0 votes
3.6k views
in Kigogo by
Fafanua aina zozote kumi za migogoro ijitokezayo katika tamthilia ya kigogo

1 Answer

0 votes
by
  1. Kwanza kuna migogoro kati ya wananchi na polisi. Polisi wanawapiga na kuwajeruhi wananchi wasio na hatia.
  2. Pili kuna migogoro kati ya polisi na viongozi wao. Viongozi wanawatisha polisi. Naye kingi mkuu wa wanapolisi anatishiwa kufutwa kazi.
  3. Kuna migogoro kati ya wananchi na viongozi wao. Majoka anawatusi wancanchi waliojataa kuenda katika sherehe zilizoandaliwa katika uwanja wa wazalendo.
  4. Kuna migogoro kati ya viongozi na vituo vya habari. Majoka anafunga vituo vyote vya habari baada ya kupeperusha mbashara mgomo uliongozwa na tunu.
  5. Kuna migogoro kati ya viongozi na wapinzani wao. Tunaona jinsi majoka anapinga kuvamiwa kwa tunu wakiwa na kenga. Majoka pia anapanga mauaji ya jabali babake tunu.
  6. Kuna mgogoro unaozuka kati ya kiongozi na mshauri wake. Kenga anapomgeuka majoka anaitwa kunguru.
  7. Migogoro ya kitabaka ambapo tabaka la juu linadhulumu watu wa tabaka la chini. Watu wa tabaka la juu wana maisha mazuri kama vile Majoka huku wa tabaka la chini wakimia kama akina Hashima. Jambo hili linaleta kutoelewana baina ya matabaka haya.
  8. Migogoro ya viongozi na wanachi. Viongozi wanaendeleza utawala wa kidhalimu, ni fisadi na hawajali raia jambo linalosababisha ktoelewana baina yao. Wanachi hata wanaanza harakati a kjikomboa mikononi mwao.
  9. Migogoro ya wanachi na askari. Askari na raia hawaelewani. Kila raia wanapogoma, askari wanafurusha na kuwatesa
  10. migogoro ya wafadhili na viongozi. Majoka hafurahishwi na wafadhili wanaosaidia akina Tunu na anawataka warudi kwao. Wafadhili hawa nao wanapinga utawala wa Majoka. 
  11. Migogoro ya viongozi na vyombo vya habari. Majoka anapendelea vituo vinavyoeneza propaganda na kupinga vinavyoelea ukweli wa mambo
  12. migogoro baina ya watetezi wa haki na vibaraka. Akina Tunu na Sudi hawaelewani kabisa na vibaraka wa Majoka kama vile Ngurumo na Boza.
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...