Kiswahili Paper 2 Form 3 Questions and Answers - Term 3 Opener Exams 2021

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  • Jibu maswali yote.
  1. SEHEMU YA A: UFAHAMU           (ALAMA 15)
    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
    “Asubuhi moja ilinipata ndani ya afisi ya mwalimu mkuu wa Shule ya Kilimo. Mwalimu Mkuu, Bi. Tamasha alisikiliza kadhia yangu kwa makini. Hakuonyeha kushtuka kwa yaliyonipata katika umri wangu mdogo hivi.
    ‘Unaweza kuanza masomo katika darasa la pili. Nitamwomba mzazi mmoja akupe hifadhi,’ alisema Bi. Tamasha. Huo ndio uliokuwa mwanzo wa maisha yangu katika makao ya wafanyikazi wa mashamba ya chai. Bwana Tenge na mkewe, Kimai, walinichukua kunilea pamoja na watoto wao watano. Wenzangu, nyinyi hamjui adha zinazowapata wafanyakazi wa kima kidogo. Mtajuaje na haamjawahi kukikalia kitanda hiki mkafahamiana a kunguni wake? Ninayowaambia ni asilimia ndogo mno ya niliyoyaona. Chumba cha wafadhili wangu kilikuwa hichohicho kimoja; ndicho cha mlazi, ndicho cha mpokezi, ndicho jikoni. Sebule na chumba cha malazi viligawanywa na shuka moja nyepesi. Usiku sisi watoto tulilala juu ya vigodoro ambavyo ni kama viliwekwa mvunguni mwa kitanda cha wazazi.
    “Usiniulize niliyaona na kuyaskia mangapi katika chumba hiki ambacho kiligeuka danguro wakati Bi. Kimai alipokuwa ameenda mashambani. Wakati huu Bwana Tenge angeamua kumleta mwanamke mmoja baada ya mwingine, hapo hapo, mbele ya macho ya wanawe, hadi usiku wa kuamkia siku ya kurudi kwa Bi. Kimai. Mara mojamoja Bi. Kimai angerudi bila kutarajiwa na kumshika ugoni mke mwenzake!Mwaa mmoja, miwili, mitatu ... hata nikaona kwamba, mbali na dhiki za kisaikolojia nilizozipata kwa kushuhudia vituko vya kila aina, nilikuwa mzigo mkubwa kwa wahisani wangu. Si kwamba waja hawa walinibagua, la! Kusema hivyo kutakuwa kuwapaka mashizi bure. Hata hivyo nilihisi kwamba nimepata mbavu za kufanya angaa kibarua kidogo, na kuwatua wawili hawa mzigo wa kuninunulia sare na madaftari.
    “Nlianza kuchuna majani chai kwa malipo kidogo nikiwa katika darasa la tano. Wakati mwingine ningerauka alfajiri na mapema kufanya kazi kabla ya kwenda shuleni saa kumi na mbili asubuhi. Jioni nilipitia huko huko. Nyakati nyingi nililala humo humo katikati ya michai, wakati mwingine kwa marafiki wanfu, kwa Bwana Tenge, na juu ya uchaga mkubwa wa saruji uliotumiwa kama karo na wauza chakula sokoni. Hakuna mmoja kati ya walimu wangu aliyejua mabadiliko haya hadi pale nilipoufanya mtihani wangu wa darasa la nane na kufuzu vyema.
    “Wakati huo Bwana Tenge alikuwa ameishi kupewa uhamisho, akaenda kufanya kazi katika shamba lingine. Ndivyo wafanywavyo wafanyakazi hawa; kuhamishwa kila uchao bila mtu kuwazia kwamba wana watoto wanaoenda shule, na kwamba kuhamahama huku kunawavurugia masomo wana hawa.”
    Maswali
    1. Eleza namna wazazi wanavyoweza kuchangia katika kuzorotesha maadili ya watoto katika jamii.(al.2)
    2. Onyesha namna haki za watoto zilivyokiukwa katika kifungu.   (al.3)
    3. Wafanyakazi wa kima kidogo hupitia dhiki zipi kulingana na kifungu?  (al.3)
    4. Eleza sifa tatu za mkewe Tenge – Kimai.  (al.3)
    5. Eleza namna ndoa inavyosawiriwa katika kifungu. (al.2)
    6. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika kifungu;   (al.2)
      1. Danguro
      2. Kisaikolojia
  2. SEHEMU YA B    (ALAMA 15)
    Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali
    Ripoti za kila mara kuhusu uharibifu wa pesa za umma katika serikali za kaunti ni za kusikitisha. Kuna mabilioni ya pesa za mlipa ushuru ambazo hufujwa katika serikali kuu, na hivyo basi wananchi wanakosewa sana wanapoona mtindo huu ukiendelea pia katika serikali za kaunti. Wakati katiba ilipopitishwa mwaka wa 2010, wakenya wengi walikuwa na matumaini mno kwamba ugatuzi ungewatatulia matatizo ambayo walikuwa wakipata katika tawala zilizotangulia, hasa katika maeneo yaliyotengwa kimaendeleo.
    Miaka tisa baadaye, kuna mafanikio ambayo yamepatikana ila hatua kubwa zaidi inaweza kupigwa katika kuboresha maisha ya raia kama mianya inayotumiwa kufuja pesa za umma itazibwa. Wizi huu unaojumuisha pia jinsi magavana wanavyobuni nafasi za kazi zisizo na maana ambazo wakati mwingi hupeanwa kwa jamaa na marafiki wao, ni sharti ukomeshwe mara moja.
    Kuna wananchi wengi ambao tayari wameanza kufa moyo kuhusu umuhimu wa ugatuzi ilhali ukweli ni kwamba hatungependa kurejelea utawala ulio chini ya serikali kuu pekee. Changamoto za ugatuzi zinazosababishwa na ulafi wa viongozi wachache zinatoa nafasi kwa wakosoaji wa mfumo huu wa uongozi kushawishi wananchi na hata wahisani wasishughulike kuchangia kaatika maendeleo ya kaunti zao.
    Juhudi zozote zile za maendeleo haziwezi kufanikisha bila ushirikiano kutoka kwa wananchi na wahisani na hivyo basi ni jukumu la viongozi kuonyesha nia ya kutumia mamlaka waliyopewa kwa manufaa ya raia. Tume ya maadili ya kupambana na ufisadi (EACC) kufikia sasa imeonekana kufanya kazi nzuri kwa kuwasaka na kuwashtaki magavana walio mamlakani na wengine walioondoka, kwa kushukiwa kufuja mali za umma. Tungependa asasi zote zinazohusika na masuala ya kupambana na uhalifu, pamoja na wadau wengine katika jamii wenye nia njema kwa wananchi wasifumbie macho maovu yanayotendwa katika kaunti zetu.
    Nchi hii inatawalwa kwa misingi ya kisheria na hivyo basi hakuna sababu kumhurumia kiongozi yeyote anayekiuka sheria anapokuwa mamlakani kwa msingi wa mamlaka aliyoshikilia. Ni kupitia adhabu kali za kisheria pekee ambapo tutafanikiwa kukomesha uongozi mbaya kwani kama wananchi watakuwa wakisubiri kuwaadhibu wahusika kwa kuwaondoa mamlakani pekee, watakuwa wametoa nafasi ya ufujaji kwa viongopzi wapya kila miaka mitano.
    Maswali
    1.  
      • Fupisha ujumbe wa aya tatu za kwanza kwa maneno 80.               (al.8, 1 ya mtiririko)
        1. Matayarisho
        2. Jibu
    2.  
      • Fupisha aya mbili za mwisho kwa maneno 70.                     (al.7, 1 ya mtiririko)
        1. Matayarisho
        2. Jibu
  3. SEHEMU YA C    (ALAMA 40)
    1.    
      1. Elezea sifa mbili za sauti /e/.  (al.1)
      2. Elezea maana ya sauti mwambatano. (al.1)
      3. Onyesha mfano mmoja wa sauti mwambatano. (al.1)
    2.  
      1. Elezea maana ya kiimbo. (al.1)
      2. Elezea umuhimu wake. (al.2)
    3. Onyesha miundo miwili tofauti ya nomino zipatikanazo katika ngeli ya U-ZI.(Al.1)
    4. Bainisha mazingira mawili ambapo alama ya kiulizi (?) hutumika.  (al.1)
    5. Bainisha aina mbili za silabi katika neno; Alhamisi. (al.2)
    6. Yakinisha katika wingi. (al.1)
      Mwalimu hakumwadhibu mwanafunzi.
    7. Andika sentensi ifuatayo katika wakati uliopita hali timilifu.(al.1)
      Mtoto analala
    8. Onyesha aina mbili za mofimu katika sentensi ifuatayo. (al.2)
      Mimi ninasoma vizuri
    9. Tunga sentensi yenye muundo ufuatao.(al.3)
      RN+RT+RN
    10. Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya mishale. (al.3)
      Mbaywayu na korongo ni ndege ambao huishi.
    11. Bainisha aina za shamirisho. (al.3)
      Mwalimu alimwandikia mwanafunzi maagizo kwa kalamu.
    12. Bainisha aina ya vishazi katika sentensi.   (al.2)
      Mwanafunzi aliyekuwa akisoma amechoka.
    13. Andika visawe vya maneno haya.   (al.2)
      1. Heshima –
      2. Ruhusa -
    14. Eleza maana mbili ya fungu hili.(al.2)
      Jua lile
    15. Onyesha matumizi ya kiambishi ‘ku’ katika sentensi ifuatayo.  (al.2)
      Opiyo atakutengenezea mpini wa jembe na kukuletea kwako.
    16. Andika sentensi hii upya ukitumia vinyume vya maneno yaliyopigiwa mstari.  (al.2)
      Mwanafunzi aliketi kisha akakitega kitendawili.
    17. Tunga sentensi moja moja ukitumia vitenzi hivi kwa kauli uliyopewa. (al.2)
      1. La – (tendeana)
      2. Vaa - (tendwa)
    18. Andika kwa msemo wa taarifa.(al.2)
      “Tusipofanya kazi yetu kwa bidii na kujitegemea, tutabaki kuwa watumwa katika nchi yetu,” Rais alisema.
    19. Tumia ‘O’ rejeshi kama kiwakilishi.  (al.1)
      Msichana ambaye huja shuleni mwetu ni mwanasheria.
    20. Bainisha aina ya virai vilivyopigiwa mstari.(al.2)
      Mhadhara huo tata ulitolewa jana jioni.
  4. SEHEMU YA D    (ALAMA 10)
    1. Taja lahaja zozote nne katika kiswahili.  (al.4)
    2. Elezea nadharia zozote tatu ambazo huelezea chanzo cha kiswahili.  (al.3)
    3. Fafanua sifa zozote tatu za salamu katika mazungumzo. Toa sababu tatu.


NAKALA YA MAJIBU

  1. UFAHAMU
    1. Kwa kuwa mfano mbaya ambao Bwana Tenge anajihusisha na mapenzi ya kiholela mbele ya watoto.
    2.  
      • Ajira ya watoto
      • Dhiki za kisaikolojia – Tenge afanyapo mapenzi mbele ya watoto
      • Makazi duni – chumba kidogo.
    3.  
      • Kuhamishwa bila kujali maslahi ya watoto wao.
      • Vyumba vidogo sana
      • Umaskini
    4.  
      • Mvumilivu
      • Mnyonge
      • Mlezi mwema
      • Mwenye utu
    5. Ndoa ina changamoto ya kukosa uaminifu ambapo Tenge aliwaleta wanawake wengine ndani ya nyumba mkewe alipoenda mashambani.
    6.  
      • Danguro – nyumba inayotumiwa na Malaya kufanyia uasherati
      • Kisaikolojia – inayohusiana na akili ya binadamu.
  2. UFUPISHO
    1.   Ripoti za uhalifu wa pesa za umma katika serikali za kaunti ni za kusikitisha.
    2. Mabilioni ya pesa hufujwa katika serikali kuu.
    3. Wananchi wanakosewa mtindo huu ukiendelea katika serikali za kaunti.
    4. Katiba mpya ilipopitishwa wakenya walidhani ingewatatulia matatizo yao.
    5. Miaka tisa baadaye kuna mafanikio ingawa yanaweza kuboreshwa.
    6. Magavana hubuni nafasi za kazi na kupatia marafiki zao.
    7. Wananchi wameanza kufa moyo kuhusiana na ugatuzi.
    8. Changamoto za ugatuzi ni ulafi wa viongozi waachache.
    9. Wakosoaji wa ugatuzi huchochea wananchi wasichangie maendeleo katika kaunti zao.
      (alama 8, 1 ya mtiririko)
  3.  
    1. Juhudi za maendeleo haziwezi kufanikishwa bila ushirikiano.
    2. Ni jukumu la viongozi kuonyesha nia ya kutumia mamlaka kwa manufaa ya raia.
    3. Tume ya maadili ya kupambana na ufisadi inafanya kazi nzuri ya kuwashtaki magavana waliofuja mali ya umma.
    4. Asasi zote a washika dau wasifumbie macho maovu.
    5. Nchi inatawaliwa kwa misingi ya kisheria hivyo viongozi wasihurumiwe.
    6. Adhabu kali pekee zitakomesha uongozi mbaya.
      (alama 7, 1 ya mtiririko)
  4. LUGHA
    1.  
      1.  
        • Irabu ya mbele
        • Irabu ya tandazwa
        • Hutamkwa ulimi ukiwa wastani.
      2. Konsonanti mbili ambazo hufuatana na hutamkwa kwa pamoja.
        /mwl,/bwl,/nywl,/chwl
    2.  
      1. Upandishaji na ushushaji wa sauti wakati wa kuzungumza.
      2.  
        • kuonyesha sentensi ambazo ni ulizi
        • Rai/ombi
        • Amri
        • Taarifa
        • Hisia ya mshangao, dharau.
    3.  
      • U-nd-k.m ulimi – ndimi
      • Wa-ny-k.m waya-nyaya
      • u- k.m ukuta – kuta
      • u – ny – k.m uwanja – Nyanja
    4.  
      • Katika kauli dadisi/ulizi – k.m. Jina lako nani? u – hisia
      • Katika kauli za kibalagha k.m – unafikiria mimi najali
    5.  
      • Al – silabi funge
      • Ha –mi-si – silabi wazi
    6. Walimu waliwaadhibu wanafunzi.
    7. Mtoto alkuwa amelala.
    8.  
      • Mimi – mofimu huru
      • Ni – mofimu tegemezi
    9. Kadiria jibu laa mwanafunzi ukifuata mfano ufuatao
      kijana mrefu  alisimama wima mbele ya gari
               RN                 RT                 RN
    10.    
      S – KN+ KT
      KN – N+U+N
      N – Mbayuwayu
      U – na
      N – Korongo
      KT – t+N+S̅
      t – ni
      N – ndege
      S̅ – ambao huishi mwituni
    11.  
      • Mwanafunzi – sh kitondo
      • Maagizo – sh kipozi
      • Kalamu – chagizo
    12.  
      • Mwanafunzi aliyekuwa – kishazi tegemezi
      • Mwanafunzi amechoka – kishazi huru
    13.  
      • Heshima – staha, taadhima
      • Ruhusa – idhini, kibali
    14.    
      • Ufahamu/uelewe/unaizi/uamizi
      • Gimba/nyota kubwa lenye joto kali/inayotoa mwanga.
    15.  
      • Atakutengeneza – nafsi ya pili umoja
      • Kukuletea – kauli ya kutenda
    16.  
      • Aliketi – alisimama
      • Akakitega – akakitegua
    17.  
      • La – liana
      • Vaa – valiwa
    18. Rais aliwaambia ya kuwa wasipofanya kazi yao kwa bidii na kujitegemea, wangebaki kuwa watumwa katika nchi yao.
    19. Ajaye shuleni mwetu ni mwanasheria.
    20.  
      • Huo tata – kirai kivumishi
      • Jana jioni – kirai kielezi
  5. ISIMU JAMII
    1.    
      • Kiamu                  kijomvu                kingozi
      • Kimvita                kipate                   chichifundi
      • Kipemba              kingwana               kingazija
      • Kiunguja              kichiini
    2.    
      • Kiswahili ni lugha ya kibantu
      • Kiswahili ni lugha mseto.
      • Kiswahili ni lahaja ya kiarabu.
    3.    
      • Kuonyesha heshima
      • Ni kitangulizi cha mazungumzo
      • Huonyesha imani ya kidini
      • Huonyesha wakati
      • Huonyesha uhusiano.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Form 3 Questions and Answers - Term 3 Opener Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest