0 votes
1.6k views
in Kigogo by

“…kulinda uhai, kulinda haki, kulinda uhuru…”

  1. Weka dondoo hili katika muktadha wake 
  2.  Taja na ufafanue maudhui mawili yanayojitokeza katika dondoo hili 
  3. Msemaji wa maneno haya alifanikiwa kulinda uhai, kulinda haki na kulinda uhuru.

1 Answer

0 votes
by
  1. Weka dondoo hili katika muktadha wake 
    • maneno ya Tunu
    • akimwambia Sudi
    • wakiwa barazani mwa nyumba ya Sudi
    • wakizungumza kuhusu jinsi ya kuzitetea haki za wanasagamoyo
       
  2.  Taja na ufafanue maudhui mawili yanayojitokeza katika dondoo hili 
    • uwajibikaji-Tunu na Sudi wanawajibika kwa kujitolea katika kulinda haki za kimsingi za Wanasagamoyo na wanachukulia jambo hili kuwa jukumu lao uzalendo-Tunu na Sudi ni wazalendo kwani wanataka kuiona Sagamoyo iliyo na ufanisi kwa wananchi wote. 
  3. Msemaji wa maneno haya alifanikiwa kulinda uhai, kulinda haki na kulinda uhuru.
    • Anaongoza maandamano Sagamoyo na kukiri kutolegeza msimamo wake hadi soko lifunguliwe
    • Anapanga kuleta wachunguzi kutoka nje kuchunguza mauaji ya Jabali
    • Anamkashifu Majoka kwa uongozi wake uliojaa mauaji
    • Anahutubia wanahabari kuhusu hali halisi Sagamoyo kwa ujasiri
    • Anapigania usalama wa kila mtu Sagamoyo bila ubaguzi
    • Anamsamehe Mamapima anapomwomba msamaha
    • Anakataa kuolewa na mhuni Ngao Junior jambo linalomwezesha kuendeleza utetezi wa haki za wanasagamoyo.
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...