Kiswahili Questions and Answers - Form 2 End of Term 3 Exams 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

INSHA AL. 20
Andika insha itakayoafiki methali
Mchumia juani hulia kivulini.
UFAHAMU AL 10
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuatia.
Nilipojiungana shule ya upili, nilisajiliwa katika chama cha wapenda mazingira. Chama hicho kilitunza na kuimarisha mazingira shuleni na hata viungani mwake. Wanachama walipenda sana kutunza njiwa, shore,kishungi na shomoro; ndege walio na rangi na maumbile ya kuvutia.
Walihifadhi kitalu katika pembe moja na uwanja wa shule ambapo ungewaona nyuki wakifurahia maua. Vipepeo na buibui wa aina mbalimbali wangepatikana hapo. Aidha, usingewa kosa chozi, ndege wapendao asali ya maua. Walifuga wanyama kama sungura, nguruwe na farasi.
Mwalimu mkuu, Bwana Hekima, alipendezwa na bidii hiyo na aka ahidi kutupeleka sisi wanachama kutalii sehemu ya mbuga ya hifadhi ya Nakuru. Kweli, mcheza kwao hutuzwa.
Safari ilikua ya wanafunzi hamsini na walimu wawili. Njiani tuliona kobe aliyekuwa akivuka barabara. Dereva akasimamisha basi nasi tukashuka kuajabia maumbile yake. Kobe hakuonyesha kuadhirika. Alifululiza akatokomea kichakani. Tukaondoka.
Tuliwasili lango kuu la hifadhi hiyo yapata saa sita mchana. tukapewa kiongozi wa safari. Ghafla bin vuu, nilisikia wenzangu wakimaka, “mtazame…. yaani ni mkubwa hivi!” nilipotazama nje kupitia dirisha la basi, nilimwona kifaru aliyetulia chini ya mti. Kando yake alipitia ngiri kwa kasi huku ameinua mkia wake. Meno yake mawili yaliyotokeza kila moja kando ya kinywa yalimfanya aonekane wa kutisha. Alielekea kidibwini ambamo viboko wawili walikuwa wakifurahia maji. Nilikubali kuwa, kutembea kwingi, kuona mengi.
Tulipokuwa tukila chakula cha mchana ndani ya basi, alikuja nyani mkubwa karibu nasi. Alionekana kupendezwa na kuwepo kwetu pale.
Tuliendelea na safari hadi sehemu iitwayo makalia maanguko ya jamii ya makalia yalitustaajabisha. Hatua chache kutoka tulipokuwa tumesimama tuliona mbuni. Miongoni mwa ndege wote tuliowaona, walokuwa wengi ni heroe. Walionekana wakitarazaki majini. Mwalimu wetu wa jiografia alitueleza mengi kuhusu ndege hao.
Kiongozi wa safari alitueleza kuwa sehemu ile ya makalia ilisifika kwa sababu wanyama mbalimbali walifika pale kutuliza kiu yao. Pia, weupe wa maji yakigonga kwenye magenge ni jambo lililovutia wengi. Sisi hatukuwana bahati nzuri kwa kuwa tulifika hapo wakati ambao wanyama wengi wakikuwa tayari wameondoka kurudi malishoni.
Saa kumi na moja jioni tulikuwa hoi. Tulifurahia safari hiyo na kuwasimulia wenzetu shuleni kwa fasili. Baada ya majuma manne idadi ya wanachama iliongezeka.
Maswali

 1. Kwa nini wanafunzi wachama cha wapenda mazingira walikwenda kuzuru mbuga ya hifadhi? (al 1)
 2. Mbali na wanyama waliotajwa katika makala haya, taja wanyama wengine wanne wanaoweza kupatikana katika mbuga za hifadhi nchini Kenya.(al 1)
 3. Tulipokuwa mbugani tulikuwa watu wangapi kwa jumla? (al 1)
 4. Kwa nini sehemu ya makalia ilikuwa maarufu? (al 1)
 5. Safari hii ilikuwa na manufaa gani kwetu? (al 1)
 6. Kwa nini idadi ya wanachama iliongezeka baada ya majuma manne?(al 1)
 7. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika taarifa (al4)
  1. Kuimarisha-
  2. Kutalii-
  3. Viungani-
  4. Wakitarazaki-

MATUMIZI YA LUGHA (AL 30)

 1. Andika maneno yaliyo na sauti tatanishi /b/ na /mb/ (al 2)
 2. Sahihisha sentensi zifuatazo (al 2)
  1. Hebu nipishe.
  2. Asha alienda sokoni alikoinunua ng’ombe mbili.
 3. Onyesha viambishi tamati katika maneno haya. (al 1)
  1. Fungiana
  2. Adimika
 4. Ni nomino gani isiyochukuana na nyingine (al 1)
  1. Damu, asali, utepe, chumvi, maji, maziwa
 5. Tunga sentensi zitakazokuwa na miundo ifuatayo: (alama 2)
  1. N + V +E +T
  2. W + V + T + E
 6. Eleza maana ya misemo ifuatayo (al 3)
  1. Mtoto wa watu.
  2. Kufanya kimasomaso.
  3. Kuwa na mizungu.
 7. Tunga sentensi katika umoja na wingi ukitumia nomino hizi pamoja na enyewe-
  1. Sikio
  2. Pahali
 8. Andika sentensi hizi kwa wingi. (al )2
  1. Mtu yuyu huyu ndiye aliyeiba nguo yangu.
  2. Nilinunua kitabu kiki hiki ulicho nacho.
 9. Tambulisha vitenzi visaidizi katika sentensi hizi (al 1)
  1. Hajaenda kusoma.
  2. Wamekuwa wakiimba.
 10. Viwakilishi vilivyotumiwa katika sentensi zifuatazo si sahihi visahihishe (al 1)
  1. Huyu kimevunjika.
  2. Wao atafika mapema.
 11. Tumia vihusishi vifuatavyo katika sentensi (al 1)
  1. Miongoni mwa.
  2. Mbali na.
 12. Andika kinyume cha maneno yafuatayo (al 1)
  1. Tandua.
  2. Kata.
 13. Kamilisha methali zifuatazo (al 3)
  1. Gangaganga ya mganga _____________________________________
  2. Mke mwema ______________________________________________
  3. Afadhali dooteni kama _______________________________________
 14. Pambanua sentensi hizi kwa njia ya mistari (al 4)
  1. Musa alienda hospitalini lakini hakutibiwa.
  2. Naimba huku ninafanya kazi
 15. Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumiwa michoro ya matawi
  Watoto wote wamelala na wazee wanakunywa pombe.(al 4)

ISIMU JAMII ( AL 10 )

 1. Fafanua sifa tano za sajili ya mtaani 

FASIHI SIMULIZI (AL 10)

 1. Eleza maana ya fasihi simulizi (al 2)
 2. Fafanua sifa zozote nne za fasihi simulizi (al 8)

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1. Mwalimu mkuu alipendezwa na bidii ya wapenda mazingira.
 2.                  
  1. Nyati
  2. Ndovu
  3. Samba
  4. Chui
 3. 54 wanafunzi 50, walimu 2, dereva, kiongozi wa safari. (al 1)
 4. Maanguko ya jamii ya makalia yalistaajabisha pia wanyama mbali mbali
  Walifika pale kuzima kiu yao.(al 1)
 5. Walipata maarifa zaidi ya kutunza na kuimarisha mazingira shuleni .(al 1)
 6. Walikuwa wamewasimulia wenzao shuleni kwa fasili. (al 1)
 7.                      
  1. Kuimarisha- kuwa imara.
  2. Kutalii – kutembelea.
  3. Viungani – sehemu zilizo karibu.
  4. Wakitarazaki – wakielea majini.

MATUMIZI YA LUGHA (AL 30)

 1.                          
  1. Bali – mbali.
  2. Baa – imba.
  3. Iba – mbuyu.
   (Mwalimu akadirie)
 2.                  
  1. Hebu nipishe.
  2. Asha alienda sokoni alikonunua ngombe wawili.
 3. Fung-iana .
  Andim-ika .
 4. Utepe.
 5. Mtoto mpole sana ameondoka.
 6.                      
  1. Alizaliwa katika familia inayojiweza.
  2. Bila kuficha.
  3. Kuwa na busara/ maarifa.
 7.                  
  1. Maskio yenyewe yana kasoro.
  2. Pahali penyewe ni pake.
 8.                          
  1. Watu wawa hawa ndio waliimba nguo zangu.
  2. Tulinunua vitabu vivi hivi ulivyo navyo.
 9.                  
  1. Hajaenda.
  2. Wamekuwa.
 10. Hiki kimevunjika .
  Wao watafika mapema.
 11.                  
  1. Juma ni miongoni mwa wanafunzi waliofukuzwa.
  2. Kwake ni mbali na kwa mwalimu.
 12. Tandika.
  Unga.
 13.                  
  1. Gangaganga ya mganga humwacha mgonjwa wa matumaini.
  2. Mke mwema mgomba hupalilia.
  3. Afadhali dooteni kama ambari kutanda.
 14. Musa alienda hospitalini lakini hakutibiwa.
  Naimba huku ninafanya kazi.
 15.                                
  15 AYTFDYTAF

ISIMU JAMII

 1.                          
  1. Lugha ya mseto.
  2. Kuchanganya ndimi.
  3. Lugha legevu.
  4. Mzaha.
  5. Lugha ya kuficha siri.
  6. Masolugha hutumika sana.
  7. Si sanifu.
  8. Hakuna urasmi wowote.

FASIHI SIMULIZI AL 10

 1. Fasihi simulizi ni kazi ya kisanaa inayotumia lugha ya mdomo au mazungumzo. katika uwasilishwaji wake kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
  1. Utendaji ambao hushirikiisha hadhira na fanani kwa wakati mmoja.
  2. Kuwepo kwa fanani ambaye huweza kusimulia kwa kuimba ama kusema.
  3. Kuwepo kwa hadhira- shiriki katika ulendaji kwa kuuliza maswali kupiga .makofi ama kulia.
  4. Kuwa mali ya jamii nzima.
  5. Kuwa na utegemezi- sanaa ya maonyesho na muziki.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 2 End of Term 3 Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest