MAAGIZO
- Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
- Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
- Kila insha isipungue maneno 400.
- Kila insha ina alama 20.
- Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
MASWALI
- Lazima
Wimbi la utovu wa nidhamu ambalo limekuwa likivuma katika shule za sekondari za humu nchini linafaa kutafutiwa suluhu la haraka.Ukiwa mhariri mkuu wa gazeti la Kurunzi umeamua kulizamia suala hili. Andika tahariri. - Mitandao ya kijamii imechangia pakubwa utovu wa nidhamu shuleni. Jadili.
- Andika kisa kitakachodhihirisha maana ya methali; Mui huwa mwema.
- Endeleza kisa kifuatacho. Niligutuka ghafla, nikashangaa ni jambo lipi limenikataza usingizi wangu wa pono. Ndipo nikasikia mayowe kutoka kwa jirani. Nikakurupuka na kutoka nje mbio. Kumulika kwa jirani, nyumba yake haikuwa inaonekana...
MWONGOZO
- Wimbi la utovu wa nidhamu ambalo limekuwa likivuma katika shule za sekondari za humu nchini linafaa kutafutiwa suluhu ya haraka. Ukiwa mhariri mkuu wa gazeti la Kurunzi umeamua kulizamia suala hili. Andika tahariri.
Bila shaka,hali hii imechangiwa na mambo mengi na ambayo yanafaa kutafutiwa suluhisho ya haraka.
Hivi itahakikisha kuwa uharibifu ambao unaendelea kushuhudiwa nchini unakomeshwa.
Ikiwa wadau hawatalivalia njuga na kulizamia suala hili basi huenda shule zikapoteza mamilioni ya pesa pamoja na sekta ya elimu nchini kuishia kulemazwa.
Muundo- Kichwa
- Jina la gazeti libainishwe
- Tarehe,mwezi na mwaka wa chapisho iwekwe bayana
- Mada ya tahariri iandikwe kwa herufi kubwa na kupigiwa mstari
Utangulizi - Utangulizi ufafanue kiasi mada husika kwa aya moja.
Mwili/maendelezo - Maelezo yote yanayotolewa kuhusiana na mada yapangwe katika aya.
- Kila dhana itolewe ufafanuzi wa kina
Hitimisho - Hitimisha kwa kuandika jina na Cheo yaani Mhariri au Mhariri Mkuu
Tanbihi
Ikiwa mtahiniwa hatotaja jina la Gazeti “KURUNZI” kwenye kichwa, atozwe 2M baada ya kutuzwa. Mfano;
C+ 10/20-2M=08
GAZETI LA KURUNZI ALHAMISI ,DISEMBA 15, 2021
UTOVU WA NIDHAMU MIONGONI MWA WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI NCHINI
Au
GAZETI LA KURUNZI
ALHAMISI, DISEMBA 15, 2020
UTOVU WA NIDHAMU MIONGONI MWA WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI NCHINI
VISABABISHI/VICHOCHEO- Kuondolewa kwa adhabu ya viboko
- Uongozi mbaya wa kidikteta usiompa mwanafunzi usikizi
- Kutokana na baadhi ya wanafunzi kudhulumiwa na wanafunzi wenza au walimu
- Ukosefu wa mawasiliano bora baina ya walimu na wanafunzi
- Wanfunzi kujiunga na makundi mabaya
- Kuongezeka kwa utumizi wa dawa za kulevya
- Shinikizo kutoka nje
- Athari ya mabadiliko ya kiteknolojia
- Wazazi kutelekeza majukumu yao katika ulezi na uelekezi wa mwana
- Wanafunzi kuparamia na kuiga mienendo hasi ya kigeni
- Walimu kuzembea katika suala zima la uelekezi wa wanafunzi
- Kutokuwepo kwa idara ya ushauri nasaha katika baadhi shule
- Kuwepo kwa idara za ushauri nasaha zinazoendeshwa na walimu wasiohitimu katika tasnia ya ushauri
- Kuwepo kwa mtaala mpana wenye masomo mengi unaishia kuwapa wanafunzi shinikizo
- Kuwepo kwa elimu ya bure ambapo wanafunzi hawawajibiki kwa wazazi wao kwa kuwalipia karo
- Kuongezeka kwa vipindi vya kufundisha kwa walimu
- Uchache wa walimu shuleni
- Wanafunzi kupewa mamlaka ya kuchunguza walimu na kuripoti
- Wanafunzi kupewa mamlaka ya kuweka rekodi ya mahudhurio ya walimu ya vipindi
- Wanafunzi kuruhusiwa kukaa katika bodi za usimamizi wa shule na hivyo wao kujilinganisha na walimu
- Kuwakubalia wanafunzi kuenda shuleni na vifaa meme; sim una tarakilishi
- Kuwepo kwa walimu wanaowachochea wanafunzi dhidi ya usimamizi wa shule
- Kuruhusu wanafunzi waliopevuka kiumri kusoma na wanafunzi wa umri mdogo
- Wazazi wametelekeza jukumu la ulezi wa mwana na kuwaachia walimu
- Mabadiliko katika mfumo wa malezi ya mtoto, tofauti na zamani ambapo mtoto alikuwa wa jamii
SULUHISHO- Sheria kuhusu adhabu ya viboko irejelewe upya
- Utumizi wa vifaa meme shuleni miongoni mwa wanafunzi udhibitiwe
- Idadi ya masomo wanayotakiwa kusoma wanafunzi iangaziwe upya ili kumpunguzia mwanafunzi shinikizo
- Walimu wawajibike katika majukumu yao; kuelekeza,kushauri,kuelimisha
- Wazazi wawajibikie kikamilifu malezi ya watoto wao, badala ya wao kulitelekeza jukumu hili na kuwaachia walimu
- Mfumo wa zamani wa jamii kushiriki malezi ya mtoto urejelewe; mtoto ni wa jamii
- Kuanzisha idara za ushauri nasaha hasa katika shule zisizo na idara hii
- Walimu wanaosimamia idara ya ushauri nasaha wamakinikie majukumu yao ili kuwapa ushauri ufaao wanafunzi wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali
- Walimu wasimamizi wa idara za ushauri nasaha wapewe mafunzo maalum kuhusu jinsi ya kuwashauri wanafunzi
- Wanafunzi na walimu wanaoshukiwa kuhusika katika vitendo hivi vya utovu wa nidhamu wachukuliwe hatua kali za kisheria
- Serikali kuajiri walimu zaidi ili kukidhi nmahiji ya wanafunzi
- Wanafunzi waruhusiwe kushiriki katika michezo ya ndani na nje ya shule ili kupunguza mwemeo
- Viongozi wa kidini wahusike kikamilifu katika kuwaadilisha watoto kupitia kwa mafunzo kule maabadini
- Walimu na usimamizi wa shule ufungue njia za mawasiliano
- Usimamizi wa shule uwe makini katika kutambua uwepo wa makundi haramu shuleni
- Wanafunzi wanaopatikana wakitumia dawa za kulevya wachukuliwe hatua kali za kisheria
- Kichwa
- Hoja za kuunga mkono
- Kutazama filamu / video mitandaoni zinazochochea kuiga na kutaka kujaribu mambo mbalimbali kama vile kuchoma shule.
- Kutazama picha na video za ponografia mitandaoni kunasababisha utovu wa nidhamu kama vile ubasha na usagaji
- Kutazama video vinavyochochea vita husababisha fujo, rabsha na kupigana kwa wanafunzi au hata wanafunzi kuwavamia walimu
- Kutazama video mitandaoni kunasababisha wanafunzi kuiga tabia za wizi.
- Kuiga tabia za wahusika wenye uraibu wa vileo / mihadharati mitandaoni huweza kusababisha matumizi au ulanguzi wa dawa za kulevya shuleni.
- Matumizi ya simu na mitandao ya kijamii miongoni mwa wanafunzi huchangia udanganyifu katika mitihani
Hoja za kupinga- Mambo mengine yamechangia utovu wa nidhamu shuleni bali sio mitandao ya kijamii.
- Malezi mabaya miongoni mwa wazazi
- Shinikizo la rika/hirimu
- Ukengeushi miongoni mwa wanafunzi
- Wanafunzi kupewa hela nyingi za masurufu
- Kutaka kujinasibisha na kundi fulani
- Msongo wa mawzo
- Sheria au adhabu kali shuleni
- Utabaka miongoni mwa wanafunzi
- Vitisho kutoka kwa wanafunzi wengine
- Uhaba wa vielelezo bora katika jamii
Tanbihi- Mtahiniwa ajadili pande zote mbili za swali; namna mitandao ya kijamii imechangia utovu wa nidhamu na namna mambo.hali zingine ziechangia katika kuendeleza uovu huo.
- Anayerejelea upande mmoja atakuwa amepungukiwa kimaudhui. Asipite ala C+ 10/20
- Insha kamili itahusisha hoja saba zilizojadiliwa kikamilifu kutoka sehemu zote mbili
- Kuwepo kwa neno ‘pakubwa’ inaashiria kwamba kuwe na upande mmoja ulio na hoja nyingi kuliko nyingine.
- Atakayetoa hoja zinazolingana au kutoshana basi sharti aonyeshe msimamo wake.
- Mtahiniwa akadiriwe alama kwa kuzingatia maudhui na viwango mbalimbali vya urefu
- Mui – mtu mwovu / mbaya /tabia potovu
Kisa kilenge mtu mwovu anayebadilika na kuwa mzuri
Mtu aliyekuwa na tabia mbovu / potovu hatimaye anageuka na kuwa na tabia njema za kupigiwa mfano.
Sehemu mbili za methali zijitokeze waziwazi.
Umui unaweza kuhusisha tabia hasi nyingi au moja. Vilevile, wema unaweza kuwa mwingi au aina moja.
Mabadiliko yaandamane na kichocheo cha aina fualni kama vile: kushauriwa, kuadhibiwa, kufungwa jela n.k
Mifano:- Mwizi sugu kushikwa, kujeruhiwa, kuponea chapuchapu na mwishowe kuacha wizi na kuanza kazi zake mwenyewe.
- Mwanafunzi kiburi kutosikiliza walimu shuleni, kufeli mtihani na baadaye kujirudi baada ya kudhurika, anakuwa mtiifu na kupasi mtihani wake.
- Msichana anayependa ukware, anaambulia ujauzito. Anapitia machungu mengi hata kuwazia kujiua au kuavya mimba. Anajirudi baada ya kushauriwa na kuamua kumlea mwanawe na kuasi tabia potovu za ukware.
Tanbihi:
Anayeshughulikia upande mmoja wa methali asipite alama C+ 10/20
Kisa kisipolenga maana batini ya methali atakuwa amepotoka kimaudhui. Atuzwe
D 03/20
Atakayesimulia kisa kisichomhusu binadamu (pengine mnyama fulani) atakuwa amepotoka kimaudhui. Atuzwe D 03/20
Atakayekariri au kunakili swali atuzwe D 02-01/20
- Endeleza kisa kifuatacho
Niligituka ghafla. Nikashangaa ni jambo gani limenikataza usingizi wangu wa pono. Ndipo nikasikia mayowe kutoka kwa jirani. Nikakurupuka na kutoka nje mbio. Kumulika kwa jirani, nyumba yake haikuwa inaonekana...
Mwongozo- Mwanafunzi aendeleze kisa hiki.
- Ajihusishe katika kisa hiki – atumie nafsi ya kwanza.
- Kuporomoka kwa nyumba kwaweza kuhusishwa namaporomoko ya ardhi, mafuriko au mlipuko.
- Kisa chote kihusu kuokolewa kwa wahasiriwa.
- Kisa kiishe usiku huo.
Utuzaji- Atakayekosa kutumia nafsi ya kwanza atakuwa amejitungia swali – atuzwe D 03/20
- Kisa kionyeshe chanzo cha mayowe na uokozi wa wahasiriwa.
- Atakayekosa kuonyesha sehemu zote mbili atakuwa amejibu upande mmoja wa swali. Asipite C+ 10/20
- Vigezo vingine vya usahihishaji vikadiriwe vilivyo.
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Kenya High Post Mock 2023 Exams.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students