Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Form 3 Mid Term 2 Exams 2021

Share via Whatsapp
  1. UFAHAMU (ALAMA 15)

    Soma kifungu kifuatacho kasha ujibu maswali yafuatao:-

    Pengine mwandishi Goerge Orwell alikuwa na maono ya jinsi mataifa mengi ya Kiafrika yangekuwa pindi baada ya kujinyakulia uhuru, alipoandika riwaya ya ‘Shamba la wanyama.’

    Riwaya hiyo inaakisi hali halisi ya mataifa haya, Kenya ikiwemo, ambapo imejikita katika dhihirisho la jinsi ujenzi wa matabaka ya kitawala, ubinafsi na ukandamizaji wa wananchi, unavyoweza kuzua maasi na hatimaye mapinduzi ya uongozi ulio mamlakani.

    Baada ya kuwaambia wanyama kuhusu maono aliyokuwa nayo ya ulimwengu ambao kila mmoja angeishi huru, nguruwe mmoja anayeitwa Old Major, alijenga ari ya wenzake ili kushinikiza ndoto yake, kwa kuandika amri saba ambazo zilihakikisha kuwa rasilimali zote katika shamba hilo zingegawanywa kwa kila mmoja.

    Lakini haya yote hayakuzingatiwa muda mfupi baadaye kwani ubinafsi uliokithiri ulichakachua amri hizo na kusambaratisha mfumo wa uongozi katika shamba hilo. Hali hiyo ndiyo tunayoshuhudia kwa sasa, wananchi wanapoandamana katika majimbo mbalimbali kulalamikia ‘kodi mpya za maendeleo’ zinazoanzishwa na serikali hizo. Huu ndio mkasa wa ubepari, uliojificha katika mfumo kandamizi wa ugatuzi, ambao kwa wazo langu,hatukuwa tumejitayarisha kabisa kuuanzisha. Tumegatua kila aina ya uovu, umero na wizi. Tulilolisahau ni kuwa ‘magavana’ hawa tulioamka mapema kuwachagua walikuwa viongozi wale wale waliokuwa wakihudumu katika serikali za hapo awali, na hawakuwa ‘,miungu wa ukombozi kama walivyotupulizia baragumu zao walipokuwa wakitunadia kila aina ya ‘ahadi’ wakati wa kampeni.

    Kwani ufisadi ndio umekithiri uovu mwingine tulioagatua ni ukabila. Kwa sasa, tofauti zilizopo si za kumchukia Mkikuyu au Mturkana akihiana na Mluo. Kila jamii kwa sasa zinaona wenzao kwa misingi ya kiukoo.

    Mathalani, mzozo wa uongozi jimboni Embu unaelezwa ‘kuchochewa’ na tofauti za uwakilishi kati ya jamii za Waembu na Wambeere. Hapo awali, hatungesikia ‘mikataba’ kama hii! Huu ni moto uwakapo, kama si safari ya kuzimu tunayoelekea!

    Kwani vita vya kikabila havitasikika tena, bali mafarakano yatakayochukua nafasi yake ni ‘mizozo ya kiukoo, ambayo katika majimbo yote 47 ni mkasa kama si saratani tuliyojiambukiza.

    Ikiwa hatutatahadhari, huenda tukashuhudia maasi ya kiukoo katika nchi ndogo 47’ – na kizungumkuti kitakuwa jinsi ya kuyazima, kwani kila koo ‘likipigania nafasi yalo.’
    MASWALI
    1. Kwa mujibu wa mwandishi wa makala haya ni mambo yapi yanayoweza kuzua maasi katika nchi ?(alama 3)
    2. Eleza mifano miwili ya maovu ambayo yamezungumziwa katika kifungu .(alama 2)
    3. “Huu ni moto uwakapo, kama si safari ya kuzimu…..” maneno haya yana maana gani kwa mujibu wa taarifa hii. (alama 3)
    4. Kwa nini mwandishi amefananisha mataifa mengi ya kiafrika baada ya uhuru na shamba la wanyama?(alama 3)
    5. Dhihirisha kauli ya mwandishi kuwa ‘tumegatua kila aina ya uovu, umero na wizi.(alama 2)
    6. Eleza maana za msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika taarifa (alama2)
      1. Inaakisi………………………………………………………………………………………….
      2. Mizozo ya kiukoo……………………………………………………………………………
  2. MUHTASARI

    Uhaba wa nafasi za kazi unaeendelea kushika kasi, nayo serikali inatoa wito kwa watu wa matabaka mbalimbali kujibidiisha kujiajiri badala ya kungojea kazi za ajira kutoka kwa mashirika mbalimbali.

    Hata hivyo, ingawa hili ni wazo nzuri, utapata kwamba kuna vikwazo mbalimbali vinavyowafanya watu kutotaka kuanzisha biashara zao ndogondogo . Ingawa kuna tumaini kuwa uchumi wa nchi umeanza kukua, baadhi ya watu hawataki kujijasirisha kuanzisha biashara zao kwa hofu ya kutofaulu.

    Wengi wanaogopa kuwekeza pesa zao kwenye biashara ambazo huenda zisiwafaidi katika siku za usoni. Ingawa kuna wale wangetaka kuanzisha viwanda vyao vidogovidogo, kuna tazizo la ukosefu wa pesa za kununulia mtaji.

    Vijana wengi wanaotaka kubahatisha katika upande huu hujipata wakiwa hawana hata hela za kununulia vifaa, sikwambii kulipia kodi ya nyumba za kufanyia kazi. Hali hii inazidishwa na tatizo la kupata mikopo kwani hawana wadhamini.

    Hakuna atakayewaamini kiasi cha kuwapa mikopo. Aidha, katika miaka ya hivi majuzi mashirika ya kutoa mikopo yamekuwa yakidai riba kubwa mno kwa wadeni wao. Jambo ambalo huwafisha moyo wawekezaji wadogowadogo . utapata kuwa hata wale ambao tayari wameanzisha biashara zao hawawezi kuzipanua kwa sababu ya riba kubwa zinazotozwa na mashirika haya.

    Baadhi ya watu hudharau kazi za kujiajiri, hasa zile za mikono, wakidai kuwa hazina pato nono. Kwa mfano ukimwambia mwanamke aanze kazi ya ususi wa vikapu, labda atasema kuwa hiyo ni kazi duni, ya pato duni na atahiari kuendelea kusagika kwa shida badala ya kufanya kazi anayoiona duni. Wengine huona kuwa itachukua muda mrefu kwa biashara hizo kuanza kuleta faida na kuweza kufidia kiasi cha pesa walizotumia kuzianzisha.

    Watu wengine huona vigumu kuanzisha biashara ndogondogo kwa sababu ya kuchelea kulipa kodi. Kuna wale wanaoona kuwa kodi watakazolipa kwa serikali ni kubwa sana na hawataweza kuzimudu. Nao ushindani kutoka kwa mashirika ambayo tayari yamestawi huwafisha moyo wafanyabiashara wadogo wadogo. Wengine hulazimika kufunga biashara zao na kubahatisha kwingine. Tatizo la ukosefu wa masoko ni kikwazo kingine.

    Kabla ya kuanzisha biashara, mtu hana budi kuwa na soko kwa bidhaa zake. Hata hivyo, utapata kuwa baadhi ya watu hukosa masoko kwani wateja wao huhiari kununua bidhaa kutoka ng’ambo au hata mashirika makubwa ya humu nchini. Jambo hili huua biashara ndogondogo. Kwa mfano, soko la mafundi wa juakali si pana kwa sababu ya wananchi wengine kudharau bidhaa zao.

    Usalama ni jambo muhimu sana kwa ufanisi wa biashara yoyote ile. Watu wengi hawataki kuthubutu kuanzisha biashara zao kwa sababu ya ukosefu wa usalama. Katika mitaa ambayo kodi si ghali, kuna visa vingi vya wizi na ujambazi ambao huwafanya watu wengi wasianzishe kazi zao huko.

    Serikali ina dhima ya kuwashawishi wananchi kujiajiri ili kupunguza tatizo la uhaba wa nafasi za kazi. Ili kufikia lengo hili, viongozi wanapaswa kuwapa vijana mikopo yenye masharti nafuu. Aidha ni wajibu wa serikali kuhakikisha kuwa vijana hawa wametozwa kodi nafuu. Serikali pia inafaa kuwalinda wafanyabiashara wadogowadogo dhidi ya ushindani mkali kutoka kwa bidhaa za kuagiza kwa kuzitoza ushuru mkubwa bidhaa zinazoingia nchini.

    Maswali
    1. Eleza mambo muhimu yanayozungumziwa katika aya ya kwanza na ya pili.(maneno 100-110) alama 10,1 ya utiririko)
      Matayarisho
      Jibu
    2. Bila kubadilisha mawazo ya mwandishi fupisha aya ya mwisho. (maneno 60-65) (alama 5, 1 mtiririko)
      Matayarisho
      Jibu
  3. MATUMIZI YA LUGHA
    1.  
      1. Eleza maana ya silabi.(alama 2)
      2. Andika silabi ya KKKI(alama 1)
    2. Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya jedwali.(alama 4)
      Mgeni ambaye amewasili ni mtoto wangu.
    3. Tunga sentensi moja moja kubainisha (alama 2)
      1. Kihusishi cha ujirani.
      2. kitenzi kushirikishi kipungufu ‘ndi’ (alama 2)
    4. Bainisha shamirisho katika sentensi hii.(alama 3)
      Mwalimu alimwandikia mwanafunzi wake mtihani kwa kalamu.
    5. Tumia kitenzi katika mabano ili kuunda nomino mwafaka kukamilisha sentensi .(alama 1)
      Hospitali hii ilikuwa na ……………………bora sana hapo zamani (huduma)
    6. Tambua maana mbili za sentensi ifuatayo.(alama 2)
      Mwalimu ametupa kitabu.
    7. Akifisha
      Bi tolo alienda kwa batu kuomba mapambo ya kujirembesha akamwambia ndugu yangu najua langu ndilo lako na lako ndilo langu naomba uniazimie marashi.
      (alama 3)
    8. Tunga sentensi zitakazodhihirisha matumizi yafuatayo ya neno’kwa’
      Kifaa kilichotumiwa kufanyia jambo.(alama 2)
    9. Tunga sentensi kubainisha.
      1. kielezi cha namna linganishi.(alama 2)
      2. kiunganishi cha masharti.
    10. Andika kwa wingi
      Punda aliumia ukwato wake alipokuwa akipita uani.(alama 2)
    11. Kanusha
      Wao wangetuazima kitabu tungemaliza kazi kwa wakati.(alama 2)
    12. Andika katika hali ya kutendesheka.(alama 2)
      Huyo mtoto hawezi kusomeshwa Historia.
    13. Bainisha vishazi katika sentensi hii kisha useme ni vya aina gani.(alama 2)
      Niliosha vyombo kisha nilikimbia sokoni.
    14. Andika upya kwa kubadilisha kivumishi kuwa kiwakilishi.(alama 2)
      Kitu kipya ni kizuri hata kikiwa kidonda.
    15. Huku ukitoa mifano, eleza matumizi manne ya herufi kubwa.(alama 2)
    16. Tunga sentensi ya neno moja kisha uonyeshe sehemu zifuatazo.(alama 3).
      1. Viambishi awali vya nafsi 1, wakati, kirejeshi.
      2. Mzizi
      3. Viambishi tamati-iw,a
    17. Eleza maana mbili za neno ‘rudi’.(alama 1)
  4. ISIMU JAMII (ALAMA 10)
    1. Eleza mitazamo mitatu kuhusu Chimbuko la Kiswahili huku ukionyesha kama mitazamo hiyo ina mashiko.(alama 6)
    2. Fafanua dhima nne za lugha ya Kiswahili nchini.(alama 4)


MARKING SCHEME

  1. Ufahamu
    1.  
      1. Matabaka ya kitawala
      2. Ubinafsi
      3. Ukandamizaji wa wananchi
        3x1=alama 3
    2.  
      1. Hali ya magavana kupigania njia za kujilimbikizia mali.
      2. Dhana ya ukabila-watu wanajitambua kulingana na jamii/ukoo wao.
        2x1=alama 2
    3. Watu kujitambua kulingana na koo zao ni sawa na moto kama uadui utachipuka kati ya watu wa jamii moja. Kwa mfano Waembu na Wambere.
      Hali hii inaweza kusababisha maafa kama vile vita vya kiukoo. (alama 3)
    4. Katika shamba la wanyama, nguruwe anayeitwa Old Major aliandika amri saba ambazo zitihakikisha kuwa rasilimali zote katika shamba zingegawanywa kwa wanyama wote. Baada ya mapinduzi wanyama waliochukua hatima ya uongozi waliendeleza ubinafsi uliosambaratisha mfumo wa uongozi.
      Kwa sasa hali hii inaendelea Kenya ambapo viongozi waliochaguliwa kuwakilisha kaunti/majimbo wanakandamiza raia kwa kuwatoza kodi, wanaendeleza ubepari n.k. (alama 3)
    5. Kila uovu kama vile ulafi, wizi n.k unaoendelezwa na viongozi magavana unasingiziwa ugatuzi. (alama 2)
    6.  
      1. Inaakisi-inaashiria
      2. Mizozo ya kiukoo-ugomvi/vita/ghasia za kikabila, watu wanaotokana na nasaba moja.
        (alama 2x1= alama 2
        Adhabu:
        • Kila kosa la sarufi litokeapo mara ya kwanza liadhibiwe kwa kutozwa (½ maki hadi makosa 6.
        • Kila kosa la hijai litakeapo mara ya kwanza liadhibiwe kutozwa (½ maki Hadi makosa 6.
  2. UFUPISHO
    1.  
      1. Uhaba wa nafasi za kazi umeendelea kushika kasi.
      2. Serikali inatoa wito kwa watu kujiibidiisha kujiajiri badala ya kungojea ajira.
      3. Kuna vikwazo vinavyowafanya watu kutotaka kuanzisha biashara.
      4. Baadhi ya watu hawataki kuanzisha biashara kwa hofu ya kutofaulu.
      5. wengi wanaogopa kuweka pesa kwenye biashara zisizowafaidi baadaye.
      6. kuna ukosefu wa pesa za kununulia mtaji.
      7. vijana wengi hawana hela za kununua vifaa wala kulipa kodi ya nyumba za kazi.
      8. Hawapati mikopo kwa kukosa wadhamini.
      9. mashirika ya kutoa mikopo yanadai riba kwa wadeni wao.
      10. jambo hili huwafisha moyo wawekezaji wadogowadogo.
      11. Baadhi ya watu hudharau kazi za kuajiri kwa kukosa pato nono.
        Zozote 10 x 1 =alama 10.
    2.  
      1. usalama ni muhimu kwa ufanisi wa biashara.
      2. Watu hawataki kuanzisha biashara bila usalama
      3. Visa vya wizi ujambazi huzuia watu kuanzisha biashara katika mitaa yenye kodi ya chini.
      4. Serikali inawashawishi wananchi kujiajiri ili kupunguza uhaba wa kazi.
      5. Viongozi wanapaswa kuwapa vijana mikopo yenye malipo nafuu.
        Serikali ihakikishe hili limetimia.
      6. Vilevile iwalinde wafanyabiashara wadogowadogo dhidi ya ushindani wa bidhaa kutoka nje kwa kuzitoza ushuru mkubwa.
        a-Alama 9
        b-Alama 4
        utiririko 2
        jumla 15
        Adhabu
        • Kila losa la sarufi litokeapo mara ya kwanza liadhibiwe kwa kutozwa ½maki hadi makosa 6.
        • Kila kosa la hijai litokeapo mara ya kwanza liadhibiwe kwa kutozwa ½maki hadi makosa 6.
        • Mtahiniwa hana idhini kuzidisha idadi kwa maneno 9. Akipita kiwango hiki atozwe ½maki kwa kila maneno matano matano.
  3. MATUMIZI YA LUGHA
    1.  
      1. Silabi ni kipashio cha kimatamshi ambacho kimsingi ni kikubwa kuliko sauti. Tamko katika mfumo wa sauti.
      2. Ngwa, ngwe, mbwa-yoyote (alama 1)
    2.  
                                       S      
                 KN             KT
          N            S   T      N      r
       Mgeni   ambaye amewasili   ni   mtoto   wangu 
      8x½=4
    3.  
      1. karibu na, kando ya ukingoni mwa, mbele ya, pembeni mwa, n.k.
        Hakiki sentensi. (alama 2)
      2. Ndiye k.m
        Huyu ndiye mwalimu. Hakiki (alama 2)
    4.  
      1. Mwanafunzi-kitondo
      2. Mtihani-kipozi
      3. Kalamu –ala (alama 3)
    5. Huduma (alama 1)
    6.  
      1. Mwalimu ameweka kitabu kando.
      2. Mwalimu ametukabidhi kitabu. (2 x 1=alama 2)
    7. Bi Tolo alienda kwa Batu kuomba mapambo ya kujirembesha, akamwambia.”Ndugu yangu, najua langu ndilo lako na lako ndilo langu. Naomba uniazime marashi”(alama 3)
    8. Mtoto alipigwa kwa rungu Hakiki   (alama 1)
    9.  
      1. Mwalimu aliniadhibu kijeshi.
        Aliongea kitoto (alama 1)
      2. Wapo, ikiwa, kama,ukitaka
        Hakiki sentensi (alama 1)
    10. Punda waliumia kwato zao walipokuwa wakipita nyuani. (alama 2)
    11. Wao wasingetuazima kitabu tusingemaliza kazi kwa wakati. (alama 2)
    12. Huyo mtoto hawezi kusomesheka Historia. (alama 2)
    13.  
      1. Niliosha vyombo
      2. Nilikimbia sokoni –vishazi huru
    14. Kipya kizuri hata kikiwa kidonda (alama 2)
    15.  
      1. Mwanzoni mwa sentensi
      2. Majina ya watu
      3. Siku za wiki, miezi n.k.
      4. Masomo.k.m.Hisabati,Kiswahili n.k.
        Yeyote 4 x ½ (alama 2)
    16. K.m. Niliyeitiwa. Hakiki(alama 2)
      • Ni –Nafsi
      • -li-wakati
      • -Ye-kirejeshi
      • -it-mzizi
      • iw-kauli
      • a-kiishio
        (au sentensi nyingine yoyote iliyo sawa).
    17.  
      1. rejea ulipotoka
      2. Nguo kuwa fupi
      3. Adhibu mtoto
        zozote 2x1=alama 2
  4. ISIMU JAMII (alama 10)
    1.  
      1. chanzo cha Kiswahili ni Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.
      2. Kiswahili ni tokeo la maingiliano baina ya waafrika na waarabu.
      3. Kiswahili kilitoka uarabuni/ni lugha ya kiarabu
      4. Kiswahili ni lugha ya kibantu
        • Mitazamo mitatu ya kwanza haina mashiko.
        • Mtazamo wa mwisho una mashiko kwani msamiati wa Kiswahili na wa kibantu unakaribiana sana.(3x2=alama 6
    2.  
      1. Ni kitambulishi cha utaifa.
      2. Lugha ya taifa
      3. Lugha rasmi
      4. Chombo cha kutolea elimu.
      5. Chombo cha mawasiliano
      6. Nyenzo ya kuwaunganisha watu wenye asili mbalimbali.
        Zozote 4 x 1=alama 4
        • Kila kosa la sarufi litokeapo mara ya kwanza liadhibiwe kwa kutozwa ½ maki hadi makosa 6
        • Kila kosa la sarufi litokeapo mara ya kwanza liadhibiwe kwa kutozwa ½maki hadi makosa 6.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Form 3 Mid Term 2 Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest