- UFAHAMU (Alama 15)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
Usasa na mabadiliko katika mitindo ya maisha kumechangia kuongezeka kwa idadi ya wasichana wadogo kupata mimba. Katika jamii ya zamani ya Kenya, msichana ambaye hajaolewa alipata mimba kwa tukizi sana. Lakini maadili ya kungani yamedidimia sana siku hizi na hivyo kujenga mazingira mwafaka ya wasichana kubeba mimba wakiwa bado wadogo. Imekuwa hali ya watoto kuzaa watoto wenzao. Sambamba ni ongezeko la wasichana wadogo wanaoshika mimba kuondolewa shuleni kwa fedheha inayoambatana na mimba nje ya ndoa.
Usasa umesambaratisha mfumo wa kitamaduni uliohakikisha kwamba akina nyanya wanawafunza wasichana mambo ya kiutuuzima. Vivyo hivyo usasa umewatenganisha wavulana na babu zao waliokuwa chanzo cha hekima ya mambo ya kiutuuzima. Wasichana chungu nzima wanazaliwa na kulelewa katika majiji na miji mbali na nyanya zao, vijana wengine wavulana kwa wasichana, wameachwa kutapatapa katika bahari ya maisha bila mwelekezo kwa vile wazazi wao wenye haya wanashindwa kuwakabili na kusema nao kuhusu mambo ya ngono. Wanabaki kuokotaokota porojo na hekaya za marika zao, majarida ya kutilika shaka, wavuti na sinema zisizoaminika. Vyanzo hivi vya maelezo kuhusu ngono vinachochea harara katika miili ya vijana hao wanaopitia mabadiliko ya kubaleghe.
Utukuzaji wa ngono unatilia shadda na kugeuza ngono kuwa bidhaa ya kibiashara. Hili huchangia dhana potovu kwamba ngono si tu chanzo cha ureda bali chanzo cha kipato. Baadhi ya wasichana wanalazimika kuchuuza miili yao ili kusaidia uzumbuaji wa riziki kwa familia zao. Mara nyingine tokeo ni kupachikwa mimba. Kuenea kwa ufukara kunawasukumiza wasichana wengine kuzika aibu zao na kutumia miili yao kama bidhaa ya kuuza.
Jamii ya leo inayopenda raha ina wanaume wenye ashiki za kinyama wanaowadandia wasichana wadogo na kuwabaka. Wakati mwingine huwaambukiza magonjwa ya zinaaa sikwambii mihadarati. Wasichana wanaotumia dawa za kulevya hawawezi kujidhibiti. Wanapoteza uhalisia wao na mtazamo wao wa kimaadili. Kwa hivyo, sio mno wao kuhusika katika utovu wa nidhamu ya kingono. Wanaweza kujiingiza katika maisha yanayowaweka katika hatari ya kupata himila. Vivyo hivyo wavulana na wanaume wanaotumia dawa za kulevya wanaweza kuwashawishi au kuwashurutisha wasichana kufanya mapenzi ya kiholela.
Kwa kweli dunia imebadilika sana siku hizi. Siku hizi kuna wasichana wengi wanaopachikwa mimba kabla ya ndoa kuliko enzi ya kabla uhuru. Athari ya himila hizo za mapema ni nyingi. Wasichana wadogo hujipata wamekuwa wazazi wa watoto ingawa wenyewe wangali watoto. Jukumu la kulea vitoto vyao huwa gumu. Hali huwa mbaya zaidi wavulana au wanaume waliowapachika mimba wanapodinda kuhusika au kukataa kusaidia gharama ya malezi. Ndipo kukawepo watoto wengi wanaolelewa na mzazi mmoja ambapo mara nyingi mzazi huyo mmoja tu ni mama. Baba anakuwa fumbo na tena mkimbizi mkubwa. Wakati mwingine msichana anapopata mimba hukataliwa na wazazi wake au kukatisha masomo yake. Aidha, anaweza akaathirika kiafya kwa kubebeshwa mimba ilihali mwili wake haujakomaa vya kutosha. Maisha humgeukia kuwa sawa na kukwea mlima Kilimanjaro.- Onyesha dhuluma nne dhidi ya jinsia ya kike katika jamii kwa mujibu wa kifungu hiki. (alama 4)
- Bainisha hali zinazoweza kulaumiwa kwa changamoto zinazowakumba vijana wasichana (alama 5)
- Eleza tofauti kati ya maisha ya zamani na maisha ya kisasa. (alama 3)
- Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika kifunguni. (alama 3)
- kunawasukumiza ..............
- harara ...................
- kupata himila ....
- UFUPISHO (Alama 15)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yafuatayo.
Katika karne hii, juhudi zetu za kushughulikia changamoto za usalama zimeimarishwa zaidi kwa matumizi ya teknolojia. Kuimarika kwa ufungaji milango, matumizi ya vifaa vya kamsa, njia za kisasa za utambuzi, utafiti na uchunguzi wa kiuhalifu ni baadhi tu ya maendeleo yaliyoafikiwa na jamii ili kujihami. Sasa hivi huduma zinazotolewa na polisi kwa umma zimewafikia watu kwa njia rahisi. Hata hivyo, maendeleo haya ya kiteknolojia yamehusishwa na hatari fulani. Baadhi ya mifumo inaweza kutumiwa vibaya au ikawa na athari zisizotarajiwa kama vile kumdhuru mtu asiyekusudiwa.
Matumizi ya sayansi na teknolojia katika kuukabili uhalifu wa jinai si suala geni. Tumeshuhudia maafisa wetu wakitumia vifaa vya utambuzi kwa alama za vidole na matumizi ya vifaa visivyotumia nyaya katika mawasiliano. Lakini kutokana na kuimarika kwa ubunifu wa wahalifu, pana haja ya vikosi vyetu kujipiga-msasa zaidi ili kuzuia au kuzima kabisa njama za kihalifu. Matumizi ya teknolojia katika kuzuia visa vya uhalifu yameanza kukubalika na wanajamii kama sehemu ya maisha yao. Leo hii kuna vifaa vya kuchunguza iwapo mtu ana kifaa chochote cha-chuma hususan-silaha ndegendege wakati aingiapo kwenye kumbi za umma au arrapoabiri magari ya uchukuzi wa umma. Kifaa hiki kimezuia pakubwa uhalifu wa tateleaji nyare uliokuwepo awali hasa miongoni mwa magari ya umma mijini. Aidha vifaa vya kudhibiti kasi ya magari vimeimarisha usalama barabarani. Uwekaji wa taa za umeme kwenye viunga vya miji huuhakikishia umma usalama wao na vilevile kuchangia kuwafichua wavamizi.
Kamera za siri kwenye ofisi za kibinafsi, majengo ya umma na kwenye baadhi ya barabara za miji mikuu huwa hifadhi ya matukio anuwai na hivyo kuwa muhimu wakati wa kesi zinazohusisha uvamizi au uhalifu mwingine wowote. Vifaa vidogo vinavyotumia mawimbi ya kielektroniki na ambavyo hutiwa mifukoni ni muhimu wakati wa mawasiliano ya dharura. Huwasaidia sana watu wenye umri mpevu ambao huwa ni windo jepesi la wahalifu. Aidha huwapa hakikisho la kuwa huru kuyaendesha maisha yao kinyume na awali ambapo maisha yao yalitawaliwa na unyanyapaa baada ya kusikia au kuhusika katika visa vya uhalifu. Kwa sasa Teknolojia inayotumia miate kufichua silaha haramu zilizofichwa au kumtambua mtu anayenuia kupenyeza mihadarati kwa kumeza vidonge inagonga ndipo. Njia hii hufanya hivi bila kumkaribia mshukiwa na kuepuka hali ya kuhatarisha maisha ya afisa wa ukaguzi. Aidha huwezesha mshukiwa kutambulika mara moja na hatari husika kutadarukiwa bila ajizi.
Licha ya ufaafu wa teknolojia ya kisasa katika kuzuia au kuzima kabisa visa vya uhalifu, athari zake hasi zimeweza kushuhudiwa. Kwa mfano matumizi ya vifaa vya kwenda kwa kasi kuwafuata wahalifu yanaweza kuwa hatari kwa mtumiaji, mshukiwa au hata raia asiyehusika. Kifaa cha kuzima kasi ya magari kwa mbali kinaweza kulisimamisha gari ghafla na kusababisha maafa makubwa. Matumizi ya mwangaza mkali au gesi kama njia ya kumdhibiti mhalifu yanaweza kusababisha ulemavu wa kuona au hata kupumua. Baadhi ya vifaa ambavyo hutumia miale vinaweza kuwa na athari ya kudumu na hata kusababisha maradhi ya kansa.
Inapendekezwa kuwa matumizi ya teknolojia kuangamiza uhalifu yazingatie haki za binadamu, Aidha njia husika iwe nafuu, pawe na uwazi na uwajibikaji katika matumizi yake na vilevile matumizi yake yazingatie maadili.- Dondoa mambo muhimu yanayojitokeza katika aya za kwanza tatu.(maneno 90-100)(alama 10, utiririko 1)
Matayarisho...
Jibu... - Ukirejelea aya tatu za mwisho, onyesha changamoto za teknolojia ya kisasa kwa maneno 45 - 50. (alama 5, utiririko 1)
Matayarisho...
Jibu...
- Dondoa mambo muhimu yanayojitokeza katika aya za kwanza tatu.(maneno 90-100)(alama 10, utiririko 1)
- MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)
- Tenganisha silabi katika neno iitwayo. (alama 1)
- Dondoa sauti zifuatazo katika neno mchungwani. (alama 1)
- Sauti mviringo .................
- Sauti mwambatano ............
- Geuza sentensi ifuatayo iwe katika kauli ya kutendesha. (alama 2)
Neto alimfanya Salim kuzoa takataka nyingi. - Andika kwa kinyume (alama 2)
Mvulana alizima moto kisha akaukunja mkeka. - Akifisha kifungu hiki.(alama 4)
wanyama fisi ndovu tembo rhino na ngiri wanyama wa pori wote hupatikana katika mbuga ya maasai mara - Andika katika wingi.
Mbuzi wa jirani wangu aliibwa na mama huyo. (alama 2) - Changanua kwa kutumia jedwali.
Mwizi alijaribu kujitetea lakini umati haukumwani kabisa. (alama 5) - Tumia kielezi kiigizi badala ya kile kilichopigiwa mstari. (alama 1)
Mbwa yule alibweka kwa hasira. - Tunga sentensi ya neno moja yenye sehemu zifuatazo za kisarufi:(alama 3)
kiwakilishi ngeli ya LI-YA wingi, wakati uliopita, kirejeshi, mzizi wa silabi moja, kauli tendwa, kiishio - Onyesha utakapoweka shadda katika maneno haya ili kutoa maana katika mabano. (alama 2)
- Walakini (kasoro)
- Nisaidie (sihi)
- Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo: (alama 2)
Tulibeba maji ya kutosha tulipoenda Tomoko. - Kwa kutolea mifano, taja matumizi matatu ya kiambishi m. (alama 3)
- Bainisha aina za nomino katika sentensi ifuatayo; (alama 2)
Uzuri amejiunga na aila yake ng'ambo. - Tunga sentensi yenye muundo ufuatao:(alama 2)
Kipozi+Kitenzi+RH cha wakati - Tumia mzizi 'erevu' kama kiwakilishi na kitenzi katika sentensi moja. (alama 2)
- Eleza majukumu mawili ya sentensi ifuatayo: (alama 2)
Panda mtini uangue matunda kwa vile yameiva vizuri. - Amrisha kwa kutumia kitenzi nywa katika nafsi ya pili wingi. (alama 1)
- Weka neno nywele katika ngeli mwafaka. (alama 1)
- Andika kisawe cha nahau funga ndoa. (alama 1)
- Andika methali anaoambiwa mtu anayefikiria kuwa ana vitu vingi na kuanza kuvitupatupa ovyo / kuvitumiatumia ovyo. (alama 1)
- ISIMU JAMII (Alama 10)
- Umepewa jukumu la kutoa ushauri nasaha (elekezi) kwa kijana mwenzako anayefikiria kujitoa uhai kuhusu manufaa ya kutojitoa uhai. Fafanua sifa sita za kimtindo utakazotumia ili kufanikisha mazungumzo yako. (alama 6)
- Kwa mifano minne, eleza namna muktadha unavyoathiri mitindo ya lugha. (alama 4)
Marking Scheme
- Ufahamu
- Onyesha dhuluma nne dhidi ya jinsia ya kike katika jamii kwa mujibu wa kifungu hiki. (alama 4)
- Kuondolewa shuleni /kukatisha masomo.
- Msichana anapopata mimba hukataliwa na wazazi.
- Wanaume kuwadandia wasichana wadogo na kuwabaka.
- Kuambukizwa magonjwa ya zinaaa.
- Kupachikwa mimba. Za kwanza 4x1=4
- Bainisha hali zinazoweza kulaumiwa kwa changamoto zinazowakumba vijana wasichana. (alama 5)
- Matumizi ya mihadarati / dawa za kulevya.
- Umaskini.
- Wanaume wenye ashiki.
- Mahitaji ya kifamilia.
- Ukosefu wa malezi bora au ushauri au mafunzo kutoka kwa wakubwa.
- Kugeuza ngono kuwa bidhaa ya kibiashara.
- Ureda
- Porojo na hekaya za marika zao, majarida ya kutilika shaka, wavuti na sinema zisizoaminika kuhusu ngono. Zozote 5x1=5
- Eleza tofauti kati ya maisha ya zamani na maisha ya kisasa. (alama 3)
- Wasichana zamani walipata mimba kinadra lakini sasa mimba kwa wasichana wadogo ni jambo la kawaida
- Zamani maadili yalizingatiwa sana lakini sasa yamedidimia.
- Zamani kina nyanya na babu walitoa mafunzo ya utuuzima kwa wajukuu jambo ambalo halipo nyakati za sasa. Zozote 3x1=3
- Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika kifunguni. (alama 3)
- Tukizi - nadra/muhali / ilikuwa ngumu
- Harara - hisia/mshawasha / nishai/tamaa/ shauku
- kupata himila-kuwa waja wazito / kupata mimba 3x1=3
Toza 1/2 alama kwa kila kosa la sarufi linapotokea mara ya kwanza hadi makosa sita.
Sarufi 1/2 hadi sita- alama 3
Hijai 1/2 hadi sita - alama 3
- Onyesha dhuluma nne dhidi ya jinsia ya kike katika jamii kwa mujibu wa kifungu hiki. (alama 4)
- UFUPISHO (Alama 15)
- Dondoa mambo muhimu yanayojitokeza katika aya za kwanza tatu.(maneno 80 - 90)(alama 10, utiririko 1)
- Juhudi za kushughulikia changamoto za usalama zimeimarishwa kwa matumizi ya teknolojia
- Huduma zinazotolewa na polisi kwa umma zimewafikia kwa njia rahisi.
- Maendeleo ya kiteknolojia yamehusishwa na hatari fulani.
- Matumizi ya sayansi na teknolojia katika kuukabili uhalifu wa jinai si suala geni.
- Kuimarika kwa ubunifu wa wahalifu.
- Vikosi vya usalama vinafaa kujipiga msasa zaidi ili kuzuia au kuzima kabisa njama za kihalifu.
- Matumizi ya teknolojia katika kuzuia visa vya uhalifu yameanza kukubalika na wanajarnii.
- Vifaa vya kuchunguza iwapo mtu ana kifaa chochote cha chuma vimezuia pakubwa uhalifu wa utekaji nyara.
- Vifaa vya kudhibiti kasi ya magari vimeimarisha usalama barabarani.
- Uwekaji wa taa za umeme kwenye viunga vya miji huuhakikishia umma usalama wao na kuwafichua wavamizi
- Kamera za siri ni muhimu wakati wa kesi zinazohusisha uvamizi au uhalifu.
- Vifaa vidogo vinavyotumia mawimbi ya kielektroniki ni muhimu wakati wa mawasiliano ya dharura.
- Wazee ni windo jepesi la wahalifu.
- Kuna teknolojia inayotumia miale kufichua silaha haramu au kumtambua mihadarati. (Yaliyomo-hoja 9x1=9) Mtiririko=1
- Ukirejelea aya tatu za mwisho, onyesha changamoto za teknolojia ya kisasa kwa maneno 45-50. (alama 5, utiririko 1)
- Vifaa vya kwenda kasi kuwafuata wahalifu huhatarisha mtumiaji, mshukiwa na raia.
- Kifaa cha kuzima kasi ya magari kwa mbali kinaweza kulisimamisha gari ghafla na kusababisha maafa makubwa.
- Matumizi ya mwangaza mkali au gesi kumdhibiti mhalifu husababisha ulemavu wa kuona na kupumua.
- Vifaa vinavyotumia miale huwa na athari ya kudumu na kusababisha maradhi ya kansa.
Yaliyomo - hoja 4 x 1 = 4 Mtiririko=1
(Alama=5) SARUFI = 6 x 1/2=3) HIJAI 6 X 1/2=3)
- Dondoa mambo muhimu yanayojitokeza katika aya za kwanza tatu.(maneno 80 - 90)(alama 10, utiririko 1)
- MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)
- i-i-twa - yo alama 1/0
-
- Sauti mviringo /u/
- Sauti mwambatano /ngw/ 2 x 1/2 = 1
- Neto alimzolesha Salim takataka nyingi. alama 2/0
- Mvulana aliwasha moto kisha akaukunjua mkeka. alama 2/0
- Wanyama ndovu / tembo, "rhino" na ngiri (wanyama wa pori wote) hupatikana katika Mbuga ya Maasai Mara. AU Wanyama ... ndovu / tembo, rhino na ngiri (wanyama wa pori wote) hupatikana katika Mbuga ya Maasai Mara.
8 x 1/2 = 4 - Mbuzi wa majirani zangu waliibwa na akina mama hao. alama 2/0
-
S S1 U S2 KN KT lakini KN KT N Ts T N T E Mwizi alijaribu kujitetea umati haukumwani kabisa - Mbwa yule alibweka bwe! alama 1/0
- Yaliyoliwa alama 3/0
-
- Wa 'lakini
- Nisaidi 'e 2 x 1 = 2
- Tulibeba maji ya kutosha - kishazi huru
tulipoenda Tomoko - kishazi tegemezi (2 x 1 = 2 - Kiambishi 'm'
- Nafsi ya pili wingi: mtakuja?
- Nafsi ya tatu umoja: alimletea
- Umbo la nomino za ngeli ya A-WA
- umoja: mtu - watu, mja - waja.
- Umbo la nomino za ngeli ya U- I umoja: mkate - mikate, mkono -mikono.
- Kuonyesha mahali ndani: mahali mle mna siafu.
- Kuonyesha weledi wa mtu/kuonyesha nomino/unominishaji: mpishi, mshoni, msomi. (3 x 1 = 3, matumizi = 1/2, mfano = 1/2)
- Uzuri-nomino ya pekee / maalum/mahsusi
Aila - nomino ya jamii / makundi 2 x 1 = 2 - Nyumba nzuri itajengwa hadi kesho. alama 2/0
- Mwerevu huumia mjinga akierevuka. alama 2/0
- Panda mtini uangue matunda - kuugiza/kuelekeza / sentensi agizi/elekezi. Yameiva vizuri - kutaarifu / kutoa ujumbe/ sentensi ya taarifa. 2 x 1 = 2
- Kunyweni! /mnyweni! alama 1/0
- U-ZI/ZI alama 1/0
- Pata jiko / asi ukapera alama 1/0
- Chovya chovya, humaliza buyu la asli. alama 1/0
SARUFI = ITEGEMEE ALAMA KWA SWALI HIJAI 6 x 1/2=3)
- ISIMUJAMII
-
- Kutumia lugha inayoeleweka/nyepesi/sahili/ya kufafanua. “Hamna faida yoyote ya kujiua."
- Kutumia maswali ya balagha ili kumshirikisha na kuvuta makini yake. "Ukijitoa uhai utanufaikaje?"
- Kutumia lugha ya mvuto/kushawishi/'Beste yangu fikiria maisha sio kifo.
- Kutumia lugha ya ucheshi 'Msee ukijimurder utanufaikaje sasa?'
- Kuchanganya au kubadili msimbo /lugha ili kusisitiza ujumbe na kurahisisha kuelewa.
"Kwani ukicommit suicide utanufaikaje?" - Kutumia viziada lugha ishara za uso, mikono, miondoko ya mwili ili kusisitiza hoja.
- Kutumia lugha ya kuelekeza/kushauri. "Maisha yako yana manufaa kuliko kifo."
- Kutumia chuku. "Ukijitoa uhai utaenda kwa shetani direct."
- Matumizi ya msamiati teule 'uhai,maisha,suicide,msongo wa akili, Mungu, Yesu Kristo.'
- Kutumia tasfida inapohitajika badala ya kutumia kauli kama kujiua unasema "kujitoa uhai."
- Matumizi ya lugha sanifu "Tafadhali fikiria tena maisha yako."
- Matumizi ya masimulizi ya visa vya watu waliofikiria kujitoa uhai lakini wakabadili nia,
- Matumizi ya nyimbo wimbo wa kumshinikiza asijiue.
- Kutumia toni /kiimbo cha ukali/ kuonya inapohitajika.
- Matumizi ya mbinu ya maombi/sala.
- Matumizi ya lugha legevu/isiyo sanifu. "msee, tumaisha uhitaji ujasiri: Punguza stress."
- Matumizi ya mbinu ya majibizano / kudadisi “Kwani ni yapi umepitia ukafikiria hivyo?"
- Kutumia sentesi/kauli fupi. "Beste yangu chagua maisha."
Za kwanza 6x1=6)
Tanbihi - mifano itolewe ili alama kamili itolewe.
- muktadha
- mzungumzaji huchota msamiati kutoka mahali anapozungumzia. Mfano: atatumia msamiati wa sokoni akiwa sokoni, lugha ya mahakamani akiwa mahakamani.
- Muktadha huathiri kiimbo. Mfano, mtu akiwa darasani huzungumzia kwa kiimbo cha chini.
- Muktadha huathiri uteuzi wa msimbo / lugha / lahaja ambayo mtu anatumia. Mfano, muktadha rasmi humtaka mtu kutumia lugha rasmi kama Kiswahili na Kiingereza. Muktadha hudhibiti kiwango cha usanifu na urasmi wa lugha. Mfano, muktadha usiyo rasmi hayahitaji kutumia lugha yenye usanifu na urasmi, mtu anaweza kutumia hata simo/misimu.
- Muktadha hudhibiti ishara anazotumia mtu. Zipo ishara nyingine na miondoko ambayo haikubaliki/ ni mwiko katika baadhi ya muktdha /tamaduni
- Muktadha hudhibiti mtindo nafsi wa mtu. Kwa mfano, mtu katika mnada au biashara ya Muktadha hud rejareja huweza kujirudiarudia ili kuwavutia wateja.
Za kwanza 4 x1 = 4
SARUFI = 4 x 1/2=2
HIJAI 4 x 1/2=2
-
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Maranda Post Mocks 2020/2021.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students