Kiswahili Questions and Answers - Form 1 End Term 3 2022 Exams

Share via Whatsapp
  1. INSHA (ALAMA 10)
    Andika ratiba kuhusu siku ya wazazi itakayoanza saa mbili asubuhi hadi saa kumi.
  2. Ufahamu (Alama 15)

    Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.
    Jamii nyingi za kiafrikaziliwadunisha wanawake. Hata hivyo, kulikuwepo na baadhi ambao waliweza kuinuka na kutetea hadhi ya wanawake katika jamii. Miongoni mwa hawa ni mekatilili wa Mennza kutoka jamii ya wagiriama.

    Wazungu walipoingia katika eneo la wagiriama waliwalazimisha kutenda mambo Fulani. Miongoni mwao yalikuwa kuwachukua wanaume wenye siha na zihi ili wakashiriki katika vita vikuu vya dunia. Wazungu pia waliwatiza kodi, wakawafanyisha kazi za sulubu kwa ujira duni. Zaidi ya hayo, waliwateulia viongozi wa mitaa. Hali hii ilizusha suitafahamu kati ya jamii hizi mbili.

    Mekatilili wa Mendza aliwaongoza Wagiriama kupiganadhidi ya dhuluma hizi za wageni. Aliwahasamisha watu kuchukua na kupambana na utawala dhalimu wa Waingereza. Mekatilili aliungwa mkono na Wanje wa Madorika. Waliweza kuwaunganisha watu wao kwa kutumia imani ya kiasili kuwalisha kiapo. Imani hii iliwaleta Wagiriama pamoja dhidi ya utawala wa wageni.

    Siku hizi wanawake wana nafasi sawa katika kuchangia maswala mbalimbali ya kijamii. Baadhi yao wamechukua nyadhifa muhimu katika jamii yetu kama mawaziri, walimu, madaktari, mahakimu, waandishi, wahandisi, marubani, makatibu wa kudumu na wengine kuchaguliwa madiwani miongoni mwa nyadhifa nyingine.

    Ulimwenguni pia kumekuwepo na wanawake waliochukua nafasi na nyadhifa kama viongozi wa nchi. Margaret Thatcher na Indira Gadhi walitawala nchi zao . Wengine ni Bi S Johnson wa Liberia na A. Merkel wa Ujerumani.

    Hapa nchini tumeshuhudia mchango wa akina mama kama Bi.Machel, Bi Rice na Bi.Tegla Lorupe katika maridhiano ya kitaifa. Kwa muhtasari, wanawake wameinua jamii kwakiwango si kidogo.

    MASWALI
    1. Taja kiongozi wa kike wa Wagiriama. (Al 2)
    2. Jamii ya Wagiriama hupatikana eneo gani hapa nchini? (Al 1)
    3. Malalamishi ya wagiriama dhidi ya wanzungu yali husu nini?(Al 2)
    4. Taja aliyekuwa mshiriki wa kiongozi wa Wagiriama. (Al 1)
    5. Taja wanawake wanne viopngozi ambao wametoa huduma kwa jamii. (Al 4)
  3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 35)
    1. Taja sauti mbili ambazo ni nazali. (Al 2)
    2. Hizi nomino ziko katika ngeli gani. (Al 3)
      1. Uovu
      2. Kiwavi
      3. Raha
    3. Kamilisha methali zifuatuazo. (Al 4)
      1. Mgala muwe na …
      2. Mwenye kovi…
    4. Tegua vitendawili vifuatavyo. (Al 2)
      1. Mfalme katikati lakini watumishi pembeni.
      2. Babu yangu amevalia koti la chuma.
    5. Andika sentensi hizi kwa wingi (Al 3)
      1. Ulimi wako ungepona kama ungeenda kwa daktari.
      2. Msasi alijihami kwa uta na mshale.
      3. Ulezi wenye aliopata ulimfaa.
    6. Andika sentensi zifuatazo kwa udogo. (Al 4)
      1. uso wa mtu yule ulitutisha.
      2. Vidole vya mtu huyo vinauma.
    7. Andika vinyume vya maneno yafuatayo. (Al 2)
      1. Jenga-
      2. Nasa-
    8. Sahihisha sentesi zifuatazo. (Al 4)
      1. Mwalimu ako katika darasani.
      2. Mama anapogonjeka hakulangi wali.
    9. Taja aina tatu kuu za sentensi za Kiswahili. (Al 3)
    10. Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli ulizopewa katika mabano. (Al 3)
      1. Inama (kutendesha)
      2. Enda (kutendeshwa)
      3. Cheza (kutendeana)
    11. Tunga sentensi mbili kuonyesha matumizi ya alama ya koloni/nukta pacha.(Al 2)
    12. Onyesha miundo ya maneno yafuatayo.(Al 2)
      1. Nchi-
      2. Imba-
    13. Eleza maana ya nomino.(Al 1)
  4. ISIMUJAMII (Al 10)
    1. Lugha ni nini? (Al 1)
    2. Taja sifa tano za Lugha(Al 5)
    3. Eleza maana ya;
      1. Lafudhi - 
      2. Sajili/rejesta -
      3. Lahaja -
      4. Isimu -
  5. FASIHI SIMULIZI (Al 20)
    1. Eleza maana ya fasihi. (Al 2)
    2. Taja dhima tano za fasihi. (Al 10)
    3. Taja sifa nne za mtambaji wa hadithi. (Al 8)


MARKING SCHEME

  1.  
  2.  
    1. Taja kiongozi wa kike wa Wagiriama. (Al 2)
      • Mekatilili wa Menza
    2. Jamii ya Wagiriama hupatikana eneo gani hapa nchini? (Al 1)
      • Pwani
    3. Malalamishi ya wagiriama dhidi ya wanzungu yali husu nini?(Al 2)
      1. Kuchukuliwa wanaume wao wenye siha ili wakapigane vita vikuu vya dunia.
      2. Wazungu kuwatoza kodi
      3. Kuwafanyisha kazi za sulubu kwa ujira duni
    4. Taja aliyekuwa mshiriki wa kiongozi wa Wagiriama. (Al 1)
      • Wanje wa Madorika
    5. Taja wanawake wanne viopngozi ambao wametoa huduma kwa jamii. (Al 4)
      1. Margaret Thatcher - Uingereza
      2. Indira Gadhi - India
      3. Bi S. Johnson - Liberia
      4. A.Merkel - Ujerumani
  3.  
    1. Taja sauti mbili ambazo ni nazali. (Al 2)
      • /m/, /n/, /ny/, /ng'/
    2. Hizi nomino ziko katika ngeli gani. (Al 3)
      1. Uovu - U - YA
      2. Kiwavi - A - WA
      3. Raha - I-I
    3. Kamilisha methali zifuatuazo. (Al 4)
      1. Mgala muwe na haki mpe
      2. Mwenye kovi usidhani kapoa.
    4. Tegua vitendawili vifuatavyo. (Al 2)
      1. Mfalme katikati lakini watumishi pembeni  Ulimi
      2. Babu yangu amevalia koti la chuma msumari.
    5. Andika sentensi hizi kwa wingi (Al 3)
      1. Ulimi wako ungepona kama ungeenda kwa daktari.
        • Ndimi zao zingepona kama wangeenda kwa madktari
      2. Msasi alijihami kwa uta na mshale.
        • Wasasi walijihami na nyuta na mishale
      3. Ulezi wenye aliopata ulimfaa.
        • Malezi yenye waliyopata yaliwafaa
    6. Andika sentensi zifuatazo kwa udogo. (Al 4)
      1. uso wa mtu yule ulitutisha.
        • Kijuso cha kijitu kile kilitutisha
      2. Vidole vya mtu huyo vinauma.
        • Vijidole vuaa kijitu hicho vinauma.
    7. Andika vinyume vya maneno yafuatayo. (Al 2)
      1. Jenga - bomoa
      2. Nasa - nasua
    8. Sahihisha sentesi zifuatazo. (Al 4)
      1. Mwalimu ako katika darasani.
        • Mwalimu yuko darasani
        • Mwalimu yuko katika darasa.
      2. Mama anapogonjeka hakulangi wali.
        • Mama anapougua hali wali
        • Mama anapoumwa hali wali
    9. Taja aina tatu kuu za sentensi za Kiswahili. (Al 3)
      1. Sentensi sahili
      2. Sentensi ambatano
      3. Sentensi changamano
    10. Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli ulizopewa katika mabano. (Al 3)
      1. Inama (kutendesha) - inamisha
      2. Enda (kutendeshwa) - endeshwa
      3. Cheza (kutendeana) - chezeana
    11. Tunga sentensi mbili kuonyesha matumizi ya alama ya koloni/nukta pacha.(Al 2)
      • Kuorodhesha
      • Kuandika tarehe
      • Kuandika saa
    12. Onyesha miundo ya maneno yafuatayo.(Al 2)
      1.  Nchi- KKI
      2.  Imba- IKKI
    13. Eleza maana ya nomino.(Al 1)
      • Ni neno linalotumika kutajia kitu au mtu 
  4. ISIMUJAMII (Al 10)
    1. Lugha ni nini? (Al 1)
      • Ni mfumo wa sauti nasibu unaotumiwa na binadamu kuwasiliana.
    2. Taja sifa tano za Lugha(Al 5)
      • Lugha ina uwezo wa kukua kwa msamiati wake kupanuka
      • Lugha ina uwezo wa kufa kwa msamiati wake kupotea.
      • Lugha zote ni sawa. Hakuna bora kuliko nyingine.
      • Lugha hubadilika kutegemea mazingira na mapito ya wakati.
      • Lugha hutofautisha binadamu na mnyama.
      • Lugha ina uwezo wa kuunganisha au kutenganisha jamii kutegemea matumizi yake.
    3. Eleza maana ya;
      1. Lafudhi 
        • upekee wa mtu kimatamshi
        • tofauti kimatamshi kwa wazungumzaji wa lugha moja.
      2. Sajili/rejesta
        • Ni matumizi ya lugha katika muktadha fulani wa jamii
      3. Lahaja 
        • Namna mbalimbali za kuzungumza lugha moja kuu
      4.  Isimu
        • sayansi ya lugha
  5. FASIHI SIMULIZI (Al 20)
    1. Eleza maana ya fasihi. (Al 2)
      • Ni sanaa inayotumia lugha kuchambua vipengele mbalimbali vya maisha ya binadamu.
    2. Taja dhima tano za fasihi. (Al 10)
      • Huburudisha jamii
      • Huelimisha jamii
      • Hukuza uwezo wa kufikiri
      • Hukuza maadili
      • Hukuza usanii na ufasaha wa lugha
      • Huonya na kushauri
      • Huelekeza
      • Huendeleza utamaduni wa jamii 
        zozote tano 5 x 2 = 10
    3. Taja sifa nne za mtambaji wa hadithi. (Al 8)
      • Mwenye ujasiri wa kuzungumza hadharani.
      • Awe na ufahamu mpana wa lugha.
      • Awe na uchangamfu na ucheshi.
      • Awe na uwezo wa ufaraguzi.
      • Awe na uwezo wa kushirikisha hadhira yake.
      • Awe na kumbukumbu nzuri
      • Aweze kubadilisha toni na kiimbo.
      • Aweze kuwa na ufasahana ujuzi wa lugha.
      • Awe na uwezo wa kutumia ishara za uso, mwili na miondoko
      • Aweze kuufahamu utamaduni wa hadhira yake.
        zozote nne 4 x 2 = 8
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 1 End Term 3 2022 Exams.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest