Kiswahili Questions and Answers - Form 2 End Term 1 Exams 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

1.INSHA (AL 20)

ANDIKA INSHA YENYE MANENO YASIYOPUNGUA MIA 400 INAYOAFIKI METHALI ‘MCHUMIA JUANI HULIA KIVULINI’

2. UFAHAMU
FUNGUA SESAME

Jina la Nimrod lilipotea mara tu alipoanza kufanya kazi jijini Nirobi. Marafiki na jamaa zake waliamini kuwa alikuwa ameajiriwa huko mjini ingawa hakuna aliyeijua kazi yenyewe vizuri. Hata hivyo waliamini kuwa lazima alikuwa na kibonge cha kazi kwa sababu alivalia kinadhifu na kuishi maisha ya starehe. Tena yeye mwenyewe alikazania kusema kuwa amejiriwa kazi ya maana. Marafiki zake walimfahamu kama “Bwana Sesame”. Mtu wa kwanza aliyempa jina hilo alisema alipendezwa na ujuzi na maarifa yake. “huyu hakosi ufumbuzi wa tatizo loote. Ni kama ule mlango wa kisa cha Ali Baba na Wezi arobaini. Ukisema ‘fungua Sesame’ unafunguka tu,” alisema mtu huyo.

Jamaa walioishi naye katika mtaa wa urumo walishangazwa na utaratibu wake wa kazi. Mchana kutwa alishinda chumbani mwake. Mara nyingi utamkuta ametulia tuli akitazama runinga yake ndogo. Wakati mwingine atakuwa akifanya kazi yake ndogo ndogo huku akipiga mluzi bubu, ambao haukusikika vizuri. Wakati mwingine atakuwa akiusikiliza muziki kwenye chombo chake cha muziki kilichotingisha jingo zima kutokana na sauti yake nene.

Kwa kawaida alitoka chumbani jioni. Waliomjua walimchangamkia kutokana na uchangamfu wake. Alipenda sana mizaha. Waliopenda kupiga soga walivutiwa na maongezi yake hasa kuhusiana na magari. Aliyajua magari mengi. Mimi naweza kuijua aina ya gari kwa kuusikiliza mlio wake tu”, alisema kila wakati. “wacha kutuvungavunga Bwana wee, haiwezekani !” atasema mwingine. “nini? Unajua mimi ndiye Bwana Sesame mwenyewe!” atasema, halafu wote wataangua kicheko.

Ilifika wakati kampuni kadha zilipoamua kuwapunguza wafanyakazi wake kutokana na hali mbaya ya kiuchumi. Lakini Bwana Sesame hakuwa mmoja wa hao. Hali yake ilibakia vile vile. Aliendelea kuvalia kinadhifu na kuishi maisha yake ya fawaishi. Wakati wenzake wanalalamikia hali ngumu ya maisha, Bwana Sesame hakuwa na lolote la kumsumbua. Aliendelea kukaa bila kazi wala bazi. Lakini watu walitambua kuwa alikua na mazoea ya kutoka chumbani majira ya jioni. Hakuna aliyejua alirejea lini.

Siku moja Bwana Sesame alitoka jioni kama kawaida na kuelekea kwenye shughuli zake za kawaida. Siku hiyo jamaa mmoja wa mtaani alikumbana naye kwenye lango kuu. “Bwana Sesame, leo wapi yahe? alimwuliza. Bwana Sesame alimwangalia na kusema, “natoka nje kidogo yahe. Jiji hili lataka ustaarabu,’ alijibu. Yule jamaa alimwangalia na kumwabia na kumwambia, “nina shida kidogo, sijui kama utanifaa mwenzangu. Wajua tena hali zenyewe siku hizi,” alisema. Nini tena?’ aliuliza Bwana Sesame. “nina gari langu ambalo halina redio. Natafuta moja ya bei nafuu…. Kitu kama sony hivi,” alisema. Bwana Sesame alimwangalia na kusema, “hiyo kazi nyepesi kwangu yahe, papai kwa kijiko!” alisema Bwana Sesame alicheka. Jamaa Yule alishukuru na wakaagana.

Bwana Sesame alishika njia kuelekea sehemu zake za kawaida majira kama haya. Naye Yule jamaa akapinda kama anaangalia mtaani, lakini baada ya muda akageuka na kuamua kumfuata Bwana Sesame.

Bwana Sesame alishika tariki mpaka sehemu ya mazoeea. Yule jamaa alimfuata kwa mbali na mwendo wa paka. Alimwona Bwana Sesame akiingia mahali palipokuwa na banda kuukuu. Muda si muda alitoka na jamaa wengine wakiwa wamevalia maguo ya ajabu. Yule jamaa aliwafuata hadi mahali palipokuwa na ujia mwembamba ulioachana na barabara kuu. Alijificha mahali, na kutokana na hali ya sehemu ile akawa haonekani.

Muda si muda palitokeza gari dogo lililokuwa likiendeshwa na mwanamke mmoja. Bwana Sesame na wenzake walitokeza na kutupa gogo lililomzuia Yule mwanamke. Ghafla bin vuu walimvamia; wakaifungua milango ya gari mbio na kujivurumisha ndani. Gari lilitimuliwa kama risasi kuelekea upande wa pili. Wakati huo Yule jamaa ashaliangalia gari lenyewe na kuzihifadhi nambari zake. Alishika njia kurudi zake chumbani.

Siku iliyofuata huyo jamaa hakuwa kazini. Alipokuwa akifungua kinywa alisikia sauti ya kugongwa kwa mlango. Aliinika na kwenda kuufungua. Bwana Sesame aliingia ndani. “vipi yahe? Kujenda kazini leo? Au umelala sana Bwana?’ alisema Bwana Sesame kwa uchangamfu wake. Muda si muda alimwonyesyesha redio ya gari aliyokuwa nayo. “umeipata mara moja hii kumbe?’ aliuliza Yule jamaa. “si nilikwambia yahe! Mimi ndiye Bwana Sesame mwenyewe. Hii kwangu si kazi. Ninafahamiana na jamaa wengi wanaoifanya kazi hii,” alisema Bwana Sesame. “naona kweli. Ehh Bwana we! Ndipo waswahili wakasema, ukitaka kuvua vua na wavuvi! Alisema Yule jamaa. “ni kweli kabisa!’” alijibu Bwana Sesame huku akicheka kwa furaha.

Yule jamaa alisimama kuelekea chumbani. Bwana Sesame alitulia akisubiri kupokea ujira wake. Muda mfupiulipita, kisha mlango wa nyumba ukagongwa. (yahe Bwana, kunagogwa huku!”  Bwana Sesame akasema. Yule jamaa alitoka chumbani na kuelekea mlangoni. Mlango ulipofunguliwa waliingia waliingia askari polisi wawili. Bwana Sesame hakuwa na upenyu wa kutokea. Alitiwa mikononi. Hakujua kumbe Yule jamaa alikuwa kachero. Hapakuwa na ujanja tena. Siku hiyo pwagu alipata pwaguzi. Fungua Sesame haikufaa tena.

Maswali

  1. Kwa nini Nimrode alibatizwa ‘Bwana Sesame’? (al 1)
  2. Kwa nini watu walioishi mtaani Urumo walishangazwa na utaratibu wa kazi wa Bwana Sesame? (al 2)
  3. Unafikiria ni kwa nini Bwana Sesame alifahamu sana juu ya magari? (al 1)
  4. Je, unafikiri yule jamaaa aliyaagiza aletewe radio alikuwa na haja sana na kifaa hicho kama alivyosema? (al 2)
  5. Bwana Sesame alikuwa kachero. Unakubali? Toa maelezo? (al 2)
  6. Yule jamaa alipoingia chumbani na kumwanch Bwana Sesame sebuleni unafikiri alikwenda kufanya nini? (al 2)
  7. Je, hadithi hii ina mafunzo gani kwako? (al 2)
  8. Eleza maana yamisemo ifuaayo kisha aitumie katika sentensi (al 3)
    1. Piga mluzi
    2. Piga soga
    3. Shika tariki

3. Matumizi ya lugha (al20)

  1.                          
    1. Taja ala sogezi mbili za kutamkia (al2)
    2. Tambua sauti yenye sifa zifuatazo (al 1)
      konsonanti, kipasuo, ghuna, sauti ya mdomo
  2. Tunga sentensi moja na uonyeshe nomino dhahania (al 2)
  3. Tambua aina za maneno zilizopigiwa mistari
    Mwanafunzi mrefu alienda Nairobi (al1)
  4. Bainisha ngeli ya nomino iliyopiwa mistari. (al 1)
    Jeshi la Kenya lilihamisha kifaru hadi mbuga ya masai mara.
  5. Taja aina mbili za mofimu. (al 2)
  6. Taja dhana zinazowakilishwa kisarufi na viambishi vilivyopigwa mistari (al 1)
    Walituchezea
  7. Bainisha kivumishi katika sentensi hii (al 2)
    Matunda mawili yaliuzwa
  8. Tunga sentensi ili kubainisha tofauti za kimaana kati ya maneno haya udogo na udongo (al2)
  9. Kwa kutumia sentensi moja onyesha vitenzi sambamba (al 2)
  10. Tunga sentensi moja na uonyeshe kiwakilishi kimilikishi (al 2)

ISIMU JAMII

  1. Eleza maana ya istihali zifuatazo za isimujamii (al 2)
    1. Isimu jamii
    2. Sajili
  2. Matumizi ya lugha hutegemea mambo kadhaa. Yaeleze yoyote manne (al 8)

FASIHI (AL 10)
Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuatia

Malenga mlotukuka, kwa tungo zenu teule
Tungo zenye kusifika, zenye na nasaha tele
Naomba la uhakika, jawabu enyi wavyele
Wa kuume tangu lini, kuukata wa kushoto!

Tangu dahari miaka, mikono ina upole
Meungana pasi shaka, ni miwili vile vile
Mmoja ukisumbuka, mwingine hujaa ndwele
Wa kuuma tangu lini, kuukata wa kushoto!

MASWALI

  1.                      
    1. Shairi hili ni la arudhi. Dhibitisha kwa kutoa sababu tatu (al 3)
    2. Nakili kibwagizo cha shairi hili (al 1)
    3. Eleza ujumbe mmoja unaojitokeza kwenye shairi (al 2)
  2.                      
    1. Taja aina zo zote mbili za hadithi (al 2)
    2. “nikitembea yuko, nikikimbia yuko, nikiingia ndani hayuko
      1. tambua kipera hiki (al 1)
      2. taja dhima moja ya kipera hiki kijumla (al 1)

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. Insha
    Mchumia juani, hulia kivulini
    Ni methali
    1. Anayefanya kazi kwa bidii baadaye/ mwishowe hufanikiwa
    2. Mtahiniwa abuni kisa kinachoendana na methali
    3. Ashughulikie pande zote mbili za methali
    4. Asipolenga mada atuzwe alama 02/20
    5. Andike kurasa mbili.(moja na robo tatu hivi)
  2. Ufahamu
    1. Alikuwa na ufumbuzi wa kila jambo (al. 01)
    2. Alikaa mchana nyumbani na kutoka jioni. Alikuwa na utaratibu wa kufanya kazi usiokuwa wa kawaida. (al 1)
    3. Alihusika nayo sana. Inaelekea kuwa alikuwa mwizi wa magari. (kila hoja alama nusu)
    4. La. Alikitumia hicho kama chambo tu. Ulikuwa mtego wa kumshika bwana Sesame. (1mks)
    5. La. hakuwa kachero bali mhalifu. Alikuwa akifanya kazi ya uhalifu. Alikuwa mwizi wa magari (1mk)
    6. Alikwenda kupiga simu. Kutoa taarifa kwa polisi.(1mks)
    7.                    
      1. siku za mwizi ni arubaini
      2. Kuchuma halali ndiko kuchuma kufaako.
    8.                
      1. A. toa sauti kwa ulimi na mdomo
      2. Kuzungumza, kupiga domo
      3. shika njia, fuata shuguli zako.

Tanbihi

  • Ondoa alama 3 za makosa ya sarufi yanapotokea mara ya kwanza (6 × ½)
  • Ondoa alama hadi mbili kwa makosa ya hijai yanapotokea mara ya kwanza (4 × ½)

3. Matumizi ya lugha

  1.                          
    1. ulimi, midomo, nyuzi sauti(2) mbili za kwanza
    2. /b/
  2. nomino zisizoshikika
    mwalimu akadirie majibu. Asipoonyesha asituzwe
    ujinga wa mwanafunzi ulimtia kwa shida
  3. mrefu – kivumishi (cha sifa)
    Nairobi – kielezi (cha mahali
  4. a-wa
  5. mofimu huru
    mofimu tegemezi
  6. tu- mtendewa/ yambwa/ shamirisho(2mks)
    e– mnyambuliko (2mks)
  7. mawili ; kivumishi cha idadi kamili.
    mwalimu akadirie majibu maneno haya lazima yawe kwenye sentensi bila maneno yote asituzwe.
  8. udogo- kutokuwa kubwa
  9. vitenzi viwili au Zaidi vifuatane katika sentensi, kwamfano; baba alikuwa akisoma kitabu
  10. mwalimu akadirie majibu kwamfano; chake mwalimu kiliibwa

FASIHI

  1.                                  
    1.                  
      1. Idadi sawa ya mishororo kila ubeti
      2. Urari wa vina (ndani kati na nje)
      3. Urari wa mizani kila mshororo
      4. Vipande viwili kila mshororo katika shairi nzima
      5. Mishororo kifu (mshororo iliyokamilika kimuundo tatu za kwanza.
    2. wa kuume tangu. Lini, kukata wa kushoto!
    3. – ushirikiano
      - kutofanyia mwenzako mabaya
      - kusaidiana
  2.                    
    1. hekaya
      Mighani/ migani
      Mbazi
      Hurafa
      Hadithi za mtanziko
      Usuli (zozote mbili)
    2.                                
      1. kitendawili (asipopata b (i) asitunzwe
      2. hataakipata
    3. huburudisha
    4. hupanua ubongo
    5. huelimisha
      hukuza lugha
      hutumiwa kuondoa uchovu baada ya kazi
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 2 End Term 1 Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest