KISWAHILI - Form 1 End of Term 1 2019 Examinations

Share via Whatsapp
  1. UFAHAMU

    Runinga na Ulimwengu wa Leo

    Siku moja nilikuwa hotelini kisiwani Lamu, au amu (kama wanavyokiita wenyeji) na rafiki yangu tukila wali na pweza. Aliingia mzee mmoja aliyefahamika kisiwani kwa ugwiji wake wa masuala ya lugha ya Kiswahili. Nilijiwa na hamu ya kumwuliza mzee huyo aliyepotea na kubobea katika Kiswahili, jinsi neno ‘runinga’ lilivyozuka.
    “Ahh, hilo” alishangaa kwa sauti kabla ya kuendelea, kijana kaa kitako nikweleze. Mswahili wa kwanza alipokiangalia kile chombo alishangaa. Kilikuwa kinaeleza na kuweka wazi mbele ya macho yake habari za ajabu. Hizi zilikotokea. Ni kitu kama uvumi hivi, huku kwetu tunasema ‘rununu’ basi ule si wa kusikia bali ni wa kuona; yaani kwa macho ambayo zamani yaliitwa maninga. Basi ikawa rununu ya maninga; mwishowe runinga’ alieleza mzee huyo kwa ufasaha mkubwa.
    Kila ninapokiwaza chombo kinachojulikana kama runinga au televisheni, kisa kile hufyatuka akilini na sura ya mzee huyo kunijia. Tangu kuvumbuliwa kwake mwanzo mwanzo wa karne ya ishirini, runinga imekuwa mojawapo wa vyanzo vikuu vya maarifa, taarifa, elimu na burudani kwa watazamaji. Kutokana na chombo hiki tunapata picha za matendo yanayotendeka kwenye maeneo yaliyoko mbali na tuishiko. Kinatufichulia majanga yanayowafika wenzetu kutokana na mbaa ya vita au njaa; huonyesha harakati za wanasayansi za kujaribu kuvumbua mambo mapya kwenye anga zetu. Aidha runinga hutusawiria matukio au ya kufurahisha. Runinga ni nyenzo muhimu ya kutuelimisha na hata kutuburudisha kutokana na vipindi vyake mbalimbali.
    Vipindi vya runinga huwa ni ishara za elektroniki ambazo hutumwa kama mawimbi ya redio na vyombo vinavyojulikana kama setilaiti au kwa matumizi ya kebo ambazo hupitishwa ardhini. Setilaiti ina uwezo wa kubadilisha ishara hizo na kuwa sauti na picha zinazoambatana na sauti hizo.
    Je, ushawahi kuwazia ni mambo yepi yanatokea katika studio za runinga hususan wakati wa kusomwa kwa taarifa ya habari? Aghalabu wakati wa kusomwa kwa taarifa ya habari ni sehemu ndogo sana ya studio inayoonekana. Asilimia kubwa huwa mefichwa pamoja na mashine za kila aina ambazo huhusika na uwasilishaji wa habari hizo. Aidha wahudumu wengine wanaohusika na majukumu mbalimbali kama udhibiti wa mwangaza, uekezaji wa wanaosoma kuhusu muda uliopo, mdhibiti wa kamera zionyeshazo picha mbalimbali anayekuza picha kuhakikisha picha zimeonekana vyema. Wapo wengine wanaoshughulika na majukumu anuai ambao hawaonyeshwi.
    Mbele ya msomaji wa taarifa hizo huwa kuna televisheni ndogo ambayo haionekani na ambayo humwonyesha picha zinazoonyeshwa. Aghalabu hatuwaoni wasomaji wengi wa taarifa za habari wakisoma habari zao kutoka maandishi wazi. Hali hii inatokana na kuwepo kwa kielekezi-runinga ambacho anakitumia. Msomaji huyu, husoma taarifa zake kutokana na maandishi yanayoonekana kwenye mulishi au kiwambo cha kielezi hicho. Maneno hayo hukuzwa kwa njia mbili mbele ya lensi za kamera na kuweza kusomeka vizuri. Yupo opareta ambaye kazi yake kuu ni kuhakikisha kuwa amedhibiti kasi ya maneno yanayoonekana kwenye kielekezi-runinga hicho. Pia msomaji wake akitumia kifaa maalum. Hata hivyo, msomaji huwa na nakala nyingine ya habari iliyoandikwa anayoweza kuisoma iwapo pana hitilafu fulani ya kielekezi-runinga.
    Wataalamu wa chumba kikuu cha kuyadhibiti matangazo hutumia vifaa maalumu vya sauti kuwakumbusha watangazaji kuhusu vipindi vya kupumzika kwa ajili ya matangazo ya biashara au mabadiliko yoyote katika mpangilio wa kipindi Fulani. Huwapo pia wataalamu wanaohakikisha kuwa picha zinazopatikana kwenye runinga ni sahihi na zinakubalika. Kutokana na majukumu mbalimbali ya wanaohusika, watazamaji wanapata picha nzuri na sauti zinazoafiki picha hizo. Hii ni siri mojawapo ya siri nyingi ambazo zimefubwatwa na uvumbuvi wa kisayansi.
    Kama watazamaji wa runinga labda tunaishia kukubaliana na Yule mzee wa Lamu kuwa chombo hiki kina maajabu ya macho. Maajabu hayo yanatuelimisha, kutujuza, kutukumbusha na kutufanya tushirikiane na wenzetu walio mbali sana katika matukio yetu. Masafa yaliyoko kati yao yanafupishwa kwa kuwa wanatujia kwenye vyumba vyetu kama nasi tunavyofanya huko kwao.  

    MASWALI
    1. Ni nini chanzo cha neno ‘runinga’? (al 2)
    2. Taja faida   nne za runinga (al 4)
    3. Tunaweza kutazama picha za runinga kutoka kwenye vituo mbalimbali vya televisheni. Ni njia gani ipi inayotuwezesha kutazama vipindi vya runinga? (al2)
    4. Wakati wa kusomwa kwa taarifa za habari kuna wataalamu mbalimbali wanaohusika. Taja watatu  (al 3)                                           
    5. Je, kwa nini mara nyingi msomaji wa habari haonekani kusoma habari bali huongea   akiangalia watazamaji tu? (al 2)
    6. Taja michezo miwili ya kimataifa iliyo maarufu zaidi inayotangazwa moja kwa moja kupitia runinga kote ulimwenguni. (al 2)
  2. MATUMIZI YA LUGHA
    1. Taja ala nne za kutamkia sauti, mbili tuli na mbili sogezi (al 4)
    2. Ni ipi tofauti kuu kati ya konsonanti na irabu (al 2)
    3. Taja sauti mbili mbili ambazo ni: (al 3)
      1. Vipasuo
      2. Nazal
      3. Viyeyusho
    4.  
      1. Maktaba ni nini? (al 1)
      2. Taja aina mbili za maktaba (al 2
    5. Andika sentensi hizi kwa wingi (al 2)
      1. Kifaru huyu ni mkubwa
      2. Kijiti kikubwa kilitumiwa kumuua nyoka.
    6. Weka shadda katika neno barabara kwa jinsi mbili na uonyeshe tofauti kimaana.                                                                                                 (al 2)
    7. Eleza maana ya kiimbo.  (al 2)
    8. Andika maneno mawili mawili yenye silabi zenye miundo hii: (al 2)
      1. KKI
      2. KKKI
    9. Taja sifa zozote nne za lugha (al 4)
    10. Kanusha sentensi hizi
      1. Amekuwa akisoma kwa miaka miwili (al 1)
      2. Tuliimba na kuvuna mahindi (al 1)
      3. Amekuja (al 1)
    11. Kamilisha methali hizi
      1. _____________________________si ndo ndo ndo  (al 1)
      2. Mkono mtupu ________________________________ (al 1)
      3. _____________________________mpende (al 1)
    12. Taja aina mbili za viambishi (al 2)
    13. Sahihisha sentensi hizi (al 3)
      1. Kitabu hii yangu nilinunuliwa na mama.
      2. Kijana mwenye alisoma vizuri alituzwa.
      3. Mtoto ambaye aliyepotea ni wa Kamau.
    14. Kamusi humsaidia mwanafunzi kwa njia gani tatu? (al 3)
  3. ISIMU JAMII
    1. Eleza maana ya Isimu Jamii (al 2)
    2. Taja mambo manne ambayo sajili lugha hutegemea. (al 4)       
  4. FASIHI (Alama 15)
    1. Taja na ufafanue aina mbili kuu za fasihi. (al 4)
    2. Fafanua dhima/umuhimu wa fasihi (al 7)
    3. Taja tanzu nne za fasihi andishi (al 4)

Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI - Form 1 End of Term 1 2019 Examinations.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest