Kiswahili Questions and Answers - Form 2 Mid Term 2 Exams 2021

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  • Jibu maswali yote.
  • Majibu yote yaandikwe 
  • Majibu yote ni lazima yaandikwe kwa lugha ya kiswahili
  1. UFAHAMU (ALAMA 15)

    Soma makalayafuatayo kisha ujibu maswali:

    Mwanamke wa kisasa anazaliwa na kukulia katika mazingira yaliyobadilika mno. Matazamio yake maishani ni tofauti na yale ya wanawake waliosihi mapote mawili yaliyopita ; wanawake makamu ya nyanyake na mamake - kuu.

    Yeye hatarajii kuzaliwa, kukua, kuolewa, kuwa mke wa bwana, kumzalia watoto, na daima dawamu kuwa “mwandani wa jikoni” akawapikia watoto na bwanake chakula ; na akitoka jikoni aelekee shambani kulima, kichakani, kuchanja kuni,, mtoni kufua nguo na kuteka maji ya kutumia nyumbani. Mwanamke wa kisasa huandamana na mwanamume. Akanyagapo mume naye papo huutia wayo wake.

    Mwanamke wa kisasa huenda shule na kujifunza yote yafunzwayo huko. Hushindana na wanawake kwa wanaume na kuibuka mshindi si mara haba. Huibuka mshindi katika masomo yake ya lugha, historia, jiografia, hesabu, sayansi na mengineyo, sawa na mwanamume.

    Mwanamke wa kisasa hutaka kufanya kazi za kibega, akazifanya. Akataka kuwa mwalimu, akawa. Akataka kuwa daktari, akafanikiwa. Almuradi, siku hizi mwanamke hufanya kazi yoyote ile afanyayo mwanamume. Kuna wanawake marubani wa ndege, masonara, waashi, wahandisi, madereva wa magari, mawakili, mahakimu, mawaziri wakuu na hata marais wa nchi. Hakuna kazi isiyofanywa na mwanamke siku hizi.

    Mwanamke wa kisasa hateswi akafyata ulimi. Anapohiniwa yeye hupigania haki kwa dhati na hamasa. Katu hakubali ‘mahali pake’ katikajamii alipotengwa na wanaumme wenye mawazo ya kihafidhina yaliyopitwa na wakati. Siku hizi mwanamke huolewa tu wakati amepata kazi ya kumwezesha kujikimu maishani au pale anapokuwa na hakika kwamba biashara yake, iwapo ni mfanyi biashara, imepiga hatua ya kutomrudisha ukutani.

    Mwanamke wa kisasa haamuliwi katikajambo lolote, bali hufanya maamuzi yake mwenyewe. Kwa upande mwingine, mwanamume wa ‘kisasa’, ambaye bado amefungwa pingu na taasubi za kiume, hapendezwi na mwanamke huyu. Huuma kidole akatamani yale ya kale, lakini wapi! Analazimika kukubali mwanamke huyu kama mshirika sawa maishani, na kuishi naye, apende asipende. Shingo upande analazimika kukubali kwamba mabadiliko haya sio mithili ya kiwingu kipitacho, bali ni ya aushi.
    1. Msemo ‘mwandani wa jikoni’ unadhihirisha bali gani ya mwanamke katikajamii? (alama 2)
    2. Jamii imefanya mwanamke kuwa hayawani wa mizigo. Fafanua (alama 2)
    3. Eleza maana ya ‘’ (alama 2)
    4. Mlinganishe mwanamke wa kiasili na wa kisasa katika maswala ya ndoa na elimu (alama 4)
    5. Mwanamume wa kisasa anamwonaje mwanamke wa kisasa? (alama 2)
    6. Eleza maana ya:
      1. Akafyata ulimu (alama 1)
      2. Ukutani (alama 1)
      3. Taasubi za kiume (alama 1)
  2. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 15)
    1. Taja sauti zozote mbili zinazotamkiwa kwenye midomo. (alama 2)
    2. Onyesha viambishi awali na tamati katika kitenzi; nilimchapa. (alama 2)
    3. Eleza maana mbili zinazojitokeza katika sentensi hlii;
      Alimpigia mpira. (alama 2)
    4. Pambanua sentensi ifuatayo kwa kutumia kielelezo cha mstari.
      Mtoto wake amepotea. (alama 3)
    5. Yakinisha sentensi ifuatayo:
      Chakula chake hakiliki. (alama 2)
    6. Unganisha kwa kiunganishi mwafaka. (alama 2)
      1. Siendi
      2. Sichezi
    7. Tia mkazo/shadda katika neno hili ili kuleta maana mbili tofauti. (alama 2)
      Walakini
    8. Akifisha sentensi hii kwa njia tatu tofauti kuonyesha umuhimu wa kiimbo. (alama 3)
      Ameenda sokoni
    9. Tambua ngeli za nomino hizi (alama 2)
      1. Mitume
      2. Kamusi
    10. Andika kwa hail wastani wingi (alama 2)
      Majibwa haya yalibweka yakayahofisha majitu yale.
    11. Taja ama mbili za mofimu kwa kutoa mfano mmoja mmoja kwa kila ama. (alama 2)
    12. Akifisha (alama 3)
      Salaale haya ndiyo mambo aliyotuitia mmoja wao aliuliza.
    13. Tunga sentensi kwa kutumia kiwakilishi ‘-ingi’ katika ngeli ya KI-VI umoja. (alama 2)
    14. Eleza maana ya misemo ifuatayo, (alama 2)
      1. Paka mafuta kwenya mgongo wa chupa.
      2. Ambulia patupu.
    15. Tunga sentensi sahihi ukitumia visawe vya maneno yafuatayo. (alama 2)
      1. Tabibu
      2. Mwalimu
    16. Tunga sentensi moja kuonyesha tofauti kati ya maneno haya: (alama 2)
      Chakura na chakula
    17. Tambua na kuainisha vitenzi katika sentensi ifuatayo (alama 4)
      Mtoto ameenda kusoma shuleni
  3. ISIMU JAMII (ALAMA 10)
    1. Eleza maana ya sajili (alama 2)
    2. Fafanua sifa nne za sajili ya hotelini (alama 8)
  4. FASIHI SIMULIZI
    1. Eleza maana ya nyimbo katika fasihi simuli. (alama 2)
    2. Taja sifa zozote tatu za nyimbo (alama 3)
    3. Fafanua aina zozote tatu za nyimbo (alama 6)
    4. Eleza dhima nne za nyimbo katika jamii. (alama 4)


MARKING SCHEME

  1. UFAHAMU
    1. Mahati pa mwanamke ni jikoni / kazi yake ni kutumikiajamii 1 x 2=2
    2. Anafanyishwa kazi nyingi; kupika, kulima, kuchanja kuni, kufua, kuteka maji n.k 1 x 2=2 
    3. Afanyayo mwanaume, mwanamke pia huifanya 1 x 2=2
    4. Ndoa
       Kiasili   kisasa 
       Ndoa ya lazima
       Alilazimika kumzalia mume watoto
       Alitumishwa 
       Alifanya kazi ya jikoni
       Aliamuliwa kwa kila jambo
       Alimtegemea mume
       Alinyamaza alipoteswa
       Ndoa si lazima
       Anazaa watoto kwa hiari
       Ana uhuru wa kufanya atakalo
       Si lazima aende jikoni 
       Anajiamulia mwenyewe
       Anajiteegemea / hujikumu
      Hujitetea akiteswa / hupigania haki
       zozote 2 x 1=2
      Elimu
       Hakuenda shuleni 
       Alikuwa na Elimu ya kiasili 
       Anaenda shuleni
       Hana elimu ya kiasili yoyote 
      1 x 2 =2
    5. Hapendezwi naye. Ni mkaidi, mshindani, mzushi 1 x 2=2
    6.  
      1. Akafyta ulimi - akanyamaza
      2. Ukutani - umaskini
      3. Taasubi za kiume - fikra za kibaguzi/wazo la kibaguzi / mapuuza kwa mwanamke  Mwanaume kuona bora kuliko mke
        3 x 1 = 3
  2. MATUMIZI YA LUGHA
    1.  /p/, /b/, /m/, /w/
    2. Ni-li-m viambishi awali
      a — kiambishi tamati
    3.  
      • Alimwelekezea mpira
      • Mpira kama chombo cha kumpiga
      • Mpira kama sababu ya kumpiga
      • Mpira ulipigwa kwa niaba yake
    4. Mtoto wake amepotea
         l        l          l
         N      V         T
    5. Chakula chake kinalika
    6. Siendi wala sichezi
      1. waLakini
      2. Wala’kini
    7. Ameenda sokoni. Kauli
      Ameenda sokonil Mshangao/hisia Ameenda sokoni? Swali
    8.  
      1. (A-WA)
      2. (l—ZI)
    9. Mbwa hawa walibweka wakawahofisha watu wale
    10.  
      • Mofimu huru — shangazi, mimi n.k.
      • Mofimu tegemezi — a-na-simam-a
    11. “Salaale, haya ndiyo mambo aliyotuitia7’ Mmoja wao aliuliza. au “Salaalel Haya ndiyo mambo aliyotuitia?” Mmoja wao aliuliza.
    12. Kingi kimeharibika
    13.  
      1. Kumpa mtu sifa zisizo zake/asizostahili
      2. Kukosa ulichotarajia
    14.  
      1. Daktari
      2. Mkutunzi
    15. Kuku anachakura chini iii apate chakula
    16. Ameenda — kisaidizi
      Kusoma - Kikuu
  3. ISIMU JAMII
    1. Sajili au rejesta ni lugha ya kimazingira inayotumika katika miktadha mbalimbali
    2.  
      • Lugha haizingatii kanuni za sarufi m.f chakula imeisha
      • Sentensi fupifupi hutumiwa; nani pilau
      • Kuna kuchanganya ndimi m.f kuku boil
      • Lugha ya heshima k.m tafadhali lipa hapa
      • Misamiati teule/maalum ya hotelini k.m karanga, sosa, choma - Lugha ya maswali na majibizano hutumika
      • Kuna utohozi wa msamiati k.v chenji, glasi
      • Lugha ya kukatizana kauli hutumika
      • Wakati mwingine lugha ya chuku hutumika
      • Lugha ya mvuto/mnato hutumika
  4. FASIHI SIMULIZI
    1. Ni maneno yanayotamkwa kwa sauti ya kupanda na kushuka; yenye mahadhi ya kuvutia 
    2.  
      • Huambatana na ala za muziki
      • Lugha yake ni ya mkato
      • Huambatana na sherehe husika
      • Ujumbe wake hufungamana na hadhira
      • Uimbaji huambatana na vitendo
      • Huwa na takriri ya sauti, maneno n.k
    3.  
      • Bembelezi/ bembezi/ bembea - za kuimbia watoto
      • Nyimbo za watoto- huimbwa na watoto wenyewe wanapocheza
      • Hodiya – nyimbo za kazi
      • Nyimbo za harusi
    4.  
      • Huburudisha
      • Hukashifu wanaopotoka
      • Husifu waadilifu
      • Hukejeli waasi
      • Hushauri kimaisha
      • Hutia moyo
      • Hukuza historia
      • Huliwaza walio na shida
      • Hupitisha maarifa
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 2 Mid Term 2 Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest