0 votes
3.3k views
in Isimu Jamii by
Eleza mambo manne yanayosababisha wingilugha.

1 Answer

0 votes
by
  • Michezo na utalii – watalii na wanamichezo huhamia na kuyazuru mataifa ambako lugha tofauti na zao huzungumzwa na kulazimika kujifundisha lugha hizo ili kufanikisha mawasiliano kati yao na wenyeji wao.
  • Elimu – mataifa huweka sera kuhusu lugha rasmi katika elimu, hali inayowalazimisha wanafunzi kujifundisha lugha zaidi ya mbili.
  • Vita na uhamiaji – hali hii huwashurutisha wakimbizi kujifundisha lugha inayosemwa ukimbizoni ili kufanikisha mawasiliano yao na ya wenyeji.
  • Dini – dini kama Uislamu na Ukatholiki huongozwa na linguafranka za Kiarabu na Kilati mtawalia, hali hii huwashurutisha haswa viongozi wake kujifundisha lugha hizi ili kufanikisha mahubiri na shughuli nyingine za kidini.
  • Shughili za kibiashara – hizi huwafanya watu kujifunza lugha za washitiri wao ili kuweza kuwasiliana nao.
  • Sanaa na burudani – hili huwapata sana wasanii wa muziki na filamu ambao hulazimika kujifundisha lugha fulani za kigeni ili kuweza kuigiza dhima fulani mahususi katika filamu.

Related questions

0 votes
2 answers
0 votes
0 answers
0 votes
0 answers
asked Apr 13, 2022 in Isimu Jamii by babushka
0 votes
1 answer
asked Dec 26, 2021 in Isimu Jamii by DomitilaMboya
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...