Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Meru Central Cluster Exam 2020

Share via Whatsapp

KISWAHILI
KARATASI YA PILI
UFAHAMU, MATUMIZI YA LUGHA NA ISIMU JAMII

MUDA: SAA 2 ½

MAAGIZO

  • Jibu maswali yote

 

  1. SEHEMU A: UFAHAMU (ALAMA 15)

    Huku ulimwengu unapoingia ya katika teknologia ya tarakilishi na sera ya utandaridhi, ukweli wa mambo ni kuwa akina mama wamezinduka. Suala la usawa wa kijinsia limeanza kushamiri kote duniani na ole wake mwanamume yeyote ambaye hajawa tayari kutembea na majira. Lakini hebu tuchunguze jambo hili kwa makini zaidi.

    Usawa wa jinsia ni nini? Usawa wa kijinsia ni usawa wa binadamu wote; wawe wake au waume. Usawa huu unapaswa kudhihirika katika kugawa nafasi za kazi, utoaji wa elimu, nafasi za uongozi na Nyanja zinginezo zozote za maisha.

    Ubaguzi wa aina yoyote ile hasa dhidi ya mwanamke ni jambo linalokabiliwa na vita vikali sana ulimwenguni kote.

    Dahari na dahari, hasa katika jamii za kiafrika kumekuwa na imani isiyotingizika kuwa mwanamke ni kiumbe duni akilinganishwa na mwanaume. Kwa hivyo mwanamke amekuwa akifanyiwa kila aina ya dhuluma ikiwepo kupigwa, kutukanwa, kudharauliwa, kunyimwa haki zake, kunyimwa heshima na mambo kama hayo, lakini je, ni kweli kuwa mwanamke ni kiumbe duni asiyefaa kutendewa haki?

    Tukichunguza jamii kwa makini tunaweza kuona mara moja kuwa hivyo ni imani potovu isiyo na mashiko yoyote. Ukimulika familia yoyote ile iliyopiga hatua kimaendeleo, uwezekano mkubwa ni kuwa mume na mke wa familia inayohusika wana ushirikiano mkubwa. Mume anamthamini mke wake na hadiriki kufanya maamuzi muhimu yanayoweza kuathiri maendeleo ya familia bila kumhusisha mke. Mume kama huyo huketi na mkewe, wakishauriana na kufikia uamuzi bora.

    Tukitoka katika muktadha wa kifamilia na kumulika ulimwengu wa kazi iwe ni katika afisi za serikali au kwenye makampuni binafsi, ukwerli ni kwamba kiongozi yeyote yule aliyefaulu katika usimamizi wake mara nyingi huwa na mke nyumbani ambaye wanashauiriana kila uchao kuhusu kazi anayofanya hata kama mke hafanyi kazi mahali pale. Hisia na mawaidha anayotoa mke kwa mume wake ni tunu na huenda asiyapate kwingineko kokote hata katika vitabu vya kupigiwa mifano. Hii ni mojawapo ya sababu ambayo huwafanya viongozi wa nchi mbalimbali kupenda sana kuwatambulisha wake na familia zao waziwazi kwa vile wanajua kuwa jamii inathamini sana msingi wa jamii. Kiongozi ambaye hana mke au familia au yule ambaye hana mke wake hatambuliki, hutiwa mashaka na jamii hata kama ni kiongozi aliye na azma ya kushikilia kazi ngumu ya kuongoza umma.

    Tukirudi nyuma kidogo na kupiga darubini mataifa ya mbali, tunaweza kuwaona wanawake mashuhuri walio uongozini ambao hadi waleo unapigiwa mfano. Wanawake mashuhuri waliotoa uongozini ambao hadi wa leo unapigiwa mfano. Wanawake hao walisimamia mojawapo ya mataifa yenye uwezo na ushawishi mkubwa Zaidi duniani. Ingawa wengi wao sasa wameng’atuka, uongozi wao bado unakumbukwa hata baada ya miaka mingi ya wao kuamua kupumzika ,mfano ni kama :Bi Bandranaike wa Sri lanka, Golda Meir wa Israel na wengine wengi katika mataifa kama Indonesia, Ufilipino, Bangladesh, Pakistani na kwingineko.

    Katika kufikia tamati, tunapozungumza kuhusu jinsia, hatuna budi kugusia kitafsili masuala nyeti. Kwanza,imani ya kushikilia kikiki tamaduni zisizofaa, ni jambo linalofaa kuchunguzwa kwa makini. Kwa mfano, kuna badhi ya jamii ambazo humlazimu mke kurithiwa baada ya kifo cha mumewe. Vile vile baadhi ya jamiii za kiafrika zinanshikilia kuwa mwanamke hana haki ya kurithi. Kutokana na Imani hii, wanawake wengi huishi maisha ya taabu baada ya kutengana na waume zao kwa vile hawana haki ya kurithi chochote kutoka kwa wazazi wao hata kama wazazi hao wana mali nyingi kupindukia. Mali ya wazazi ni haki ya watoto wa kiume wala si watoto wa kike! Hili ni jambo la kusikitisha mno.

    Isitoshe, wanawake hukumbukwa na kizingiti kingine wanapojaribu kumiliki mali ya waumezao baada ya waume hao kukata kamba .sababu ni kuwa,baada ya hao wenda zao kuwekwa kaburini, vita vya umiliki wa mali huanza mara moja na mwishowe yule mke maskini hujikuta hana hata mahali pa kulala sembuse mali waliyochuma na mali yake yote kunyakuliwa na aila ya mumewe . Jambo hili linaonyesha namna tulivyoachwa nyuma na uhalisia wa mambo. Ni lazima jamii izuinduke na itoke kwenye kiza hiki chenye maki nzito.

    MASWALI
    1. Ina maana gani kusema kuwa wanaume hawana budi “kutembea na majira” (alama 2)
    2. Kabla ya uzinduzi huu kuhusu usawa wa jinsia, wanawake wamekuwa wakitendewa dhuluma za kila aina. Taja tatu. (alama 3)
    3. Je, ni kwa nini viongozi wengi hupenda kujitambulisha na familia zao?(alama 2)
    4. Je, unaamini kuwa hisi na mawaidha anayatoa mke wa mume wake ni tunu na huenda yasipatikane kwingineko? Fafanua (alama 2)
    5. Je, licha ya kunyimwa haki yake ya kujiamulia, ni matatizi yapi mengine yanayoweza kumkumba mke anayelazimishwa kurithiwa? (alama 3)
    6. Eleza maana ya maneno yafuatayo jinsi yalivyotumiwa katika hali muktadha. (alama 3)
      1. Kushamiri
      2. Hulka
      3. Azma

  2. SEHEMU B: MUHTASARI(ALAMA 15)
    Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali yafuatayo.
    Idadi kubwa ya wanafunzi huingiwa na wasiwasi wakaribiapo kufanya mtihani kwa sababu mbalimbali, kubwa likiwa ni hofu kwa jinsi ambavyo watafanya katika mtihani huo. Asilani mambo hayafai kuwa hivyo. Wataalamu wa masuala ya saikolojia na wale wa elimu wanashauri kuwa mtahiniwa anafaaa kupata muda mwingi wa mapumziko wakati anapokaribia kufanya mtihani ili aweze kuituliza akili asije akapatwa na mzongo wa akili.

    Moja katika mashauri ni kuwa mtahiniwa anafaa kupata usingizi wa kutosha wakati akijiandaa na pia wakati akifanya mtihani. Hii ni kwa sababu mtihani wa mwisho si tofauti na mitihani mingine ambayo mtahiniwa amekuwa akifanya, pamoja na kuwa ni maswali ya jumla tu kutoka viwango vyote vya masomo. Hivyo basi, mtihani unapokaribia, mtahiniwa anafaa kudurusu na kufanya majaribio mbalimbali ya mtihani pamoja na kujikumbusha yale aliyofunzwa na mwalimu wake. Wale asimdunishe au kumdharau mwalimu hata kama stadi zake za kufundisha kazikumsisimua – alikupa kito cha thamani kitakachokufaa kama silaha wakati wa mtihani.

    Mtihani unapokaribia, mtahiniwa anafaa kuwa amekwisha kutambua udhaifu wake na kutia bidii kuudhibiti kupitia udurusu, mijadala na mashauriano. Kumbuka kuwa bidii haiui ila hulipa. Hivyo basi, kila unaposhirikisha bidii na ujasiri wa wako na kuimarisha uelewe wako wa somo, na hatimaye ukaboresha matokeo katika somo hilo. Vilevile, kujadili au kufafanua mada unayoielewa vyema kwa m wenzio aiyeielewa kutakuwezesha kuielewa hata Zaidi na hivyo kuimarisha uwezo wako wa kuzoa alama nyingi katika mtihani endapo swali litatoka katika mada hiyo.

    Pamoja na hayo, mtahiniwa anafaa kujihadhari na majuto ya kufanya kile ambacho hakupaswa kufanya. Anaweza kuhakikisha hili kwa kuyapitia maswali kwa makini Zaidi, na kuyatafakaria, kuyapangia na kuaandikia majibu sawasawa kasha kuyasoma tena majibu yake ili kuwa na uhakika kwamba hajapotoka.

    Ikiwezekana (kwa sababu ya tofauti za kimapato na uwezo wa wazazi au walezi) mtahhiniwa anafaa kula visuri kabla kuenda kufanya mtihani. Vilevile, anapaswa kufika katika chumba cha mtihani kwa wakati unaofaa – mapema kabla ya muda wa kuanza kwa mtihani – na ahakikishe amebeba kila kifaa atakachokihitaji katika mtihani huo.

    Ikiwa utashindwa kujibu swali Fulani, usipotezee muda mwingi. Baadala yake, enelea na swali linalofuatia kasha ulirejelee swali lile lililokutatiza baadaye ukishamaliza maswali yale mengine. Usipoteze muda kutafuta jibu ambalo huna kwa wakati huo. Juu ya yote, usidhubutu kuifanya hila katika mtihani kwa kuwa kitendo kama hicho kitasababisha matokeo yako kufutiliwa mbali, nayo bidii yako ya miaka mine itakuwa imeishia gizani, ukasalia kujuta.

    Maswali.
    1. Tumia maneno 60 kueleza ujumbe ulio katika aya mbili za mwanzo. (alama 6)
      Nakala chafu
      Jibu
    2. Mwandishi anatoa ushauri gani kwa mtahiniwa katika aya ya tatu hadi ya mwisho? Eleza kwa maneno 100 (alama 9)
      Nakala chafu
      Jibu

  3. SEHEMU C: MATUMIZI YA LUGHA.(ALAMA 40)
    1. Eleza ufauti ya kimsingi iliyopo kati ya irabu na konsonanti. (ala2)
    2. Taja sifa tatu bainifu za irabu /O/ (ala 3)
    3. Andika maneno yenye muundo ufuatao
      1. KKKIKI
      2. KKIKI (ala2)
    4. Andika tungo ya neno moja yenye viambishi vifuatavyo.
      1. Nafsi
      2. Njeo
      3. Kirejeshi
      4. Shamirisho
      5. Mzizi
      6. Kauli ya kufanyiza
      7. Kiishio (ala3)
    5. Andika vitenzi vifuatavyo katika hali ya kutendeana. (ala2)
      1. –la
      2. – nywa
    6. Andika sentensi ifuayo kulingana na maagizo. (ala2)
      1. Mhalifu alisamehewa kwa sababu alinyenyekea .
        Geuza maneno yaliyopigiwa mstari kuwa nomino.
    7. Andika kwa wingi
      Kelele ya amchaye Mungu ni baraka.
    8. Tambua aina ya vishazi katika sentensi hii
      Utazawadiwa ukicheza vizuri. (ala2)
    9. Tofautisha matumizi yapo katika sentensi hizi. (ala2)
      1. Alipomwona alimhoji.
      2. Amwonapo humhoji
    10. Bainisha aina za virai vilivyopigiwa mistari. (ala2)
      Ubaguzi wa kijinsia umekashifiwa mno na viongozi wenye msimamo thabiti mno.
    11. Unda nomino kutokana na vitenzi (ala2)
      1. Jaribu
      2. Chuma
    12. Eleza matumizi ya ‘na’ katika sentensi
      Wageni na wenyeji walikimbiliana  (ala 2)
    13. Andika katika msemo wa taarifa. (ala3)
      “Nitakuarifu nikimwona” Maria alisema
    14. Eleza maana mbili za sentensi (ala2)
      Tuliitwa na Juma
    15. Tumia “0” rejeshi katika sentensi ifuatayo
      Mtu ambaye hutupa tope hujichafua mwenyewe. (ala 2)
    16. Tumia visawe vya maneno yaliyopigiwa mstari kuandika tena sentensi ifuatayo.
      Ukuta umemwuumiza mvulana alipokuwa akiuparaga. (ala3)
    17. Changanua sentensi kwa njia ya jedwali.
      Ouma alianguka mtihani ila Kamau alifuzu vizuri. (ala4)

  4. SEHEMU D: ISIMUJAMII(ALAMA 10)
    Mtu 1: Wewe njoo hapa (kwa sauti kubwa) fanya upesi.
    Mtu II : (anakimbia mbio) Naja Sir
    Mtu I : (anamtazama) unajifanya mwelevu?
    Mtu II : Hapana Sir……eh…..afande
    Mtu I : Jina
    Mtu II : Samwel Kioko
    Mtu I : (Huku akiandika) Lete kitambulisho
    Mtu II : Sina hapa sir
    Mtu I : Huna kitambulisho? Utafanyiwa booking vipi?
    Mtu II : Naomba
    Mtu I : Naomba ! naomba! Unaomba nini? Wazururaji kama nyinyi tunawajua. Mnajifanya hamjui kuna curfew. Mnajiponza, “zerikali saidia”. Usiniharibie muda wangu (akiashiria) ingia ndani! Utakuwa mgeni wetu leo. Tutakukarimu chakula cha chumba.(anamsukuma ndani)
    1. Bainisha sajili ya makala haya. (ala2)
    2. Eleza sifa nne za sajili kwa kurejelea makala haya.(ala 8) 

MAAKIZO

  1. UFAHAMU
    1. Lazima wakubali mabadiliko / kuwa swala la mabadiliko kuhusu jinsia haliwezi kupuuziliwa mbali.(alama 2)
    2.    
      1. Kutukanwa
      2. Kudharauliwa
      3. Kunyimwa haki
      4. Kunyimwa heshima
      5. Kunyimwa nafasi za ajira, elimu, uongozi
        zozote tatu 3 x 1 = 3
    3.        
      1. Jamii inathamini sana misingi ya familia / mume na mke wa familia inayohusika wana ushirikiano mkubwa
      2. Kiongozi ambaye hana mke au familia au Yule ambaye mke wake hatambuliki, hutiwa mashaka na jamii hata kama kiongozi aliye na azma ya kushikilia kazi ngumu ya kuongoza umma. (alama 2)
    4.      
      1. Kwa sababu yatalenga mafanikio ya familia na mume.
      2. Kiongozi aliyefaulu katika usimamizi wake mara nyingi huwa na mke ambaye wanashauriana.
      3. Tunaweza kuwaona wanawake mashuhuri waliotoa uongozi ambao hadi wa leo unapigiwa mfano (2×1 = alama 2)
    5.        
      1. kukosa urithi
      2. Maisha ya dhiki.
      3. Kubaguliwa
      4. Magonjwa yanayoweza kuangamiza k.v ukimwi zozote tatu 3 x 1 = 3
    6.         
      1. Kushamiri - Kunawiri
      2. Hadiriki –hafai / hastahili
      3. Azma - Nia/ kusudi
        3 x 1 = 3
  2. UFUPISHO: MAJIBU
    1.    
      1. Wanafunzi wengi huhofia jinsi ambavyo watafanya katika mtihani.
      2. Wataalamu wanashauri kuwa mtahiniwa anafaa kupata muda mwingi wa kupumzika.
      3. Mtahiniwa anaweza kupata mzongo wa akili kwa kukosa mapumziko.
      4. Mtahiniwa apate usingizi wa kutosha wakati akifanya mtihani.
      5. Mtihani wa mwisho si tofauti na mwingine.
      6. Mtahiniwa afanye udurusu na majaribio ya mtihani mbalimbali.
        6x1
    2.      
      1. Awe ametambua udhaifu wake na kutia bidii . kaudhibiti kupitia udurusu, mijadala na mashauriano.
      2. Aulize maswali kuhusu mada asioielewa.
      3. Ajadili na kufafanua mada anayoielewa kwa mwenzake asieilewa.
      4. Ajihadhari na majuto ya kufanya kile hakupaswa kufanya.
      5. Ayapitie maswali kwa makini saidi na kuyaafakari kuyapangia nakuyaandika majibu sawasawa.
      6. Ayasome tena majibu kuhakikisha kuwa hajapotoka.
      7. Ale vizuri kabla ya kwenda kufanya mtihani.
      8. Afike katika chumba cha mtihani kwa muda unaofaa na akiwa amebeba kila anachohitaji.
      9. Asipoteze muda mwing kwa swali linalomshinda bali alirejelee baadaye.
      10. Asifanye hila katika mtihani kwani matokeo yake yatafutiliwa mbali.
        9x1 =9

  3. MAJIBU YA MATUMIZI YA LUGHA.
    1. Wakati wa kuamka konsonanti sauti hubanwa ihali katika kutamka irabu sauti hainanwi. (ala2)
    2.    
      1. irabu ya nyuma
      2. Irabu ya wastani
      3. Irabu ya viringwa (ala 3)
    3.     
      1. Ndwele
      2. Pweza (ala2)
    4. Niliowaimbisha, tunayemkimbiza, ninayempikisha. (ala3)
    5.      
      1. Liana
      2. nyweana (ala2
    6.        
      1. Kusamehewa kwa mhalify kulitokana na unynyekevu wake. (ala2)
      2. Msamaha ulitolewa kwa mhalifu kwa sababu ya unyenyekevu.
      3. Kunyenyekea kwa mhalifu lulifanya msamaha kutolewa.
    7. Kelele za wachao Mungu ni Baraka. (ala2)
    8.       
      1. Utazawadiwa - kishazi hur
      2. Ukicheza vizuri - kishazi tegemezi (ala2)
    9.       
      1. Wakati maalum (uliopa
      2. Wakati wa mazoea (ala2)
    10. Kwa kijinsia – RH
      Viongozi wenye msimamo thabiti mno - RN (ala2)
    11.      
      1. Jaribio/kujaribu
      2. Uchumi/kuchuma
        chumo/mchumi (ala2)
    12.       
      1. Na - kiunganishi
        Na = kutendeana (ala2)
    13. Maria alimwambia kuwa angemwarifu angewuona. (ala 3)
    14.        
      1. Juma alituhitaji kwenda kwake
      2. Mimi pamoja na Juma tuliitwa na mtu Fulani.
      3. Sisi pamoja na juma tuliitwa na mtu Fulani. (ala 2)
    15.       
      1. mtu anayejichafua mwenyewe ni yule atupaye tope.
      2. Mtu ajichafuaye mwenyewe ni yule atupaye tope.
      3. Mtu atupaye tope hujichaua mwenyewe
      4. Mtu atupaye tope ndiye ajichafuaye mwenyewe. (ala2)
    16.      
      1. Ukuta - kiambaza/sera
      2. Mvulana - mvuli/shababi/ghulamu
      3. Akiuparaga – panda, mwea, paramia, somber (ala 3)
    17.     
          S   
      S1    S2   
       KN KT     KN KT  
       N  T
      Ouma  alianguka  mtihani  ila  Kamau  alifuzu  vizuri 
  4. MAJIBU YA ISIMU JAMII
    1. Kituo cha polisi, mtu I anarejelewa kama afande. Anamhoji mshukiea/mtu II
    2.    
      1. Msamiati maluum – booking, curfew
      2. Lugha yenye toni kali – usiniharibie muda wangu,! Ingia ndani!
      3. Lugha yenye unyenyekevu (mshukiwa) mtu II amrejelea mtu I kama sir, afande, anaomba
      4. Kauli fupi fupi – Jina , Samwel Kioko
      5. Kuchanganya/kubadili msimbo – sir, curfew
      6. Lugha dadisi – maswali
      7. Uradidi/takriri – naomba naomba
      8. Lugha yenye kejeli – serikali saidia, naomba baada ya kujiponza.

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Meru Central Cluster Exam 2020.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest