Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 3 Term 3 Opener Exams 2021

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  • Jibu maswali manne pekee.
  • Swali la kwanza ni la LAZIMA.
  • Chagua maswali mengine matatu kutoka sehemu nne zilizobaki yaani; Ushairi, Riwaya,Hadithi fupi na Tamthilia.
  • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
  • Kila swali lina alama 20
  • Majibu yote yaandike kwa lugha ya Kiswahili.


MASWALI

SEHEMU YA A: FASIHI SIMULIZI

  1.  
    1. Taja mifano minane ya vipera vya utanzu wa semi katika fasihi simulizi. (alama4)
    2. Fafanua sifa zozote tatu za mawaidha katika fasihi simulizi (alama3)
    3. Eleza umuhimu tatu wa ngomezi. (alama3)
    4. Eleza istilahi hizi za fasihi simulizi. (alama3
      1. Maghani
      2. Mapisi
      3. Misimu/simo
    5. Fafanua sifa zozote tatu ambazo mtambaji wa hadithi anastahili kuwa nazo. (alama3)
    6. Taja methali zozote mbili zilizo na dhana ya tashibihi. (alama2)
    7. Eleza sifa zozote mbili za nyimbo. (alama2)

SEHEMU YA B: USHAIRI

  1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata

    Mkata ni mkatika,harithi hatoridhiwa
    Sina ninalolishika,wala ninalochukuwa
    Mlimwengu kanipoka, hata tone la muruwa!
    Mrithi nini wanangu?

    Sina ngo’mbe sina mbuzi,sina konde sina buwa
    Sina hata makaazi,mupasayo kuyajuwa
    Sina mazuri makuzi,jinsi nilivyoachwa
    Mrithi nini wanangu?

    Sina kazi sina bazi ila wingi wa shakawa
    Sina chembe ya majazi mno ni kukamuliwa
    Nakwa’cheni upagazi,ngumu kwenu ku’tuwa
    Mrithi nini wanangu?

    Sina sikuachi jina,mkata hatasifiwa
    Hata nifanye la mana,mno mi kulaumiwa
    Poleni wangu sana,sana kwenu cha kutowa
    Mrithi nini wanangu?

    Sina leo sina jana,sina kesho kutwaliwa
    Sina zizi sina shina,wala tawi kuchipuwa
    Sina wanangu mi sina,sana la kuacha kuraduwa
    Mrithi nini wanangu?

    Sina utu sina haki,mila yangu meuliwa
    Nyuma yangu ili dhiki,na mbele imakaliwa
    N’na wana na milik,hadi nitakapofukiwa
    Mrithi nini wanangu?

    Sina ila kesho kwenu,wenyewe kulongowa
    Muwane kwa nyinyi mbinu,mwende pasi kupumuwa
    Leo siyo kesho yenu,kama mutajikamuwa
    Mrithi nini wananngu?

    MASWALI

    1. Taja mambo yoyote mawili ambayo mtunzi angewarithisha wanawe. (alama2)
    2. Eleza sababu ya mtunzi kutoweza kuwarithisha wanawe. (alama3)
    3. Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (alama4)
    4. Dondoa mifano miwili miwili ya: (alama2)
      1. Inkisari
      2. abdila
    5. Chambua shairi hili kwa upande wa:
      1. Dhamira (alama2)
      2. Muundo (alama4)
    6. Eleza maana ya vifungu vifuatavyo kama vilivyotumiwa katika shairi. (alama3)
      1. Mlimwengu kanipoka
      2. Sina konde sina buwa.
      3. Wingi wa shakawa.

SEHEMU YA C: RIWAYA
A.K Matei: Chozi la Heri

  1. Malezi ya watoto katika riwaya ya Chozi la Heri ndicho kitovu cha ufanisi na matatizo yote yanayowapiku watoto. Jadili (alama 20)
  2. “…, Di, ni mimi… niko hai. Auntie Sauna alishikwa na polisi. ’’
    1. Liweke dondoo hili katika muktadha wake (alama 4)
    2. Fafanua sifa za msemaji. (alama 6)
    3. Eleza tamathali moja ya lugha iliyotumika katika dondoo hii. (alama2)
    4. Sauna alishikwa na polisi? Elezea kikamilifu (alama 8)

SEHEMU YA D: HADITHI FUPI
A.Chokocho na D.Kayanda:
Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyinginezo

  1. "Penzi lenu na nani? . . . . Mgomba changaraweni haupandwi ukamea. Potelea mbali mkate wee!"
    1. Eleza muktadha wa dondoo hii. (alama 4)
    2. Taja na ufafanue mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili. (alama 4)
    3. Onyesha vile maudhui ya utabaka yanavyojitokeza katika hadithi nzima. (alama 6)
    4. Eleza sifa sita za mzugumzaji kwenye dondoo. (alama 6)
  2. Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika diwani ya, ‘Tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine.’ Jadili maudhui ya nafasi ya wazazi katika malezi. (alama 20

SEHEMU YA E: TAMTHILIA
P.Kea: Kigogo

  1. Tamthilia ya “Kigogo” ni kioo cha uhalisia wa maisha ya jamii nyingi za Kiafrika. Thibitisha.


MWONGOZO WA MAJIBU

SEHEMU YA A: FASIHI SIMULIZI

  1.  
    1.  
      1. Methali
      2. Misemo
      3. Nahau
      4. Vitanza ndimi
      5. Vitendawili
      6. Misimu / simo
      7. Lakabu
      8. Mafumbo.                                                Zozote8x½= (alama4)

    2. Sifa za mawaidha.
      • Huwa na mawazo mazito kuhusu maisha
      • Hutumia lugha iliyojaa misemo, methali na tamathali za sauti.
      • Hutumia lugha ya kuvutia na ya kubembeleza.
      • Huhitaji ustadi wa ulumbi.
      • Hutolewa na mtu mmoja.
      • Ujumbe ni wa mfululizo /moja kwa moja.
      • Mambomuhimuyenyemafunzohuibuka.
      • Hulengamaudhuimbalimbalikm.unyago.
      • Mtambaji anaweza kuwa kijana au mzee bora awe na ujuzi wa jambo hilo.    Zozote3x1=3

    3. Umuhimu wa ngomezi
      • Hutoa taarifa ya kuwafahamisha watu juu ya jambo fulani.
      • Hutahadharisha juu ya hatari.
      • Hutoa matangazo rasmi kuhusu jambo lolote katika jamii kv harusi.
      • Hudhihirisha ufundi wa kisanaa.
      • Huwatambulisha watu mashuhuri kv.wafalme,machifu,mashujaa au waganga Zozote3x1=3.

    4.  
      1. Maghani ni utungo wa kishairi ambao hutongolewa kwa kutumia sauti iliyo kati ya uimbaji na uzungumzaji / kalima. 1x1=1
      2. Mapisi ni maelezo ya historia ambayo hayana ubunifu wowote. 1x1=1
      3. Misimu ni maneno au semi ambazo huzuka wakati au kipindi Fulani miongoni mwa makundi ya watu. 1x1=1

    5. Sifa za mtambaji
      • Uwezo wa kuwasilisha hadithi /ngano kwa namna inayochangamsha.
      • Awe mbunifu.
      • Anayeifahamu hadhira – wake/waume/watoto/wazee.
      • Ufahamu mpana wa lugha.
      • Anayefahamu utamaduni wa hadhira.
      • Mcheshi - kunasa makini ya hadhira.
      • Uwezo wa ufaraguzi na kufahamu mbinu zifaazo za Sanaa na maonyesho.
      • Ufahamu wa tabia za binadamu – mambo yanayofurahisha / udhi. (alama 3)

    6. Mifano ya methali zilizo na tashbihi
      1. Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza.
      2. Kawaida ni kama sheria.
      3. Utajiri ni kama umande. (alama 2)
    7.   
      • Huwa na mahadhi ya kupanda na kushuka na mapigo ya kimziki.
      • Huandamana na ala za muziki kama vile ngoma.
      • Hufungamana na muktadha wa Fulani kwa mfano, harusi.
      • Huwasilishwa kwa hadhira hai.
      • Huwa na sehemu zinazoradidiwa. Zozote 2x1= 2

SEHEMU YA B: USHAIRI

  1.  
    1.  
      • Makazi mabovu
      • Upagazi
      • Kutothaminiwa
      • Dhiki
      • Kufanya kesho ya wengine nzuri. (zozote2x1=2)
    2.  
      • Ni maskini hohehahe / hana kitu
      • Aliporwa kila kitu. -
      • Hana mifugo.
      • Hana kazi yoyote.
      • Hana sifa / umaarufu.
      • Ana makazi mabovu.                    (zozote3x1=3)

    3. Sina jina nitakalowacha kwani maskini hasifiwi.
      Hata nikifanya jambo la maana ninalaumiwa tu.
      Poleni sana wanangu kwa kuwa sina la kuwatolea.
      Mtarithi nini wanangu?                        (zozote4x1=4)
      1. Inkisari
        Mana - Maana
        Meuliwa - Imeuliwa
        Nitapofukiwa – Nitakapofukiwa. (zozote2x½=1)
      2. Tabdila
        Muruwa -Murua
        Kutowa-Kutoa
        Kushipuwa -Kuchipua
        Kwongowa -Kuiongoa
        Kupumuwa –Kupumua (zozote2x½=1)
    4.  
      1. Dhamira
        Kuwahimiza watu kufanya bidii wakiwa vijana.
        Kulalamika kwamba maskini hana haki / huonewa / hapewi nafasi. (1x2=2)
      2. Muundo
        • Shairi ni aina ya tarbia / unne.Lina mishororo minne katika kila ubeti.
        • Mishororo ya kwanza mitatu imegawika katika sehemu mbili (ukwapi na utao). Kila kipande kina mizani minane na kila mshororo una mizani kumi na sita
        • Vina vya kati vinatofautiana kutoka ubeti mmoja hadi mwingine, lakini vina vya mwisho ni sawa katika shairi zima.
        • Shairi hili lina kibwagizo ambacho kimefupishwa. Mrithi nini wanangu?
        • Shairi hili lina beti saba. (Hoja zozote4x1=4)
    5.  
      1. Mlimwengu kanipoka – Mlimwengu kanipokonya.
      2. Sina konde sina buwa –Sina shamba sina chochote.
      3. Wingi wa shakawa – mashaka mengi. (3x1=3)

SEHEMU YA C: RIWAYA
A.K Matei: Chozi la Heri

  1.  Malezi ya watoto
    • Kuna ndoa kati ya Ridhaa na Terry inayowalelea watoto wao vizuri licha ya kuwa Terry anatengana na mume wake wa mkasa uliowapata.
    • Mwangeka alimuoa Lily Nyamvula aliyekutana naye katika Chuo kikuu.walikuwa na motto mmoja kwa jina Becky. Malezi yao hayadumu kwani Lily na Becky waliangamia kwenye janga la moto.
    • Mwangeka hapo baadaye alimwoa Apondi.Walibarikiwa na mwana wa kiume kwa Jina Ridhaa. Aidha ,Apondi anakuja na motto wake Sophie aliyekuwa wa Mandu mumewe wa awali kabla ya kufia ughaibuni alikokuwa ameenda kudumisha Amani. Mwangeka na Apondi wanawalea watoto wao vizuri kwa kuwapa elimu na mashauri. Dick na Umu wanashukuru kwa malezi yao.
    • Apondi anamshukuru Umu kwa malezi mazuri ya wadogo wake aghalabu anapokuwa mbali nao.
    • Mwangemi alimwoa mwanamke kwa jina Neema hawakupata mwanao ila walipanga Mwaliko ambaye wamemlea vyema kwa kumpa elimu na kusoma hadi Kitengo cha uzamili katika isimu na lugha.
    • Kangata alimuoa Ndarine na kubariki wana; Lunga Kiriri,Lucia Kiriri na Akelo Kiriri.waliwalea vyema kwani waliweza kuwapa elimu iliyowasaidia.
    • Kaizari alikuwa na mke kwa jina Subira.Walibarikiwa na mabinti wawili,Lime na Mwanaheri. Familia inapatwa na tatizo la kulea wanao kwa sababu ya ubaguzi wa mama mkwe kwa Subira jambo linalosababisha kifo chake.
    • Lunga alimuoa Naomi walibarikiwa na watoto watatu,Umu,Dick na Mwaliko.Ndoa hii ina changamoto katika malezi kwani Naomi anamtoroka mumewe jambo Linalosababisha kifo cha Lunga na watoto kama vile Dick kuingizwa katika ulanguzi wa dawa za kulevya.
    • Familia ya Pete ilikuwa ya watoto sita baada ya kugunduliwa kuwa hakuwa na mshabaha na babake aliweza kurudishwa kwa bibi jambo linalosababisha ndoa ya mapema.
    • Pete aliozwa na wajombake kwa Fungo alipoingia darasa la saba na baada ya kupashwa tohara Pete anaozwa kwa Fungo akiwa bibi wanne . Anapogundua kuwa anapata watoto watatu akiwa chini ya miaka ishirini na moja alitamani kujiua.Mtoto wake wa kwanza hakupata malezi yake kwani alimuacha kwa Fungo na kasha hawa wawili anawapata katika vibarua vya pombe.
    • Kuna wazazi wengi ambao wanatupa watoto wao na pia kuavya.Tunambiwa kuwa Neema aliweza kukiokota kitoto ambacho kilikuwa kimetupwa.Aidha alipokuwa chuo kikuu alikuwa ameweza kuavya.
    • Wazazi wa Zohali wanamkandamiza jambo ambalo linamfanya kutoroka nyumbani na kuwa mwana wa mtaani.Aidha kwake anasema kuwa hana wazazi anapohojiwa kwani walimkataa alipowahitaji Zaidi.
    • Babake Kairu hamsaidii mkewe katika malezi jambo ambalo halimpi Amani Kairu katika masomo.
    • Wazazi wake Chanda chema yaani ndoa kati ya Rehema na mwalimu wake (Fumba) ambaye sasa ni mhadhiri hawashughuliki na malezi ya mwanao Rehema jambo ambalo linamfanya maisha yake kuwa ya ombaomba.
    • Bwana Maya (mzazi mlezi) anamwingilia Sauna kimapenzi na kusababisha kupata ujauzito jambo linalomtia Sauna ujabali na unyama wa kujiingiza katika ulanguzi wa wa watoto. Zozote 20x1= al 20
  2.   
    1. Maneno haya yalisemwa na Mwaliko. Alikuwa akiwaambia Umulkheri na Dick. Tendo hili lilitukia katika mkahawa wa Majaliwa walipokutana kisadfa. Hii ni baada ya Mwaliko kumpeleka babake mlezi maeneo yale kusherehekea siku ya kuzaliwa kwake. (alama 4)
    2. Msemaji ni mwaliko.
      Mwenye maadii mema- Mwaliko alipopangwa na Mwangemi na Neema aliinukia kuwa ghulamu mwenye nidhamu ya hali ya juu akiwaheshimu wazazi na majirani na kuwatii wazazi.
      Mwenye shukrani- Mwaliko aliamua kumnunulia Mwangemi chakula kwenye hoteli ya Majaliwa
      Mwenye bidii- alifanya bidii masomoni hadi kufikia Chuo kikuu.Alijisajili kwa shahada ya uzamili katika taaluma ya mawasiliano na kuhitimu. Mwaliko anafanya kazi yake kwa bidii ya mchwa. Zozote 3x2= 6

    3. Kuchanganya ndimi- Auntie Di. Ni kwa nini Auntie (alama 2)

    4. Baada ya Umu kupiga ripoti kwenye kituo cha polisi kuwa nduguze wanuna wamepotea, Polisi walifanya uchunguzi na kujua kuwa walitekwa nyara. Aliyetekeleza kitendo hiki ni kijakazi Sauna. Sauna alikuwa akimfanyia biashara Bi. Kangara. Polisi walipojua mahali alikokuwa akijificha Bi. Kangara, walishika njia hadi nyumbani kwake ambako waliwatia mbaroni Bi Kangara na Sauna. Walifikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kosa la ukiukaji wa haki za watoto hivyo basi wakafungwa miaka saba gerezani na kazi ngumu. (alama 8)

SEHEMU YA D: HADITHI FUPI
A. Chokocho na D. Kayanda:
Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyinginezo

  1. "Penzi lenu na nani? . . . . Mgomba changaraweni haupandwi ukamea. Potelea mbali mkate wee!"
    1. Eleza muktadha wa dondoo hii. (alama 4)
      Mzungumzaji ni Penina. Anamzungumzia Dennis Machora (msimulizi)
      Wako nyumbani kwao (Machora na Penina) katika mtaa wa New. Zealand.
      Dennis Machora alikuwa amerudi nyumbanikutoka kampuni ya kuchapisha magazeti alikoenda kutafuta kazi lakini akaambuliapatupu.
    2. Taja na ufafanue mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili.(alama 4)
      Methali - Mgomba Changaraweni haupandwi ukamea
      Swali balagha - penzi lenu na nani?
      Nidaa . . . Mkata wee!
      Msemo - potelea mbali.
      Mdokezo (.....)
    3. Onyesha vile maudhui ya utabaka yanavyojitokeza katika hadithi nzima. (alama 6)
      Maudhui ya Utabaka.
      • Wazazi wa Dennis walijitahidi kumsomesha kwa kuwalimia matajiri mashamba.
      • Wazazi wa Penina walipinga uhusiano waDennis na Penina kwa kuwa alitoka tabaka la chini ilhali wao walikuwa matajiri.
      • Dennis anakunywa uji kama chamcha kwakukosa chakula ilhali Penina hupokea shilingi elfu tano kila wiki.
      • Dennis hangejiunga na shule aliyoalikwa kwa umaskni ilhali wenzake walisomea shule za hadhi kubwa.
      • Penina anapangiwa nyumba katika mtaa wa New Zealand. wanakoishi watu wenye mapato ya Kadri.
      • Penina anamkataa Dennis kwa kuwa hana uwezo wa kifedha kwa kukosa kazi na hangeweza kudumisha maisha yake ya kifahari.
      • Wazazi wa Dennis walimtegemea asome ili kuwatoa umaskinini ilhali wazazi wa Penina wanamkimu hata baada ya kumaliza masomo.
    4. Eleza sifa sita za mzugumzaji kwenye dondoo. (alama 6)
      • Msaliti - Alimsaliti mchumba wake Dennis kwa kumfukuza na kuwaibisha sababu ya umaskini.
      • Mwenye dharau - alimfokea Dennis kwadharau akimwita mkata.
      • Mwenye tamaa - ana tamaa ya mapenzi na akatafuta mchumba kwa bidii.
      • Mwenye bidii masomoni – alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha kivukoni.
      • Ni jasiri - alimwendea Dennis kutafata mapenzi na uchumba na mambo yanapokwenda kombo anamfukuza bila woga.
      • Mpyaro - alimtusi Dennis akimwita mkata
  2. Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika diwani ya, ‘Tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine.’ Jadili maudhui ya nafasi ya wazazi katika malezi. (alama 20
    • Tulipokutana Tena
      wazazi wa Bogoa - ni walezi wema ingawa ni maskini hawataki. Bogoa alelewe na wazazi wengine
    • Mapenzi ya kifaurongo
      wazazi wa Penina Bw & Bi Kitane) wamewajibika katika kumlea Penina. Wanampa fedha za kutosha kila wiki
      licha ya kuwa maskini wazazi wa Dennis wanajizatiti sana kumpeleka chuoni hadi chuo kikuu
    • Shoga yake Dada ana ndevu
      wazazi wake Safia na Lulua wanawapenda sana wanao
      wanawapeleka wanao shuleni na kuwapa safia nafasi ya kusoma pale nyumbani
      wazazi hawa pia wana mapuuza. Wanamwamini mwanao kupita kiasi
    • Mame Bakari
      babake Sara ni mkali sana, Sara anapobakwa anaogopa kumwambia kuwa ana ujauzito
      baadaye anabadilika wa kuwa mpole, anamfariji mamake Sara ni dhaifu, hawezi kumsaidia Sara 
    • mtihani wa maisha
      wazazi wa Samueli wanajinyima ili kuwasomesha watoto wao
      Babake Samueli aliuza ng’ombe wengi ili kumsomesha Samueli
      mamake Samueli anatumiwa kuonyesha mapenzi ya mzazi ni ya kudumu babake Samueli anatumiwa kuonyesha kukata tamaa / kutamauka.

SEHEMU YA E: TAMTHILIA
P. Kea: Kigogo

  1. Uhalisia wa jamii za kiafrika katika Kigogo
    • Uongozi mbaya- Majoka hajali haki za raia, wala kujali uhuru wa vyombo vya dola haheshimu katiba.
    • Mauaji ya watu – watu wasio na hatia katika Sagamoyo wanuawa kwa mfano mpinzani wake Jabali, waandamanaji.
    • Usaliti – Sagamoyo imesalitiwa na viongozi.Majoka anasaliti wananchi kwa kushughulikia mambo yake binafsi. Asiya anamsaliti mumewe ndoani kwa kushiriki uroda ili apate mradi wa kuoka keki.
    • Ulipaji wa kisasi – Majoka anamtia nguvuni Ashua ili alipe kisasi kwa Sudi kwa kuwa alimuoa hurulaini ambaye Majoka alimpenda.
    • Suala la migogoro – kundi la akina Tunu linazozana na watawala kwa kudai haki za Wanasagamoyo ziheshimiwe.
    • Ubinafsi –utawala wa Majoka ni wa kibinafsi.wanafunga soko la Chapakazi kwa manufaa yao wenyewe.
    • Ukoloni mamboleo – kuna kutegemea misaada kutoka nch za kigeni. Majoka anapokea mkopo kutoka mataifa ya nje ambao unatakiwa kulpwa kwa muda wa miaka mia moja.
    • Athari za ulevi na mihadarati – sagamoyo imejaa vijana waraibu wa unywaji pombe haramu. Ngurumo na waraibu wenzake wanaonekana mangweni kwa mama pima. Wanafunzi wa Majoka Academy wanatumia dawa za kulevya ambazo huwageuza makabeji.
    • Ufisadi – Ngurumo anadai kuwa watu kigogo wanapitia pale wakipewa vijisenti. Kenga anatoa ushauri mbaya kwa Majoka ili ajinufaishe.
    • Matumizi mabaya ya viombo vya dola – Chopi na askarijela ni wakatili na wapyaro.
    • Unyakuzi wa ardhi – Majoka ananyakua uwanja wa Chapakazi ili ajenge hoteli ya kifahari.
    • Kuangamiza wapinzani – Jabali aliuawa na utawala wa Majoka .
    • Tenga tawala – Majoka anagawanya wanasagamoyo ili awatawale kwa urahisi.
    • Elimu duni – wanafunzi wanatumia dawa za kulevya na kuwa makabeji.
    • Utawala wa kiimla – Majoka anatawala kwa kutumia mabavu.
    • Ulevi – pale mangweni Ngurumo wanaathirika kwa ulevi.
    • Matabaka- kuna vigogo wenye mali huku wale wengi wakiwa walalahoi wasio na kipato.
    • Ukosefu wa uwajibikaji – njaa inatokana na kufungwa kwa soko la Chaakazi
    • Ufujaji wa mali ya umma – Kenga anamrubuni Sudi kwa fedha nyingi.
    • Uchafu - mandhari ya soko ni machafu na Sudi anasema kuwa wanasumbuliwa na aina nyingi ndwele .
    • Uharibifu wa mazingira.
    • Migomo na maandamano. Zozote 20x1=20
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 3 Term 3 Opener Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest