Kiswahili Karatasi ya 3 Form 3 Questions and Answers - End Term 2 Exams 2021

Share via Whatsapp

Kiswahili Karatasi ya 3 End Term 2 Exams 2021 with Marking Schemes

MAAGIZO:

  1. Jibu maswali manne pekee
  2. Swali la kwanza ni la lazima.
  3. Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu tatu zilizobaki ,yaani Riwaya,Tamthilia naFasihi simulizi.
  4. Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
  5. Watahiniwa ni lazima wahakikishe kuwa maswali yote yamo na kurasa zote zimepigwa chapa sawasawa.

SEHEMU A (LAZIMA): USHAIRI (alama 20)

  1. USHAIRI:

    Soma shairi hili kasha ujibu maswali yanayofuata.

    SABUNI YA ROHO

    Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?
    Ndiwe suluhu la zama, waja wa kukimbilia,
    Waja wana kutazama, madeni wakalipia,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Ndiwe mafuta ya roho, walisema wa zamani,
    Utanunua majoho, majumba na nyumbani,
    Umezitakasa roho, umekuwa mhisani,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Matajiri wakujua, wema wako wameonja,
    Nguo zao umefua, wakupata kwa ujanja,
    Sura zao mefufua,wanazuru kila Nyanja,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Ndiwe mvunja mlima, onana na maskini,
    Watazame mayatima, kwao kumekua wa duni,
    Wabebe waliokwama, wainue waliochini,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Ndiwe mvunja mlima, wapi kupata uwezo?
    Umezua uhasama, waja kupata mizozo,
    Ndiwe chanzo cha zahama, umewaitia vikwamizo,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Umevunja usuhuba, familia zazozana,
    Walokuwama habuba, kila mara wagombana,
    Roho zao umekaba, majumbani wa chinjana,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Nakutafuta kwa hamu, sabuni unirehemu,
    Sinilipue ja bomu, sije kawa marehemu,
    Niondoe jehanamu, ya ufukara wa sumu,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Naondoka wangu moyo, nikuitapo itika,
    Fulusi wacha uchoyo, tatua yalonifika,
    Nichekeshe kibogoyo, name nipate kuwika,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Maswali
    1. Mshairi anaongea na nani katika shairi hili? [alama1].
    2. Taja majina mengine matatu aliyopewa huyu anayesemeshwa[alama3].
    3. Anayezungumziwa katika shairi hili anasababisha balaa gani?[alama2]
    4. Mshairi anatoa mwito gani kwa mwenziwe?[alama4]
    5. Fafanua maudhui ya ubeti wa sita.[alama2]
    6. Mbinu kadha za uandishi zimetumiwa na msanii kuwasilisha ujumbe wake. Taja mbinu zozote tatu na uzitolee mifano katika shairi.[alama3]
    7. Fafanua maana ya : sura zao ’mefufua, wanazuru kila nyanja’[alama1]
    8. Andika ubeti wa saba katika lugha nathari.[alama4]

SEHEMU B: CHOZI LA HERI [alama 20]

Jibu swali la 2 au 3

  1. Eleza jinsi mbinu ya majazi imetawala kazi ya kisanaa ya mwandishi wa chozi la heri.[alama 20]
  2. Jadili dhana ya chozi katika riwaya ya chozi la Heri.[alama 20]

SEHEMU C: TAMTHILIA (alama 20)

Tamthilia: kigogo

Jibu swali la 4 au 5.

  1. “Dalili ya mvua ni mawingu, lazima fume macho.”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili.[alama4]
    2. Ni kitu gani kilichopelekea msemaji kutamka kauli hiyo.[alama2]
    3. Taja sifa za msemaji.[alama6]
    4. Eleza methali zingine tano zilizotumika katika tamthilia hii.[alama8]
  2.  
    1. Eleza matumizi ya vipengele vya ushairikatikatamthiliayakigogo.[alama7
    2. ukombozi wa jamii yoyote unahitaji uvumilivu kupiga moyo konde .Thibitisha kauli hii ukirejelea tamthilia ya kigogo.[alama6]
    3. Tofautisha kwa mifano thabiti mbinu za litifati na tadmini kama zilivyotumika katika tamthilia ya kigogo.[alama7]

SEHEMU D: FASIHI SIMULIZI. (alama 20)

Jibu swali la 6

  1. Soma utungo ufuatao kasha ujibu maswali.

    Ndimi mwimo mdumishaji ukoo,
    Ndimi ndovu mtetemesha ardhi,
    Aliyegigang vita, ukoo kiauni,
    Ziliporindima zangu nyayo
    E dui alinywea, mafahali na mitamba akatukabidhi.
    Kwenye misitu sikuwa na kifani
    Paa na hata visungura
    Vilijikabidhi kwangu
    Kwa kuinusatumata
    Nani aliyewahi
    Ngomani kunifiku?
    Makoo hawakunisifu, wakalilianikaha?
    Kwenye Nyanja zamichuano
    Nan iangethubutu, ndoro kunipigia?
    Sikuwa bwaga chini, kwaya ngumaozi, hata kabla hatujavaana?
    1. Andika aina ya sifo hii na utaje sifa za kembili. (alama 4)
    2. Bainisha shughuli mbili za kiuchumi na mbili za kijamii zinazoendelezwa n ajamii inayosawiriwa na utanzu huu. (alama 5)
    3. Eleza mambo matano ambayo yanaweza kuzingatiwa ili kufanikisha uwasilishaji wa utungo huu. (alama 5)
    4. Eleza faida sita za matumizi ya nyimbo katika uwasilishaji wa ngano. (alama 6)

Majibu

  1.  
    1. Mshairi anaongea na nani katika shairi hili?
      • Pesa 
    2. Taja majina mengine matatu aliyopewa huyu anayesemeshwa
      • Sabuni ya royo
      • Mvunja milima
      • Mafuta ya roho
      • Fulusi
      • Tu ya ntima
      • Suluhu la zama
    3. Anayezungumziwa katika shairi hili amasababisha balaa gani?
      • Amesababisha uhasama/uadui
      • Ugomvi kati ya wapanzi
      • vifo
    4. Msahairi anatoa mwito gani kwa mwenziwe?
      • Awaarike maskini na mayatima.
      • Asimwangamize bali bali amwandoe ufukara
      • Amwitapo uchoyo/amtatulie shida zake
      • Amechekeshe/ amfurahishe
    5. Fafanua maudhui ya ubeti wa sifa.
      • Pesa zimezua uhasama katika ndoa nyingi na kusababisha vifo.
    6. Mbinu kadha za uandishi zimetumiwa na msanii kuwasilisha ujumbe wake. Taja mbinu zozote tatu na uzitolee mifano katika shairi.
      • Istiara- pesa ni sabuni /mafuta 
      • Semi –mvunja mlima
        -sabuni ya roho
      • Tashhisi- umevuna usuhubai
        -Umezua uhasama
      • Balagha- kwa nini wanikimbia?
        Wapi kapata uwezo?
      • Takriri- ndiwe mvunja mlima
    7. Fafanua maana ya : sura zao’mefufua, wanazuru kila nyanja’
      • Pesa zimewaletea furaha hata wanatalii sehemu zozote wanazotaka.
    8. Andika ubeti wa saba katika lugha nathari.
      • Mshairi anasema kuwa anamtafuta pesa sana ili amsaidie. Anamsihi asimpige kwa kumtoroka na kumwacha hoi bila uwezo. Anamwomba amuondoe katika lindi hili la umaskini kwa vile yeye ndiye anayetuliza watu na kuwaondolea matatizo ya kila namna.

SEHEMU B: CHOZI LA HERI

  1. Mbinu ya majazi

    Majina mengi ya wahusika yamejengwa kimajazi ambapo majina hayo yamebeba tabia za mhusika mwenyewe.

    Ridhaa; jina hili linabeba maana ya hali ya kukubali au kutosheka na jambo Fulani. Mhusika Ridhaa anakubaliana na hali ya upweke uliomkuta baada ya kufiwa mkewe Terry,mwanawe Tila,mkaza mwana wake Lily na mjukuu wake Beky. Katika kukubaliana na hali hiyo,Ridhaa anaacha kundoa majivu ya miili hiyo iliyotekea kwa moto ili kukubaliana na hali hiyo

    Tenge; jina hili linarejelea kwenda kombo. Kitendo cha Bwana huyu hususan kitendo kitendo cha kuigiza wanawake ndani na kushiriki nao ufuska wakati mkewe ameenda kazini kinasawiri kabisajina lake.

    Wahafidhina; hili nalo ni jina la kimajazi likiirejelea jamii isiyotaka kubadili mtazamo wa mambo .Mwandishi ametumia jinahilo kwa kuwakatika jamii bado kuna watu wameshikilia msimamo kwamba mwanamke hawezi kupewa madaraka ya juu ya kiuongozi.

    Msitu wa Heri; hii ni ardhi iliyokuwans rutuba.Bwana Lunga-Kiriri Kangata aliweka makazi yake hapa akajikuta heri imemwangujia kutokana na kufaidi mazo ya kilimo. Hata hivyo,kitumbua kiliingia mchanga walipofurushwa na dola kwamba wanaishi hapo kiharamu.

    Mwekevu Tendakazi; jina Mwekevu limetokana na nenola Kiswahili “wekeza” lenye maana ya kufanya jambo Fulani kwa lengo la kuzalisha Zaidi baadaye.Jina Tendakazi ni mwambatano wa manen “tenda” na “kazi” kwa maana ya kufanya shughuli. Mwekevu Tendakazi aliweka juhudi nyingi katika kuwainua raia alipokuwa mkurugenzi wa Shirika la Chemchemi ambazobaadaye zlizaa matunda kwa wnanchi kumwamini na kumchagua

    Majina mengine ya kimajazi ni kama vile Dhahabu,Mwenge,Chandachema,Hazina,Waridi,Subira,Neema,Nyangumi,Kipanga,Tindi na kadhalika 1×20= alama 20
  2. Jadili dhana ya chozi katika riwaya ya chozi la heri
    • Wahusika wengi katika riwaya hii wamepitia mikasa mingi mizito iliyowapelekea kuwa na huzuni na kutoa machozi
    • Kuna waliotao machozi ya huzunina wengine wakatoa machozi ya furaha wakati walipofikia hatima yajanga au majanga yaliyowakabili.
    • Vilio vya kite vilihanikiza wakati makundi mawili yalipopambana.Kundi liliomwuunga mkono Mwekevu na lililomwunga mkomo mpizani wake mwanaume.
    • Aghalabu machozi ya huzuni yamewabubujikia wahusika kama Ridhaa .Ridhaa alilia machozi wakati familia yake na juma lake la fahari lilipoteketezwa kwa moto.
    • Neema alilia kwa uchungu wakati alipokumbuka kisa cha Riziki Immaculata kitoto alichookota na akaoga kukichukua na kukitunza .
    • Baadaye alidondokwa na machozi ya furaha wakati motto Mwaliko alipokubali kuwa motto wao wa kupanga.
    • Umulkheri alilia mara nyingi alipowakumbuka ndugu zake wawii Dickson na Mwaliko.
    • Aidha alihuzunika kwao nyumbani.
    • Watoto wote watatu wa Lunga Kiriri Kangata walilia machozi ya furaha walipokutana katika hoteli ya Majaliwa.
    • Mwangeka na Racheal Apondi walipofunga ndoa ,Ridhaa alilia machozi ya furaha.
    • Mwangeka alilia machozi ya kujihurumia wakati baba yake Ridhaa alipomweleza kwa nini hakutaka kuzika mabaki ya familia yake. Yeye aliachilia machozi yamcharaze bila kujali miiko ya nyanyayake. Nyanya aliusia kwamba haipasi mwanamume kulia machozi.
    • Mwageka na Annatila pamoja na watoto wengine walilia machozi wakati walipoigiza mbolezi ya mazishi ya mdogo wao Kim.
    • Wenyeji walilia wakilizunguka kaburi ktika viviga vya motto wa Ridha,Kim ambaye alifariki akiwa na miaka sita.
    • Kumbukumbu za Tila na Mukeli zilimfanya Mwangeka kutoa tone moja la chozi.
    • Machozi ya uchungu yalmtirika Umu alipotoka katika kituo cha polisi kutoa taarifa kuwa ndugu zake walikuwa wametoroshwa na Sauna ili wakafanywe vitega uchumi
    • Wakati Umu alipo alipokutana na Hazina alitokwa na machozi yenye mseto wa furaha na majonzi .Alifurahia kwa Hzina alijitoa kwenye maisha ya mtaani ya utegemezi na kupata kazi. Machozi ya uchungu yalitokana na fikira kwamba huenda ndugu zake wamo mitaani kama Hazina zamani
    • Dkt Ridhaa alilia wakati alipompoteza motto wake huyo aliyekuwa na miaka sita.
    • Kairu ,mama yake na familia yake walilia machozi ya uchungu wakati mnuna wake mchanga alipofia mgongonimwa mama yake na wakamzika porini.
    • Subira alikuwa na majonzi kutokana na chuki ya mama mkwe wake kwa vile hakuwa ametoka jamii moja na yeye.
    • Mwanaheri alidondosha matone mazito ya machozi wakati akiwasimlia wenzake kifo cha mama yake.Aidha udhaifu alio nao Kaisari kutokana na unyama waliotendwa na pia kifo cha Subira.
    • Mara nyingi Umu alipofikiria ndugu yake Dick machozi yalimtiririka mno;ingawa alikuwa na wazazi wa kupanga waliompenda mno.
    • Wakati Umulhei na Dickson walikutana kisadfa katika uwanja wa ndege walitokwa na machozi ya furaha.
    • Wakati Mwangeka na Mwangemi walipomtania babu Mwino Msubili walipopigwa na kulia kwa uchungu.
    • Kaizari alitoa machozi ya huzuni wakati alipoona vijana wakipigwa risasi vifuani na askari baadae ya kusimama baabarani na kukataa kuondoka .Walisema “Hatungatuki”.
    • Kuna kilio cha Ridhaa alipobaguliwa katika mchezo ‘kavuta” wakati walipohamia ‘msitu wa Heri’ .
    • Kuna machozi ya mamba –yanayowatirirka viongozi wanafiki wakati wakigombea uongozi ;kujifanya kwamba wamewasikitikis wananchi wananchi zmbzo wamebanwa nz umasikini kupita kiasi.
    • Wale waliochomewa ndani ya mgari na vijana walilia vilio vya uchungu.
    • Ridhaa alilia machozi ya uchungu alipomwelezea Mwangeka mkasa wa kupoteza majumba yake.
    • Aidha Ridhaa akiwa katika gofu la jumba lake alikumbuka kilio cha Mwangeka akiwa kitoto kichanga.
    • Wakati Ridhaa alipokumbuka majadiliano yake na Terry macho yalifurika machozi akajijutia kuwa angelijua angemuuliza maswali yake yoke.
    • Vitoo venye njaa katika kambi za wakimbizi walilia machozi ya uchungu kabla kuzimia kwa maumivu.
    •  Subira naye alikuwa akikilovya kifua chake kila siku kwa sababu a shutuma za mama mkwe, Alisikitika sana kumwacha mumewe na watoto.
    • Selume alipolazimika kuacha nyumba yake na motto kwa sababu ya tofauti za kikabilaalilia.

      1×20=alama 20

SEHEMU C: TAMTHILIA (alama 20)

Tamthilia: kigogo

  1. “ dalili ya mvua ni mawingu, lazima fume macho.”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili.
      1. Msemaji wa ndondoo hili ni mzee kenga.
      2. Alikuwa akizungumza na majoka.
      3. Walikuwa katika ofisi ya majoka , walikuwa wana mazungumzo ya faragha.
      4. Mzee kenga alisema hayo baada ya kusoma gazetini kwamba idadi ya watu asilimia sitini ilikuwa tayari kumpigia tunu kura iwapo angesimama kupigania uongozi, kenga alisema hayo kumtaadharisha.
    2. Ni kitu gani kilichopelekea msemaji kutamka kauli hiyo.
      • Habari katika gazeti Fulani zilikuwa zimeeleza kuwa watu walipendekeza tunu awanie uongozi sagamoyo. Asilimia zaidi ya sitini walikuwa tiyari kumpigia kura Tunu iwapo angewaia uongozi. Majoka anasema kuwa huo ni upuzi na kuwa wafadhili wa Tunu wanampa sifa asizostahili. Hata hivyo, kenga anamtahadharisha kuwa awe macho kwa sababu huenda mengine makubkwa yakawafika kwani dalili ya mvua ni mawingu.
    3. Taja sifa za msemaji.
      • Msaliti- ameusaliti umma wa sagamayo kwa vitendo viovu vya kikatili alivyowafanyia. Anaidhinisha mauaji ya Tunu.
      • Mbinafsi- anafuata amri zote za majoka ili afaidike. Anatengewa kiwanja katika soko la chapa kazi.
      • Katili- alishiriki kupanga njama za kumuua jabali na alishiriki njama za kumuua Tunu lakini hakufanikiwa.
      • Kigeugeu- anakengeushwa na nguvu ya umma siku ya uhuru anaugana na watu waliofurika katika soko kuu la chapakazi kudai haki yao.
      • Ana dharau- anamdunisha sudi kuwa kinyago anachotengeneza hakiwezi kununuliwa.
      • Mpyoro- anamuita Tunu kuwa ni hawara wa Sudi.
      • Ana taasubi ya mfumo- dume! Anasema kuwa sagamoyo haiwezi kuwa na shujaa mwanamke.
    4. Eleza methali zingine tano zilitumika katika tamthilia hii.
      1. Maskini akipata matako hulia bwata- boza anansuta Sidi baada a Sudi kuizima redio aliyoisikiliza kwanye kijirununu chake. Boza anachukulia suala hilo kama hali ya kuwa na majivuno sawa nay a maskini aliyepata utajiri.
      2. Mavi ya kale hayaachi kunuka- Sudi anamwambia kenga kuwa mambo hayataendelea kama kawaida. Anasema kuwa nyakati si kama zile za zamani. Kenga kupitia methali hii anamwonya kuwa mabadiliko haya hayana nafasi kubwa.
      3. Mla ni mla leo, mla kesho kalani?- kombe anamwambia Sudi wakati Sudi anapowakejali kwa kukimbilia kula masazo ya kijikeki walichopewa na kenga. Boza na Kombe wanafikiria kuwa kula wakati huu ni muhimu, kasha ni ya mungu.
      4. Usitukane wakunga uzazi ungalipo- Majoka anamkejeli Ashua kutokana na Ashua kupingana na matakwa yake maovu na kusema kuwa wanafunzi shuleni mwake wanatumia madaw ya kulevya. Anachukulia haya kama matusi hivyo anamtishia kuwa huenda akamhitaji.
      5. Kila mwamba ngoma huvutia kwake- Kenga anamwambia Majoka kuhusu wafadhili ambao kumpiga debe Tunu na wanaharakati wengine kwa sababu wana mielekeo sawa kuhusu uongozi.1×5=5
  2.  
    1. Eleza matumizi ya vipengele vya ushairi katika tamthilia ya kigogo.
      • Wimbo wa kipropaganda: wimbo huu unachezwa katika redio mara baada ya tangazo la mjumbe kuhusu sherehe za uhuru wa sagamoyo. Wimbo huu unasafia jimbo la sagamoyo kwamba lina kiongozi ngao ambaye ni shupavu na anasujudiwa daima. Hata hivyo, sifa hizo ni za kinaya kwa kuwa jimbo la sagamoyo linasherehekea miaka sitini ya uhuru ilhali hakuna maendeleo ya kujiinia.
      • Wimbo kupitia sauti ya Hashima: wimbo huu unaimbwa na B. Hashima kuonyesha kuwa alikuwa amekata tama ya maisha. Katika wimbo huu B. Hashima anaongea na marehemu mume wake kwamba naye alikuwa njiani kufa kwamba hali inayeendelea katika jimbo la sagamoyo inadhihirisho kuwa muda wowote anaweza kumfuata mumewe peponi.
      • Shairi katika wimbo wa mamapima: mamapima anaimba wimbo huu kishairi ili kuwakashifu wale ambao wanajiingiza katika masuala ya kisiasa badala ya kuachana nayo na kujipatia raha. Wimbo huu umejaa maudhui ya kukajeli jitihada zote zaTunu na Sudi kupigania haki na usawa.
      • Shairi katika ndoto ya Majoka: shairi hii linadokeza mapenzi aliyo nayo Majoka juu ya Ashuaa, kupitia kwa ushairi huu tunafahamishwa kuwa Majoka juu ya Ashua hakumpenda Husda bali alimwoa fu ili kutimiza wajibu kwa kuwayeye ni kiongozi.
      • Sauti ya babu inayochukua muundo wa kishairi kupitia kwa shairi hili, Babu anamuasa Maajoka azinduke na atumie uwezo wake kujua kwamba mambo yamebadilika. Amkumbusha Majoka kuwa uovu aliotenda akitarajia apate ustawi ndio unaommaliza.
      • Wimbo wa ngurumo akimwimbia Tunu: huu ni wimbo wa kejali unamsuta Tunu kuwa ingawa ni msomi bado hajaolewa. Wimbo huu unaonyesha mtazamo hasi wa wanaume juu ya wanawake ambao huwa jaolewa.
      • Wimbo wa Asha: wimbo huu unasuta uongozi dhalimu kwamba umepinduliwa na hivi basi soko limefunguliwa tene bila kizuizi. Nyoka katika muktadha huu ni Majoka na vikaragosi wake. Huu ni wimbo ambao unabeba mauhui ya ukombozi wa wanasagamoyo dhidi ya udhalimu wa utawala wa Majoka.
      • Wimbo wa sauti ya watu: wimbo huu unaimbwa na umati wa watu waliokusanyika katika lengo la soko la chapakazi. Umuhimu wa wimbo huu ni kuwachochea wananchii wamuunge mkono Tunu katika harakati za kuikomboa sagamoyo. Sauti inasikika ikiimba kuwa yote yanawezekana naye Tunu na yote yanawezekana bila Majoka.1×7=7
    2. ukombozi wa jamii yoyote uanahitaji uvumilivu kupiga moyo konde.
      • Utangamano: ukombozi huhitaji umoja na mshikamano wa wanyonge. Tunu na Sudi wanashikamana na wanyonge wa sagamoyo kwa kukaidi kwenda kusherehekea uhuru katika viwanja vya ikulu. Umoja na mshikamano wao ndio unaafanikisha lengo lao la ukombozi.Utangamano: ukombozi huhitaji umoja na mshikamano wa wanyonge. Tunu na Sudi wanashikamana na wanyonge wa sagamoyo kwa kukaidi kwenda kusherehekea uhuru katika viwanja vya ikulu. Umoja na mshikamano wao ndio unaafanikisha lengo lao la ukombozi.
      • Ujasiri thabiti: kuwapo kwa vitisho vya hapa na pale kutoka kwa utawala wa Majoka haukuwavunja moya Tunu na Sudi.
      • Hata baada ya Tunu kupigwa na kuvunjwa mguu bado anaendelea kuwa na moyo uvumilivu na anaendelea na harakati za kuisaka haki.
      • Kushinikiza: wakati mwingine katika suala la ukombozi wa jamii, maandamano na migomo haviepukiki. Maandamano na migomo hutumiwa kama nyenzo ya kujikomboa panapokosekana muafaka wa kidiplomasia. Maandamano na mikutano isiyona kikomo inafanyika katika jamii ya sagamoyo, baada ya utawala wa Majoka kutosikiliza shida za wananchi.
      • Msimamo thabiti: watetezi wa haki za sagamoyo wanaonekana kuwa na msimamo thabiti dhidi ya vishawishi na hali za Majoka. Tunu anashawishiwa kuazwa kwa ngao junior.
      • Sudi anaraiwa kuchonga kinyongo cha Marara bin Ngao. Endapo atakubali atafadhiliwa apewe likizo ya mwezi mzima ughaibuni. Wanaharakati hao wanageuziwa kisogo hila hizo na wanaendelea na mapambano ya kuikomboa jamii.
      • Nguvu ya ushawishi katika harakati za ukombozi wa sagamoyo, Tunu na Sudi wanafanya jitihada mbalimbali za kuwashawishi wanchi waungane kudai soko la chapakazi lifunguliwe. Kwa ,fano,Sudi anatumia muda mwingi kuwashawishi Boza na Kombe. Hatimaye Kombe anaonyesha kumuelewa Sudi.
      • Tunu anashawishi wanasagamoyo wakusanyike eneo la langa kuu la soko la chapakazi siku ya sherehe za uhuru.
      • Kujitoa mhanga; Tunu anajitoa mhanga kuwapigania wanasagamoyo, anatumia elimu yake ya sheria kugai na kutetea haki za wanasagamoyo.
      • Huduma za kimsingi; watetezi wa haki wanadai wananchi wapate haki ya kufunguliwa soko lao,kupelekewa huduma muhimu kama vile shule,hosipitali na maji.
      • Uadilifu wa mkuu wa polisi;Kingi anakataa amri ya Majoka aliyetaka wananchi wapigwe risasi. Kingi anadai kuwa wananchi hao hawajavunja sheria hivyo hawawezi kupigwa. 1×8=8
    3. tofautisha kwa miano thabiti mbinu za litifati na tadmini kama zilivyotumika katika tamthilia ya kigogo.
      • Litifati ni mtindo ambao maneno yaliosemwa au kuandikwa na mandishi mmoja yananukuliwa na mwandishi mwingine. Yaani usemi wa mtu mwingine unachukukuliwa na kutumiwa katika matini nyingine. Katika tamthilia ya kigogo mbinu hii imetumika kwa kiasi Fulani hasa katika matumizi ya nyimbo.
      • Kwa mfano kuna wimbo za kizalendo unaochezwa katika redio baada ya tangazo la miumbe kuhusu maadhimisho ya miaka sitini ya uhuru wa sagamoyo. Wimbo huu unaosifia na kulitukuza jimbo hilo unafanana na wimbo uliozoeleka kusikia katika redio ya KBC. Nairobi uliokuwa ukjisifia taifa la Kenya.
      • Aidha kuna wimbo unaoimbwa na Ngurumo pamoja na walevi wenzake. Wimbo huu unatumika kumkejeli Tunu kwamba umri wake ni mkubwa lakini bado hajaolewa. Huu ni wimbo ulioimbwa na msanii Daudi Kabaka.
      • Licha ya nyimbo mifano mingine ya litifati ni wakati Majoka akiiga sauti ya Ashua “la koma! La koma! La koma! Siwezi mimi sitaki kuwa gurudumu la akiba”
      • Kwa upande mwingine , mbinu ya tadmini inahusisha unukuzi ambapo mtunzi au mwandishi anayanukuu maandishi fulani, hususan yanayoheshimiwa kama vile korani au biblia katika tamthilia hii, mwandishi amenukuu mtindo wa maandishi ya kibiblia wakati Babu akizungumuza na Majoka katika ndoto.

        Vifungu vya biblia vilivyonakiliwa ni;
        -Binadamu ni mavumbi na mavumbi atarejea
        - Amin Amin nawaambia. 1×5=5
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Karatasi ya 3 Form 3 Questions and Answers - End Term 2 Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest