwita 'hatibu mstahiki' licha kutoa hotuba ya kumuumbua

SEHEMU D: TAMTHILIA; KIGOGO
Jibu Swali la 6 au la 7

  1. Takwimu zako wazitia na kuzitoa visivyo
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili (al. 4)
      • Anaveongea ni majoka, anamwambia Ashua, wako ofisini kwa majoka, Ashua alikuwa anamsihi majoka afungue soko kwa sababu watoto wanalala njaa.
    2. Jadili sifa sita za mzungumziwa (al. 6)
      • (Majoka) Ni kiongozi wa jimbo la Sagamoyo.
      • Ni katili - Anaamuru Tunu auliwe, anavunjwa mfupa wa muundi. Anamwambia kingi awapige watu risasi katika soko Chapakazi
      • Ni mkware - Anapanga njama ta kumpata Ashua, anamtaka kimapenzi licha ya kuwa na mke na mtoto. Ashua anapofika ofisin mwake, antaka kumkumbatia na kumbusu.
      • Mwenye hasira - Anakasirika Ashua anapokutaa asimkumbatie na kusema kuwa hasira yake imeanza kufunganya virago, (ul 20)
      • Mwenye majisifu - Majoka anataka sifa, anauirahi sana Ashua anapomwita Ngao jina lake la ujana. Anajisifu kuwa yeye pia anajua kuzaa na wala si kuzaa tu bali kuzaa na kulea (uk.22) Mwenye dharau. - Anamdharau watoto wa Ashua kwa kuwai vichekechea (uk 22)
      • Mwenye dharau - Anamdharau Sudi mumewe Ashua kwa kumwita zebe. Anamdharau Tunu kuwa ni daktari na hana kazi ya maana. Tunu anapokataa poza ya Ngao Junior anamdharau kuwa msichana mdogo hata ubwabwa wa shingo haujamtoka
      • Mpenda anasa - Majoka amwambia Ahua asilie bali aseme ampendaye, astache kwenye kifua cha shujaa wake, (uk 22)
      • Anataka kumpa Ashua huba, anamwita muhibu wake, uk 21)
      • Mnafiki. - Anamwambia Ashua kuwa haja zako ni haja zangu shida zako ni shida zangu na kiu yako yangu." Nia yake ni kumteka Ashua kimapenzi, hana moyo wa kujali.
        Anadai kuwa hapendi rafu Ashua wanapopigana na Husda ofisini huku ni yeye huzua rafu Sagamoyo kwa kupanga mauaji hadi watu kuandantana
      • Mpyoro - Anawatusi wanasagamoyo kuwa wajinga katika soko la Chapakazi. Anamwita Sudi mumewe Asa Zebe." uliona nini kwa huyo zebe wako." (uk 24) .
      • Mwenye kiburi. - Anajita mwana wa shujaa kwamba ana akili ndipo kuwa mwana wa shujaa. Anasema kuwa anajifananisha na Samsoni Myaudi na shujaa Lyona wa Waswahili. Anadai kuwa Ashua amembandika jina la kumkwaza kwa kumwita mzee
      • Ni katili - Anamfungia Ashua licha ya kumwomba msamaha kuwa ananyonyesha
        Anapanga njama za muuaji bila kujali haki za raia. Anawafungia wanasagamoyo soko ambalo ni tegemeo lao bila kujali.
      • Ni dikteta - Majoka hutoa amri, polisi watawanye waandamanaji.Kenga anasubiri amri Majoka iliamkomeshe Tonu kufanya uchunguzi kuhusu kifo cha jabali.

    3. Fafanua kwa kina matatizo kumi yaliyowakumba Wanasagamoyo (al. 10)
      • Wanasagamoyo - Wataka soko lao lifunguliwe na kujengwa upya pia lisafishwe
      • Hawana usalama, askari wanatumiwa kuwatawanya na kuwatishia.
      • Wanaishi kwahofu. - Hawana uhuru wa kutangamano kwani viongozi wao wanahofia maandamano.
      • Haki zao zimekiukwa. Mauuaji yanapangwa kwa njama za kuwaangamiza .
      • Wanataka kujengewa hospitali, barabara na vyoo. Waletwe nguvu za umeme.
      • Wanataka wapate elimu Sagamoyo na ajira kwavijana
      • Wanasagamoyo wana njaa.
      • Walimu na wauguzi Sagamoyo wanamishahara duni. 
      • Kuna vilio Sagamoyo, mauaji yanapangwa. Wanasagamoyo wanataka mauaji haya yakome na haki kutendua.
      • Wanasagamoyo wananyanyaswa na viongozi, bei ya chakula inapandishwa ilihali wengi wa wananchi ni maskini
      • Mazingira Sagamoyo ni chafu hadi kuhatarisha maisha yao
      • Wanataka soko kusafishwa

  2. "Nilikuwa ninawaponza.......nilijua ninawadhuru wanasagamoyo lakini nilimezwa na tamaa."
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili (al. 4)
      • Ni maneno ya Mama pima/ Asiya Anamwambia Tunu/
      • Wanasagamoyo Wako nje ya lango kuu la soko la Chapakazi. Ni baada ya mapinduzi kutokea jimboni na pombe ya Mamapima ikawa imemwagwa na kwa hivyo akaamua kujiunga na raia wengine na kuwaomba msahama kwa kuwauzia pombe ambayo imewadhuru.
    2. Bainisha tamathali moja ya usemi inayojitokeza katika dondoo hili (al. 2)
      • Tashihisi - nilimezwa na tama

    3. Jadili sifa nne za mzungumzaji (al. 4)
      • Fisadi - Anapata kandarasi ya kuoka keki kwa kuwa yeye ni mkoi wa Husda; mkewe Majoka.
      • Mwenye vitisho. Anawaambia Sudi na Tunu kwamba amewapa dadika moja kuondoka nyumbani kwake la sivyo, watajua kwa nini anaitwa Mamapima
      • Katili - Anapika pombe ambayo imewaua na kuwapofusha wengi lakini haachi,
      • Mzinifu - Anazini na Ngurumo ilhali ana mumewe; Boza
      • Muungama. Anabadilika na kuomba msamaha kwa kupika pombe haramu iliyodhuru raia.

    4. Kwa kutukia hoja tano, onyesha jinsi tama ilivyowameza baadhi ya Wanasagamoyo (al. 10)
      • Tamaa inawasababisha wanaokusanya kodi kuitisha hongo kutoka kwa wafanyabiashara sokoni Chapakazi. -
      • Majoka anawapokonya raia ardhi ya soko ili kujenga hoteli yake na kuwaacha wafanyabiashara wakitaabika kwa maana hawana mahali pa kuuzia bidhaa zao.
      • Tamaa ya mali inamsababisha Kenga kukubali kutengewa kipande cha ardhi ya soko la Chapakazi ambayo imenyakuliwa na majoka
      • Tamaa ya pesa inamsababisha Ngurumo kutotaka soko lifunguliwe. Anasema kuwa tangu soko lifungwe mauzo ya pombe yalikuwa maradufu kwa maana wafanyabiashara wengi walihamia huko
      • Tamaa ya pesa inasababisha utawala wa Majoka kupandisha kodi wanayotozwa walimu na wauguzi baada ya kuwaongeza mshahara ili waendelee kulipwa mshahara duni
      • Tamaa ya kimwili inamfanya Majoka kumtamani Ashua na kutaka kuzini naye ilhali ana mkewe Husda.
        Aidha, tamaa ya uroda/ kimwili inamfanya Ngurumo kuzini na mkewe Boza, mamapima ilhali ana mkewe. -
      • Tamaa ya pesa inasababisha mkurugenzi katika kampuni ya Majoka kupandisha bei ya chakula kwenye kioski cha kampuni maradufu, hivyo kuwasababisha wafanyakazi kuandamana kupinga hali hiyo.
      • Tamaa ya mali inasababisha Majoka kumuua Jabali: kiongozi wa chama cha Mwenge ili kudhoofisha upinzani.
      • Tamaa ya kutaka kupata kandarasi ya kuoka keki inamsabisha Asiya kumpa Ngurumo uroda ili apate mradi huo
      • Tamaa ya pombe inawafanya wafanyabiashara kwenda kulewa badala ya kuungana na wenzao katika kupigania kufunguliwa kwa soko la Chapakazi
      • Tamaa ya kutaka kusalia uongozini daima inamsababisha Majoka kutaka kumrithisha mwanawe Ngao Junior uongozi wa Sagamoyo
      • Tamaa inasababisha Ashua kutoridhika na kila chopewa na mumewe Suudi Anataka zaidi ya uwezo wa Sudi
      • Majoka anatawaliwa na tamaa ya pesa hadi hataki kumfidia Bi. Hashima mumewe anakufa akifanya kazi kampuni yake.
      • Tamaa ya wanaume inamfanya Bi. Husda kumtazama Chopi kwa macho ya uchu licha yakuwa na mumewe Majoka
      • Tamaa ya pesa inasababisha Mamapima kuwapikia raia pombe haramu bila kuwazia madhara iliyowasababishia upofu na kifo.

SEHEMU E: USHAIRI
Jibu Swali la 8 au la 9

  1. Maswali

    1. Fafanua mambo matatu ambayo wanaonenewa wameuza (al. 3)
      • Utamaduni
      • Lugha asili
      • Utu
      • Uhuru
      • Imani
      • Uwezo
    2. Eleza kea kutoa mifano mitatu mbinu ambazo mshairi ametumia kutosheleza mahitaji ya kiarudi(al. 6)
      • Amefupisha maneno ili kupata mizani;
        • ilotaka - iliyokatika,
        • mettilia - wametulia
      • Kuinyanga sarufi ilia pate vina;
        • Ni fisadi kichungua, walinyonya jasho letu (kichungua wao ni fisadi)
      • Ritifaa ili kupata mizani sawa
        • Tenda-tutaenda; zin'toka
        • zinatoka
    3. Ainisha shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo(al. 3)
      1. Mpangilio wa vina 
        • ukaraguni kwa sababu hakuna urari wa vina
        • Pindu/ nyoka mkufu

      2. Mpangilio wa maneno
        • ____itamaduni hatuna

      3. Idadi ya mishororo katika beti
        • Ubeti II utamaduni hatuna, _________
          Ubeti ______ hatuma twajitia
          Ubeti III-uyatima twajitia ________
          _______uhuru wametuhini
          Ubeti IV Uhuru wametuhini___________

          Unane kwa sababu lina mishororo minane katika kila ubeti

    4. Bainisha nafsineni katika shairi hili (al. 2)
      • Nafsineni ni mzalendo/ mwananchi mkereketwa

    5. Fafanua toni ya shairi hili. (al. 2)
      • Toni ya huzuni kashfa malalamiko

    6. Bainisha umuhimu wa tamathali mbili za usemi zilizotumika katika shairi hili (al. 4)
      • Jazanda-vyote tumeuza kuwa tumekubali wageni kutuongoza katika hali zote hatuwezi kujiamulia mambo hatuna haki
      • Msemo - desturi mezichana-tomeweka toa desturi setu. Hatuna cha kujivunia. Kujikaza kisabuni, kujitahidi, kuonyesha jinsi waafrika wanajihidi kuufuata yaw engine hasa lagha.
      • Uhuishi - Ufikiri wetutata-kura umaskini mkubwa mwingi kila mahali. Hili kuonyesha jinsi wafrika wanaandamana na umaskini kwa sababu ya uchumi kuharibika. (geza mifano ya wanafunzi na madomo yao) (kutaja 1, kueleza I)


  2. Maswali
    1. Ni haki gani za kibinadamu zinarejelewa katika mashairi haya?Toa hoja mbilimbili kwa kila shairi(al. 4)
      • Mimba kutunzwa vyema
      • Makao
      • Mavazi
      • Chanjo
      • Aya njema
      • Tabia njema
      • Uzima
      • Usafi

    2. Katika shairi B mtoto ana wasiwasi gani?(al. 2)
      • Haki ya elimu
      • Chakula
      • Mtoto anahofia asikose elimu

    3. Linganisha mashairi haya upande wa umbo(al. 6)
      • Mashairi yote in tarbia kwa sababu yana mishororo mine katika kila ubeti
      • Yana vipande viwili ukwapi na utao (manthari/ mathnawi)
      • Hayana kibwagizo (Sabilia - Mizani ni kumi na sita katika kila mshororo
      • Kina cha kati ni'a' katika kila ubeti
    4. Uhuru wa kishairi umetumika katika mashairi haya. Thibitisha kwa mifano minne, miwili kutoka kwa kila ushairi(al. 4)
      • Shairi A 
        1. Inkisari-
          • Sikia-sitiliza
          • Zidi - uzidi
          • Nipatia- kunipatia
          • kunifunza-ukinifunza
          • Ma-mama 
        2. Tabdila 
          • Afia-afya
        3. Ritifaa
          • lipatia - alinipatia
          • Mafikia - umefikia
        4. Kufinyanga sarufi
          • 'siwe mwisho mefikia wa tumbo kinyazia' badala ya; Usiwe umefika mwisho wa kunijazia tumbo (Geza majibu ya wanafunzi)
      • Shairi B
        1. Inkisari
          • tumia - utatumia
          • hajatoka-itakuja kunitoka
        2. Mazida
          • Pima-pimia
        3. Kufinyanga sarufi
          • tunayo mengi mashaka-tunayo mashaka mengi
        4. Ritifaa
          • n'ongezee niongezee
            (geza)
    5. Eleza maana ya(al. 2)
      Haki zote lipatia, nikala na kusinzia
      • Haki zote lipatia, nikala na kusinzia - Ulindinda vyema kwa kunipa haki zote, nikakula na kulala
        (kule ndani ya mimba)
    6. Andika ubeti wan ne shairi 'A' kwa lugha nathari (al. 4)
      • Niongezeke kimo niliwa na afya hadi wenye ufata furaha raha
      • Niweze kukaa mahali ambapo hapana kero/ usumbufu
      • Mimi bado ni mtoto sijatimia/ sijakaa vizuri na ninasikiliza
      • Niweke mbali na matusi matukana tafadhali mama usije ukanitupa.
        (Akijibana kishairi asituzwe. Iwe aya moja tu na asipoteze maudhui)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Mang'u Mock 2020 Exam.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest