MAAGIZO
- Jibu Maswali yote
- Swali la kwanza ni la lazima
Swali la lazima
- Andika dayalojia baina ya mtu na rafiki yake ambao ndiyo kwanza wakutane toka walipoachana katika shule ya msingi.
- Andika insha juu ya methali “Mti mkuu ukigwa wana wa nyuni huyumba”
- Kuboresha maisha katika magereza ni kukuza uhalifu. Jadili
- Niliskia jina langu likitajwa. Mmoja akaniita nikatoka nje. Nilisikia msongamano wa watu nyimbo za ushindi zikapanda juu!.................... Endeleza kisa hiki.
MARKING SCHEME
Makosa ya Sarufi
- Sahihisha kwa makini sana ukionyesha makosa yote yanayotokea. Makosa ya sarufi huwa
Kuakifisha vibaya: Mifano, vikomo, vituo, alama ya kuuliza n.k. - Kutumia herufi ndogo au kubwa mahali si pake.
- Matumizi mabaya ya ngeli na viambishi, nyakati, vihusiano, muundo mbaya wa sentensi na mnyambuliko wa vitenzi na majina.
- Kuacha au kuongeza maneno katika sentensi kwa mfano, „kwa kwa‟
- Matumizi ya herufi kubwa.
Tazama: Matumizi ya herufi kubwa- Mwanzo Wa sentensi.
- Majina ya pekee
- Majina ya mahali, miji, nchi n.k.
- Siku za juma, miezi ak.
- mashirika, masomo, vilabu u.k.
- Makabila, lugha u.k.
- Jina la Mungu.
Makosa ya Hijai/ tahajia
Haya ni makosa ya maendelezo. Sahihisha huka ukionyesha yanapotokea mara ya kwanza tu Makosa ya tahajia huwa katika:
- Kutenganisha maneno kama vile „aliye-kuwa‟
- Kuunganisha maneno kama vile „kwasabahu‟
- Kukata silabi vibaya kama vile „ngan-o‟
- Kuandika herufi inayofaa katika neno karna „mahari‟ badala ya mahali‟
- Kuacha herufi katika neno kama aliekuja badala ya aliyekuja.
- Kuongeza herufi isiyofaa katika neno kama piya badala ya pia
- Kuacha alama inayotarajiwa kuwepo katika herufi
- Kutoandika kistari cha kuunganisha neno ufikiapo pambizo au mwisho; au kuandika mahali si pake.
- Kuandika kistari pahali pasipofaa
- Kuacha ritifaa au kuiweka mahali pasipofaa.
- Kuandika maneno kwa ufupi mfano k.m nk, v.v
Mtindo
Mambo yatakayochunguzwa.
- Mpangiiio wa kazi kiaya.
- Mtiririko wa mawazo.
- Hati nzuri inayosomeka kwa urahisi.
- Namna anavyotumia methali, misemo, tamathali za usemi na mengineyo.
- Unadhifu wa kazi.
- Kuandika herufi vizuri k.rn: Jj, Pp, Uu, n.k.
- Sura ya insha.
Msamiati
Jumla ya maneno yaliyotumiwa kuafikiana na mada au kichwa kilichopendekezwa.
Swali la lazima
- Andika dayalojia baina ya mtu na rafiki yake ambao ndiyo kwanza wakutane toka walipoachana katika shule ya msingi.
JIBU- Tanbihi: Dayalojia ni mazungumzo ya kawaida ya ‘nipe nikupe’ /fuata mtindo /mpangilio huu
- Mtahiniwa abainishe wahusika kwa majina yao.
- Semi koloni iwekwe baada ya jina la mhusika
- Alama za usemi halisi zisitumiwe kamwe
- Maelezo ya ziada yawekwe kwenye mabano
- Viingizi/ vihisishi vitumiwe ili kuyapa mazungumzo uhalisia (uhai)
- Mawazo yatiririshwe kwa namna inayoonyesha uhalisia
- Mada tofauti zaweza kuzungumziwa.
- Andika insha juu ya methali “Mti mkuu ukigwa wana wa nyuni huyumba”
Kugwa ni kuanguka: Nyuni ni ndege.- Methali ni mafumbo yenye maana fiche. Lazima mtahiniwa aguzie sehemu mbili za methali husika. Akiegemea upande mmoja aadhibiwe
- Maana ya methali
Mtu ambaye ndiye tegemeo la jamii au la mtu binafsi akiaga au aende asipatikane tena waliomtegemea wataumia. - Tanbihi
Mtahiniwa aandike kisa au visa vinavyothibitisha ukweli wa methali hii.
- Kuboresha maisha katika magereza ni kukuza uhalifu. Jadili.
- Hii ni insha ya mjadala: Mtahiniwa aweza kushughulikia upande wa kuunga pekee au ashughulikie upande wa kupinga pekee.
- Mtahiniwa aweza kushughulikia pande zote mbili na kutoa uamuzi au msimamo wake
HOJA: KUUNGA- Wafungwa wengine watakwepa majukumu
- Si adhabu tena ikiwa wataishi raha mstarehe
- Magereza yakiboreshwa watu watataka kuishi huko kukwepa majukumu yao
- Watu wavivu watavunja sheria maksudi ili wawekwe korokoroni
- Ukosefu wa usalama utafanya watu kukatalia gerezani
- Si adhabu tena
KUPINGA - Rekodi ya kuwa mfungwa humnyima mtu nafasi ya ajira katika viwango Fulani
- Mtu huko kujiendeleza maishani
- Mateso ya kifungoni ni makali kwa hivyo kifungo ni adhabu kubwa kwao.
- Aibu ambayo hutokana na kuwa mfungwa humfanya mtu asipende kuishi gerezani.
- Niliskia jina langu likitajwa. Mmoja akaniita nikatoka nje. Nilisikia msongamano wa watu nyimbo za ushindi zikapanda juu!.................... Endeleza kisa hiki.
- Hii ni insha ya mdokezo. Lazima mtahiniwa aendeleze kisa hiki wala asimalizie kwa mdokezo huu.
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 3 Mid Term 2 Exams 2021.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students