Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Maranda Post Mocks 2020/2021

Share via Whatsapp
  1. Insha ya lazima
    Umesoma tangazo katika gazeti la Mzalendo kuhusu nafasi ya kazi ya Udaktari katika hospitali kuu kwenye kaunti yako. Andika barua ya kuomba kazi hiyo na uiambatanishe na tawasifu-kazi yako.
  2. Nchini Kenya, michezo ya kamari imeharibu vijana wengi sana na inastahili kupigwa marufuku. Jadili.
  3. Andika insha itakayothibitisha uweli wa methali 'Mwenye pupa, hadiriki kula tamu.'
  4. Andika insha itakayomalizikia kwa maneno haya.
    ...tangu siku hiyo sijawahi kuuasi ushauri wa wakuu.


Majibu

  1. Umesoma tangazo katika gazeti la Mzalendo kuhusu nafasi ya kazi ya Udaktari
    katika hospitali kuu kwenye kaunti yako. Andika barua ya kuomba kazi hiyo na
    uiambatanishe na tawasifu-kazi yako.
    • Hi ni barua Rasmi ya kuomba ajira ya udaktari
    • sura ya barua lazima iwe ifuatavyo:
      1. Anwani mbili ziwepo ya mwandishi na anayeandikiwa.
        Anwani ziwe wima:
        Mtajo;Kwa Bwana/bibi,
        MADA/KIINI/KUH kwa mfano KUH:KAZI YA UDAKTARI
      2. Utangulizi-uwe wa moja kwa moja bila salamu
      3. Mwili-Maudhui
        1. Tangazo alilipataje?gazeti lipi?Tarehe n.k.
        2. Maelezo ya kibinafsi-uraia, mahali pa kuzaliwa, n.k.
        3. Masomo/kiwango cha elimu kuanzia chekechea,msingi, upili na chuo kikuu.ufanisi katika vyango hivi vyote vya elimu.
        4. Tajiriba au ujuzi wa kazi hiyo na ufanisi tangu upate kazi inayohusiana na udaktari pengine uliyokuwa ukifanya ilikuwa ya kujitolea tu.
      4. Hitimisho-sahihi na jina la mwandishi
    • TAWASIFU-KAZI
      1. Kichwa kiwe na neno Tawasifu-kazi
      2. Habari ya maelezo ya kibinafsi k.m
        Jina-rasmi...............
        Tarehe ya kuzaliwa........
        Mahali pa kuzaliwa...........
        Jinsia...........
        Umri........
        Lugha......
        Dini................
        Anwani....
        Nambari ya kitambulisho......
        Barua pepe....
        Nambari ya simu............
      3. Elimu
        Kuanzia kiwango cha juu hadi cha chini
        Katika upande wa kushoto mwaka au wakati uandikwe ukiambatanishwa na viwango vya elimu
      4. Tajiriba
        1. Maelezo ya tajiriba ya kazi hii
        2. Anaweza kuonyesha tajiriba nyinginezo
      5. Uraibu km kusakata ngoma, kusoma n.k
      6. Uanachama k.m Chama cha Mazingira
      7. Wadhamini/Warejelewa-Mtahiniwa aonyeshe angalau wawili, majina yao, vyeo vyao,anwani na nambari zao za simu/barua pepe.
  2. Nchini Kenya michezo ya kamari imeharibu vijana wengi sana na inastahili kupigwa marufuku. Jadili.
    Michezo ya kamari imeleta faida kwa vijana kwa njia zifuatazo:
    1. Huleta ajira kwa vijana katika mashirika hayo ya kamari
    2. Serikali hupata ushuru
    3. Njia ya kujitajirisha kwa haraka
    4. Ni aina ya burudani inapotoka katika televisheni na Redio
    5. Kampuni hizi huweza kufadhili michezo na elimu
    6. Husaidia kupitisha wakati
    7. Husaidia katika kuinua jamii au kuzalisha mali kwa mfano mshindi atawapa wengine ajira.
      Michezo ya kamari imeharibu vijana kwa njia zifuatazo:
    8. Huchangia utovu wa nidhamu kwa mfano wizi ili wapate pesa za kushiriki katika michezo.
    9. Kufilisisha jamii kwa sababu ya utegemezi.
    10. Washiriki kutopanwa mawazo yao ya jinsi ya kupata riziki
    11. Ni njia ya kuvunja sheria
    12. kupotosha jamii kwa mfano washiriki hutumia pesa kwa mfano za kulipa karo na matumizi mengine kuucheza mchezo wa kamari.
    13. Huchangia wanafunzi kuacha shule.
    14. kuruhusu watu wa umri mdogo kushiriki
    15. Huwafanya vijana kuwa wavivu.
      Lazima ashughulikie pande zote mbili za swali na akishughuikia upande mmoja tu asipite alama 10.
  3. Andika insha itakayothibitisha ukweli wa methali :Mwenye pupa hadiriki kula tamu
    • Afanyaye mambo kwa pupa au kwa haraka bila uangalifu hupata madhara.
    • kisa kiguzie pande mbili za methali; kwanza kionyeshe hali ya kutokuwa na subira na pili, kionyeshe athari za kukosa subira.
    • maana si muhimu mradi tu atunge kisa ambacho ni kimoja tu.
    • lazima ashughulikie pande zote mbili za methali na akizingatia upande mmoja asipite alama 10
    • lazima awe na kichwa ambacho ni methali yenyewe na akikosa aadhibiwe kimtindo.
  4. Andika insha itakayomalizia kwa maneno haya.
    ...tangu siku hiyo sijawahi kuuasi ushauri wa wakuu.
    • Mtahiniwa atunge kisa kinachoashiria aliyeenda kinyume cha ushauri au Wosia au mawaidha aliyopewa akadhurika
    • Lazima awe na kichwa na bila kichwa ataadhibiwa kimtindo
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Maranda Post Mocks 2020/2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest