Kiswahili Questions and Answers - Form 2 End Term 1 Exams 2021

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  • Jibu maswali yote

INSHA

Andika ratiba ya siku ya wazazi itakayofanyika shuleni kwenu. (alama 20)

  1. UFAHAMU
    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.

    Changamoto kubwa inayowakabili watu wengi katika mataifa yanayoendelea ni suala la chakula. Suala hili linaweza kuangaliwa katika sawia mbili tofauti. Kuna tatizo linalofungamana na uhaba wa chakula chenyewe. Uhaba huu unaweza kutokana na utegemezi mkubwa kwa zaraa kama nyenzo kuu ya uzalishaji wa chakula.

    Zaraa katika mataifa mengi hususan yanayoendelea, hutegemea mvua. Kupatikana kwa mvua huathiriwa na mabadiliko ya tabianchi ulimwenguni. Matendo na amali za watu kama ukataji wa miti na uchafuzi wa mazingira huwa na athari hasi kwenye tabianchi hiyo. Mabadiliko ya tabianchi huweza kuvyaza ukame kutokana na ngambi ya mvua.

    Kibinimethali kutokea wakati mafuriko yanapotokea na labda kuyasomba mazao mashambani na kusababisha baa la njaa. Hali hizi mbili husababisha matatizo makubwa ya chakula na kuathiri pakubwa suala zima la usalama wa chakula. Ili kuzuia uwezekano wa kuwepo kwa shida hii, pana haja ya kuwepo kwa mikakati na sera za kuhakikisha kuna usalama wa chakula. Kwa mfano, pana haja ya kukuza kilimo cha umwagiliaji ili kuepuka adha inayosababishwa na ukosefu wa mvua. Kwa upande mwingine, sharti zichukuliwe hatua mufidi za kuzuia na kupambana na athari za gharika.

    Changamoto nyingine inahusiana na usalama wa chakula chenyewe. Chakula kilichosibikwa na vijasumu au kwa njia nyingine ile huweza kumdhuru anayehusika. Msibiko wa chakula unatokana na vyanzo tofauti. Mathalan uandalizi wa chakula kilichochafuliwa na choo, kutozingatia mbeko za usafi, uandaaji wa chakula na kukiweka katika hali ya uvuguvugu kabla ya kukipakua – hali inayochochea ukuaji wa viini na ulaji wa chakula kisichoandaliwa vyema.

    Ili kuepuka uwezekano wa kuathirika, pana haja ya kuzingatia usafi wa chakula na uandalizi unaofaa. Fauka ya hayo, vyombo vya uandalizi viwe safi, kanuni za usafi zifuatwe, upikaji na uandaaji uwe kamilifu. Hali hii isipozingatiwa, siha za raia wenyewe zitaathirika pakubwa.

    Maswali.
    1. Taja aina mbili za kuangalia suala la chakula katika mataifa yanayoendelea. (alama 2)
    2. Taja hatua mbili zinazoweza kuchukuliwa kupambana na tatizo la chakula.
      (alama 2)
    3. Eleza jinsi nne tofauti namna chakula kinavyoweza kuwa si salama? (alama 4)
    4. Kwa nini ni rahisi kukipakua chakula baada ya kukiandaa tu? (alama 1)
    5. Ni mapendekezo gani anayoyatoa mwandishi kuhakikisha kuwa chakula kinafaa? (alama 4)
  2. MATUMIZI YA LUGHA
    1. Kwa kutoa mifano eleza tofauti kati ya: (alama 2)
      1. Silabi funge
      2. Silabi wazi
    2. Onyesha sauti zenye sifa zifuatazo: (alama 2)
      1. Kipasuo cha ufizi
      2. Kikwamizo cha kaakaa laini
    3. Tambua aina ya nomino katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
      Mchanga hufanya miti kumea.
    4. Bainisha mofimu katika kitenzi. (alama 2)
      Kilipikika
    5. Tambua vivumishi katika sentensi ifuatayo na ueleze ni vya aina gani. (alama 2)
      1. Mtoto wake ameng’oka jino.
      2. Msemo wenye tafsida hupendwa.
    6. Andika kinyume cha: (alama 1)
      Tulinunua nguo aliizozianika jana.
    7. Nomino ‘uki’ iko kwenye ngeli gani. (alama 1)
    8. Ainisha vitenzi kwenye fungo zifuatazo: (alama 3)
      1. Yatakuwa yangali yanakoma.
      2. Maria na Atieno ni wanafunzi watiifu.
    9. Onyesha vielezi katika sentensi zifuatazo. (alama 2)
      1. Rais ametutembelea mara sita mwaka huu.
      2. Nendeni haraka shuleni.
    10. Eleza maana inayojitokeza kwenye sentensi ifuatayo. (alama 1)
      Waiteni watu wale.
    11. Tumia kiwakilishi kisisitizi kutungia sentensi ya wingi wakati uliopita. (alama 2)
  3. ISIMU JAMII
    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.

    Haya ng’ara … Ng’ara leo! Nguo motomoto. Ng’ara leo kwa bei rahisi. Hamsini hamsini shati. Kuona ni bure. Bure kwa bure. Shika mwenyewe ujionee. Bei nafuu. Bei ya starehe. Haya, haya. Usikose mwanangu! Hamsa! Hamsa! Fifty!Hamsa! Fifty! Hamsa na nyingine.
    Maswali.
    1. Bainisha sajili ya mazungumzo haya. (alama 1)
    2. Eleza sifa nane za sajili hii kwa kurejelea kifungu hiki. (alama 4)
  4. FASIHI SIMULIZI.
    1. Fafanua maigizo. (alama 2)
    2. Ainisha kipera cha maigizo. (alama 4)
    3. Eleza sifa za maigizo. (alama 4)


Marking Scheme

  1. UFAHAMU
    Maswali
    1. Taja aina mbili za kuangalia suala la chakula katika mataifa yanayoendelea. (alama 2)
      • Uhaba wa chakula, ukosefu wa chakula au upungufu wa chakula unaoweza kutokana na utegemezi mkubwa kwa kilimo kama njia ya uzalishaji wa chakula.
      • Usalama wa chakula chenyewe kwani chakula kilichosibikwa na vijasumu huweza kumdhuru anayehusika.
    2. Taja hatua mbili zinazoweza kuchukuliwa kupambana na tatizo la chakula.
      (alama 2)
      • kuwepo kwa mikakati ya kuhakikisha kuna usalama wa chakula kwa kukuza kilimo cha umwagiliaji ili kuepuka adha inayosababishwa na ukosefu wa mvua na kuchukuliwa hatua mufidi za kuzuia na kupambana na athari za gharika.
      • Kuwepo kwa sare za kuhakikisha kuna usalama wa chakula.
    3. Eleza jinsi nne tofauti namna chakula kinavyoweza kuwa si salama? (alama 4)
      • Uandalizi wa chakula kilichochafuliwa na choo
      • Kutozingatia mbeko za usafi.
      • Kukiandaa chakula na kukiacha katika hali vuguvugu kabla ya kukipakua.
      • Ulaji wa chakula kisichoandaliwa vyema.
    4. Kwa nini inahalisi kukipakua chakula baada ya kukiandaa tu? (alama 1)
      • Chakula kipakuliwe baada ya kuandaa tu ili kuzuia hali inayochochea ukuaji wa viini na kwa njia hiyo kuhakikisha kuwa chakula hakitakuwa na viini.
    5. Ni mapendekezo gani anayoyatoa mwandishi kuhakikisha kuwa chakula kinafaa? (alama 4)
      • Haja ya kuzingatia usafi wa chakula.
      • Uandalizi unofaa.
  2. MATUMIZI YA LUGHA
    1. Kwa kutoa mifano eleza tofauti kati ya: (alama 2)
      1. Silabi funge
        • Mak-ta-ba
        • Dak-ta-ri
        • Muh-ta-sa-ri
      2. Silabi wazi
        • Ba-ba
        • Li - a
    2. Onyesha sauti zenye sifa zifuatazo: (alama 2)
      1. Kipasuo cha ufizi
        • /t/ na /d/
      2. Kikwamizo cha kaakaa laini
        • /gh/
    3. Tambua aina ya nomino katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
      Mchanga hufanya miti kumea.
      • Mchanga – nomino ya wingi
      • Miti – nomino ya kawaida
    4. Bainisha mofimu katika kitenzi. (alama 2)
      Kilipikika 
      KI-           LI -            PIK -       IK -          A
      Ngeli        wakati        mzizi      kauli        kiishio
    5. Tambua vivumishi katika sentensi ifuatayo na ueleze ni vya aina gani. (alama 2)
      1. Mtoto wake ameng’oka jino.
        • Wake – kimilikishi
      2. Msemo wenye tafsida hupendwa.
        • Enye - pekee
    6. Andika kinyume cha: (alama 1)
      Tulianua nguo aliizozianika jana.
      • Tulianika nguo alizoanua jana.
    7. Nomino ‘uki’ iko kwenye ngeli gani. (alama 1)
      • Ngeli ya u-u
    8. Ainisha vitenzi kwenye fungo zifuatazo: (alama 3)
      1. Yatakuwa yangali yanakoma.
        • Vitenzi sambamba
      2. Maria na Atieno ni wanafunzi watiifu.
        • Kitenzi kishirikishi kipungufu
        • Kitenzi kikuu
    9. Onyesha vielezi katika sentensi zifuatazo. (alama 2)
      1. Rais ametutembelea mara sita mwaka huu.
        • Mara sita – idadi
      2. Nendeni haraka shuleni.
        • Haraka – namna hali
    10. Eleza maana inayojitokeza kwenye sentensi ifuatayo. (alama 1)
      Waiteni watu wale.
      • Wale – kivumishi kiashiria cha mbali
      • Watu  waje wale chakula
    11. Tumia kiwakilishi kisisitizi kutungia sentensi ya wingi wakati uliopita. (alama 2)
      • Wawa hawa walituletea zawadi. (mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi)
  3. ISIMU JAMII
    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.

    Haya ng’ara … Ng’ara leo! Nguo motomoto. Ng’ara leo kwa bei rahisi. Hamsini hamsini shati. Kuona ni bure. Bure kwa bure. Shika mwenyewe ujionee. Bei nafuu. Bei ya starehe. Haya, haya. Usikose mwanangu! Hamsa! Hamsa! Fifty!Hamsa! Fifty! Hamsa na nyingine.

    Maswali.
    1. Bainisha sajili ya mazungumzo haya. (alama 1)
      • Hii ni sajili ya biashara ya kunadi au kutangaza bidhaa (nguo) sokoni au barabarani. Msamiati uliotumika ni msamiata  maalaum wa biashara ya sokoni. Kwa mfano shati, bei, hamsa na fifty.
    2. Eleza sifa nane za sajili hii kwa kurejelea kifungu hiki. (alama 4)
      • Sajili hii hutumia msamiati maalum wa biashara ili kurejelea shughuli zinazoendelezwa pale. Kwa mfano, shati, nguo, hamsini, bei, hamsa na fifty.
      • Matumizi ya chuku ili kuonyesha ubora wa bidhaa zao. Kwa mfano, kuona ni bure, bure kwa bure, bei ya starehe, nguo motomoto.
      • Urudiaji ili kusisitiza ubora wa bidhaa zake na kumshawishi mteja kununua. Kwa ng’ara, haya haya.
      • Matumizi ya misimu ya biashara ili aeleweke katika muktadha huo wa kibiashara. Kwa mfano nguo motomoto, hamsa, ng’ara.
      • Lugha shawishi ili kuwavuta wateja wao kununua bidha . kwa mfano: shika mwenyewe ujionee, usikose mwanangu, bei nafuu.
      • Kauli huwa fupifupi hasa wakati wa kujadiliana bei kwa sababu muuzaji na mnunuzi hawataki kuchoshana au kuna wateja wengine wa kuhudumiwa. Kwa mfano, kuona ni bure , bei nafuu. Tangazo hili kwa jumla ni fupi.
      • Lugha huwa nyepesi au sahili ili iweze kueleweka na watu wenye viwango vyote vya elimu. Kifungu hiki kinaeleweka bila tatizo lolote.
      • Kuchanganya ndimi ili  kuwanasa wateja wote na kuwaonyesha ukaribu (ukuruba) kwa kuzungumza lugha nayodhani wateja wanailewa zaidi. Mbinu hii huwafanya wateja anaowazungumzia kumpelea yeye muuzaji na kununua bidhaa zake. Kwa mfano: fifity, fifty au hamsa fifty.
  4. FASIHI SIMULIZI.
    1. Fafanua maigizo. (alama 2)
      • Maigizo ni sanaa ya mazungumzo yanayoambatana na matendo.
    2. Ainisha kipera cha maigizo. (alama 4)
      • Maigizo
      • Michezo ya jukwaani
      • Vidokesho 
      • Ngojera
      • Miviga 
      • Ngomezi 
    3. Eleza sifa za maigizo. (alama 4)
      • Hutolewa mbele ya hadhira
      • Lazima pawe na fanani na hadhira
      • Hutolewa mahali maalum
      • Waigizaji huvalia maleba
      • Huiga hali ya maisha ya kisasa
      • Lazima pawe na tendo la kuigizwa
      • Hufungamana na shughuli za kijamii
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 2 End Term 1 Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest