Kiswahili Karatasi ya 1 Form 3 Questions and Answers - End Term 2 Exams 2021

Share via Whatsapp

Kiswahili Karatasi ya 1 Form 3 End Term 2 Exams 2021 with Marking Schemes

MAAGIZO:

  1. Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
  2. Kisha chagua insha moja nyingine kutoka kwa hizo tatu zilizobakia.
  3. Insha yako isipungue maneno 400.
  4. Kila insha ni alama 20.

Maswali

  1. Kamati inayoshughulikia usalama barabarani imekuwa na mkutano hivi karibuni.Ukiwa katibu wakamati hiyo , andika kumbukumbu za mkutano huo (Al 20)
  2. Ufisadi umechangia pakubwa kuwepo kwa maendeleo duni nchini. Jadili (Al 20)
  3. Andika insha inayoafikiana na methali Baniani mbaya kiatu chake dawa. (al 20)
  4. Andika insha itakayomalizikia kwa “…ndiyo maana nimeapa ya kwamba usiku siwezi nikamfungulia mlango yeyote nisiyemjua (Al 20)

Majibu

  1. Kamati inayoshughulikia usalama barabarani imekuwa na mkutano hivi karibuni.Ukiwa katibu wa kamati hiyo , andika kumbukumbu za mkutano huo (Al 20)

    - Mwanafunzi afuate utaratibu wa kuandika kumbukumbu
    - Insha yake iwe na:
    • Kichwa ( kumbukumbu za mkutano wa kamati/jopo gani,kuhusu nini,uliofanyika wapi,tarehe gani na saa ngapi
    • Waliohudhuria (mwenyekiti,katibu,mweka hazina,wanakamati)
    • Waliotuma udhuru kwa kutohudhuria
    • Waliokosa kutuma udhuru kwa kutohudhuria
    • Waalikwa
    • Ajenda
      1.  Kufunguliwa kwa mkutano
      2. Kusoma na kudhibitishwa kumbukumbu za mkutano uliotangulia
      3. Masuala yaliyotokana na kumbukumbu hizo
      4. Ajenda kuu za mkutano husika
      5. Shughuli nyinginezo
      6. Kufunga mkutano
    • Thibitisho
  2. Ufisadi umechangia pakubwa kuwepo kwa maendeleo duni nchini. Jadili

    - Hili ni swali la kujadili. Mtahiniwa anahitajika ashughulikie pande zote mbili za mada.
    • Mtahiniwa aweza kukubaliana na mada kuwa kwa kiwango kikubwa maendeleo duni yamechangiwa na ufisadi na kuwepo kwa ufisadi au aonyeshe kuwa si kwa kiwango kikubwa vile kwani kuna sababu nyingine zinazochngia maendeleo duni nchini.
    • Kwa vyovyote vile, pande zote za mada zishughulikiwe. Haijailishi kama upande mmoja utakuwa na hoja nyingi kuliko upande mwingine.





    - Baadhi ya hoja ni:

    Kuunga mkono
    • Kwa sababu ya hongo, kiasi fulani cha pesa za miradi hutolewa kama hongo. Hali hupunguza kiasi cha pesa za kuteleleza mradi husika.
    • Kwa sababu ya ufisadi, utekelezaji wa miradi huwa wa kiwango cha chini.
    • Wanaofaa kuhakikisha kuwa kuna viwango vya juu vya utekelezaji wa miradi huhongwa na hivyo kuidhinisha kazi duni.
    • Kandarasi za miradi ya maendeleo hutolewa kwa wanakandarasi fisadi ambao pengine hawana ujuzi katika kufanikinisha mradi husika au ambao watatumia vifaa duni ili faida yao iwe kubwa.
    • Wafadhili hukataa kuipa nchi pesa za kufadhili miradi fulani kwa hofu ya pesa hizo kutumika vibaya, hivyo basi miradi mingi haipati pesa za kutosha.
    • Kuna ubadhirifu wa pesa za miradi na wanaosimamia hazina za maendeleo hivyo kuinyima miradi ya maendeleo pesa zinazohitajika.

    Kupinga
    • Hakuna pesa za kutosha nchini za kufadhili miradi mingi ya maendeleo.
    • Utekelezaji mbaya wa miradi waweza kutokana na ukosefu wa vifaa bora nchini kwa hivyo vinavyotumiwa vikawa na matokeo duni.
    • Kwa sababu ya siasa, miradi ya maendeleo ikatelezwa visivyo hasa katika sehemu ambayo ni ngome ya mpinzani.
    • Wakati mwingine pesa za kutekeleza miradi hutumika kununulia vitu kama magari, kulipa mishahara, kulipa marupurupu nk badala ya kugharamia miradi.

      TANBIHI
      - Zingatia hoja zozote nyingine mwafaka
  3. Baniani mbaya kiatu chake dawa.

    - Maana. kiatu cha baniani ni kitu ambacho mtu au kundi la watu limechukia au kudharau
    - Dawa: Kitu husika huenda kikawa ndicho jibu au jawabu au suluhisho kwa tatizo fulani maishani mwa mtu au katika jamii
    - Mtahiniwa aandike kisa kuthibitisha matumizi haya ya methali
    - Methali nyingine zenye maana sawa ni;
    • Matango na matikiti ndio maponya njaa
    • Wembamba wa reli gari moshi hupita
    • Nyumba nzuri si mlango fungua uingie

    Utuzaji
    • Pande zote za methali zishughulikiwe.Anayeshughulikia upande moja asipite alama C 08/20
      Anayetaja tu upande wa pili bila maelezo kikamilifu achukuliwe kuwa amelenga lakini ana udhaifu wa maudhui
    • Anayekosa kulenga katika kisa chake amepotoka kimaudhui alama D 03/20
  4. Andika insha itakayomalizikia kwa “…ndiyo maana nimeapa ya kwamba usiku siwezi nikamfungulia mlango yeyote nisiyemjua (Al 20)
    - Ni lazima mtahiniwa amalize insha yake kwa maneno aliyopewa bila ya kuyaacha mengine wala kuongeza yake.
    - Insha iwe na kichwa
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Karatasi ya 1 Form 3 Questions and Answers - End Term 2 Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest