Kiswahili Questions and Answers - Form 1 End Term 3 Exams 2021

Share via Whatsapp

MAAGIZO
Jibu maswali yote.



MASWALI

SEHEMU YA KWANZA
Mwandikie mwalimu mkuu barua ukimweleza kilichokufanya kutofungua shule mapema
mwanzoni mwa muhula wa kwanza.

SEHEMU YA A: UFAHAMU

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuatia.
Sagamba aliikodolea macho saa ya ukutani. Saa kumi na moja kasoro dakika tano. Hapo alianza kuyarudisha mapazia ya dirisha la ofisi. Alipanga ya kazi na kuanza kutoka. Mara rununu ikatoa mlio. Kisha ikazima. Aliitazama majalada na kuona aliyiempigia. Alitabasamu na kuirudisha rununu mfukoni.

Zilizala ilikuwa baa maarufu sana mjini. Sagamba na wenzake waliitwa ‘wanachama wa kudumu’ kwa uzoefu wao wa kwenda hapo. Mara simu lilia tena. Sagamba aliichukua na kuitazama kwa muda. Alisonya kwa hasira kabla kuisogeza sikioni. “Halo! Tafadhali rudi nyumbani mapema, mtoto hasikii vizuri,” sauti hiyo ilisema. Alikuwa mkewe. Sagamba aliizima simu kabisa huku akisema, “Sitaki kusumbuliwa. Yaani mtoto anakuwa mgonjwa mwisho wa mwezi ambapo nimepata donge langu nono?” Sagamba alikuwa amepata mkopo wa laki mbili kutoka kwa chama cha akiba na mikopo kwao kazini. Mifukoni alifutika vitita vya noti za elfu elfu. Ndani ya baa alizingrwa mithili ya nyuki wanapozuru ua lenye mbelewele.
Huko nyumbani mkewe alijaribu kumpigia simu mumewe asimpate. Simu ilikuwa imezimwa. Mtoto alizidiwa maradhi na kuwa hoi. Mama hakusubiri, kwani uchungu wa mwana aujuaye mzazi. Alimfunga mbeleko mwanawe na kupiga milundi hadi kwa jirani. Jirani alipomwona mtoto amekodoa macho na punmzi kumpapa alijua maji yamezidi unga. Aliwasha gari lake mara moja na kufululiza hadi hospitali ya mkoa mjini. Mwna alipokelewa upesi upesi na kuanza kupewa matibabu. Ilikuwa mnamo saa saba usiku jirani alipoomba kurudi nyumbani.

Kule Zilizala mambo yalimwendea sanjae Sagamba. Alilewa akalewalewa. Pombe ilimkolea na kusaha kuwa ‘utamu wa kidonda umemuua nzi.’ Alipoletewa bili ya kulipa vinywaji, alitumbukiza mikono mfukoni kutoa pesa. Apate nini! Hela zilikuwa zimefagiliwa zote! Alipiga ukwenzi kama mwehu. Macho yaliingia kiwi na akabaki kuchanganyikiwa. Mara alimshika mashati bwana mmoja kifefe aliyeketi karibu naye na kumwambia amrudishie pesa zake. Yule bwna hakuwa na nafasi ya kukaribisha matusi yoyote. Vurumai ikaanza kupikika. Joto likakolea na kuiva hadi vita vikazuka. Sagamba alipigwa akapigika na kutupwa nje ya baa. “Hajalipa hela ya vinywaji!” Wahudumu walilalamika. Ulevi uliomjaa kichwani haukuruhusu miguu yake kuchana mbuga. Alianguka katikati ya barabara ya lami, nusura gari dogo limgonge. Alikuwa amechubuka usoni na magotini. Leo pombe imemweza Sagamba. Kwa kweli, ‘maji huua mwogeleaji hodari’. Yule mwenye gari alipiga breki ghafla. Mara gari la polisi waliokuwa zamu likafika.

“Nitajitolea kumbeba tumpelekek hospitali, alisema Yule mwenye gari ndogo, bila kutambua kuwa ni jirani yake”. Polisi waliliaandama gari lhilo la msmaria mwema hadi hospitalini.
Huko hospitali, mama mtoto alipoona mwanawe amepata lepe la usingizi, naye alijinyoosha kwenye kitanda kilichokuwa hakina mgonjwa karibu na cha mwanawe. Ghafla alishtuka alipoamshwa na mwuuguzi, “Tafadhali tunakuomba utupishe, tunataka kumlaza mgonjwa mwingine hapa”. Mama alijizoazoa kitandani kumpisha mgonjwa. Hakujishughulisha na mgonjwa huyo. Alisimama na kutafuta mahali pengine pa kuzipanga mbavu zake.
Usiku ulipita haraka. Majogoo yalisikika kwa mbali. Sagamba alipata fahamu. Alipofungua macho alijikuta yumo hospitalini. Bado akiwa na chelewa, alijipapasa na kuipata rununu yake mfukoni mwa koti. Aliiwasha na kusoma arafa: BASI UJUE SHAZI AMELAZWA HOSPITALI YA MKOA WADI YA WATOTO KITANDA 8. MKEO.

Arafa hiyo ilitosha kumtia kiwewe. Alihisi maumivi mwilini, kupoteza pesa zake na sasa, mwana hospitalini. Kwa kweli “hakuna msiba usio na mwenziwe”. Sagamba alitembea dede kwa maumivu hadi wadi ya watoto.
Mama aliyekuwa bado hajaamka aligutushwa na sauti aliyoitambua kwa mbali “Shazi mwanangu, kwani umelazwa hapa hospitalini?” Mama alikiendea hima kitanda alicholazwa mwanawe. Alimkuta mumewe aliyekuwa amefungwa bendeji kichwani na kitata mkonono. Mama, baba na mwana walitazamana. Mara jirani aliyerauka kumletea Shazi staftahi alifika. Naye aliduwaa na kuduwazika. Baada ya juma, bili ya hospitali ililetwa; ya mtoto elfu kumi na ya Sagamba elfu tano. Sagamba alikumbuka mawaidha ya mkewe ya kumtaka aache ulevi. Kwa kweli, “akuambiaye usikombe mboga ataka ushibe”.

MASWALI:

  1. Sagamba alikuwa mtu wa tabia gani? (alama 2)
  2. Eleza masaibu yaliyompata Sagamba. (alama 2)
  3. Ni mambo gani yanayoonyesha kuwa Sagamba hakuijali familia yake? (alama 3)
  4. Eleza matumizi ya lugha yafuatayo: (alama 3)
    1. alisonya –
    2. kupiga milundi –
    3. Maji yamezidi unga –

SEHEMU YA B: MATUMIZI YA LUGHA: (ALAMA 30)

  1. Andika sifa za kutambulisha sauti zifuatazo: (alama 2)
    /d/
    /th/
  2. Taja vigezo vyovyote vitatu vya kuainisha konsonanti za Kiswahili. (alama 3)
  3. Tofautisha kati ya Kiimbo na Shadda (alama 2)
  4. Tunga sentensi iliyo na muundo huu: (alama 3)
    Nomino, Kivumishi nomino, Kielezi
  5. Eleza maana ya kiambishi. (alama 2)
  6. Ainisha maneno katika utungo huu (alama 3)
    Kucheza kule kumenichokesha
  7. Tofautisha kati ya kivumishi na kiwakilishi. (alama 1)
  8. Ainisha (alama 3)
    Aliyemlimisha
  9. Nomino hizi zimo katika ngeli gani? (alama 4)
    1. Uovu –
    2. Msemo –
    3. Njia –
    4. Uso –
  10. Eleza matumizi ya mshazari (alama 3)
  11. Eleza maana mbili za neno “panga” (alama 2)
  12. Onyesha hali na wakati katika sentensi hii (alama 2)
    Nimempata alipoketi
  13. Andika sentensi hii katika hali ya mazoea. (alama 2)
    Wakulima wanalima mashamba yao.
  14. Eleza dhana ya kirai. (alama 1)
  15. Toa maana ya msemo huu. (alama 1)
    Kufanya kimasomaso
  16. Andika sentensi kwa wingi. (alama 1)
    Ulimi utakutia matatani

SEHEMU YA C: FASIHI SIMULIZI (ALAMA 10)

  1. Eleza maana ya fasihi. (alama 1)
  2. Taja sifa zozote tatu za mtambaji. (alama 3)
  3. Fafanua tofauti kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi. (alama 6)


MARKING SCHEME

  1. Sagamba alikuwa mtu wa tabia gani? (alama 2)
    • alikuwa mzoefu wa ulevi
    • alikuwa mshari
    • alikuwa na kiburi
    • alikuwa karimu ulevini
    • mwenye mapuuza
  2. Eleza masaibu yaliyompata Sagamba. (alama 2)
    • kuibiwa pesa
    • kupata majeraha
    • kuaibika
    • kuingia katika deni – ulevi na hospitali
  3. Ni mambo gani yanayoonyesha kuwa Sagamba hakuijali familia yake? (alama 3)
    • alikataa kuchukua simu ya mkewe alipompigia
    • kutojishughulisha alipoambiwa mtoto wake alikuwa mgonjwa
    • kuchukua mshahara wake wote na kwenda nao ulevini.
  4. Eleza matumizi ya lugha yafuatayo: (alama 3)
    1. alisonya – alitoa sauti ya kuchukizwa
    2. kupiga milundi – kutembea, kwenda kwa miguu
    3. Maji yamezidi unga – mambo yameharibika

SEHEMU YA B: MATUMIZI YA LUGHA: (ALAMA 30)

  • Andika sifa za kutambulisha sauti zifuatazo: (alama 2)
             /d/
    • Ni kipasuo
    • Hutamkiwa kwenye ufizi
    • Ni sauti ghuna

      /th/
    • Sauti hafifu/si ghuna
    • Kikwamizo
    • Hutamkiwa menoni
  • Taja vigezo vyovyote vitatu vya kuainisha konsonanti za Kiswahili. (alama 3)
    1. Mahali pa kutamkia
    2. Namna/jinsi ya kutamka
    3. Mtetemeko wa nyusi za sauti
  • Tofautisha kati ya Kiimbo na Shadda (alama 2)
    Kiimbo ni kupanda na kushuka kwa sauti mtu anapoongea
    Shadda ni mkazo unaotiwa katika silabi ya pili kutoka mwisho wa neno katika lugha ya Kiswahili.
  • Tunga sentensi iliyo na muundo huu: (alama 3)
    Nomino, Kivumishi nomino, Kielezi
    Mwalimu mzee  sana.
  • Eleza maana ya kiambishi. (alama 2)
    Mofimu au viungo vinavyoambatanishwa au kuunganishwa na mzizi wa neno ili kutoa maana mbalimbali.
  • Ainisha maneno katika utungo huu (alama 3)
    Kucheza kule kumenichokesha
    Kucheza – Nomino ya kitenzi jina
    Kule- kivumishi
    Kumenichokesha- kitenzi
  • Tofautisha kati ya kivumishi na kiwakilishi. (alama 1)
    Kivumishi – Neno ambalo hufafanua zaidi kuhusu nomino ilhali Kiwakilishi ni neno au kiambishi ambacho huwakilisha nomino
  • Ainisha (alama 3)
    Aliyemlimisha
    A         -        li     -     ye   -       m    -     lim    -    ish     -      a
    Nafsi ya     wakati   kirejeshi   mtendwa   mzizi       kauli        kiishio
    Tatu umoja                 ‘O’
  • Nomino hizi zimo katika ngeli gani? (alama 4)
    1. Uovu – U - YA
    2. Msemo – U - I
    3. Njia – I - ZI
    4. Uso – U - ZI
  • Eleza matumizi ya mshazari (alama 3)
    • Baba/Abu
    • Hutumiwa katika kuandika akisami
      2.7 3/8 7/10
    • Hutumiwa kuonyesha ama au la
      Utafika kesho/leo
  • Eleza maana mbili za neno “panga” (alama 2)
    • Orodhesha kwa kufuatanisha
    • Kifaa kinachotumiwa kukata vitu
  • Onyesha hali na wakati katika sentensi hii (alama 2)
    Nimempata alipoketi
         Me – hali timilifu
         Li – wakati uliopita
  • Andika sentensi hii katika hali ya mazoea. (alama 2)
    Wakulima wanalima mashamba yao.
    • Wakulima hulima mashamba yao.
  • Eleza dhana ya kirai. (alama 1)
    Sehemu ya sentensi yenye maana isiyo kamilifu
  • Toa maana ya msemo huu. (alama 1)
    Kufanya kimasomaso
    • Kufanya wazi bila kuficha
  • Andika sentensi kwa wingi. (alama 1)
    Ulimi utakutia matatani
    • Ndimi zitawatia matatani.

SEHEMU YA C: FASIHI SIMULIZI (ALAMA 10)

  1. Eleza maana ya fasihi. (alama 1)
    Sanaa ya kutumia lugha kwa ubunifu kuwasilisha masuala kuhusu maisha ya
    binadamu na mazingira yake.
  2. Taja sifa zozote tatu za mtambaji. (alama 3)
    1. Awe mcheshi
    2. Anapaswa kuwa jasiri
    3. Anapaswa kuimudu lugha yake vizuri
    4. Ahusishe hadhira
    5. Anapaswa kuwa na uwezo wa ufaraguzi
    6. Awe na ubunifu wa kiwango cha juu
  3. Fafanua tofauti kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi. (alama 6)
    1. Fasihi simulizi huhifadhiwa akilini na kusambazwa kwa njia yam domo ilhali fasihi andishi huhifadhiwa kwenye maandishi na kusambazwa kwa njia ya maandishi.
    2. Fasihi simulizi huwa ina anzu nyingi kama vile semi, ushairi simulizi, maigizo, mazungumzo, hadithi ilhali fasihi andishi ina tanzu chache kama vile, tamthilia, riwaya, hadithi fupi na ushairi.
    3. Fasihi simulizi haihitaji maandalizi kabla ya kutolewa lakini fasihi andishi huhitaji maandalizi ya kutunga.
    4. Fasihi simulzi ni mali ya jamii ilhali fasihi andishi ni mali ya mtu binafsi.
    5. Fasihi simulizi ina historia ndefu (kongwe) ilhali fasihi andishi ilianza baada ya kubuniwa fasihi simulizi.
    6. Yaliyomo katika fasihi simulizi huweza kusahaulika kwa haraka kwa kuwa huhifadhiwa akilini lakini fasihi andishi hayasahauliki kwa kuwa yamehifadhiwa.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 1 End Term 3 Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest