0 votes
666 views
in Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine by

Mame Bakari- (Mohammed Khelef Ghassary)
“Haikuwa stahiki yake kubebeshwa mzigo kama ule.”

  1. Fafanua muktadha wa dondoo hili. 
  2. Taja na kueleza tamathali iliyotumiwa kwenye dondoo hili. 
  3. Onyesha jinsi mrejelewa alivyoathirika kwa kubebeshwa mzigo. 

1 Answer

0 votes
by
  1.  
    1. Maelezo ya mwandishi/msimulizi
    2. Ni kumhusu Sara.
    3. Sara alikuwa amebakwa na janadume moja alipokuwa akirejea jioni moja kwa masomo ya ziada.
    4. Hali hii ilimsababishia huzuni na kilio cha siku nyingi kwa kuwa jitu lile liliyabadilisha maisha yake milele.
  2.  
    1. Jazanda (alama 1)
    2. Kubebeshwa mzigo (alama 1)
    3. Maana- kuathirika kutokana na ujauzito wa mapema/ mateso kutokana na ujauzito.
  3.  
    1. Kujeruhiwa- baada ya kubakwa, Sara alijeruhiwa vibaya na damu nyingi kuvuja (uk. 67).
    2. Maisha yake kuingiliwa na kuharibiwa kabisa kwa kutiwa mimba
    3. Kuvunjiwa ujanajike wake na utu wake.
    4. Kunyimwa furaha- maisha yake kutawaliwa na kilio siku zote. Anazongwa na mawazo mengi yanayomliza (uk. 67).
    5. Mawazo ya kutengwa, kusutwa, na kukashifiwa na jamii yake yalimsumbua sana.
    6. Aliona kuwa angelaaniwa na kila mtu wa karibu na wa kando (uk. 48) (jamaa zake na jamii kwa ujumla)
    7. Mawazo ya kupigwa na kufukuzwa nyumbani na babake yalimtia wasiwasi sana.
    8. Hali ya kutoaminiwa na wazazi endapo angewaeleza ukweli kuhusu kubakwa kwake. Aliona kuwa wazazi wake hawangemwamini kwa kushtakia unyama aliotendewa njiani. Badala ayake wangemlaumu kwa kushindwa kujitunza (uk 48)
    9. Kukatiziwa masomo yake- aliwazia jinsi angefukuzwa skuli (uk. 48)
    10. Kejeli- mwalimu mkuu angemkejeli kwa kumweleza kuwa ile ilikuwa ni skuli ya wanafunzi sio ya wazazi na kuwa hawafundishi wanawake pale wanafundisha wasichana.
    11. Kutengwa na wanafunzi wenzake ambao anasema wangelimsusuika na kumtenga kama mgonjwa wa ukoma. (uk.49)
    12. Kuingiwa na wazo la kujitoa uhai ambalo baadaye alilikataa.
    13. Kuingiwa na wazo la kuavya mimba ambalo licha ya kukiangamiza kitoto chake, lingeweza kuyatia maisha yake katika hatari. Aliwazia kukimbia kwao kama njia ya kujisalimisha na dhuluma na shutuma za babake.
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...