Kiswahili Questions and Answers - Form 1 Opener Exam Term 3 2022

Share via Whatsapp

KISWAHILI
KIDATO CHA KWANZA
MUHULA WA 3 2022

MAAGIZO:

  • Jibu maswali yote

SEHEMU YA A: INSHA . (ALAMA 20)

Fafanua namna ajali za barabarani zinaweza kuzuiwa nchini Kenya.

SEHEMU B: SHAIRI (ALAMA 15)

Soma ushairi ufuatao kisha ujibu maswali.

Kila mdharau chake

Kuzimu wenda kuona, kila mdharau chake
Cha kwake akikana, kutumai cha mwenzake
Fahamu anayo laana, mpiga chake mateke
Kila mdharau chake, kuzimu enda kuona

Siringe na kujivuna, chako ukakipa teke
Unavunja lako jina, ili watu wakucheke
ana laana kwa Rabana, kila mdharau chake
Kila mdharau chake, kuzimu enda kuona

Awe Fatu na Amina, au Asha ndugu yake
Katu hawatafanana, kila mtu hadi yake,
Kila mjuzi wa mana, huwa hadharau chake
Kila mdharau chake, kuzimu enda kuona

Tama naomba amina, kilicho chetu tushike
Kidumu na kulingana, na tukipe hadhi yake
Ana laana kwa Rabana, kila mdharau chake
Kila mdharau chake, kuzimu enda kuona

(Diwani ya Akilimali na Akilimali Snow-White, K.L.B)

Maswali:

  1. Elezea ujumbe unaojitokeza katika ushairi huu. (al 2)
  2. Nakili kibwagizo cha ushairi huu. (al 1)
  3. Elezea aina za ushairi huu kwa kuzingatia: (al 6)
    1. mishororo
    2. vina
    3. vipande
  4. Elezea mambo matatu ambayo mshairi anatuonya dhidi yake. (al 3)
  5. Elezea maana ya maneno haya: (al 3)
    1. siringe
    2. katu
    3. hadhi

SEHEMU YA C: MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)

  1. Elezea tofauti kati ya sauti /d / na / z/ (al 2)
  2. Onyesha silabi inayowekwa shadda katika maneneo haya. (al 3)
    1. umio
    2. kinywa
    3. mmomonyoko
  3. Tunga sentensi moja ukitumia nomino ya kitenzi jina. (al 2)
  4. Andika sentensi ifuatayo kwa wastani. (al 2)
    Magoma hayo yatachezwa mawanjani.
  5. Tambua viambishi awali na tamati katika neno: (al 3)
    Achezaye
  6. Taja vipashio vya lugha kisha utolee mfano kwa kila kipashio: (al 4)
  7. Ainisha maneno yaliyopigiwa mstari. (al 2)
    Naam, amekula kichache
  8. Jaza pengo kwa kutumia kinyume sahihi cha kitenzi kilichopigiwa mstari. (al 2)
    1. Mimi nilim----------------- kunguru aliyokuwa amenaswa.
    2. Alivaa sare asubuhi kisha ------------------ jioni
  9. Tunga sentensi moja kubainisha maana mbili za neno: chuo (al 2)
  10. Onyesha KN na KT katika sentensi ifuatayo. (al 2)
    Mpishi yule hodari atatuzwa vizuri sana.
  11. Tunga sentensi tatu kudhihirisha matumizi mawili tofauti ya kibainishi. (al 3)
  12. Elezea maana ya kiimbo (al 2)
  13. Andika sentensi ifuatayo katika umoja. (al 2)
    Hao wenyewe hawakusomea mafunzo ya ukulima bora.
  14. Tunga sentensi kuonyesha matumizi ya kielezi . (al 2)
  15. Bainisha ngeli za majina haya. (al 3)
    1. zeruzeru
    2. ugwe
    3. saa
  16. Yakinisha: Hukuja kunitembelea kazini. (al 2)
  17. Kamilisha methali: (al 2)
    Maiti haulizwi ----------------------

SEHEMU D: FASIHI SIMULIZI (ALAMA 15)

  1. Taja vipera vine vya semi. (al 4)
  2. Eleze:
    1. Sifa za semi (al 4)
    2. Umuhimu wa semi (ala4)
  3. Elezea maana ya nahau hizi. (al 2)
    1. kukunja jamvi -----------------------------------------------------------------------
    2. kupata jiko ------------------------------------------------------------------------
  4. Fanani ni nani katika fasihi simulizi? (al 1)

SEHEMU E: ISIMU JAMII (ALAMA 10)
Elezea sifa tano za sajili ya hospitalini.

MAAKIZO

  1. INSHA
    1. Magari mabovu kuondolewa barabarani.
    2. Barabara ziboreshwe.
    3. Adhabu kali kwa madereva wasababishao ajali.
    4. Wananchi kuripoti madereva wasio wakini barabarani.
    5. Madereva waelimishwe tena kuhusu sheria na ishara za barabara.
    6. madereva wahimizwe watumie vidhibiti mwendo.
    7. kutobeba abiria zaidi ya kiwango kinachofaa.
  2. USHAIRI
    1.        
      1. Usidharau ulicho nacho hata kikiwa duni. (2 x1)
      2. Tunacho kimiliki tukipende bila ya kujivuna ili kitufae.
    2. Kila mdharau chake, kuzimu enda kuona. (al 1)
    3.       
      1. Tabia
      2. mtiririko
      3. mathnawi
        al 1 - kuelzea
        al 1 - kutaja (2 x3=6)
    4.           
      1. dhidi ya kuringa
      2. kudharau kilicho chetu/kukikana
      3. namna ya kuepuka laana ya Rabuka
      4. Kutokipa hadhi kilicho chetu. (1x3)
    5.        
      1. usiringe/usijitape/usijivune
      2. kamwe/hata/bilikuli/kabisa
      3. heshima/thamani/cheo


  3. MATUMIZI YA LUGHA
    1. d - kipasuo
      z - kikwamizo (1x2)

    2.      
      1. u’mio
      2. ‘ kinywa
      3. mmomo’nyoko (1x3)
    3. kucheza kwake kunapendeza. (al 2)
    4. ngoma hiyo itachezwa uwanjani (al 2)
    5. A - kiambishi awali
      a – ye - vimbishi tamati lazima atenganishe viambishi tamati.
    6. Sentensi
      Neno
      Silabi
      Sauti
    7.        
      1. nasua
      2. vua (al 1x2)

    8. chuo - shule/ndoa/shule inayofundisha kusoma kurani k.m Juma alijiunga na chuo kikuu kusoma udaktari baadaye alifunga ndoa.
      (atunge sentensi moja pekee)

    9. mpishi yule hodari - KN
      atatuzwa vizuri sana - KT
    10.      
      1. Ng’ombe anakula nyasi. (maneno yenye ung’ong’o) (1x3)
      2. N’shafika shuleni (ufupisho)
      3. NIlizaliwa mwaka wa ’79. (tarakimu iliyoachwa)
    11. Kiimbo ni kupanda na kushuka kwa sauti (al 2)
    12. Huyo mwenyewe hakusomea funzo la ukulima bora. (al 2)
    13. Mwalimu akadirie (al 2)
    14. A – WA
      U – ZI 
      I - ZI
      atumie herufi kubwa (al 3)
    15. ulikuja kunitembelea kazini (al 2)
    16. sanda (al 2)

SEHEMU D: FASIHI SIMULIZI

  1.          
    • methali
    • vitendawili
    • misimu
    • lakabu
    • vitanza ndimi
    • mafumbo na chemsha – bongo
    • nahau
    • misemo (zozote 1 x4)
  2.              
    1. SIFA ZA SEMI
      • semi hufumba ujumbe wake
      • hutumia picha na ishara kupitisha ujumbe wake
      • maana ya semi hupatikana katika jamii.
      • huwasilisha ujumbe mrefu kwa maneno machache
      • semi hutokea kuambatana na tanzu nyingine - tanzu ni semi tegemezi
    2. UMUHIMU WA SEMI
      • Huelimisha mfano haraka haraka haina Baraka.
      • hukuza utangamano katika jamii.
      • huburudisha mfano vitendawili
      • hutafsidi lugha
      • hukuza lugha
      • huhifadhi utamaduni. (1x4)
        (kadiria majibu mengine)
  3.           
    1. kumaliza shughuli
    2. kuoa (1x2)
  4. fanani - ni mtendaji katika fasihi simulizi (al 1)

SEHEMU E:

SIFA ZA LUGHA YA HOSPITALINI

  1. msamiati wa hospitalini kama dawa
  2. upole na huruma
  3. utohozi: bendeji
  4. majibizano kati ya mgonjwa na daktari
  5. sentensi fupi: Jina lako?
  6. kupa mtu moyo: Utapona
  7. kupotosha lugha/sarufi
  8. kuchanganya ndimi: Gani doctor. (zozote 5x2)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 1 Opener Exam Term 3 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest