Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Lainaku 1 Joint PreMock Exams 2023
Get the complete Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Lainaku 1 Joint PreMock Exams 2023 PDF on WhatsApp by tapping on the button
Maagizo
- Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima
- Kisha chagua insha nyingine moja kati ya tatu zilizobakia
- Kila insha isipungue maneno 400
- Kila insha ina alama 20
- Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
- Watahiniwa wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
- Lazima
Umepata tangazo la nafasi ya kazi ya ualimu katika shule moja maarufu nchini kwenye gazeti la Pambazuko. Andika barua ya kuomba nafasi hii na uiambatanishe na wasifukazi wako. - Wanafunzi wa shule za kutwa wanakabiliwa na changamato nyingi katika juhudi zao za kupata elimu wakilinganishwa na wa shule za bweni. Jadili.
- Tunga kisa chenye kudhihirisha ukweli wa methali; Mchumia juani hulia kivulini.
- Andika kisa kitakachokamilika kwa maneno haya;
… tulifumukana huku nyuso zetu zikiwa na tabasamu la matumaini ya kuneemeka kwa maisha yetu ya baadaye.
MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA
- Insha ya Lazima
Ni insha ya barua rasmi
Sura- Muundo wa barua rasmi uzingatiwe
- Anwani mbili; ya mwandishi na ya mwandikiwa.
- Tarehe iandikwe chini ya anwani ya kwanza.
- Maamkizi; Bwana/Bi.
- Mada /kichwa
Mwili wa barua- Utangulizi- Aeleze kwa kifupi alipolisoma au kuliona tangazo
- Mwili- ufaafu wake katika hiyo nafasi.
- Hitimisho
- Ataje kuwa ameambatanisha barua yake na wasifukazi.
- Taratibu za kutamatisha barua zidhihirike kv. Wako mwaminifu, sahihi na jina lake
Wasifukazi / Tawasifu kazi / wasifutaala- Habari za kibinafsi
- Jina
- Jinsia / uana
- Umri / Tarehe ya kuzaliwa
- Hadhi katika ndoa
- Anwani – barua pepe/nambari ya simu
- Dini
- Lugha azijuazo
- Elimu
- Orodha ya shule alizohudhuria masomo – aanze kwa kiwango cha juu zaidi kwenda chini.
- Abainishe kipindi cha masomo kwa kuandika miaka kv. 1974 – 1980.
- Ataje cheti alichohitimu katika kila daraja ya masomo yake.
- Tajriba – ujuzi wa kikazi/maarifa.
- Ufanisi – Aeleze ufanisi wake – popote alipokuwa akifanya kazi hii anayoitafuta.
- Uraibu – Aorodheshe mambo anayopenda kufanya nje ya mazingira ya kazi rasmi.
- Wadhamini / warejelewa wawili au zaidi
- Jina la mdhamini.
- Vyeo / cheo chake.
- Anwani.
- Nambari ya simu.
- Barua pepe.
Tanbihi: Ni insha moja iliyo na vipengele viwili vikuu; - Sehemu ya barua rasmi.
- Tawasifukazi / wasifukazi
Kadiria kazi ya mwanafunzi ipasavyo ukizingatia muundo na maudhui.
- Habari za kibinafsi
- Ni insha ya mjadala wa kuunga au kupinga.
Hoja za kuunga- Kusafiri safari ndefu za kuelekea shuleni asubuhi na nyumbani jioni.
- Kukosa wakati wa kutosha kufundishwa saa za ziada.
- Kukubwa na changamoto za kifamilia nyumbani.
- Uwepo wa kuingizwa kwa matumizi ya mihadarati.
- Wasichana kutungwa mimba na baadaye kuingizwa katika ndoa za mapema.
- Makini yao kutekwa na vyombo vya kitekinolojia kama vile runinga na rununu, hivyo kukosa wakati murwa wa kudurusu.
- Kupewa majukumu mengi nyumbani baada ya kutoka shule.
- Athari za hali ya anga kv. Kunyeshewa na kutembea kwenye matope.
- Uchovu wa kutembea masafa marefu; kwenda shule na kurudi nyumbani.
- Kukosa kawi kama mafuta taa ama umeme kwao nyumbani – hivyo hawawezi kusoma jioni au usiku.
- Wengine kulazimika kufanya ajira ya watoto wakiwa nyumbani.
Hoja za kupinga - Hutangamana na wazazi kila siku – hivyo hawawezi kupotoka kwa urahisi.
- Wanakula vyakula wavipendavyo nyumbani wakilinganishwa na wenzao katika shule za bweni.
- Uhuru wa kusoma wakati wowote wakiwa nyumbani.
- Si rahisi kuathirika na shinikizo la rika kama wenzao katika mabweni.
- Wana nafasi ya kusaidia wazazi nyumbani; hivyo huwajibika.
- Gharama ya masomo katika shule za kutwa si kubwa kama ya shule za bweni.
Tanbihi: kadiria hoja nyingine sahihi.
- Ni insha ya methali
Atunge kisa chenye kudhihirisha maana na matumizi ya methali husika.
Pande zote mbili za methali zibainike- Kuchumia juani
- Kulia kivulini
Atakayeshughulikia upande mmoja tu, maki zake zisizidi (C+ 10)
- Insha ya mdokezo tamatishi
- Aandike kisa chenye kuafiki mwisho aliopewa.
- Utungo wake ukamilike kwa maneno aliyopewa.
- Kisa kijikite katika nafsi ya kwanza wingi.
- Asipotamatisha kwa maneno aliyopewa lichukuliwe kuwa kosa la kimtindo tu.
- Muundo wa barua rasmi uzingatiwe