KISWAHILI
GREDI LA 4
MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA WA 2
SEHEMU YA KWANZA
KUSIKILIZA NA KUONGEA (Alama 15)
-
- Andika maneno ambayo mwalimu atakusomea.
Sikiliza kwa makini, kisha uandike(Alama 5) - Tegua vitendawili hivi (Alama 2)
- Teketeke huzaa gumugumu na gumugumu huzaa teketeke
_______________________________________________
(yai, macho, nyayo) - Huwa safi kikiwa cheusi na kichafu kikiwa cheupe
_______________________________________________
(kalamu na kitabu, ubao)
- Teketeke huzaa gumugumu na gumugumu huzaa teketeke
- Taja wakati wa maamkuzi na maagano haya. (Alama 3)
(asubuhi, jioni, adhuhuri, wakati wowote, usiku)- Hujambo
- Lala unono
- Sabalkheri
- Kamilisha methali hizi.(Alama 2)
- Pole pole ndio
- Mtoto wa nyoka
- Ambatanisha maneno haya ya upole ipasaavyo. Fuata mfano.
- Andika maneno ambayo mwalimu atakusomea.
SEHEMU YA PILI SARUFI (Alama 20)
-
- Soma kifungu hiki kisha uchagua nomino kutoka kifungu (Alama 5)
Mwalimu wangu anapenda kufunza lugha ya Kiswahili. James husoma vizuri katika kipindi cha lugha. Jumatatu masomo ya asubuhi, Naomi pia husoma ufahamu kwa ufasaha, kweli watu wa Mombasa hupedna kiswahili kuliko wengine. - Tafuta vitendo kumi katika mraba huu. (Alama 10)
Mfano pika
Vitendo - Andika sentensi hizi upya. Tumia viwakilishi.
(sisi, wewe, yeye, w 10) badala ya maneno yaliyopigiwa mstari.(Alama 2)- Damiana analima shamba
______________________ - Wanafunzi tutafunga lini?
______________________
- Damiana analima shamba
- Pigia mstari viunganishi katika sentensi hizi.(Alama 2)
- Maembe,machungwa na mananasi ni matunda.
- Nilimshauri ila hakusikia.
- Maneno polepole, vizuri, haraka haraka, upesi na darasani ni (Alama 1)
____________________________________________
(nomino, vielezi, viwakilishi, viunganishi)
- Soma kifungu hiki kisha uchagua nomino kutoka kifungu (Alama 5)
SEHEMU YA TATU KUSOMA (Alama 10)
Soma kifungu kisha ujibu maswali.
Asubuhi moja, mama alikuwa tayari kuondoka akielekea kazi pale, Tembea Tuonane. Aliwaita watoto wake na kuwaambia wamsikilize kwa makini.
“Ninaenda kazini. Nimeacha kila kitu kikiwa sawa hapa nyumbani. Ninajua mnapenda mchezo. Nikirudi nipate nyumba na vyombo vyote vichafu. Nipate pia mmekula chakula chote hata cha mtoto, sawa?" mama aliwambia,kwa kujua mazoea ya watoto wake. “Sawa, mama!" wote walijibu. Mama aliondoka akaenda kazini.
Maswali.
- Nani alikuwa anaenda kazi asubuhi ile?______________________
- Mama aliwataka watoto wasikilize kwa______________________
- Mama anaposema, nikirudi nipate nyumba na vyombo vyote ni vichafu ana maanisha nini?______________________
- Watoto wale walikuwa na mazoea yapi?______________________
- Je, unafikiri mama aliporudi jioni alipata watoto wamefanya nini?______________________
INSHA
Andika insha kuhusu: Sherehe Nyumbani Kwetu
MAAKIZO
sehemu ya kwanza
-
- Mwanafunzi anapaswa kuandika maneno ambayo mwalimu atamsomea.
-
- yai
- ubao
-
- wakati wowote
- usiku
- asubuhi
-
- mwendo
- ni nyoka
-
sehemu ya pili
-
-
- Mwalimu
- James
- Jumatatu
- Naomi
- Mombasa
-
- pakua
- amsha
- andika
- tandika
- kaa
- fagia
- anika
- sugua
- shona
- panga
-
- Yeye
- Sisi
-
- na
- ila
- vielezi
-
sehemu ya tatu
- mama
- makini
- anamaanisha kinyume/ anamaanisha wasifanye jinsi alivyosema/ anamaanisha kuwaonya wasifanye hivo alivyosema
- ya kucheza
- alipata vyombo safi/nyumba safi/ chakula hakijaliwa chote/ chakula cha mtoto hakijaliwa
Download Kiswahili Activities Questions And Answers - CBC Grade 4 End of Term 2 Exam SET 2 2021.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students